Tuache utani jamani, where is Nchimbi?

Wewe wasema. Neno laki sio Sheria. Kama kafukuzwa kama mbwa ndio apewe ulinzi na serikali? Saa zingine tuangalie mambo kama yalivyo siyo nadharia
 
Kama wa nyumbani kwake wako kimya kiasi hiki ina maana yuko salama huko aliko.
Tofauti na hivyo tungesikia malalamiko I kama ilivyo kwa ndugu zake Polepole.
Nchimbi alikua kiongozi bwana lazma wananchi waulize sio kuwaachia familia ya nchimbi waanze kuuliza wakati na wao ni raia tu tena usikute wapo humu nao wanauliza hivi hivi nchimbi yuko wapi?

Kuna mdau humu juzi kaleta uzi wa mkuu wa mkoa wa dar kuagiza familia ya bwana nani sikumbuki, ikamatwe yoote, wakikamatwa wote kwao pakabaki patupu majirani wasiulize hyo familia ilipo?

Familia itaulizaje wakati yote imekamatwa na mkuu wa mkoa?

Sijui nimeandika nini hapo!

#kaso
 
Punguza ujuaji. Nani alikuambia anapewa miezi sita? Sheria Gani hiyo?. Mtu kafukuzwa chama kama mbwa Bado mnadai analindwa na serikali.
 
Ukimya wa familia yake unatia shaka kwamba hakuna hata mmoja anaeweza kusema lolote au ndo michezo yao ya kiccm baadae Imma anaibuka shujaa anasamehewa na chama 2030 bendera mabegani wapinzani chali
Watakuwa wanafanya utoto wao wenyewe. Kama wanaweza kupigisha kura milioni 31, Nini kiwafanye watumie njia ndefu sana.
 
Alisusa au alifukuzwa? Nadhani alifukuzwa.
 
Hujui. Kasome vizr mara baada kutoka Dodoma Aboud Jumbe alikuwa wapi.
Sisi wengine wala hatuoni tofauti kinachotokea kwa Nchimbi na ilivyotokea kwa Jumbe tu baada ya wawili hao kutoka kwenye Umakamu
 
Hujui. Kasome vizr mara baada kutoka Dodoma Aboud Jumbe alikuwa wapi.
Sisi wengine wala hatuoni tofauti kinachotokea kwa Nchimbi na ilivyotokea kwa Jumbe tu baada ya wawili hao kutoka kwenye Umakamu
Jumbe alinyang'anywa ndege ya serikali akaenda Kigamboni Mjimwema, lakini pia alienda Migombani Zanzibar kuonana na wake zake.

Zaidi, hata kama kinachoyokea ni kile kile, what is your point? Kwamba ni sawa tu kitokee kwa sababu kilikwishatokea?
 
Hivi hivi, kimasikhara aliyekuwa katibu mkuu na makamu wa rais haonekani, haijulikani yuko wapi. Hii inakuwaje?. Maisha yanawezaji kuwa normal wakati hali ni abnormal?.
Taifa lina haki ya kuelezwa Nchimbi yuko wapi?
Alifanya kosa la Kipumbavu sana na la Kiufundi mno kuanzisha Vita akiwa ndani ya Mfumo ambao si tu Unamjua bali Unammudu pia. Naomba niishie hapa tafadhali.
 
Wewe unaongelea kutembelewa Kigamboni, hiyo ni baada ya miaka minigi tu. Hata Nchimbi atatembelewa tu. Issue je Abood Jumbe alitolewa leo kesho yake watu wakaenda kumtembelea?
Sijui miaka mingi inaanzia mingapi, mimi nimemuona Jumbe mwaka 1987. Sikuona dalili zozote za mtu aliye kizuizini.
 
Sijui miaka mingi inaanzia mingapi, mimi nimemuona Jumbe mwaka 1987. Sikuona dalili zozote za mtu aliye kizuizini.
Yaani ulimwona miaka mitatu baadye. So kwa Nchimbi tusubiri at least mwaka mmoja tu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…