Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,488
- 13,608
Mheshimiwa Msukuma amepata umaarufu mkubwa siku za karibuni haswa kwa kumkejeli Profesa Muhongo mwenye kuamini kwamba umeme wa gesi ni suluhisho la suala zima la nishati hiyo. Ni mawazo ya Profesa Muhongo na anao uwezo wa kuyatetea kwa hoja kila anaposimama na kuongea bungeni.
Naona kama Msukuma anakwenda mbali sana anapoamua kumkejeli Profesa na akawaweka katika kundi moja maprofesa wote kwa kigezo cha kutokubaliana tu na mitazamo yake. Ujinga ni mzigo mzito sana na upo uhakika hao mabilionea na mamilionea wanaojulikana kila kona wanawategemea wasomi wenye elimu za juu.
Tutakuwa tunapotea kama Taifa tukianza kukubaliana na dhana hizi za darasa la saba kuwa na manufaa na mafanikio kiasi cha wenye elimu kubwa kuanza kuonekana hawana maana. Ni kosa kubwa sana tutakuwa tunalifanya.
Wanaokesha usiku ndani ya maabara kubwa za mataifa yaliyoendelea wakitafuta kila aina ya chanjo dhidi ya Covid19 ni wasomi wa viwango vya juu. Na matokeo ya elimu zao wameanza kuzaa matunda kwani miezi michache ijayo dunia kwa maana ya ile ya watu kuchanganyika wakifanya shughuli mbalimbali itaanza kurudi kama ilivyokuwa zamani.
Wanaoandika ilani na kuwawezesha wagombea wanaopanda majukwaani ni wataalam wa fani mbalimbali. Hivyo Msukuma kuwepo kwake mle bungeni ni matunda ya hao hao wasomi anaowakejeli kisa tu ametofautiana kimtazamo na Prof Muhongo.
Ujinga kama alivyowahi kusema Hayati Mwalimu Julius Nyerere pale Karimjee miaka ya nyuma ni sawa na uchi wa akili. Ndio sababu hata wanamichezo ambao wanafanikiwa wakiwa na elimu ndogo, wakishapata pesa za kutosha huamua kutafuta elimu ambayo waliikosa hapo kabla, lengo ni kuuvalisha nguo ubongo.
Wenye elimu ya darasa wanaoweza kufika alipofika Mheshimiwa mbunge Msukuma ni wachache sana. Na sekta zetu nyingi zimekuwa zikikwama kwa kukosa maarifa sahihi ya wakati husika. Uendeshaji wa taasisi zetu nyingi ukiuchunguza kwa undani unagundua upungufu mwingi unaotokana na elimu kuwa ni ndogo pamoja na wahusika kukosa ufahamu mpana wa kitu wanachokifanya, wanakosa exposure.
Nimemuelewa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu kumkabidhi wizara ya mambo ya nje Mama Liberata Mulamula, anataka aitumie exposure yake kubwa katika kujenga taswira chanya ya Tanzania kimataifa. Inakuwa ni aibu unapomsikia mbunge anakejeli elimu wakati ndio silaha namba moja ya mataifa yaliyoendelea.
Kejeli anazokutana nazo Prof Muhongo zinawahusu pia maprofesa wengi ambao wamefanya mengi ya maana na yenye kuonekana kwa faida ya taifa. Ni mawazo fulani duni kuiponda elimu eti kwa sababu ya kutofautiana mitazamo na msomi mmoja