Tume ya Uchunguzi wa Uvunjifu wa Haki na Amani Katika Wiki ya Uchaguzi Mkuu 2025: Naomba Nakala ya Tangazo Husika Katika Gazeti la Serikali

Tume ya Uchunguzi wa Uvunjifu wa Haki na Amani Katika Wiki ya Uchaguzi Mkuu 2025: Naomba Nakala ya Tangazo Husika Katika Gazeti la Serikali

Doctor Mama Amon

Platinum Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
2,311
Reaction score
3,490
1763806401858.png

Wadau,

Kwa mujibu wa kifungu cha 20 cha Sheria ya Tume za Uchunguzi (Commissions of Inquiry Act), Sura ya 32, Toleo la 2023, Rais anapounda Tume ya Uchunguzi husika, Tume hiyo inapaswa kuanza kazi baada ya Uamuzi wa Rais kuchapishwa kwenye Gazeti la Serikali .

Taarifa ya gazetini inapaswa kutaja mambo kadhaa yakiwemo: (1) Jina rasmi la Tume, (2) muundo na Wajumbe wa Tume, (3) majukumu ya Tume, (4) Ratiba ya kazi, (5) Hadidu za rejea za Tume husika, na (6) Maelekezo maalum kwa Tume husika.

Mwaka 2006, Rais Jakaya Kikwete alifanya hivyo alipounda Tume ya Uchunguzi wa mazingira, sababu na matokeo ya mauaji ya Ephraim Chigumbi na Wenzake (Kiambatanisho A).

Tayari Rais Samia ameunda Tume ya Kuchunguza Mazingira, Sababu na Matokeo ya Uvunjifu wa (Haki na) Amani katika wiki ya uchaguzi Mkuu wa 2025.

Lakini bado sijapata nakala ya Tangazo la Serikali lenye kutaja mambo hayo hapo juu.

Tangazo la Ikulu kwa umma kupitia vyombo vya habari (KIambatanisho B) halitoshelezi matakwa ya kisheria.

Nataka Kufuatilia kwa karibu utendaji wa Tume hii.

Hivyo, nomba mtu yeyote mwenye nakala yake aniwekee hapa kwa ajili ya kazi maalum.

Naambatanisha:

  1. Kiambatanisho A: Tangazo la serikali kuhusu sakata la chigumbi na wenzake mwaka 2006
  2. Kiambatanisho B: Taarifa ya ikulu kwa vyombo vya habari kuhusu Tume ya Uchunguzi wa matukio ya Wiki ya Uchaguzi Mkuu 2025

KIAMBATANISHO A: TANGAZO LA SERIKALI KUHUSU SAKATA LA CHIGUMBI NA WENZAKE MWAKA 2006

E1.PNG

E2.PNG

E3.PNG

E4.PNG

E5.PNG

E6.PNG

E7.PNG

KIAMBATANISHO B: TAARIFA YA IKULU KWA VYOMBO VYA HABARI
1763806292949.png
 
Attachments

Tume ya kudeki uchafu wa samuya!
Tuandae Tume Kivuli ili kuweka rekodi sawa.
Unaonaje?
Kama unakubali pendekeza yafuatayo:

(1) Jina Rasmi la Tume,
(2) muundo/wajumbe (watoke humu humu JF kwa majina yao ya humu humu),
(3) majukumu ya Tume,
(4) ratiba ya Tume,
(5) Hadidu za rejea, na
(6) maelekezo maalum kwa Tume husika.
 
View attachment 3505822
View attachment 3505824

Wadau,

Kwa mujibu wa Sheria ya Tume za Uchunguzi, sura ya 32, Toleo la 2023, Rais anapounda Tume ya Uchunguzi anapaswa kuchapisha kwenye Tangazo la Serikali taarifa rasmi yenye mambo kadhaa.

Mambo hayo ni: (1) JIna, (2) muundo, (3) majukumu, (4) ratiba, (5) Hadidu za rejea, na (6) maelekezo maalum kwa Tume husika.

Mwaka 2006, Rais Jakaya Kikwete alifanya hivyo alipounda Tume ya Uchunguzi wa mauaji ya KIna Ephraim Chigumbi na Wenzake (tazama kiambatanisho).

View attachment 3505821

Tayari Rais Samia ameunda Tume ya Kuchunguza Chanzo cha Uvunjifu wa (Haki na) Amani katika wiki ya uchaguzi Mkuu wa 2025. Lakini bado sijapata nakala ya Tangazo la Serikali lenye kutaja mambo hayo hapo juu.

Tangazo la Ikulu kwa umma kupitia vyombo vya habari (attached) halitoshelezi matakwa ya kisheria.

Nataka Kuunda Tume Kivuli ya Kufanya Uchunguzi wa Uvunjifu wa (Haki na) Amani uliotajwa hapa, kwa kutembea kwenye hadidu za rejea zile zile. Hivyo, nomba mtu mwenye nakala yake aniwekee hapa.
View attachment 3505823
Asante kwa kutukumbusha tunalifanyia kazi na J3 u tali on a tsngazo kwenge gazeti la Uhuru, mfanyakazi, Mzalendo na Habari leo
 
Unadhani watakupa hicho kitu? CPD kazi kushinda na chama cha mawakili wa serikali kuendekeza uchawa kwa samia.

Hawajui hata majukumu yao. Hii nchi imeshajifia.
 
View attachment 3505822
View attachment 3505824

Wadau,

Kwa mujibu wa Sheria ya Tume za Uchunguzi, sura ya 32, Toleo la 2023, Rais anapounda Tume ya Uchunguzi anapaswa kuchapisha kwenye Tangazo la Serikali taarifa rasmi yenye mambo kadhaa.

Mambo hayo ni: (1) JIna, (2) muundo, (3) majukumu, (4) ratiba, (5) Hadidu za rejea, na (6) maelekezo maalum kwa Tume husika.

Mwaka 2006, Rais Jakaya Kikwete alifanya hivyo alipounda Tume ya Uchunguzi wa mauaji ya KIna Ephraim Chigumbi na Wenzake (tazama kiambatanisho).

View attachment 3505821

Tayari Rais Samia ameunda Tume ya Kuchunguza Chanzo cha Uvunjifu wa (Haki na) Amani katika wiki ya uchaguzi Mkuu wa 2025. Lakini bado sijapata nakala ya Tangazo la Serikali lenye kutaja mambo hayo hapo juu.

Tangazo la Ikulu kwa umma kupitia vyombo vya habari (attached) halitoshelezi matakwa ya kisheria.

Nataka Kuunda Tume Kivuli ya Kufanya Uchunguzi wa Uvunjifu wa (Haki na) Amani uliotajwa hapa, kwa kutembea kwenye hadidu za rejea zile zile. Hivyo, nomba mtu mwenye nakala yake aniwekee hapa.
View attachment 3505823
Tume ya kisayansi sio hii ya kisiasa
 
Back
Top Bottom