Tume ya Vyuo Vikuu yafungua awamu ya Nne ya Udahili kwa Wanafunzi wa vyuo

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
0f74b793-0864-4622-b9f6-ac5d59578b5b.jpeg

Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), Prof. Charles Kihampa, akizungumza na Waandishi wa Habari, Dar es Salaam, leo Oktoba 13, 2023 kuhusu kufunguliwa kwa dirisha la Awamu ya Nne ya dirisha la Udahili kwa programu ambazo bado zina nafasi kwa mwaka wa masomo 2023/2024.

Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) imefungua awamu ya nne ya udahili kwa wanafunzi wa shahada ya kwanza na wanafunzi wametakiwa kutumia fursa hiyo vyema kwani hiyo ni nafasi ya mwisho kabisa waliyoitoa.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mtendaji wa TCU, Charles Kihampa wakati akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

3faa2c74-e7d2-45b1-9fdf-470bbf43c035.jpeg

f9e93779-5a40-43ef-b424-e786db035d45.jpeg
 
Ukiritimba umekua mwingi mpaka TCU imekua useless watoto wanapigwa pesa ya application kila wanapo apply, huo ni wizi mtupu inatakiwa mtu alipie mara moja TCU kwa vyuo vyote, sio kufanya kila chuo kutoza application pesa.
 
Chini ya mfumo wa CAS maombi yalipelekwa tcu lakini baada ya mwenda zake kuupiga marufuku mfumo huo na kurudisha maombi ya moja kwa moja chuoni inabidi malipo yawe kwa kila chuo naukirudia kuomba tena walipa. Kuna vyuo havina application fee. Chuo chenye ushindani mkubwa mfano udsm hapa huchuma.
 
Sasa vyuo vinatumia udhaifu huo kujiongezea mapato imagine mtoto anae Apply MD kwenye chuo zaidi ya viwili ka apply mara 4×50000=200,000×2= 400,000 kama wanafunzi 1000 wote wameapply mara nne na wamekosa watakua wamepoteza kiasi gani cha pesa, hapo mtoto wamasokini atakufa masikini, kwanini wasiorodhesha slot za nafasi zilio bakia kila chuo ili mtoto awe sure na kozi gani anapply na chuo gani?
 
Chini ya mfumo wa CAS maombi yalipelekwa tcu lakini baada ya mwenda zake kuupiga marufuku mfumo huo na kurudisha maombi ya moja kwa moja chuoni inabidi malipo yawe kwa kila chuo naukirudia kuomba tena walipa. Kuna vyuo havina application fee. Chuo chenye ushindani mkubwa mfano udsm hapa huchuma.
Miaka hii ukikosa dirisha la kwanza madirisha yanayofuatia haulipii tena
 
Dah kuna madogo wa mocu (moshi_ushirika) wametoka kupga sup mpaka leo matokeo hajapelekwa tcu.
 
Back
Top Bottom