Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

  • Thread starter Return Of Undertaker
  • Start date
Return Of Undertaker

Return Of Undertaker

JF-Expert Member
Jun 12, 2012
4,347
2,000
IMG-20190120-WA0019.jpg
Tundu Lissu MP
HARDtalk

HARDtalk's Stephen Sackur speaks to Tanzanian opposition MP, Tundu Lissu.

Tanzania is one of Africa's fastest growing nations economically and demographically - it's also governed by one of the continent's most controversial leaders: president John Magafuli, otherwise known as the 'Bulldozer'.

Tundu Lissu is one of his leading domestic opponents, at least he was, until gunmen pumped more than 20 bullets into his body in 2017.

Lissu survived and has rejoined the fight against a ruler he describes as a petty dictator. But maybe Tanzanians like strong man rule?

The Tanzanian opposition politician, Tundu Lissu says he is "more than ready" to run for the presidency of Tanzania in 2020 if his party wants him to.

Mr Lissu, who is chief whip for the Tanzanian opposition party Chadema, is currently living in Belgium where he has been undergoing medical treatment after an assassination attempt in Tanzania in 2017. He has undergone 20 operations.

He told Hardtalk's Stephen Sackur he would return to Tanzania when the doctors declared him "fit to go". When he returned, the government would have a responsibility to ensure he was safe.

Mr Lissu also said he believed Tanzania's laws against homosexuality violated people's right to privacy and so were unconstitutional.

"We should never allow the government to start peeping into people's bedrooms," he said.

----------------------
Naomba niyaweka hapa kwa Kiswahili ili twende sawa.

STEPH: Tundu Lissu karibu HARDtalk.

LISSU: Asante sana Stephen kwa kunialika.

STEPH: Tuna furaha kuwa nawe hapa. Siyo kidogo, kwa sababu miezi 16 iliyopita, ilivyoonekana pengine ungekufa. Kimiujiza kiasi fulani, ulinusurika jaribio la kukuua ambalo lilishuhudiwa risasi 20 zikiingia mwilini mwako. Unajisikiaje leo?

LISSU: Nipo vizuri sana, vizuri sana ukilinganisha na nilivyokuwa miezi 14 iliyopita. Kama ulivyosema nilipigwa risasi nyingi. Kwa usahihi nilipigwa risasi 16.

STEPH: Baadhi ya risasi zilipiga gari badala ya kukupiga wewe, maana zilisambaa eneo la tukio?

LISSU: Zilizonipiga mimi ni 16. Zile zilizosambaa kwenye gari naambiwa ni 38. Hivyo, mapigo 16 ya risasi, na upasuaji mara 20 baadaye, na leo nipo hapa kama nilivyo.

STEPH: Unaonekana unaamini kulikuwa na dhamira ya kisiasa kwenye shambulio ulilofanyiwa.
LISSU: Ndiyo, hakika.

STEPH: Una uthitibitisho gani?

LISSU: Uthibitisho ni mazingira yaliyoongozana na lile shambulio. Kwa kama wiki sita kabla sijashambuliwa kwa risasi, kulikuwa na watu waliokuwa wananifuatilia, wanafuatilia gari langu kila sehemu niliyokwenda. Kila sehemu niliyokwenda kulikuwa na gari nyuma lililonifuatilia. Kisha nilifanya... (Alikatishwa na Steph)

STEPH: Kuna kitu tukiweke sawa ikiwa kuna watu hawakujui. Wewe ni mtu mashuhuri Tanzania, siyo tu kwa sababu ni mwanachama mwandamizi wa chama cha upinzani, wewe ni mnadhimu wa kambi ya upinzani bungeni, lakini pia ulikuwa kiongozi mkuu wa chama cha wanasheria.

LISSU: Ni chama cha wanasheria Taifa.

STEPH: Safi kabisa, hivyo, labda kulikuwa na watu wengi wabaya, wangeweza kuwa na nia mbaya dhidi yako, kwa hiyo huwezi kuwa na uhakika ni nani.

