Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Huyo hajali na hana uchungu na nchi, once a traitor always a traitor.
Sasa anataka kuwa raisi kwenye nchi anayoipaka matope?!
Ataongozaje sasa si itakuwa koloni tena hivihivi tena kwa bei rahisi kabisa ya juisi na biskuti tu
Wewe hapa unaongea hivi hata mate hujatemewa, vipi kama ungenyeshewa risasi sijui ungeandikaje?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..nadhani wengi humu wamezoea kuangalia interviews zinazoongozwa na waandishi wa habari wa Tz.

..waandishi wa habari ya nje ni lazima wakutingishe-tingishe ili kuona kama hicho unachowaambia ni kitu unachokiamini kwa dhati kabisa-kabisa.

..yule mtangazaji alijaribu kumbabaisha TL ili amuone kama yuko madhubuti. Na kilichokiona ni kwamba TL hakutetereka. Zaidi hakupandwa na jazba.

..Nakumbuka Raisi Mkapa alikwenda kwenye Hardtalk na alipandwa na jazba kwelikweli.

..Jiwe aliulizwa swali moja akiwa Uganda ikabidi Mzee Museveni amsaidie kuli-simplify na kumtafsiria swali.

..Kwa maoni yangu TL amethibitisha kwamba anaweza ku-handle vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi.
Nakubaliana nawe asilimia mia moja... Mwandishi alikuwa anajaribu kumweka Lissu kwenye kona mbaya lakini alishindwa

Jr[emoji769]
 
Key words ya majibu ya Lissu ni haya;
’If they violate and I think they violate the right to privacy''
Kwa maana nyingine Tundu Lissu anasema sheria ya kuzuia ushoga inavunja haki za faragha.

..sasa hizo si sheria zilizopitishwa na bunge la ccm?

..kuchungulia watu wakiwa vyumbani ni kuingilia faragha zao.

..msimamo wa TL ni sawa na wa Dr.Mahiga. Na ndiyo maana ktk jibu lake amemtaja kwa jina.
 
Tundu Lisu miasira kibao utafikiri anataka kupigana, hayuko composed, hafikirii kabla ya kujibu yeye miasira tu na atashindwa vibaya kwa maana ameonyesha chuki dhidi ya Raisi wetu na hakuwa objective, Tundu Lisu ana low IQ na miasira kama female!
TL was very composed..
Mkuu, Ulitaka amuongelee vizuri mtu alietaka kumuuwa??hahahahahaha.

Zaidi ya hapo hawa Waandishi wa Habari Wazungu wanapouliza maswali lazima wakutingishe sana ili wapate your innerself but TL was very composed..huwezi compare Hard Talk aliyofanyiwa Mkapa na PK..walitaka kurusha ngumi studio.
 
Tundu Lissu ameyasema hayo wakati akihojiwa na mwandishi wa habari wa shirika la utangazaji la Uingereza (BBC), Stephen John Sackur.

Pamoja na kuulizwa maswali mengi yanayohusu siasa za Tanzania na Rais Magufuli. Mengi ya majibu ambayo ameyasema sio mapya kwa sababu amekuwa akiyasema tokea utawala wa awamu ya tano ulipoingia madarakani.

Swali ambalo lilikuwa ni jipya lakini pia hajawahi kuliongolea sana ilikuwa ni pale alipoulizwa kama akiwa Rais wa Tanzania ataweza kufuta sheria inayozuia ushoga nchini ambayo adhabu yake ni miaka 30.

Tundu Lissu alijaribu kuliepuka swali hilo lakini baada ya kubanwa sana na mtangazaji atoe jibu la ndio au hapana hatimaye Lissu alisema kama akiwa Rais wa Tanzania ataifuta sheria hiyo kwa sababu inakiuka haki za binadamu ambazo zinatambuliwa na Katiba ya Tanzania.

Tundu Lissu amedai Katiba ya Tanzania inatambua uhuru wa wananchi na haki ya faragha. Katika Ibara ya 16 inasema. ‘’Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi.

Tundu Lissu amedai kwa sababu Katiba inatambua haki ya faragha kwa sababu hiyo atafuta sheria inayopingana uhuru wa fargha ikiwa ni pamoja na sheria inayozuia Ushoga.

Mtangazaji Sackur alimuuliza, ''Many around the world they would like to know is a senior Africa opposition politician prepared in public to say this law we have currently in our country on homosexuality punishment up to 30 years are utterly unacceptable and if I achieve power we will get lid of those law''.

Tundu Lissu alijibu, ‘’If they violate and I think they violate the right to privacy that is protected by the constitution then those laws are definitely unconstitutional’’.

