Tuandamane Aisee! Ubungo Tanesco Isivunjwe...

Tuandamane Aisee! Ubungo Tanesco Isivunjwe...

Jengo siyo LA umma,tanesco ni mpangaji

Cha msingi ni kusema bora uandamane tanesco wapate jengo lao ili wasiendelee kutumia fedha ya umma Kwa ajili ya kulipa pango kwenye jengo ambalo siyo LA umma
 
Kuna Taarifa zinazagaa sasa kuwa gorofa la Tanesco Ubungo litavunjwa kupisha flyover na Jengo la wizara ya maji pia litavunjwa.

Huu ni upotevu wa kodi ambazo ni pesa zetu...
Tuandamaneni kuzuia uharibifu usiokuwa wa lazima aisee...
Hapo tunapoteza zaidi ya Bilion 60.
Hapa kuna kila sababu sasa tupate uchungu na mali zetu...pengine zinabomolewa kulipizia kisasi tu...
Unaandamna kupinga jengo la Bilioni 60 lisivunjwe,unajua serikali itaingiza kiasi gani kwa kuwa na hiyo flyover..??
 
Aliyetoa kibali cha ujenzi anastahili adhabu kali!! Halmashauri haikujua ni sehemu ya barabara? Hasara yote alipe mhusika aliyeaminika na serikali kwa kutoa kibali cha ujenzi.
Hapo sasa utakapogundua kwamba mwenye jengo ndiye aliyeamrisha kwa njia moja au nyingine kibali kitolewe cha ujenzi
 
Kwani lile jengo ndimo mlimo na mitambo ya kuzalisha umeme?
Wananchi wanyonge wamevunjiwa hujaandamana, avunjiwe Rostam Azizi uandamane wewe!
Hata pale Tanesco hawakuwa wanakaa bure, walipanga hivyo watapanga sehemu nyingine.
Note: ubomoaji wa kupisha ujenzi wa reli karibia zoezi zima litatutia hasara.
 
Badala ya kuandamana bei ya unga wa mahindi ishuke ili uweze kuipatia familia yako hata milo miwili ya uhakika kwa siku! Wewe unataka kuandamana jengo la Tanesco lisivunjwe,wakati umepanga kwenye chumba hakina hata umeme!
Nenda kaandamane mkuu. MOI wameleta kontena za vyuma vya kuungia mifupa,haswa wa ugoko.
 
Watanzania kuna ulazima mkubwa kufanya maandamano yanye lengo la kulinda masilahi ya nchi yetu na kwa vizazi vijavyo, haiwezekani viongozi wa serikali kila siku ni matamko yanayolenga kujipatia popularity na wala si kuleta maendeleo kwa taifa. Haiji akilini raisi kutamka jingo la tannesco livunjwe wakati limeghalimu kodi za wananchi mnaowaita wanyonge at the same time jengo lile limejengwa na mamlaka ya serikali ambao hadi sasa wanasuasua kuwalipa wastaafu wanaodai mafao yao kwa kukosa pesa na wakati huo huo walifanya environmental impact assessment kuangalia wapi kuweka jingo kulingana na umbali kutoka barabarani, je PPF na mhandisi aliyeshinda kandarasi hiyo hawakufanya environmental impact assessment.

Ikumbukwe mkuu wa mkoa paul makonda alidai kwamba washamaliza maandalizi ya kujenga stend mpya kule mbezi mwisho kwa ajili ya mabasi yanayotoka kaskazini na pia kule mbagala kwa mabasi yanatokea kusini sasa kama huo ndio mpango iyo foleni ya mabasi itatokea wapi adi kuleta shida kwenye jengo ambalo hata ile return on investment harijarudisha?

Huu mtindo wa kuchezea kodi za watanzania kuanzisha miradi ambayo haimalizi japo hata miaka 10 ikioperate utatuletea maendeleo gani? Najiuliza tu kama kila mtawala atakuja na kutimiza matakwa yake na si ya maendeleo ya nchi tutaishia wapi?

Kwanza serikali inatakiwa ututake radhi wananchi kwa kuchezea kodi zetu kama stendi ya ubungo inahamishwa kulikuwa na ulazima gani kuweka madaraja ya juu pale wakati pesa hizo zingeelekezwa kwenye miradi yenye tija kwa taifa.
 
Linavunjwa kupisha flyover pale, foleni ya pale kila siku inakula ela nyingi kwa upotevu wa mafuta ambayo kwa mwaka ni bilions of money.
Solution wakaja na flyover na ili ijengwe lile jengo linabidi liondoke.
Kuliko kulalamika ungeonyesha njia mbadara la jengo kubaki lakini foleni ikaondolewa.
Opportunity cost....
 