LISSU: Ambao wanapaswa kuwa na uthibitisho kuwa kulikuwa na watu wenye nia mbaya juu yangu ni Serikali. Mwaka kabla ya shambulio dhidi yangu, Septemba 7, 2017, nilikamatwa mara nane, nilishitakiwa mahamani kwa makosa mbalimbali kama uchochezi, uhuru wa kujieleza na mengineyo, mara sita.

Kulikuwa na wito wa wazi kutoka kwa watu tunaowajua ni wanachama wa chama tawala waliotangaza waziwazi niuawe, baada ya mimi kumkosoa Rais, nilipofichua siri ya moja ya miradi yake pendwa, ununuzi wa ndege mpya ya Air Tanzania, iliyozuiwa Canada kwa sababu ya uvunjaji mkataba kinyume na sheria alipokuwa waziri wa ujenzi.

STEPH: Ulitoa tuhuma nzito kuhusu rushwa na Rais alizikataa na kuzitupilia mbali zote, ni sawa na ukweli kuwa katika kipindi cha miezi 14 au 15 tangu shambulio lako, Serikali na Mamlaka za Tanzania zimesema hakuna ushahidi unaoihusisha taasisi yoyote na Serikali juu ya shambulio hili. Unatoa tuhuma na malalamiko ambayo kwa kiasi kikubwa yanajenga uchochezi kwa Tanzania ya leo, na huna ushahidi.

LISSU: Sikiliza Steph, mimi ni mnadhimu mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni, mimi ni kiongozi ndani ya bunge. Naishi kwenye nyumba za Serikali ambazo hulindwa saa 24 kwa wiki. Kila jengo hulindwa saa 24 kwa wiki.

Na siku ya shambulizi, jua likiwa linawaka, ilikuwa saa 7:00 mchana, wakati wa mapumziko ya chakula cha mchana katika vikao vya Bunge, watu wenye bunduki walinifuatilia kutoka bungeni mpaka ndani ya nyumba za Serikali ambazo huwa na ulinzi mkali, ambako mawaziri, wabunge, naibu spika na wengine wanaishi humo. Na siku hiyo hakukuwa na ulinzi kabisa. Hakukuwa na walinzi getini na sehemu zote. CCT... (anakatishwa)

STEPH: Naelewa, ila nakumbushwa na tamko la kisheria, Rais alisema baada ya shambulio, kwanza alilaani vikali na kuagiza vyombo vya dola kuwakamata wahusika na kuwachukulia hatua kali.

LISSU: Rais hajawahi kabisa kuzungumza na umma kuhusu hili jaribio la kaniua, kamwe hajawahi. Aliandika kidogo Twitter. Ujumbe wa haraka sana Twitter, baada ya hapo alinyamaza. Kamwe, Rais hajawahi kuzungumza na umma. Hili linatoka kwa Spika, kwamba Rais ndiye alizuia nisitibiwe kwa gharama za Bunge, wakati ni haki yangu kisheria.

STEPH: Kufanya watu wawe na taarifa ya kilichotokea tangu uliposhambuliwa, ulitibiwa Kenya, ukapata matibabu makubwa zaidi Ubelgiji, kwa hiyo umekuwepo Ubelgiji kwa muda mrefu.

Ulifikiriaje kuna maneno uliyasema wakati wa majira ya joto mwaka 2017 kabla ya jaribio la kukuua. Ulimwita Rais dikteta na ukataka jumuiya za kimataifa ziichukulie Tanzania kuwa ni najisi ya ulimwengu, kwa nini ulifika huko?

LISSU: Serikali ambazo zinaua raia wake. Serikali zinazotumia vyombo vya usalama kuwinda washindani wake wa kisiasa. Serikali zinazopiga marufuku haki za kisiasa ambazo zinalindwa na Katiba. Serikali zinazosababisha raia watekwe na kupotea kama hali ilivyokuwa mbaya sana kwa madikteta wa Latini Amerika miaka ya 1960 na 1970. Serikali ambazo zimeshuhudia uhai wa watu ukipotea, maisha ya watu wasio na hatia yakiharibiwa, hizo Serikali zinastahili kutambuliwa kuwa ni najisi ya ulimwengu.

