Mwanahalisi: Nchimbi agoma kujiuzulu

Mwanahalisi: Nchimbi agoma kujiuzulu

Parabolic

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2013
Posts
2,880
Reaction score
3,168
Screenshot 2026-08-06 134528.png

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Emmanuel Nchimbi, "amegoma kujiuzulu," kwa mujibu wa gazeti la Mwanahalisi.

Taarifa mikononi mwa gazeti hilo zinasema, Dk. Nchimbi amekuwa akikabiliwa na shinikizo la kumtaka kujiuzulu wadhifa wake, kufuatia kuibuka kwa madai ya kutoelewana na bosi wake, kuchonganisha chama chake na wananchi, kutoa kauli zinazozusha taharuki kwa jamii na kuondosha umoja serikalini.

"Huyu bwana amekuwa katika shinikizo kubwa la kumtaka ajiuzulu, lakini amekataa kuachia ngazi. Amesema, hana kosa na hajatenda kosa lolote linalomfanya afikie uamuzi huo," kimeeleza chanzo cha taarifa kinachofahamu kwa undani suala hilo.

Alipoulizwa iwapo kuna uwezekano wa Dk. Nchimbi kuridhia kujiuzulu, mtoa taarifa huyo amesema,

"...kwa jinsi ninavyomfahamu, sioni kama hilo litawezekana. Ninamfahamu vizuri Nchimbi. Simwoni akichukua uamuzi huo.

Bali aliyekuwa kiongozi mwandamizi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na sasa ni mjumbe wa Halmashauri ya Taifa (NEC) ya chama hicho, amemweleza mwandishi wa gazeti hilo kuwa hakuna namna ambayo Makamu wa Rais Dk. Emmanuel Nchimbi anaweza kusalimika kuondolewa kwenye wadhifa wake.

"Amesha elekezwa kibla. Ni lazima atachinjwa. Ninavyoifahamu CCM, uwezekano wa Nchimbi, kujinasua na kitanzi hiki ni mdogo sana," ameeleza mwanasiasa huyo.

Anayetajwa kumfikishia Makamu wa Rais ujumbe wa kujiuzulu ni kigogo mmoja mwandamizi serikalini. anayedaiwa kuwa yuko karibu na kiongozi huyo.

Taarifa hizi zimepatikana, wiki moja, baada ya wajumbe wa NEC, waliokutana mjini Unguja, kuridhia pendekezo la kumfikisha Makamu wa Rais huyo, kwenye Kamati ya Maadili.

Hoja ya kutaka Dk. Nchimbi kufikishwa Kamati ya Maadili, illtolewa na Paul Makonda, mjumbe wa NEC, kupitia kapu la wabunge wa CCM.

Akizungumza kwenye mkutano huo, Makonda alisema, “Mheshimiwa mwenyekiti, huyu Emmanuel Nchimbi, anatuvuruga sana. Amekuwa akitoa kauli zinazokwenda kinyume na mwelekeo wa serikali na chama chetu.”

Akaongeza, "Ninayo mifano zaidi ya sabini, lakini kwa leo, nitataja mitatu. Moja, ni kauli yake ya juzi ya kutaka wananchi wapambane kupata Katiba mpya."

Akahoji, "Unawataka wananchi wapambane kupata Katiba mpya, ili iweje na wapambane na nani?”

Alisema, akiwa ziarani nchini Ufaransa alikutana na kiongozi mmoja wa viongozi wanaongoza mashirika ya kimataifa na kumweleza kuwa Maria Sarungi, mwanaharakati wa Tanzania aishiye uhamishoni nchini Kenya, alimhakishia kuwa amepata ushahidi wa mauaji yaliyotokea nchini.

Alisema, "Mwenyekiti, mimi nilikuwa kule Ufaransa. Nilikutana na kiongozi mmoja wa kimataifa, akanithibitishia kwamba huyu Maria Sarungi, ambaye Emmanuel Nchimbi, anasema anatamani kufanya naye kazi, amemhakikishia kuwa anao ushahidi wa matukio ya 29 Oktoba.

Akaongeza, "Kauli za Emmanuel Nchimbi, zinanipa wakati mgumu sana wa kutekeleza majukumu yangu ya uwaziri. Unawezaje kusema unatamani kufanya kazi na watu wanaovuruga serikali kila siku? Haiwezekani. Hayo mapenzi yanatoka wapi kama siyo kutaka kutuvuruga? Naomba huyu Emmanuel Nchimbi, afikishwe Kamati ya Maadili.”

Makonda alienda mbali zaidi akasema, kitendo cha Nchimbi, wakati akiwa katibu mkuu wa chama hicho, kumtetea John Mnyika, katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), wakati wa mauaji wa Ally Mohamed Kibao, kilichangia kuzorotesha uchunguzi.

