ROBERT MICHAEL
JF-Expert Member
- Oct 23, 2012
- 5,054
- 2,872
Semeni suuu..................!!!!
Suu.Mkuu unanikumbusha enzi hizo mkitaka kupigana lazima mpute mchanga chini.
Semeni suuu..................!!!!
Namshukuru Mungu mi sikuwa mtukutu. İla sitasahau nilivofoji tiketi za kuangalia mazingaombwe ya Eyeso, nilivosogeza saa mbele ili kuwahi mapumziko nikiwa time keeper na chai iliyonimwagikia baada ya kubinua meza mbele ya wageni, kisa???
Sitasahau siku ya kwanza kupiga punyeto...ilikua mtoni nimekwenda kufua....nijifungia ndani siku nzima kwa aibu na woga.....yaani kila saa nalichungulia dushe kama lipo. Na nguo niliziacha mtoni.
Semeni suuu..................!!!!
Semeni suuu..................!!!!
Semeni suuu..................!!!!
Sitasahau siku ya kwanza kupiga punyeto...ilikua mtoni nimekwenda kufua....nijifungia ndani siku nzima kwa aibu na woga.....yaani kila saa nalichungulia dushe kama lipo. Na nguo niliziacha mtoni.
Ilikua darasa la tatu miaka ya tisini Sinza kuna Maskani flani ya wavuta bangi (WAKUSH CAMP) Nilivutishwa bangi kwa mara ya kwanza na Mjomba wangu mdogo wake mama..Macho yalibadilika rangi yakawa kama matunda damu na kumbukumbu nikawa napoteza nikitaka kupiga story kufikia katikati nasahau nilichokua nakiongelea.Basi kufika home mama alichanganyikiwa natembea nikinyatanyata akiniita najificha eti nyuma ya ndoo wakajua malaria imepanda kichwani..nikakimbizwa Zahanati nikachekiwa malaria nikakutwa na mdudu mmoja nikapewa dawa na kufika home nikapewa huduma zote muhimu kuanzia chakula mpaka matunda na shule sikwenda wiki nzima.Na hii siri sikumwambia mtu yeyote mpaka leo hii naandika hapa
uliacha ama bado unaendelea?
Thats the point ...well said MentorAhahaha Rural Swagga naomba nikujibie hili swali, lol! Wewe kuacha bangi ni siku Tanzania tutaacha kutegemea misaada ya nje...
what doesn't kill you, always makes you stronger.....uliacha ama bado unaendelea?
Nakumbuka siku moja tulikuwa home bored, wakati huo dingi alikuwa amesafiri.
Tukasema ngoja tukaangalie mpira kwa jirani nakumbuka siku hyo ilikuwa fainali ya Yanga na Sc Villa ya Uganda.
Hatuna hili wala lile tukarudi home usiku kama wa saa 4 hivi, hamadi dingi yule pale kibarazani, hatujui amerudi sangapi.
Tulivyokuwa wajinga tukaendelea kujificha nyuma ya kisima kama nusu saa hivi, kwahyo tukaenda home kama saa 4;30
Ilikuwa balaa, tulipokea kichapo toka kwa baba na mama kwa mpigo, mbaya zaidi wakasema turudi tukalale tulipotoka.
Tulivyokuwa wajinga tukarudi kweli, tukawagongea wakatufungulia tukaliangusha.
Kuamka asubuhi tukasema ngoja turudi home inaweza kuwa shwari, ilikuwa afadhali ya jana, tukapigwa tena na tulitakiwa kurudi tulipotoka tukamlete alioturuhusu kulala kwake.
Tukamuita, dingi alimfokea mama wa watu utadhani mwanae, mara yule jirani yetu akapaniki akaenda serikali za mitaa kushitaki ametukanwa.
Dingi akaitwa akatupeleka na sisi, tulikaa nje wao wakaingia ndani kuyamaliza, tulikwa tunasikia wanafokeana balaa.
Walipomalizana tukawa tunarudi home huku tunachezea stiki, siku hiyo ilikuwa jehanamu kwetu.
Enzi hizo mshua na mama walikuwa kituo cha polisi. Ukifanya kosa mama anakuanzishia, baba akija wanakuanzishia upya, wanakupa stiki za haja.
Tulikuwa tunafuga mbwa home ,baba alikuwa na kawaida ya kila wikend akitoka job anarudi na furushi la mabaki ya vyakula vinono kwa ajili ya chakula cha mbwa...........siku hiyo nakumbuka alileta ukoko wa pilau ulokuwa umechanganyikana na mchuzi na mabakibaki ya nyama za kuku,baada ya shughuli zake akawa amewatengea wale mbwa kwenye chombo chao kila mbwa na sahani yake....... Bwana weeee nkaona mbwa wanafaidi, nkicheki pilau kula hadi xmas haa nkamtaimu mzee katoka tu pale nkazama kwa mbwa mmoja ye anakula huku mi huku .........kilichokuja kutokea baadaye nilishtukia nimedakwa juujuu nilichezea bakora nashukuru mama alikuwepo akaniokoa .........dah RIP my dadi jamani loh!!