STEPH: Kwa namna gani unavunjika moyo, Watanzania wanakusikiliza wewe, wanamsikiliza Rais, wanapokea ujumbe tofauti, lakini sasa hivi Rais anainjoi asilimia za kukubalika, kuna ambazo anazidi asilimia 50 na nyingine asilimia 70. Na kuna kila dalili kuwa Rais na chama tawala watapa ushindi mkubwa kwenye uchaguzi ujao.

LISSU: Mr Sackur nitasema hivi; mwaka wa kwanza wa uongozi wa Rais Magufuli, tuliambiwa kuwa kukubalika kwake kulikuwa zaidi ya asilimia 80. Mwaka mmoja baadaye, mapema mwaka jana, moja kati ya hizo taasisi za kukusanya maoni, ilitoa ripoti kuwa kiwango cha kukubalika Rais Magufuli kimeshuka mpaka asilimia 61.

Unajua nini kilitokea? Mkurugenzi mtendaji wa hiyo taasisi ya ukusanyaji maoni alihojiwa uraia wake, alinyang'anywa hati yake ya kusafiria. Kwa hicho kilichotokea, maana yake hawawezi kurudia. Na baada ya hapo sheria mpya ya takwimu ilipitishwa, ambayo inasema ukitoa takwimu zenye kuipa sura mbaya Serikali ni uhalifu.

STEPH: Kabla hatujafika huko. Ikiwa Rais anaonekana na watu wake anafanya kazi nzuri. Zingatia baadhi ya mafanikio. Aliahidi angedhibiti rushwa, wiki chache za uongozi wake tulishuhudia maelfu ya wafanyakazi hewa wakiondolewa kwenye mfumo wa malipo. Vigogo wa Mamlaka ya Bandari na Mamla ya Mapato waliondolewa kwa sababu za rushwa. Ukiwauliza Watanzania leo, na kutokana na ushahidi uliopo, wanaona nchi sasa ni safi ukilinganisha na alipoingia ofisini, wanaona rushwa imepungua, na kwa Afrika hayo ni mafanikio.

LISSU: Tumeona pia Rais akijenga uwanja mpya wa ndege kijijini nyumbani kwao, kama alivyofanya Mobutu Sese Seko, kijijini kwao kwenye msitu mmoja Kongo. Tumeona Rais akinunua ndege kwa ajili ya Shirika la Ndege Tanzania, hii siyo kazi ya Rais.

STEPH: Wewe unataja kitu kimojakimoja, mimi nazungumzia mifumo. Kwa mfano, mapato ya kodi yameongezeka tofauti na ilivyokuwa Magufuli hajashika uongozi. Hii maana yake anatimiza ahadi ya kuwafanya Watanzania walipe kodi, ili kuwafanya wawe jamii yenye ufanisi na ya uwajibikaji.

LISSU: Hiyo ni kinyume. Kulikuwa na kuongezeka kwa mapato mwanzoni, mwaka 2016 na 2017, lakini kuanzia hapo mapato ya kodi yalishuka, kwa nini? Kwa sababu Rais ameishambulia jumuiya ya wafanyabiashara, amewashambulia wawekezaji katika sekta binafsi, uwekezaji unakufa.

STEPH: Umesema anawashambulia wawekezaji, anachokifanya ni kitimiza ahadi aliyotoa kuwa atayabana mashirika ya nje, yakiwemo makampuni makubwa ya uchimbaji madini ambayo yamekuwa yakitengeneza faida kubwa kwa miaka mingi kwenye rasilimali za Tanzania, hicho ndicho anafanya, na Watanzania kulingana na ripoti za utafiti, wanapenda anachofanya.

LISSU: Utafiti uliofanywa na nani tunaouzungumzia hapa? Ikiwa Rais na Serikali yake wamepitisha sheria inayopiga marufuku taasisi binafsi kuwa na takwimu zenye kukinzana na Serikali, nani mwingine atatokeza aseme hizo namba ni sahihi?