“Mheshimiwa mwenyekiti, Nchimbi akiwa katibu mkuu wa CCM, aliwahi kutoa kauli tata iliyomtetea Mnyika, kwamba hahusiki na mauail ya Kibao. Eti anavyomfahamu Mnyika, hata panya anamwogopa. Kauli yake hii, imesababisha hata vyombo vya dola, kushindwa kufanya uchunguzi,” alieleza.

Ni baada ya kauli ya Makonda, ndipo mwenyekiti wa kikao, Rais Samia akahoji wajumbe na kuridhia hoja ya kumfikisha Makamu wa Rais, Kamati ya Maadili, inayoongozwa na Stephen Wassira, makamu mwenyekiti wa chama hicho, Tanzania Bara.

Kwa mujibu wa katiba ya CCM, mara baada ya Kamati ya Maadili kumaliza kumhoji Dk. Nchimbi, Sektarieti ya chama hicho, Itawasilisha taarifa na mapendekezo, mbele ya Kamati Kuu (CC).

Nayo Kamati Kuu, baada ya kupokea na kujadili mapendekezo kupokea ya Kamati ya Maadili, yaweza kufikisha suala hilo NEC na kwamba, iwapo bado Dk. Nchimbi ataendelea kung'ang'ania kiti chake, huku wanaotaka ang'olewe wakiendelea na msimamo huo, suala hilo linaweza kufikia uamuzi wa kupigiwa kura.

Miongoni mwa adhabu anazoweza kupewa, ikiwa atapatikana na hatia, ni pamoja na onyo, karipio au kufukuzwa uanachama.

Hata hivyo, Ibara ya 103 ya Katiba ya chama hicho, pamoja na kuwa na uwezo wa kumwachisha au kumfukuza uongozi, kiongozi yeyote wa chama hicho, lakini uteuzi wa mwisho wa kiongozi huyo, uwe umefanywa na NEC.

Uteuzi wa Makamu wa Rais ambaye alikuwa mgombea mwenza wa Rais aliyepo madarakani, hufanywa na mkutano mkuu, jambo linaloweza kusababisha sakata la Nchimbi kufikishwa kwenye mkutano mkuu

Ibara ya 128 ya katiba ya chama hicho, imeweka utaratibu wa kufikia uamuzi. Kwamba utafikiwa kwa kufuata makubaliano ya jumla au wingi wa kura za wajumbe waliohudhuria na kupiga kura za siri.

Aidha, kabla ya suala hili kufikishwa kamati kuu, linaweza kufikishwa kwenye Baraza la Ushauri la Viongozi Wakuu Wastaafu.

Baraza hilo linaloundwa na marais wastaafu wa Jamhuri ya Muungano na Zanzibar, pamoja na makamu wa wenyeviti wastaafu wa chama hicho, limepewa mamlaka ya kutoa ushauri kwa CCM na serikali zake.

Vile vile, Ibara ya 123 (3) ya Katiba ya CCM inasema, "Kwa madhumuni ya kutoa ushauri katika jambo mahususi, wajumbe wa baraza hilo, wanaweza kualikwa, ama wote kwa pamoja au kwa mwakilishi wao, kuhudhuria vikao vya ngazi za taifa pale ambapo busara zao zitahitajika. hususan katika masuala muhimu na nyeti

Akifungua mkutano mkuu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu nchini (THRDC), jijini Dar es Salaam, Dk. Nchimbi aliwataka wananchi, kupigania upatikanaji wa Katiba mpya

Alisema, kama angepewa nafasi ya kuwaambia Watanzania jambo moja tu, angewaambia, "Pambaneni mpate Katiba mpya,” na akaongeza, haki za binadamu si suala la sheria pekee, bali linagusa maisha ya kila siku ya kila Mtanzania.

Kauli ya Makamu wa Rais, imekuja katikati ya shinikizo la wananchi kutaka kuwepo kwa Katiba mpya na mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi, mambo yanayotajwa kuchangia kuwapo kwa maandamano ya 29 Oktoba mwaka jana.

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema, hoja ya kutaka kumchomoa Nchimbi kabla ya kumaliza muda wake, inasukumwa na mbio za urais kuelekea 2030 kwa kila kundi kutaka kulidhoofisha jingine.

Huyo Makonda, ambaye pia ni Waziri wa Habari, Michezo na Utamaduni, inadaiwa yuko kambi ya urais ya Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Lameck Nchemba.

Tayari hoja ya sasa, imeanza kuchukua sura ya U-Zanzibar na U-Tanganyika, kufuatia madai ya usaliti dhidi ya Dk. Nchimbi, kuibuliwa kwa mara ya kwanza na Simai Mohamed Said, mbunge wa Bunge la Muungano, kutokea Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

Akichangia bajeti ya wizara ya fedha, bungeni mjini Dodoma, tarehe 5 Juni 2026b, mwakilishi huyo wa Tunguu, Unguja, alidai kuwa ndani ya serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan, "kuna Yuda anayesaliti dhamira yake.

