Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) iwafutie usajili wanafunzi wanaorekodi na kusambaza video chafu mitandaoni

Wakuu Salaam:

Siku za karibuni kumekuwa na usambaaji wa video chafu kwenye mitandao ya kijamii na jambo hili linaendelea kukua miongoni mwa wanafunzi wa Elimu ya juu.

Na waliohusika katika video wapo pamoja na kwamba kumekuwa na matamko toka uongozi wa vyuo lakini bado hakuna fundisho.

Hawa wanafunzi wa vyuo vikuu watakapohitimu ndiyo wanaotegemewa kuwa viongozi na wazalishaji katika sekta mbalimbali ili kuinua maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

TCU wanatakiwa kuwafuta usajili wote waliohusika kwenye hizo video na wasipewe nafasi ya kusoma chuo chochote kabisa.

Kila mtu ni kama kashazoea habari kama hizi kusikika, hakuna maadili tena. Unakaa siku 2,3 unapata habari mpya.

Wanafunzi wa elimu ya juu tatizo liko wapi hadi kufikia hatua hii?

TCU chukueni hatua.
picha
 
Kwanini wenye mamlaka wasipige ban mitandao yote inayoonyesha hizo picha chafu?

Yaani kijana wa chuo anafanya huo ujinga je elimu aliyopata haijamsaidia?

Serikali badilisheni huu mfumo wa elimu.
 
Wakuu Salaam:

Siku za karibuni kumekuwa na usambaaji wa video chafu kwenye mitandao ya kijamii na jambo hili linaendelea kukua miongoni mwa wanafunzi wa Elimu ya juu.

Na waliohusika katika video wapo pamoja na kwamba kumekuwa na matamko toka uongozi wa vyuo lakini bado hakuna fundisho.

Hawa wanafunzi wa vyuo vikuu watakapohitimu ndiyo wanaotegemewa kuwa viongozi na wazalishaji katika sekta mbalimbali ili kuinua maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla.

TCU wanatakiwa kuwafuta usajili wote waliohusika kwenye hizo video na wasipewe nafasi ya kusoma chuo chochote kabisa.

Kila mtu ni kama kashazoea habari kama hizi kusikika, hakuna maadili tena. Unakaa siku 2,3 unapata habari mpya.

Wanafunzi wa elimu ya juu tatizo liko wapi hadi kufikia hatua hii?

TCU chukueni hatua.
Nikuulize Tu.. Wewe ni Mkamilifu?

Video mmeona ni Kigezo cha Kufutia mtu Usajili?

Yale ni Maisha ya Mtu Binafsi.. atajuana na Huko atakapofanyia Kazi au Jamii yake inayomzunguka. TCU wao wanaangalia Vigezo vya Msingi..

Mbona kuna WEZI.. WALEVI..? mbn wapo wanaovaa Mavazi yasiyo na Heshima?
 
Back
Top Bottom