STEPH: Tuache ukusanyaji wa maoni, tuje kwenye uchambuzi. Kuna mchambuzi anayeheshimika sana Tanzania, anaitwa Dan Paget, aliwahi kuandika: Magufuli ameishinda dhana kuwa nchi za Afrika haziwezi kupambana na mashirika makubwa ya kimataifa na kushinda. Alipambana na makampuni ya madini, hatimaye Barrick Gold wakakubali dili lenye umuhimu mkubwa kwa Tanzania. Kwa vile wewe ni mpinzani ndio hujapenda hilo.

LISSU: Barrick hawajakubali dili lolote. Tuliambiwa na Rais mwenyewe kuwa Barrick walikubali kulipa Dola 300 Milioni, sijui tutaiitaje labda ya uhusiano mwema, mimi sijui. Rais alisema waliahidi wangelipa haraka dola 300 Milioni lakini hawajalipa hata mia. Walipewa bili ya kodi dola 194 bilioni, hawajalipa hata mia.

STEPH: Unaonekana hutaki Serikali ipambane na mashirika ya kimataifa. Umekuwa ukilalamika kuwa "ooh tunatakiwa kuwa watu wazuri kwao".

LISSU: Sijawaji kusema hivyo kabisa. Nimetumia miaka 19, kuanzia mwaka 1999, wakati huo kila mtu, Magufuli akiwa miongoni mwao, wakiimba nyimbo za kuwatukuza hawa wawekezaji wa sekta ya madini walipokuwa wakituibia. Miaka 19 ya sauti yangu pekee, kinyume chake.. (Alikatishwa)

STEPH: Kama ipo hivyo kuwa Magufuli na utawala wake, wanawaporomosha Watanzania. Mwaka jana, namba muhimu, inategemea na unavyosoma, wabunge 10 kitu kama hicho, wengine wakiwa vigogo wa upinzani dhidi ya Magufuli, walihama na sasa wapo upande wake.

LISSU: kulikuwa na biashara kubwa katika siasa za Tanzania ndani mwaka mmoja uliopota.

STEPH: Unamaanisha nini?

LISSU: Namaanisha kuwa watu walipewa pesa ili kuhama vyama. Watu waliahidiwa kuwa wakihama wangerudishwa kugombea tena nafasi zao zilezile na kuhakikishiwa kushinda kwa kutumia nguvu yoyote ile, na hicho ndicho kilichotokea.

STEPH: Wewe ni mwanasheria mkubwa na unajua kuliko mimi, kwamba ni hatari sana kujifunga na hizi tuhuma nzito bila kuwa na ushahidi. Watu unaowatuhumu wengine ni wanasiasa wakubwa na hawapo hapa kujitetea na bila shaka watakanusha hizo tuhuma.

LISSU: Aaa, unaweza kuwasiliana nao.

STEPH: Mfano Laurence Masha, alikuwa Waziri wa Mambo ya Ndani wakati wa utawala wa Kikwete, kisha akawa mpinzani wa Magufuli, lakini hivi karibuni aliamua kwamba anachokiona kwa Magufuli ni chanya kwa maisha ya Watanzania.

LISSU: Mr Sackur, ndani ya miaka mitatu tangu Rais Magufuli alipoingia madarakani, wananchi 380, wanakijiji, wilayani Kibiti, Rufiji, Mkuranga, Kilwa, wamepotea. Maiti zilionekana Mto Rufiji, kwenye fukwe za Bahari ya Hindi, hii ni mpya katika historia ya Tanzania. Wapinzani wa kisiasa kwa Serikali na chama chake wanauawa mchana kweupe. Hii ndiyo gharama tunayotakiwa kulipa ili kudhibiti rushwa?

STEPH: Hii ndiyo Tanzania unayoitaka? Lugha inayotumika, madai yanayotolewa yanakuwa ya uchonganishi. Serikali inahofia hili, inaamua kuchukua hatua ambazo wengine watasema zinakandamiza uhuru wa kutoa maoni. Serikalini wanaona uhuru wa kutoa maoni unatumiwa vibaya, watu wanatoa tuhuma za uongo, wanatengeneza habari, ndiyo maana inadhibiti mitandao ya kijamii, bloggers, pia mara kwa mara wanafungia magazeti, redio. Hoja zako za kisiasa ni kwa ajili ya kuchochea moto au kupoza jazba?

