TCU yasema hakuna Mwanafunzi atakayelazimishwa kusoma katika chuo ambacho hakitaki

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
adac58eb-c52a-4c4d-845e-b74a75575bb8.jpg

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa

Baada ya kuibuka kwa malalamiko kadhaa mitandaoni kuhusu udahili wa Wanafunzi wanaofanya maombi ya kujiunga na Vyuo Vikuu wakati huu ambao dirisha la udahili limefunguliwa, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo kadhaa.

Wanafunzi kukwama kufanya machaguo
Inadaiwa kuwa kuna baadhi ya Wanafunzi ambao wamepata nafasi katika vyuo zaidi ya kimoja, hivyo wanapata wakati mgumu kwa kuwa kuna ambao wamekuta tayari majina yao yameshathibitishwa kwenye vyuo kadhaa bila ridhaa yao.

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa anasema: “Kwanza ieleweke wazi kuwa kuna changamoto za ujumla hasa inapotokea waombaji wapya wanakuwa kwenye mchakato wa kufanya maombi hayo.

“Wapo ambao wanashindwa kutumia vizuri mfumo unaotumiwa, muhimu Vyuo vikatoa elimu kwa Wanafunzi na watumiaji wote wa mtandao wa kufanya maombi hayo ili kupunguza au kuondoa changamoto za matumizi mbalimbali.

“Wapo ambao wanaweza kufanya machaguo ya chuo fulani lakini baadaye wakashindwa kufanya mabadiliko kwa kutojua nini kinatakiwa kufanyika, wanatakiwa kuomba msaada kwenye vyuo husika ili wapate usaidizi wa teknolojia inayotumika.

“Pamoja na hivyo nasisitiza kuwa hakuna Mwanafunzi ambaye atashindwa au kunyimwa fursa ya kusoma kwenye chuo anachokitaka ilimradi amefikisha vigezo vinavyohitajika.

“Muombaji akikwama awasiliane na TCU, katika tovuti yetu kuna namba zetu na njia nyingine za mawasiliano yetu ikiwemo barua pepe, wenye changamoto wawasiliane na sisi kwa ajili ya kutatua changamoto husika.

“Yeyote ambaye amepata chuo zaidi ya kimoja atakwenda kwenye chuo anachokitaka yeye mwenyewehata kama amekutana na changamoto.

“Ambaye amechagua chuo XX anatakuwa kuingia katika mfumo huohuo walioutumia wakati wanajisajili na kufanya mabadiliko wanayoyataka.”

Madirisha matatu ya udahili
Kuna hawamu tatu za kufanya udahili na ikiwezekana tutafanya madirisha manne kama kutakuwa na changamoto ambazo zimewakwamishwa wadahiliwa kukamilisha mchakato.

92de7188-9cb4-4f19-b36f-cb0a7179435d.jpg

Madai ya vyuo kuingilia mfumo
Hivo taarifa tumezipata tunazifanyia kazi na kama itabainika kuna chuo ambacho kinafanya michezo hiyo basi hatua kazi za kisheria zitachukuliwa.

Vyuo vinatakiwa kuelimisha umma namna sahihi ya kutumia mifumo ambayo inatumiwa.

MWENENDO-WA-UDAHILI-WA-SHAHADA-YA-KWANZA-KATIKA-MWAKA-WA-MASOMO-2023-2024_page-0001.jpg

MWENENDO-WA-UDAHILI-WA-SHAHADA-YA-KWANZA-KATIKA-MWAKA-WA-MASOMO-2023-2024_page-0002.jpg

MWENENDO-WA-UDAHILI-WA-SHAHADA-YA-KWANZA-KATIKA-MWAKA-WA-MASOMO-2023-2024_page-0003.jpg

Pia soma > TCU tunaomba msaada, Chuo cha St. Joseph kinatoza ada na direct costs kwanza ndipo uweze ku-confirm udahili wako
 
View attachment 2732635
Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihamba

Baada ya kuibuka kwa malalamiko kadhaa mitandaoni kuhusu udahili wa Wanafunzi wanaofanya maombi ya kujiunga na Vyuo Vikuu wakati huu ambao dirisha la udahili limefunguliwa, Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imetoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo kadhaa.
Eti mawasiliano yetu yapo. Wakati simu zingine hazipatikani na zinazopatikana ziko busy muda wote na zikiita hazipokelewi.

Tanzania upande wa customer service tuko nyuma sana
 
Back
Top Bottom