Msukuma ni mgonjwa wa akili, kutoelewa kwake hoja ya Prop Mhongo ndiko kulikosababisha personal attack zake..
Speaker naye ni wakuaumiwa kwa kuruhusu bunge kufanya personal attacks na sio kujikita kwenye hoja. Speaker ndio msimamizi wa hii mijadala sasa kama anashindwa kusimamia na kuwa mshabiki kwa maslahi yake binafsi mbeleni huko tutapata shida..
Kuruhusu elimu inakejeliwa ndani ya Bunge na bunge linashangilia maana yake ni kuiambia jamii iachane na shule maana haina umuhimu wala msaada...effect yake ni kubwa kuliko tunavyodhania.
Awamu ya tano nayo ni ya kulaumiwa kwa kulazimisha watu watumie fikra za mtu mmoja na ukipingana naye basi wewe msaliti, sio mzalendo, mpiga dili, kibaraka nk.
Prop Mhongo aliwakilisha fikra zake na kuzitetea kwa ufahamu wake bila kumkejeli mtu, Msukuma kama hakubaliana alipaswa kuweka hoja zake mezani tupime na sio kufanya personal attack.