LISSU: Stephen, nilichosema kuhusu mauaji eneo la Rufiji. Nilichosema kuhusu kupotea kwa wapinzani wa kisiasa. Nilichosema kuhusu ukandamizaji wa vyombo vya habari. Nilichosema kuhusu bloggers, au watu wanaotuma ujumbe kwenye makundi ya WhatsApp. Ndiyo yamekuwa yakisemwa na makanisa, na vyombo vya habari, yamekuwa yakizungumzwa bungeni, yamekuwa yakisemwa na jumuiya ya kimataifa, yamerejewa na Umoja wa Ulaya katika maazimio yao ya hivi karibuni. Ninayoyasema hapa hakuna kipya kwa wale wanaojua kinachoendelea Tanzania kwa miaka mitatu iliyopita.

STEPH: Kuna hili la mabadiliko ya sheria ili kuvibana vyama vya siasa kutofanya hiki ambacho kimekuwa kikiitwa harakati mitaani. Je, mtapokea matokeo, au mtaikabili Serikali waziwazi na sheria yao kandamizi katika njia ambayo inaweza kuzua machafuko, au mtatafuta njia ya amani ya kuikabili Serikali bila mapigano yoyote?

LISSU: Siku zote tumekuwa tukipambana kisiasa kwa amani. Hatujawahi kutumia machafuko kama silaha yetu ya kisiasa.

STEPH: Ngoja tuongelee hasa sababu ya jumuiya ya kimataifa katika miezi michache iliyopita kutoa taarifa nzito kuhusu kinachoendelea Tanzania na kile ambacho utawala wa Magufuli unafanya.

Benki ya Dunka imeghairi kuikopesha Tanzania dola 300 milioni, baada ya Serikali ya Tanzania kuzuia watoto wa kike wanaopata ujauzito kuendelea na masomo. Balozi wa Umoja wa Ulaya alieleza kuhusu dhamira ya Serikali kuwakamata watu wa mapenzi ya jinsia moja na kuwafunga jela miaka 30 jela.

LISSU: Hiyo imekuwa ni sheria kwa muda sasa.

STEPH: Nafahamu, ila kuna hatua mpya za Serikali kuwasaka na kuwaadhibu watu wa mapenzi ya jinsi moja. Sasa swali langu ni hili, wewe kama mwanasiasa wa upinzani mwenye nguvu, umejiandaa kutokeza hadharani kuzipinga hizia hatua kandamizi kijamii zinazofanywa na Serikali?

LISSU: Tupo kwenye kumbukumbu, watoto wa kike wajawazito kuendelea na masomo ni Sera ya Serikali. Ipo ndani ya ilani ya chama chao. Ipo kwenye sheria zetu. Hivyo kitendo cha Rais kusema Serikali haitasomesha wanafunzi wa kike kwa sababu ya ujauzito, siyo kwamba ni kwenda kinyume na sheria, bali pia sera iliyowekwa na chama chake.

STEPH: Hilo umeeleweka, vipi hizi sheria kandamizi dhidi ya watu wa mapenzi ya jinsia moja, wewe kama kiongozi mkubwa wa upinzani unaweza kupitia hapa HARDtalk kuzungumza na kuzipinga hizo sheria?

LISSU: Rais Marufuli alisema hivi... (akakatishwa)

STEPH: Sijauliza hilo hapa, tunafahamu yeye ni mhafidhina hasa kijamii (hakubaliani kabisa na ushoga).

LISSU: Tuweke rekodi sawa Steph. Waziri wa Mambo ya Nje, Dk Mahiga alisema, hatua zilizochukuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, siyo sera ya Serikali.

STEPH: Nataka kujua, watu ulimwenguni wanataka kujua, huyu mwanasiasa mwandamizi wa upinzani kutoka Afrika, amejiandaa hadharani kusema kuwa hizi sheria tulizonazo kwenye nchi yetu dhidi ya ushoga, kifungo jela miaka 30, haikubaliki, na nikishika mamlaka tutaziondoa hizo sheria.