Kwa wale wenye MB chache wanaweza kuangalia kuanzia dakika ya 20:40

VIDEO:
Vipi ameulizwa swala la TZ kushtakiwa MIGA na acacia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mabeberu nimeamini sio watu wazuri. Naomba Lissu apewe zaidi interview
Nimesikiliza interview mbili kwa ndugu yetu na mabeberu, aisee the agony is real. Tundu lissu alijua akienda na nyuzi za Salary Slip BBC atakuwa amemaliza mchezo akajua kwa vile beberu Steve halijui kiswahili basi kumbe jamaa ana kila data.
Beberu lina polls zote ,sio data kutoka Tanzania tu mpaka kwa watafiti wa Oxford. Lissu aliishiwa nguvu pale jamaa alipomquote Lawrence Masha.
Upinzani rudini kwanza square one mmpange vizuri TL.,haya mabeberu yatawaachia harufu tu hamna cha maana
 
Hapa ninahasira sana
Lissu na wapambe wako nakuuliza ni faida gani umeipata kuichafua Tanzania hii na kumchafua Rais Magufuli?
Kweli umeshindwa kuelezea hata jema moja alilofanya huyu Rais?kweli tunamponda magufuli lakini sio huko mnakoenda huo sii utamaduni wetu watanzania.
Wakenya pamoja na tofauti zao hawawezi fanya huu ujinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nakubaliana nawe asilimia mia moja... Mwandishi alikuwa anajaribu kumweka Lissu kwenye kona mbaya lakini alishindwa

Jr[emoji769]

..Hardtalk hutakiwi kwenda kama akili zako "hazi-charge."

..Pili lazima uwe quick ktk ku-counterpunch.

..Style ya muongoza kipindi ni kumu-attack mgeni wake. Ndiyo maana ukaona alikuwa akimkatiza-katiza TL.

..ni jukumu la anayehojiwa kujibu mapigo na kuhakikisha ujumbe wake unawafikia wasikilizaji.

..Kwa maoni yangu, TL alisimama imara na hakupoteza muelekeo.
 
Tindu Lisu ni low IQ, mfundisheni kurelax na kufikiria kidogo swali aliloulizwa kabla ya kujibu.

Utafikiri ilikuwa ni ugomvi? Miasira kibao.

..hardtalk siyo sawa na interviews za Clouds.

..pale lazima uwe ngangari, vinginevyo muongoza kipindi anaweza kukutawala.

..nadhani wewe ulitegemea TL atakuwa intimidated kitu ambacho hakikutokea.
 
The truth is..Lissu is being grilled here, he thinks he has a point, but he is just moving around the bush with no evidence, he tries to reject everything with no critical evidence..thats where I like the interviewer..give concrete evidence not just words like a parrot..🤗🤗🤗
 
Steve 'Do you have evidence'?.
Lissu "the car,the car told me"
Steve "so your not happy with your country achievement"
Lissu 'Steve people are murdered,the ruling party is blah blah"
Steve "do you have evidence?
Lissu "i call people they tell me"🙉
🤣🤣🤣
mwingereza umetuachia majanga mfwate lawyer wako huku.
 
AKILI ZA MASKINI NI ZA MASKINI TUU!


Tajiri anaaamka asubuh saa 11 Anatafuta funguo za Range sport anaenda Collosium Gym kuondoa Cholesterol mwilini, ww apeche alele unaamka saa 11unatafuta charge ya ki tecno chako uicharge uanze kuleta udaku halaf unarud kulala unaamka tena Saa nne unatafuta yebo yebo unaenda kwa Mangi kununua Maandazi ya Azam uongeze Cholesterol level, Asalaaaale kweli maisha ni kuchagua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa ninahasira sana
Lissu na wapambe wako nakuuliza ni faida gani umeipata kuichafua Tanzania hii na kumchafua Rais Magufuli?
Kweli umeshindwa kuelezea hata jema moja alilofanya huyu Rais?kweli tunamponda magufuli lakini sio huko mnakoenda huo sii utamaduni wetu watanzania.

Sio utamaduni wa Tanzania ku attempt kuuana vile
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Tundu Lisu miasira kibao utafikiri anataka kupigana, hayuko composed, hafikirii kabla ya kujibu yeye miasira tu na atashindwa vibaya kwa maana ameonyesha chuki dhidi ya Raisi wetu na hakuwa objective, Tundu Lisu ana low IQ na miasira kama female!
Uzuri hata English hujui kwahiyo unaongea kama ulivyoelekezwa. Embu tafsiri kaongeaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo hajali na hana uchungu na nchi, once a traitor always a traitor.
Sasa anataka kuwa raisi kwenye nchi anayoipaka matope?!
Ataongozaje sasa si itakuwa koloni tena hivihivi tena kwa bei rahisi kabisa ya juisi na biskuti tu
We una uchungu?
Amepigwa risasi mmechukua hatua zozote?
 
..inaelekea umezoea interviews za Clouds.

..kwa wenye uzoefu wa kuangalia Hardtalk wanajua TL handled himself well.

..kitendo tu cha kukubali kuhojiwa hardtalk kinadhihirisha kwamba TL anajiamini.

..sikuona kama interview ile ilikuwa mtihani mkubwa sana kwa TL.
 
Back
Top Bottom