Kwani wewe unaingiliwa na nini likivunjwa au na wewe ulikilikuwa mpanda lift kwenye hilo jengo
hii serikali inafaa kushitakiwa ni kwanini walilijenga hilo jengo maeneo yale ........
limetumia mapesa ya kutisha na linavunjwa kipuuzipuuzi tu, ifike mahali serikali iwe na yenyewe inashtakiwa maana wao wenyewe walichota mapesa kujenga na sasa wanachota kulivunja

maana yake hapo itatumika pesa nyingine ya kujenga nyumba kama hii hii watumie kodi zetu y?

nani alihusika kwanini tusiwashitaki kwanini walijenga mahali ambapo si sahihi ?
 
Hii inawezekana ikawa ni ngumu kuingia akilini kwa wengi, ila ndo hivyo imeshasemwa na imeshaagizwa. Kama ni mpirani tunasema refa ameshapiga filimbi, mpira uwekwe kati.

Raia namba moja ameagiza jengo la Tanesco pale Ubungo livunjwe, ili kupisha mradi wa barabara za juu (interchange).

Binafsi nadhani fidia ya jengo, kuvuruga kwa mitambo iliyopo pale Tanesco, re-erection ya jengo jingine (kwa sababu ni lazima wapate sehemu nyngn ili waendeleee na kazi), pamoja na shida nyngn nyingi, gharama zake ni kubwa sana kuliko wale ndugu zetu wa Mwanza waliopewa favor ya kutokubomolewa nyumba zao. Sidhani hata kama fidia yao itafika robo ya gharama za Tanesco na idara ya maji.

Concern yng ipo kwa hao Tanesco na gharama ambazo serikali itaingia.
 
Mimi naona kama halinihusu vile. Sijui kwa kuwa sioni direct benefit nayoipata kutoka huko? Lakini bora hata barabara zikijengwa nitakuwa napita
 
hii serikali inafaa kushitakiwa ni kwanini walilijenga hilo jengo maeneo yale ........
limetumia mapesa ya kutisha na linavunjwa kipuuzipuuzi tu, ifike mahali serikali iwe na yenyewe inashtakiwa maana wao wenyewe walichota mapesa kujenga na sasa wanachota kulivunja

maana yake hapo itatumika pesa nyingine ya kujenga nyumba kama hii hii watumie kodi zetu y?

nani alihusika kwanini tusiwashitaki kwanini walijenga mahali ambapo si sahihi ?
Mkuu je wale walio vunjiwa nyumba zao na hilo jengo kipi kinakuuma zaidi?
 
Kila jambo lina faida na hasara.
Muhimu kama limejengwa nje ya 22.5m na kuanzia 2007 kurudi nyuma muhusika apewe compasation stahiki.

Na kama ni jengo la Tanesco watakuwa washaandaliwa eneo jingine.
Wahusika wameona lishuke lishuke tu,no discussion.
Tumewaamini tuwaache wafanye wanachokiamini.
 
Kuna Taarifa zinazagaa sasa kuwa gorofa la Tanesco Ubungo litavunjwa kupisha flyover na Jengo la wizara ya maji pia litavunjwa.

Huu ni upotevu wa kodi ambazo ni pesa zetu...
Tuandamaneni kuzuia uharibifu usiokuwa wa lazima aisee...
Hapo tunapoteza zaidi ya Bilion 60.
Hapa kuna kila sababu sasa tupate uchungu na mali zetu...pengine zinabomolewa kulipizia kisasi tu...
Watanzania watanzania watanzania, watu wamevunjiwa nyumba zao eneo lote hilo hadi kibaha. Watu wamekosa makazi na hadi leo wamekuwa ni wakuhifadhiwa na ndugu na jamaa kutokana na 'utekelezaji wa sheria' leo hii wanatokea watu wanatetea kuhusu utekelezaji huo huo wa sheria kwa jumba la umma. WHAT HYPOCRISY
 
Ngoja ivunjwe huenda ile baatani ya kukatika umeme inaweza ikafikiwa kulingana ilivyojifukia
 
Mm kinachoniuma ni kwamba lile Jengo ilikuwa alama yangu mm wa mkoani ,nlkuwa nkishaliona tu namwambia mwenyej nshafika Ubungo ss si watanipoteza hawa
 
Back
Top Bottom