LISSU: Kila mtu ana haki ya faragha. Hatutaruhusu Serikali kuanza kuchungulia vyumba vya watu.

STEPH: Hivyo, utazifuta hizi sheria zinazosema ushoga ni uhalifu?

LISSU: Kama zinaingilia na nafikiri zinaingilia haki ya faragha inayolindwa na Katiba, moja kwa moja hizo sheria hazikubaliki kikatiba. Kwa Katiba ya Tanzania, siongelei Katiba ya sehemu nyingine yoyote. Katiba yetu inasema haya ni mambo ya faragha na yanapaswa kubaki kuwa mambo ya faragha.

STEPH: Katika maeneo mengi umesema Rais anaipeleka nchi mahali pabaya. Umeshapata matibabu, je, sasa hivi upo tayari kurejea Tanzania, kumkabili huyu Rais kisiasa. Jina lako liwepo kwenye karatasi ya kupigia kura katika uchaguzi wa rais?

LISSU: Matibabu yangu bado yanaendelea. Lakini nilishasema wazi kuwa siku madaktari watatamka kuwa nimepona na naweza kwenda, nitakwenda Tanzania, hilo ni moja. Sipo uhamishoni. Nipo Ubelgiji kwa sababu nilipigwa risasi 16.

STEPH: Unajiandaa kurejea Tanzania bila ulinzi wa uhakika na bila kuhakikishiwa usalama?

LISSU: Nitarudi Tanzania nikishapona kabisa. Rais na Serikali yake, wanatakiwa kuuambia ulimwengu kama kurejea kwangu Tanzania, nitalindwa na Serikali kama ninavyostahili. Serikali inao wajibu wa kuhakikisha nipo salama. Mimi bado ni mbunge. Nitarejea kufanya kazi ambayo nilichaguliwa kuifanya. Kuhusu kugombea, nimesema, ikiwa Watanzania, wanachama wa chama changu, wataamini kuwa mimi ni mtu sahihi kumkabili Rais Magufuli mwaka 2020, nipo tayari mno kufanya hivyo.

STEPH: Tundu Lissu, tutaendelea kuwa pamoja. Asante sana.

LISSU: Asante sana Steph.
---

Credits: Luqman Maloto.
 
sheremaya

sheremaya

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
2,873
2,000
Atasema nini tena! Tutamskia
 
B

Benmpo

JF-Expert Member
Mar 23, 2015
416
500
Kumeibuka mjadala mkubwa katika mitandao kijamii kufatia kile kilichodaiwa kuwa ni kauli ya Mh. Spika Ndugai, iliyomtaka arejee nchini na kuendelea na shughuli zake za kibunge vinginevyo sheria itachukua mkondo wake dhidi yake.

Hivi karibuni TAL akihojiwa na moja ya vyombo vya habari huko Uingereza, alisema kwamba kwa sasa amepona na atarudi nchini muda wowote; pia alitumia wasaa huo kuwaweka wazi Watanzania na jumuiya ya kimataifa kuwa yupo tayari kugombea nafasi ya juu kabisa ya uongozi katika nchi yetu hapo mwaka 2020 kama chama chake kitaridhia apeperushe bendera yake.

Kinachoshangaza ni kuwa wapambe wake wamekuwa na wasiwasi juu ya usalama wa Lissu kuliko Lissu mwenyewe. Wakati yeye akisema yuko tayari kurejea nchini wakati wowote, wao wanasema asirejee hata kama atapoteza nafasi ya Ubunge huku wakidai kuwa wanahofia usalama wake na wengine wamesema aombe “Political Asylum” katika moja ya nchi hizo, sijui kwa vigezo vipi. Viongozi wa juu wa CHADEMA bado wapo kimya kabisa katika hili. Kuna siri nzito ambayo Lissu na dereva wake wanajua.

Nilichojifunza hapo ni kuwa wapambe wake wanakubali wazi kuwa TAL anavunja sheria kwa kutojishughulisha na masuala ya Kibunge bila kibali cha Spika wakati akiwa na afya njema kabisa, na badala yake anafanya ziara nje ya nchi zenye malengo hasi kwa nchi yetu. Hivyo wapambe wake hawatashangazwa iwapo Spika ataamua kutomtambua Lissu kama Mbunge, lakini tutarajie malalamiko yao kama kawaida ya kulalamikia kile wasichokiamani.