Simai hakutaja jina la aliyemuita Yuda, lakini wote waliomkabili mbunge huyo, akiwamo mbunge wa Tarime Vijijini (CCM), Mwita Waitara na Jacqueline Msongozi, mbunge wa Viti Maalum, kutokea mkoani Ruvuma, walimtaja Dk. Nchimbi.

Alisema, kiongozi huyo aliyeaminiwa na rais na kisha kugeuka Yuda, amekuwa akitumia nyumba za ibada na jina la John Magufuli, kutafuta uungwaji mkono kwenye safari yake ya kisiasa, hali Inayotajwa kuwa chama hicho, kina wakati mgumu…

Chanzo: Mwanahalisi.

Pia soma: Dkt. Nchimbi: Hakuna sheria inayotengua Katiba. Watanzania pambaneni kupata Katiba mpya
 
View attachment 3644324
Makamu wa kisha kugeuka Yuda, amekuwa akitumia nyumba za ibada na jina la John Magufuli, kutafuta uungwaji mkono kwenye safari yake ya kisiasa, hali Inayotajwa kuwa chama hicho, kina wakati mgumu…



Chanzo: Mwanahalisi.
Hii mivurugani itakuwa ni matokeo ya damu ya Oktoba 29. Tusipotubu, hakika tutaendelea kuona mivurugano mpaka tutakapotubu kama taifa mana damu ni nzito kuliko maji!
 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Dk. Emmanuel Nchimbi, "amegoma kujiuzulu," kwa mujibu wa gazetui la Mwanahalisi.


Chanzo: Mwanahalisi.

Pia soma: Dkt. Nchimbi: Hakuna sheria inayotengua Katiba. Watanzania pambaneni kupata Katiba mpya
Hapo mama teuzi zake za kina Yûpo tu atatuwekea konda makamu. Natumaini kama hii habari sio uzushi Nchimbi hatakubali kujiuzulu kwani anasema kweli. Mama haoni wala haelewi maana itikadi yake ni kula kwa urefu wa kamba halafu ameng'ang'ana kuongoza chama cha kijamaa. Yeye uongozi kwake ni kazi tu kupata riziki na kupiga hela. Tanzania wanataka marais wenye maono; maarifa; wazalendo, na jasiri. Ujasiri wa kupora uchaguzi ndani ya chama chako na uchaguzi mkuu sio ujasiri wanaotaka umma wa wananchi.
 
Emmanuel Nchimbi anayo nafasi nzuri na adhimu sana ya kujijengea heshima ndani ya taifa hili.

Hii ni fursa ya kipekee kabisa aliyonayo kama atajuwa namna ya kuitumia ipasavyo.

Natumaini hatateteleka. Awe mtulivu tu, na ajue namna ya kuwakabili hawa watu waovu kabisa waliowahi kutokea katika taifa hili.
 
Emmanuel Nchimbi anayo nafasi nzuri na adhimu sana ya kujijengea heshima ndani ya taifa hili.

Hii ni fursa ya kipekee kabisa aliyonayo kama atajuwa namna ya kuitumia ipasavyo.

Natumaini hatateteleka. Awe mtulivu tu, na ajue namna ya kuwakabili hawa watu waovu kabisa waliowahi kutokea katika taifa hili.
Huenda ana backup ya kutosha najaribu kurejea ile kauli ya yule jamaa aliyesema mkutanoni Mgombea awapishe wanachama wajadili zawadi yao kwake lakini mgombea akagoma
 
Huenda ana backup ya kutosha najaribu kurejea ile kauli ya yule jamaa aliyesema mkutanoni Mgombea awapishe wanachama wajadili zawadi yao kwake lakini mgombea akagoma
Pamoja na ubovu ilioufikia CCM; siamini hata mara moja kwamba ndani ya chama hicho hawamo waTanzania wanaoumizwa sana na hali ilivyo sasa katika taifa hili.

Kama waTanzania hawa watashindwa angalau kujipanga nyuma ya huyu mmoja anayejaribu kuonyesha uthubutu mbele ya Genge lililokiteka chama chao, hawa wanaCCM tuwaelewe vipi?

Hii ni fursa nadra sana inayojitokeza kwao kuanza kukiokoa chama chao; maana sioni ni jinsi gani CCM itaendelea kwa mtindo huu unaotumiwa sasa hivi na hili Genge chini ya Samia.
 
Ni ngumu sana kuhimili vita ya nje na ndani. Werevu ni kuchagua vita lakini ukiamua kupigana vita zote hakuna historia ya yeyote kushinda.

Kwasasa hakuna utayemshauri aelewe! Lakini huu moto tunaochoma joto lake litatuunguza wenyewe! Daima usiache hekima nyuma.
 
Back
Top Bottom