badiebey
JF-Expert Member
- Nov 29, 2013
- 5,875
- 3,118
Nilikua kama miaka 6 au 7 hivi,tunakaa mkoa flani hapa TZ,sasa siku ya christmass ilikuwa watoto wengine wanaruhusiwa na wazazi wao kwenda kutembea,mara disco toto nk,mama angu alikuwa kashapiga marufukuu na mkwara wa kutosha kuwa hakuna mtu kwenda kuzurura,mhh badiebey nikaona hapana aisee mama mbona ananinyima raha mwanae miee wakati na gauni jipya nnalo ,enzi zile gauni na kipochi chake na moka na soksiii ,wadada mnazikumbuka lakiniii,,,,,
basi nkaona isiwe shida,mama katupikia,tumekula vizuri, kaingia chumbani nafikiri me nikavaa zangu mbio kwa jirani etu anaitwa happy tukaishia kutembea,basi hata hamna la maana mnanunua icecream tu,mnashangaa shangaa na kwenda kwenye bembea ili mradi mda ukaenda hadi sa 1 usiku ndo najirudisha home gauni chafu halieleweki,
mama namkuta kakaa nje kiboko kaweka nyuma ya kiti,basi ananiuliza ehe mwanangu za huko,me kwa furaha kabisa namuambia nzurii na kumsimulia yote yaliyojiri,hhehhehe kiboko kilipotokea sijui nilichezea kichapo mfano hakunaaa,baba ndo alininusuru kidogo na kichapo,nilisinzia huku nalia,tangu siku hyo sina passion na uzururaji aisee....