Lissu bado anaamini kuwa Tanzania ni nchi ya amani tofauti na wapambe wake wanavyoamini na ndiyo maana ameweka wazi mipango yake kisiasa. Tujiulize maswali haya, iwapo ataomba hifadhi nje kama wapambe wake wanavyotaka, “Plan Yake” ya kuwa Rais itakuwaje? Je, atafanya kampeni na kuchaguliwa kutoka huko huko aliko?

Katika hili, Lissu na wapambe wako hamko pamoja kabisa.
 
Mushi92

Mushi92

JF-Expert Member
Oct 5, 2013
3,917
2,000
wewe unaongea tu kwenye mitandao...huna athari yoyote wala hujui pain za Lissu......ikiambiwa uandamane hapo ulipo....hata comments zako hazitaonekana kwa uwoga wako....huku unajifanya jasiri
Kama mmepanga kumuua mkashindwa.....amepona anakula bat a kidg tayr figisu zshaanza.
Thrust me bro akifika anafikia mahabusu na kesi kibao we utaona

Sent using Jamii Forums mobile app
 
R

Retired

JF-Expert Member
Jul 22, 2016
22,719
2,000
Kumeibuka mjadala mkubwa katika mitandao kijamii kufatia kile kilichodaiwa kuwa ni kauli ya Mh. Spika Ndugai, iliyomtaka arejee nchini na kuendelea na shughuli zake za kibunge vinginevyo sheria itachukua mkondo wake dhidi yake.

Hivi karibuni TAL akihojiwa na moja ya vyombo vya habari huko Uingereza, alisema kwamba kwa sasa amepona na atarudi nchini muda wowote; pia alitumia wasaa huo kuwaweka wazi Watanzania na jumuiya ya kimataifa kuwa yupo tayari kugombea nafasi ya juu kabisa ya uongozi katika nchi yetu hapo mwaka 2020 kama chama chake kitaridhia apeperushe bendera yake.

Kinachoshangaza ni kuwa wapambe wake wamekuwa na wasiwasi juu ya usalama wa Lissu kuliko Lissu mwenyewe. Wakati yeye akisema yuko tayari kurejea nchini wakati wowote, wao wanasema asirejee hata kama atapoteza nafasi ya Ubunge huku wakidai kuwa wanahofia usalama wake na wengine wamesema aombe “Political Asylum” katika moja ya nchi hizo, sijui kwa vigezo vipi. Viongozi wa juu wa CHADEMA bado wapo kimya kabisa katika hili. Kuna siri nzito ambayo Lissu na dereva wake wanajua.

Nilichojifunza hapo ni kuwa wapambe wake wanakubali wazi kuwa TAL anavunja sheria kwa kutojishughulisha na masuala ya Kibunge bila kibali cha Spika wakati akiwa na afya njema kabisa, na badala yake anafanya ziara nje ya nchi zenye malengo hasi kwa nchi yetu. Hivyo wapambe wake hawatashangazwa iwapo Spika ataamua kutomtambua Lissu kama Mbunge, lakini tutarajie malalamiko yao kama kawaida ya kulalamikia kile wasichokiamani.

Lissu bado anaamini kuwa Tanzania ni nchi ya amani tofauti na wapambe wake wanavyoamini na ndiyo maana ameweka wazi mipango yake kisiasa. Tujiulize maswali haya, iwapo ataomba hifadhi nje kama wapambe wake wanavyotaka, “Plan Yake” ya kuwa Rais itakuwaje? Je, atafanya kampeni na kuchaguliwa kutoka huko huko aliko?

Katika hili, Lissu na wapambe wako hamko pamoja kabisa.
Kwa sheria ipi?
 
