Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Kweli ni Hard Talk. Nimemvulia kofia Tundu Lissu kwa Ung'eng'e safi. Vijana wa Tanzania jifunzeni kiingereza. Mengine yaliyoongelewa sina comment.
 
Nimesiliza kwa kina sana mahojiano ya Bwana LISSU huko nchini Uingereza, hakika atakuwa sio wa Singida huyu.

Mtu anayewania Urais 2020 anashabikia USHOGA hapo tu amekosa KURA ZA WAISLAM WOTE NA WAKRITO WOTE, Labda apate kura za watt wake aisee.

Na waliokupiga Risasi wapo kwenye chama chako umeng'ang'ania Selkari ya MAGU tu..na bado ukirudi sijui kama hatutakuona unaokota makopo mtaani kwako SINGIDA kwa kupigwa KIPAPAI..maana kwenye chama chenu kila mtu anataka Urais 2020.

Ni mtazamo tu nisipigwe mawe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Queen unaniangusha bana!
Ina maana kama dereva angekufa uchunguzi usingefanyika?
Vipi kama tukio linatokea na watu wote wanauawa hapo uchunguzi ufanyika vp?

Sent using Jamii Forums mobile app

Dereva hajafa so inakuwa rahisi kuchunguza coz ye ndo shahid wa kwanza sasa dereva mwenyewe mmekataa asiulizwe kitu na hajulikani alipo so mnataka watu wawaze nini.
Yan risasi zote zile dereva haijampata hata moja???? Bado kuna ukakasi hapo.
 
Hakika mimi nimeipenda sana. Ukipewa kila kitu lakini ukanyimwa uhuru bado wewe sio huru. Ndio maana wanawake matajiri wanazaa na wauza mikaaa au wanaume matajiri wanatoka na mahousgirl hii ina apply sana katika maisha ya Democracy
 
Nimemsikiliza Tundu Lissu akikata nyanga huko BBC.
Aisee huyu jamaa ni kichwa, ni hazina ya Taifa.
Nimefurahi jinsi alivyokuwa akimwaga mapoint huku akitumia kiingereza safi kabisa utadhani kazaliwa na kukulia kwa Malkia.

Baadhi ya maswali ya Mitego ni kwamba yeye kama kiongozi wa upinzani je yuko Tayari kuondoa sera za kupinga mashonga?.Hili swali lilikuwa la mtego mno maana angeharibu hapa wazungu wangemuona pimbi.

Lissu nikaona anareflect, anavuta pumzi kisha akamjibu WHAT IS IN THE BEDROOM REMAINS IN THE BEDROOM!. Dah yule Steven Surkur akaona keshamalizwa, akang'ang'ania swali lake hilohilo Lissu akawa ameshammaliza

Steven Sutkur akamuuliza tena swali la Mtego kwamba Je wewe uko tayari kurudi bongo na kupambana kumuondoa Jiwe madarakani, Lissu akasema any moment Daktari wake akimruhusu na kumwambia yuko fiti kuendelea na Majukumu atarudi bongo na pia akasema kama chama chake kitamuamini na wananchi kumuunga mkono yuko Tayari kulifyekelea mbali Jiwe

Kisha Jamaa akamuuliza Je huogopi kurudi nyumbani kwa usalama wake?. Lissu akamwambia Serikali ya Jiwe itakuwa na jukumu la kumhakikishia ulinzi wake kwa sababu ana haki hiyo na pia serikali ya Jiwe itakuwa na jukumu la kuionyesha dunia kuwa kweli imetimiza jukumu lake!

Aisee!. Hiki kichwa ni hatari, Lissu nje ya nchi ni hatari kwa Siasa za Jiwe kuliko kubaki humuhumu ndani kwa kipindi hiki. Mimi nasema hivi aendelee kukandamiza kutokea hukohuko!!
Mkuu, kuna watu leo baada ya kuisilikiliza hii Hard Talk, boxer zao zimejaa unyevunyevu.
 
Tundu Lissu anza kuwavulia nguo hao mabwana zako huko huko wakuhemee kisogoni. Kama unaweza kukubali kuhalalisha ushoga ili upate support ya kugombea urais na kwa akili yako ukasahau kama si mila na desturi za hao unaodhani wanaweza kukupigia kura basi ujue wewe si kiongozi. Kiongozi ni yule anaekumbatia matakwa ya watu wake walio wengi no matter what. Binafsi nimechukia mno na hii interview yako na hawa mabwana zako. Tunafahamu siasa za kimataifa na tunafahamu nini kinatafutwa na hao wazungu. Hatutakupa kura ndugu yangu. Hufai hata ubalozi wa nyumba kumi kumi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi uliyaelewa vizuri yale majibu ya Tundu juu ya homosexuality?au ulikuwa unasikiliza ilhali upo tayari kumhukumu?
 
Magonjwa mtambuka kasafiri sijamsikia tangu asubuhi kanenda kwa mkadala Lufufu ngoja akirudi sasa mtamkoma
 
Hata ufanye kitu gani kizuri wapo watakaofurahi na kukusifu lakini kumbuka kwenye msafara wa mamba na kenge wapo .
 
Hapa ninahasira sana
Lissu na wapambe wako nakuuliza ni faida gani umeipata kuichafua Tanzania hii na kumchafua Rais Magufuli?
Kweli umeshindwa kuelezea hata jema moja alilofanya huyu Rais?kweli tunamponda magufuli lakini sio huko mnakoenda huo sii utamaduni wetu watanzania.
Kupiga watu risasi sio utamaduni wetu.
 
Jamaa karuka ruka interview nzima
Then kasema upinzani ikichukua serikali wataruhusu ushoga.😵
 
..nadhani wengi humu wamezoea kuangalia interviews zinazoongozwa na waandishi wa habari wa Tz.

..waandishi wa habari ya nje ni lazima wakutingishe-tingishe ili kuona kama hicho unachowaambia ni kitu unachokiamini kwa dhati kabisa-kabisa.

..yule mtangazaji alijaribu kumbabaisha TL ili amuone kama yuko madhubuti. Na kilichokiona ni kwamba TL hakutetereka. Zaidi hakupandwa na jazba.

..Nakumbuka Raisi Mkapa alikwenda kwenye Hardtalk na alipandwa na jazba kwelikweli.

..Jiwe aliulizwa swali moja akiwa Uganda ikabidi Mzee Museveni amsaidie kuli-simplify na kumtafsiria swali.

..Kwa maoni yangu TL amethibitisha kwamba anaweza ku-handle vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi.
Asante kwa kunikumbusha kitu[emoji122]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa ninahasira sana
Lissu na wapambe wako nakuuliza ni faida gani umeipata kuichafua Tanzania hii na kumchafua Rais Magufuli?
Kweli umeshindwa kuelezea hata jema moja alilofanya huyu Rais?kweli tunamponda magufuli lakini sio huko mnakoenda huo sii utamaduni wetu watanzania.
Unge kuwa wewe uliye miminiwa risasi sijui kama ungesubutu kuandika haya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom