Tukio lako la kusisimua ukiwa mdogo

Tukio lako la kusisimua ukiwa mdogo

TUPAC WA MWAKALELI

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2014
Posts
354
Reaction score
109
Nakumbuka ilikuwa ni pasaka mwaka siukumbuki, nyumbani tumepika bata.

Watu wakiwa kanisani wakimsifu Mungu kwa nyimbo na mapambio, niliachiwa nyumba ili niilinde na kukatakata kachumbari.

Waliwa kanisani, pepo wa Yuda Eskarioti akanikumbuka, akanituma nikaonje kipande kimoja cha nyama.

Nikaenda nikadokoa, kasha mfupa nikaenda kuuficha chumbani kwangu.

Kilikuwa ni kitamu sana sijawahi kuuona utamu ule. Nikaenda nikaongeza cha pili, asikuambie mtu, kilikuwa ni kitamu kuliko kile cha kwanza, kudadadeki. Mfupa nikausukumizia chumbani kwangu.

Baada ya nusu saa, kukawa hamna kachumbari iliyokatwa na kuna mabawa mawili tu yamebaki.

Muda wa kutoka kanisani ukawadia, mara si mara watu hao na wageni wawili, Mchungaji na mwinjilisti. Mama na haraka zake za kutaka tule mapema, kataka kuanza maandalizi ya msosi.

Kufungua chungu, anakutana na mabawa mawili tu.

Mama akauliza mboga yote imeenda wapi? Maana bata alikuwa ni mkubwa sana.

Nikajibu, yule paka shume wa jirani kafungua mfuniko kisha kala mboga.

Mama akauliza, alipo maliza kula akafunika? Nikajibu, mama yule ni paka shule, ukooo wao wanatenda miujiza mikubwa, ndio maana wanapendwa na wachawi.

Mama akabloo, akaona sasa atumie uwezo wa kimama.
Akaniuliza tena, mifupa iko wapi?

Nikajibu labda mepelekea marafiki zake.
Dah....
Mama akaamua aanze msako wa kila sehemu.

Msako uliishia nje, nikaona mama akija nakibakuli na lundo la fimbo.
Nilipigika siku ile kama paka mwizi.

Akasema haya toa mifupa yote huko uvunguni na ukawape mbwa.

Thanks God, mama alikuwa na mahusiano mazuri na majirani, Mchungaji na Mwinjilisti wahakushtukia mchezo.

Mchungaji Mwamlima na Mwinjilisti Mwaibofu mpumzike mahali pema .
 
Mimi mwaka 1987 nilipigwa jiwe na Wamakonde.

Tatizo niliwachokoza mwenyewe. Nilikuwa mchokozi sana nilipokuwa mtoto.

Sasa wale watoto kila mara nilipowaona mtaani nilikuwa nawatania 'nangu mene' (hata maana yake nshasahau).

Siku ya siku nipo barazani kwetu nikawaona wanapita mtaani kwa mbali.

In true NN form...nikaanza uchokokozi....'nangu mene'.

Jamaa si wakanilia timing bana...wakarusha jiwe likanipata juu ya jicho la kushoto kwenye nyusi.

Damu zikaanza kuchuruzika. Nikarudi ndani nimeshikilia kidonda nalia. Bahati nzuri alikuwepo mjomba.

Chap chap akafanya mipango na kunikimbiza zahanati. Kufika zahanati kuangalia kidonda, daktari akasema hakuna jinsi - ni lazima tu kukishona.

Hilo tukio kamwe sitalisahau maana lile jiwe lingeshuka kidogo tu na kutua flush kwenye jicho, leo hii ningekuwa chongo.

Shori gani wa ukweli angenikubali leo hii kama Rais wa wabeba maboksi ningekuwa na chongo?

Kwa hiyo hilo tukio siwezi kulisahau kwa sababu uchokozi wangu ulinitokea puani siku hiyo.

Nahisi kama vile uchokozi upo kwenye DNA yangu ingawa sasa umetulia kwa sababu ya utu uzima.
 
Hapo bold I beg to differ :nerd:
 
Tulikuwa tunafuga mbwa home ,baba alikuwa na kawaida ya kila wikend akitoka job anarudi na furushi la mabaki ya vyakula vinono kwa ajili ya chakula cha mbwa.

Siku hiyo nakumbuka alileta ukoko wa pilau ulokuwa umechanganyikana na mchuzi na mabakibaki ya nyama za kuku,baada ya shughuli zake akawa amewatengea wale mbwa kwenye chombo chao kila mbwa na sahani yake.

Bwana weeee nkaona mbwa wanafaidi, nkicheki pilau kula hadi xmas haa nkamtaimu mzee katoka tu pale nkazama kwa mbwa mmoja ye anakula huku mi huku.

Kilichokuja kutokea baadaye nilishtukia nimedakwa juujuu nilichezea bakora nashukuru mama alikuwepo akaniokoa.dah RIP my dadi jamani loh!!
 
Ni nakumbuka nilikuwa na miaka ya tisini nikiwa teenager msumbuliwa na balehe, nilikuwa nakamendea kabinti Fulani hivi shombeshombe. Basi kakawa kamenikubali, kakapanga muda ya SAA NNE asubuhi niende kwao kula mzigo wazazi wake wakiwa kazini na wadogo wake shule.

Basi SAA NNE kamili juu ya alama, msumari Wima kama mwavuli ndani ya mfuko wake mzee nikagonga geti kwa mapooooozi. Out of expectations si akafungua mama yake.

Haraka haraka nikasema mama kanituma kuku hamsini hela ataleta baadae. Nikapewa kuku hamsini huku nikiwa nimebaki na swali kubwa kichwani nitawapeleka wapi kuku hawa?
 
Nakumbuka siku moja tulikuwa home bored, wakati huo dingi alikuwa amesafiri.

Tukasema ngoja tukaangalie mpira kwa jirani nakumbuka siku hyo ilikuwa fainali ya Yanga na Sc Villa ya Uganda.

Hatuna hili wala lile tukarudi home usiku kama wa saa 4 hivi, hamadi dingi yule pale kibarazani, hatujui amerudi sangapi.

Tulivyokuwa wajinga tukaendelea kujificha nyuma ya kisima kama nusu saa hivi, kwahyo tukaenda home kama saa 4;30

Ilikuwa balaa, tulipokea kichapo toka kwa baba na mama kwa mpigo, mbaya zaidi wakasema turudi tukalale tulipotoka.

Tulivyokuwa wajinga tukarudi kweli, tukawagongea wakatufungulia tukaliangusha.

Kuamka asubuhi tukasema ngoja turudi home inaweza kuwa shwari, ilikuwa afadhali ya jana, tukapigwa tena na tulitakiwa kurudi tulipotoka tukamlete alioturuhusu kulala kwake.

Tukamuita, dingi alimfokea mama wa watu utadhani mwanae, mara yule jirani yetu akapaniki akaenda serikali za mitaa kushitaki ametukanwa.

Dingi akaitwa akatupeleka na sisi, tulikaa nje wao wakaingia ndani kuyamaliza, tulikwa tunasikia wanafokeana balaa.

Walipomalizana tukawa tunarudi home huku tunachezea stiki, siku hiyo ilikuwa jehanamu kwetu.

Enzi hizo mshua na mama walikuwa kituo cha polisi. Ukifanya kosa mama anakuanzishia, baba akija wanakuanzishia upya, wanakupa stiki za haja.
 
Mchungaji Mwamlima?
Nilipata mahubiri yake sana pale kanisa la moravian
Ni maeneo ya soko matola, nimesahau jina ni miaka mingi.

Aisee, ukala je mboga jamani, loooh?
Si ajabu nikamfahamu hata maza wako aise;

R.I.P. Mchungaji Mwamlima.

TUPAC WA MWAKALELI
 
Tulikuwa tunafuga mbwa home ,baba alikuwa na kawaida ya kila wikend akitoka job anarudi na furushi la mabaki ya vyakula vinono kwa ajili ya chakula cha mbwa...........siku hiyo nakumbuka alileta ukoko wa pilau ulokuwa umechanganyikana na mchuzi na mabakibaki ya nyama za kuku,baada ya shughuli zake akawa amewatengea wale mbwa kwenye chombo chao kila mbwa na sahani yake....... Bwana weeee nkaona mbwa wanafaidi, nkicheki pilau kula hadi xmas haa nkamtaimu mzee katoka tu pale nkazama kwa mbwa mmoja ye anakula huku mi huku .........kilichokuja kutokea baadaye nilishtukia nimedakwa juujuu nilichezea bakora nashukuru mama alikuwepo akaniokoa .........dah RIP my dadi jamani loh!!

hahahahahahahs kumbe ulikuwa mtukutu
 
Nilikuwa mtoro sana wakati nikiwa darasa la pili, nikienda shule nikiulizwa kwanini jana hukuja kazi yangu ilikuwa nikijibu nyumbani kulitokea msiba.Niliua watu wengi sana kwenye ukoo mpaka nikawa nawarudia kuwaua tena.

Mwishoni mwalimu wa darasa akaja kujua mimi muongo,nikiwa sijaenda shule na kesho yake nikawepo mwalimu wa darasa akawa ananiwahi kuniuliza na leo ndugu yako nani kafa Robert nabaki kukenua meno.

Mwisho darasani wakawa wananiita Mzee wa kuua ndugu.
 
mi nakumbuka kuna manzi alikua na shundu balaa nlivokua a lvl miaka ya tisini sasa ile kuimbisha imbisha nn manzi kaingia king afu mfukoni niko kapaa hamna pesa ya lodge........

plan b ikawa nimpigie hm tu maana kwao ilikua nyomi nyomi sa nkavizia bi mdashi kaenda job maana ni teacher home nabakigi na hg basi nkamtuma hg shop ile kasepa tu nkazamisha mzgo aisee kumbe bi mdashi alikua hayuko poa so akaomba ruhusa aje apumzke home na alikuaga na tabia ya kulala chumbani kwangu mchana ile anaingia tu akanikuta mzee ndo nko juu ndo nakaribia kufika........

aisee nlikula kipigo dushelele likanywea na safari ikaishia pale ila yule manzi ndo alipigwa mpk nkamuonea huruma aisee.........

wiki nzima nkawa sina hamu ya kumtazama maza usoni
 
Namshukuru Mungu mi sikuwa mtukutu. İla sitasahau nilivofoji tiketi za kuangalia mazingaombwe ya Eyeso, nilivosogeza saa mbele ili kuwahi mapumziko nikiwa time keeper na chai iliyonimwagikia baada ya kubinua meza mbele ya wageni, kisa???
 
mi nakumbuka kuna manzi alikua na shundu balaa nlivokua a lvl miaka ya tisini sasa ile kuimbisha imbisha nn manzi kaingia king afu mfukoni niko kapaa hamna pesa ya lodge........

plan b ikawa nimpigie hm tu maana kwao ilikua nyomi nyomi sa nkavizia bi mdashi kaenda job maana ni teacher home nabakigi na hg basi nkamtuma hg shop ile kasepa tu nkazamisha mzgo aisee kumbe bi mdashi alikua hayuko poa so akaomba ruhusa aje apumzke home na alikuaga na tabia ya kulala chumbani kwangu mchana ile anaingia tu akanikuta mzee ndo nko juu ndo nakaribia kufika........

aisee nlikula kipigo dushelele likanywea na safari ikaishia pale ila yule manzi ndo alipigwa mpk nkamuonea huruma aisee.........

wiki nzima nkawa sina hamu ya kumtazama maza usoni

Mkuu ulipigwa na bi mdashi ukiwa A level basi bi mdashi wako alikuwa mkali sana.
 
Back
Top Bottom