Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefafanua msimamo wake kuhusu hatua zilizochukuliwa dhidi ya aliyekuwa Katibu wa Chama na Makamu wa Rais Dkt. Emmanuel Nchimbi.
Akizungumza katika mahojiano ya Medani Kuu na Mwandishi Edwin Odemba, Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (Itikadi, Uenezi na Mafunzo), Kenani Kihongosi, ameeleza kuwa kauli zilizotolewa na kiongozi huyo kabla ya kuondoka madarakani zikiwataka Watanzania kupigania Katiba Mpya hazikuingiliana moja kwa moja na taratibu za kikatiba za chama.
"Kiongozi anaposema wananchi wapiganie Katiba Mpya—Katiba Mpya ipiganiwe? Inapiganiwaje?, Chama Cha Mapinduzi kina ilani na jambo la Katiba lipo ndani ya ilani. Wajibu wa kiongozi, Baraza la Mawaziri na Waziri Mkuu ni kutekeleza ilani; sasa unaposema tukapiganie tena maana yake unataka kujenga kitu ambacho hakieleweki."
Kihongosi ameongeza kuwa ingawa kila mtu ana haki ya kutoa maoni yake, viongozi wana wajibu wa kusimamia mambo yanayokubaliwa kwa pamoja badala ya kutoa kauli zinazokiuka misingi hiyo katika mihadhara ya umma.
Kuhusu alipo Dkt. Emmanuel Nchimbi, ambaye hajaonekana hadharani tangu alipowasilisha barua yake ya kujiuzulu, Kihongosi amesema kuwa kuonekana au kutokuonekana kwa kiongozi ni uamuzi wake binafsi na si jambo linalopaswa kutafutwa na chama.
"Mimi binafsi sijui yuko wapi lakini naamini yupo," amesema Kihongosi.