BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,119
Je, wajua Sheria ya Vyuo Vikuu ya mwaka 2005 na Kanuni za Mwaka 2013 zimepiga marufuku Wanafunzi kujihusisha na shughuli za Chama cha Siasa ndani ya Majengo ya Chuo?
Kifungu cha 57 cha Kanuni ya Vyuo Vikuu inasema "Mwanafunzi yeyote au Mfanyakazi wa Chuo Kikuu anayejihusisha katika
shughuli za Chama cha Siasa ndani ya Majengo ya Chuo Kikuu ATASHUGHULIKIWA kama ifuatavyo:-"
a. Atapewa Onyo la Kinidhamu kwa kukiuka Kifundu cha 51 cha Sheria ya Vyuo Vikuu ya mwaka 2005
b. Atasimamishwa Chuo Kikuu, akisubiri kukamilika kwa Uchunguzi wa Kinidhamu (ambao utakamilika ndani ya mwezi mmoja usimamishwaji ulipotolewa kwa Mwanafunzi au Mfanyikazi)
c. Mara baada ya Uchunguzi kukamilika, Mwanafunzi au Mfanyakazi atatokea mbele ya Kamati ya Nidhamu kujibu shitaka hilo
d. Akipatikana na hatia, kwa upande wa Mwanafunzi, atasimamishwa masomo kwa muda usiozidi MIAKA MIWILI na kwa Mfanyakazi atashughulikiwa kwa mujibu wa masharti ya Kanuni za Maadili na Nidhamu ya Wafanyakazi