Ngonidema

Ngonidema

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
2,577
2,000
Mtaweweseka sana nabado ilo ni pigo moja tu la bbc mmechanganyikiwa ivo, nawaambien laana ya Mungu juu ya Damu ya Lissu haitawaacha salama, labda nikukumbeshe urejee mahojiano ya rais wetu mtarajiwa Lissu,alisema doctor wake akimruhusu tu siku ya pili atakuwa dar esalaam
 
N

Nyanjomigire

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
5,650
2,000
true ...hawako pamoja Lissu na wapambe wake.....
Wewe unajua huyo uliyeweka Avatar yake aliishachizi, naona na wewe uko njiani. Shauri yako.
 
King Kong III

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
34,457
2,000
Kumeibuka mjadala mkubwa katika mitandao kijamii kufatia kile kilichodaiwa kuwa ni kauli ya Mh. Spika Ndugai, iliyomtaka arejee nchini na kuendelea na shughuli zake za kibunge vinginevyo sheria itachukua mkondo wake dhidi yake.

Hivi karibuni TAL akihojiwa na moja ya vyombo vya habari huko Uingereza, alisema kwamba kwa sasa amepona na atarudi nchini muda wowote; pia alitumia wasaa huo kuwaweka wazi Watanzania na jumuiya ya kimataifa kuwa yupo tayari kugombea nafasi ya juu kabisa ya uongozi katika nchi yetu hapo mwaka 2020 kama chama chake kitaridhia apeperushe bendera yake.

Kinachoshangaza ni kuwa wapambe wake wamekuwa na wasiwasi juu ya usalama wa Lissu kuliko Lissu mwenyewe. Wakati yeye akisema yuko tayari kurejea nchini wakati wowote, wao wanasema asirejee hata kama atapoteza nafasi ya Ubunge huku wakidai kuwa wanahofia usalama wake na wengine wamesema aombe “Political Asylum” katika moja ya nchi hizo, sijui kwa vigezo vipi. Viongozi wa juu wa CHADEMA bado wapo kimya kabisa katika hili. Kuna siri nzito ambayo Lissu na dereva wake wanajua.

Nilichojifunza hapo ni kuwa wapambe wake wanakubali wazi kuwa TAL anavunja sheria kwa kutojishughulisha na masuala ya Kibunge bila kibali cha Spika wakati akiwa na afya njema kabisa, na badala yake anafanya ziara nje ya nchi zenye malengo hasi kwa nchi yetu. Hivyo wapambe wake hawatashangazwa iwapo Spika ataamua kutomtambua Lissu kama Mbunge, lakini tutarajie malalamiko yao kama kawaida ya kulalamikia kile wasichokiamani.

Lissu bado anaamini kuwa Tanzania ni nchi ya amani tofauti na wapambe wake wanavyoamini na ndiyo maana ameweka wazi mipango yake kisiasa. Tujiulize maswali haya, iwapo ataomba hifadhi nje kama wapambe wake wanavyotaka, “Plan Yake” ya kuwa Rais itakuwaje? Je, atafanya kampeni na kuchaguliwa kutoka huko huko aliko?

Katika hili, Lissu na wapambe wako hamko pamoja kabisa.
Yeye kashasema hawatoweza full stop.
 
K

kantalambaz

JF-Expert Member
Dec 24, 2017
1,556
2,000
Mtaweweseka sana nabado ilo ni pigo moja tu la bbc mmechanganyikiwa ivo, nawaambien laana ya Mungu juu ya Damu ya Lissu haitawaacha salama, labda nikukumbeshe urejee mahojiano ya rais wetu mtarajiwa Lissu,alisema doctor wake akimruhusu tu siku ya pili atakuwa dar esalaam
Hana impact yeyote huko BBC no bora hata angelikua hapa. Hata azunguke dunia nzima bado hatakua na impact.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Q-liner

Q-liner

JF-Expert Member
Nov 4, 2017
287
500
Mzee pumua kwanza alafu utuambie concern yako ya kuanzisha huu uzi ni nin?Pengine wewe ni Afisa usalama uliyemtishia kumuua Zitto kabwe,au pengine na wewe ulihusika kumiminia risasi Lisu!!Au ni mmoja wa mashangingi mjin mnaotegemea maisha yenu yaendeshwe na CCM?usilishe maneno watu we kaa pemben tulia halafu utaona what next kuhusu Lisu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom