Tundu Antipas Lissu on BBC HARDtalk - 21 January 2019

Binafsi nimeangalia hard talk ya TL BBC news kidogo initoe machozi. Wengi walijua kama TL anainanga Tanzania ila hali imekuwa tofauti kiti kimekuwa kama kimesimikwa kwenye TANURU na kama bado ana mpango wa kwenda kwenye Tv za kimataifa nadhani arudi tu akaliombe radhi taifa.

Naamini wengi hawajaiona hard talk ila naaminia itawashangaza wengi. Siyo siri Magufuli ni story nyingine kimataifa.

Kwa assessment yangu binafsi kama TL hakuangukia pua basi atakua katengua kiuno, so sad. wanaobishi walete mrejesho wa maswali yote na majibu.
 
Hivi kufanya ziara ndio ushindi wa urais?

Je tundu kuhutubia au kuhojiwa BBC...ndio kuna TIJA gani kwa mpiga kura wa nchi hii.?

Je kuna kick gani ya kisiasa kwa chama chenu?

Hata KAMA wazungu watamtuma lissu sisi tunampiga kwa ndebe ya kura.
Nchi hii kamwe hatutaiachia kwa wajasiliamali wa siasa mangimeza kama huyu mtoro wa bunge.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona mnakasirika sana, kwani mnaumia?

Tulieni dawa iingie tu, hajuna namna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuletee maswali ya chumbani ya wazazi wako ,Halafu tujadili hayo ya Uingereza

Ya chumbani kwa wazazi wako yamekushinda utayaweza ya wazungu

Amedondokea pua, Hivi wewe uliwahi saidia shika mguu wakati Mzee akiendelea na kazi
mkuu sikiliza ndo uje na mrejesho.
 
Hapa ninahasira sana
Lissu na wapambe wako nakuuliza ni faida gani umeipata kuichafua Tanzania hii na kumchafua Rais Magufuli?
Kweli umeshindwa kuelezea hata jema moja alilofanya huyu Rais?kweli tunamponda magufuli lakini sio huko mnakoenda huo sii utamaduni wetu watanzania.
 
Hapa ninahasira sana
Lissu na wapambe wako nakuuliza ni faida gani umeipata kuichafua Tanzania hii na kumchafua Rais Magufuli?
Kweli umeshindwa kuelezea hata jema moja alilofanya huyu Rais?kweli tunamponda magufuli lakini sio huko mnakoenda huo sii utamaduni wetu watanzania.
Hivi ile convoy iliyotaka kummaliza kwa kummiminia mvua ya risasi ilishawahi kuchukuliwa hatua zozote?

Jr
 
Tundu Lissu ameyasema hayo wakati akihojiwa na mwandishi wa habari wa shirika la utangazaji la Uingereza (BBC), Stephen John Sackur.

Pamoja na kuulizwa maswali mengi yanayohusu siasa za Tanzania na Rais Magufuli. Mengi ya majibu ambayo ameyasema sio mapya kwa sababu amekuwa akiyasema tokea utawala wa awamu ya tano ulipoingia madarakani.

Swali ambalo lilikuwa ni jipya lakini pia hajawahi kuliongolea sana ilikuwa ni pale alipoulizwa kama akiwa Rais wa Tanzania ataweza kufuta sheria inayozuia ushoga nchini ambayo adhabu yake ni miaka 30.

Tundu Lissu alijaribu kuliepuka swali hilo lakini baada ya kubanwa sana na mtangazaji atoe jibu la ndio au hapana hatimaye Lissu alisema kama akiwa Rais wa Tanzania ataifuta sheria hiyo kwa sababu inakiuka haki za binadamu ambazo zinatambuliwa na Katiba ya Tanzania.

Tundu Lissu amedai Katiba ya Tanzania inatambua uhuru wa wananchi na haki ya faragha. Katika Ibara ya 16 inasema. ‘’Kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi kwa nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na unyumba wake, na pia heshima na hifadhi ya maskani yake na mawasiliano yake ya binafsi.

Tundu Lissu amedai kwa sababu Katiba inatambua haki ya faragha kwa sababu hiyo atafuta sheria inayopingana uhuru wa fargha ikiwa ni pamoja na sheria inayozuia Ushoga.

Mtangazaji Sackur alimuuliza, ''Many around the world they would like to know is a senior Africa opposition politician prepared in public to say this law we have currently in our country on homosexuality punishment up to 30 years are utterly unacceptable and if I achieve power we will get lid of those law''.

Tundu Lissu alijibu, ‘’If they violate and I think they violate the right to privacy that is protected by the constitution then those laws are definitely unconstitutional’’.

Kwa wale wenye MB chache wanaweza kuangalia kuanzia dakika ya 20:40

VIDEO:
 
Back
Top Bottom