Enheeeeee ukiwa mtundu utotoni visa haviishi!!!!!
Hivi mnakumbuka kutengeneza upinde na mshale mbele unaweka msumari halafu mnaenda kuwinda!!!!
Basi siku hiyo tumeenda kuwinda hamna kitu tumerudi nayo giza likaingia tukasema leo tuoneshe muvi,basi mi na mwanangu mmoja akiitwa Majid,muvi ni kwamba tuchukue tochi halafu tukae kwenye ngazi (tunakaa maghorofani hapo)basi mi kaingia ndani nikaiba tochi tukaandaa steji gizani, mmoja ashike tochi akiwa nyuma yangu akimmulika Majid wengine wakae gizani mi namlenga yeye steringi anakwepa ikakubali kama mara mbili hivi mishale inaisha tunaokota muvi linaendelea! !!!!!
Stering akazidisha mbwembwe sasa badala ya kukwepa akataka kudaka mshale bhana, mie tena nishalenga paja adake waapi sasa mshale kwenye paja bana tuuf msumari wote ndani midamu mwa mwa mwaaa, watu wooote eenheeee eneheeee umemuumiza mtoto wa watu yeye steringi kaangua kilio cha maana siri ya muvi ipo
tena hapo!!!!!?????
Watu kutoka wanamkuta midamu ya maana sijui nilimtoboa artery au vein masikini, basi yeye hospitali mie sasa kichapo home cha maana kwanza nimeiba tochi ya mshua unabonyezea nyuma ndio inawaka,pili kuchelewa kurudi, tatu nimemuumiza mtoto wa watu!!!!
Tukikaa na marehemu shangazi na dada wa kazi nao gombezwa sana kwa nini niko nje muda ule na sijaoga ,natumai mnakumbuka kuogeshwa na mtu mwenye hasira sabuni mpaka machoni dodoki mpaka ngozi inawaka moto!!!!!!
Mungu amrehemu auntie bhana mwenyewe alikuwa akinipenda sana!!!!
miss neddy,
Deo Corleone