Siasa inavyoharibu elimu na kuwapumbaza wananchi

Kiranja wa jamii

JF-Expert Member
Jan 2, 2023
222
528
Karibu kila mwaka takwimu za wanaofaulu kutoka elimu ya sekondari kwenda vyuo vikuu na vya kati inazidi kuongezeka hii inaenda sambasamba na idadi ya wanaohitimu vyuo vikuu na vya kati kila mwaka wanaongezeka mtaani

Kuongozeka kwa ufaulu darasa la saba na kidato cha nne kila mwaka ni vema wadau waelewe kabisa kuwa sio kwamba kizazi hiki kina akili sana! La hasha!

Kwanza walimu wanapewa maelekezo maalumu ya usahihishaji. Fanya uchunguzi binafsi kwa walimu wanaosahihisha mitihani ngazi ya NECTA

Pili mitihani ya siku hizi ni rojo rojo sana! Ukilinganisha na mitihani ya miaka kadhaa nyuma utacheka mwenyewe

Hali hii imepelekea kushuka kwa taaluma za vyuo vikuu. Kulibaini hili angalia wahitimu wetu lakini pia chunguza wahadhili wa vyuo vikuu

Matokeo ya haya yote ni nini?

Taifa linazalisha vijana wasioweza kuhoji chochote. Leo NHIF inazozana na vituo binafsi vya kutolea huduma za afya kwa ubadhilifu walioufanya wenyewe wa kujikopesha zaidi ya Bil.41 za michango ya wanachama halafu mzigo wanatafuta wa kuwatwisha badala ya kulipa.

Wachangiaji wa NHIF ni wasomi lakini hawana uwezo wa kuhoji haki yao. Waziri wa afya anajiongelesha tu kwasababu anajua hakuna raia wa kumuhoji chochote na kushinikiza aachie ngazi

Leo wasitaafu wanaandaliwa kikokotoo ambacho kitawaacha na fedha kiduchu ya pensheni. Hapa wanafidia pengo lililosababishwa na kujikopesha pesa za NSSF kujenga UDOM. Wanafanya haya kwasababu wanajua hakuna wenye nguvu za kuhoji

Taifa limeua elimu na sasa shule, vyuo vikuu na vyuo vya kati vinazalisha machawa wa wanasiasa na viongozi ambao kila kitu ni ndioo na kusifia ujinga.

Dharau ya serikali kwa wananchi inazidi kuwa kubwa kwasababu wanafahamu walishaua ubongo tayari.

Hata hivyo, hatima ya yote haya ni Taifa kuanguka kwa wasiowaaminifu na kutawaliwa kama familia ya mtu
 
Sisi ambao tumemaliza elimu ya msingi miaka 90 tunajua Hali ya elimu kipindi kile
Ilikuwa IPO juu Sana tofauti na Miaka hivi karibuni hata waalimu walikuwa deep mno na masomo wanayofundisha..
Nahisi baada ya vyuo vikuu kuanza kuwa vingi hapa ndipo elimu yetu ilianza kushuka.

Hata wanasiasa pia hawa ndiyo wamechangia kuuwa elimu ya Tanzania
 
CCM INAANDAA TAIFA LA WASOMI WAJINGA ILI IWE RAHISI KUTAWALIKA NA IMEANZA KUFANIKIWA KWA WASOMI WETU KUGEUKA MACHAWA WA KUSIFIA VIONGOZI KWA KUTEGEMEA KUTEULIWA
 
Elimu ya siku hizi haina quality ndo maana waajiri wanalalamika wahitimu wengi wapo empty headed
Hapa mimi binafsi huwa napenda sana kupima kwa kuangalia ufaulu wa kidato cha pili kwenda cha tatu.

Miaka ya nyuma (sio mbali sana, nadhani hadi miaka ya 2012) kuingia kidato cha pili iliamuliwa kwa wastani wa 30. Yaani angalau katika masomo saba ya msingi mwanafunzi apate alama 30. Lakini siku hizi pamoja na siasa kuingia kwenye utunzi na usahihishaji wa mitihani, lakini vigezo vimeshushwa.

Mwanafunzi anapita kuingia kidato cha tstu kwa kupass masomo mawili kwa alama 30 (yaani D mbili) au hata akipata alama 45 ya somo moja tu na mengine yote sita akapata F yeye anakuwa ameibuka kidedea. Ufaulu wa hivi umefichwa ndani ya kitu wanachoita "DIVISION"

Kuna vitu vingi vinaendelea katika sekta ya elimu ukiviangalia unaweza kusikitika sana
 
Yajayo ni magumu sana na hata hvo bado mtaala haupo sawa
 
Back
Top Bottom