Mwinyimadi
New Member
- Aug 13, 2022
- 3
- 0
Habari ndugu wana JF,
Leo nimependa kuzungumza nanyi mada kuhusu vyuo vikuu kufundisha ASTASHADA na STASHAHADA. ni ukweli usiopingika sera ya elimu inabidi kufanyiwa marekebisho kwasababu vyuo vikuu siku hizi zinachukua watoto wanaomaliza kidato cha nne (4) wengi wao chini ya miaka ya 18 ambapo tunachukulia kama watu wazima kinyume na sheria ya nchi kwani vyuo vikuu vyote vinasema ni elimu ya watu wazima kwahiyo wanafunzi hawa wa Astashahada (Certificate) na Stashahada (Diploma) wanakuwa wahanga kubwa wa unyanyasi wa kingono na ukatili wa kijinsia kwasababu anakuja pahala ambapo hakuna mchunga yaani ana kuwa huru kufanya lolote lile atakalo kwa uhuru.
Kwa kipindi nilichofanya kazi moja ya chuo kikuu nchini nimeweza kugundua wanafunzi hawa ndio wamekuwa swala wa vyuo na ndio waathirika wakubwa wa ukatili wa kingono, unyanyasi wa kijinsia na mimba za utotoni.
Ninatoa wito kwa wadau wa elimu kuangalia upya sheria zetu vizuri kwasababu watoto hawa wamekuwa wakibadilika kimaadili kwa muda mfupi mwishoe wanaingia katika uraibu.
Hivyo rai yangu vyuo vikuu vibadilishe mtazamo wake au viache kufundisha non- degree kwa mustakabali mpana wa vizazi.