Tukio lako la kusisimua ukiwa mdogo

Tukio lako la kusisimua ukiwa mdogo

Sitasahau siku ambayo nilimtania jamaa mmoja ambaye ni bubu na kiziwi kwa kumuonyeshea vitendo kama watumiavyo viziwi kuwasiliana.

Basi jamaa akanivizia nikiwa na mwenzangu nikiendesha gari la kamba (kamba ya katani inafungwa mimi mbele kama dereva na mwingine nyuma tunaiwamba kuipa "shape" na katikati wanaingia abiria)
Jamaa akaninyatia huku ameshika kitanzi akaniwahi nacho shingoni akanipa mgongo na kuanza kunivuta kwa upande wake kitanzi akiwa amekishikilizia begani na akiwa hanitazami. Nilijaribu kupiga kelele bila mafanikio maana jamaa hakuwa akisikia (kiziwi) na baada ya muda sauti ikawa haitoki sababu ya kubanwa na kamba.

Nilikuja okolewa na msamaria mmoja alietokea kupita eneo lile na kushuhudia tukio lile maana wenzangu walinikimbia mapema sana baada ya kudakwa.
Sitasahau...

Khaaaa huyo jamaa mumiani kabisa
 
Pamoja na yote ila tukio ambalo hadi leo sitaki kusikia habari za kuogelea ni hili la kutaka kufia kwenye bwawa maarufu kama lambo, hapo CYBERTEQ ananielewa vizuri kwenye hiyo lugha ya malambo.

Nilikua sijui kuogelea, ila kwa vile nilikua mdogo nikawa nachukua dumu la lita tano likiwa tupu, nafunga mfuniko nalishikilia naogelea kama kama kawaida. Tatizo la hiyo stail nilikua naona kama inaninyima uhuru wa kujiachia na kufanya makeke kwa sababu mikono yote inabidi iwe imelishikilia hilo dumu ili niendelee kuelea.

Kuna siku nikaenda kuogelea mchana na nilikua peke yangu nikiwa na kigaloni changu kama kawaida. Safari hii nikaona nibadili mtindo kidogo ili kufurahia maji. Nilikua nafikiri miguu ndio kikwazo kikubwa kwenye zoezi la kuogelea, hivyo nikaifunga yote kwa kamba na kulifunga lile galoni tupu hukohuko miguuni. Nikijidanganya kua mikono ntaitumia kunizuia nisizame na kwa kua miguu itakua inaelea kutokana na kulifunga lile dumu.

Baada ya maandalizi yote kukamilika nikaanza kurukaruka kuelekea kwenye kina kirefu cha maji ili nijiachie. Nilipofikia usawa wa maji ya magoti nikaruka kuelekea kwenye kina kirefu huku nikiamini mikono itaanza kazi yake ya kufanya makeke. Kilichotokea ni kwamba lile dumu lililazimika kubaki juu na kufanya miguu ibaki juu huku kichwa kikilazimishwa kuzama chini ya maji (Ikumbukwe nilikua peke yangu) nilikunywa kiasi cha kutosha cha hayo maji kisha nikawa mpole.

kilichofuata ikabidi kuendelea kupapasapapasa huko chini kwa chini hadi nilipokamata matope na kuanza kutembea kwa mikono huku nikiendelea kunywa maji kuelekea nilipotokea. Bahati nikafanikiwa kurudi sehemu yenye kina kidogo na baadae nchi kavu kabisa. Sikua na hamu tena na maji tangu siku hiyo.

Huwa kila nikikumbuka naona kama siku hiyo nilikufa na najiuliza watu wangesema kitu gani kilikua kinaendelea kwa mazingira ambayo wangenikuta nayo? Naishia kuona jinsi gani kazi ya upelelezi ilivyo ngumu japo naipenda sana.
 
Last edited by a moderator:

daaah, mkuu sasa hiyo ilkuwa suisaidi, mara ya mwisho kuogelea nakumbuka ilikuwa beach moja inaitwa bangwe magereza, kigomaaaa, wenyewe tulikuwa tukitengeza mitumbwi ya mashina ya migomba, siku hiyo wenyewe si tukaenda maji marefu, hukooo karibu na jiwe moja linaitwa jiwe nundu, si tukaanza kupiga stori za kutishiana mamba, wacha tujitose majini....hakyanani sku hiyo kama si wafungwa tungeshaimbiwa buriani!
 
Ha ha haaaaa daaaanh humu ndani kuna balaaaa CYBERTEQ mzee ukapewa ze utamu hata hujui ni nini!!!!!!

Ila jamani hebu tujuiulize sasa kama sie haya ndio mambo yetu leo tukiwa na watoto watukutu tunalalamika!!!????
Mie maza aliniauliza vipi mwanao......wakati huo nina mmoja wa kiume nikamwambia mama mjukuu wako ni mtundu hatari........alicheka saaana akaniambia usije kusema hivyo mbele ya babako wala watu wanaokujua......wewe ulikuwa ni balaaa.....!!!!!!

hahahaa, kaka nikapewa ze utamu kwa mara ya kwanza, huwezi amini kijana nilikuwa nalia kwa raha ya ajabu, lile bao sitokaa nilisahau mpaka leo, mule ndani ilikuwa ni makelele tu mi kivyangu na mwenzangu na ye analia kivyake tumesahau hata kama tuko home, kibarazani bro anashangilia vibaya!

sasa mkuu kwa tabia hiyo mwanao utamkemea kweli, si utakemea kizushi huku ukishangilia kimoyomoyo "kamua jogooo langu".....lol!
 
nakutafuta tukazurure sabasaba
Nilikua kama miaka 6 au 7 hivi,tunakaa mkoa flani hapa TZ,sasa siku ya christmass ilikuwa watoto wengine wanaruhusiwa na wazazi wao kwenda kutembea,mara disco toto nk,mama angu alikuwa kashapiga marufukuu na mkwara wa kutosha kuwa hakuna mtu kwenda kuzurura,mhh badiebey nikaona hapana aisee mama mbona ananinyima raha mwanae miee wakati na gauni jipya nnalo ,enzi zile gauni na kipochi chake na moka na soksiii ,wadada mnazikumbuka lakiniii,,,,,
basi nkaona isiwe shida,mama katupikia,tumekula vizuri, kaingia chumbani nafikiri me nikavaa zangu mbio kwa jirani etu anaitwa happy tukaishia kutembea,basi hata hamna la maana mnanunua icecream tu,mnashangaa shangaa na kwenda kwenye bembea ili mradi mda ukaenda hadi sa 1 usiku ndo najirudisha home gauni chafu halieleweki,
mama namkuta kakaa nje kiboko kaweka nyuma ya kiti,basi ananiuliza ehe mwanangu za huko,me kwa furaha kabisa namuambia nzurii na kumsimulia yote yaliyojiri,hhehhehe kiboko kilipotokea sijui nilichezea kichapo mfano hakunaaa,baba ndo alininusuru kidogo na kichapo,nilisinzia huku nalia,tangu siku hyo sina passion na uzururaji aisee....
 
Back
Top Bottom