TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Mkonga mnao nyie lakini tamaa, usimamizi mbovu, business plan mbovu, hamna vifurushi vizuri, bei za ajabu, broadband bei juu, mngekuwa mbali sana kwani ni kampuni ya zamani na ni yetu lakini mnaenda enda tu!
 
Jamani hamieni Airtel hiyo menu ili kuipata ni *149*99*5# alafu unachagua 1 smartika. Thank me later.
Screenshot_20210207-202935_Phone.jpg
Screenshot_20210207-203425_Phone.jpg
 
Nyumbani hakujanoga tena bali kumedoda !!!!!!!!!
Aisee nimeingia Mjini leo toka porini huko nimekuta :-
Hakuna tena toboa tobo ya kushushia mizigo, Bandika bandua nayo nikijaribu kuunga kile cha 10GB kwa 2500 napata ujumbe " sorry,your input is invalid" wamekiacha kile cha 4GB tu.
Nikasema niende Boom nako wanakupa 350M kwa Jero japo kwenye Menu wanasema ni 600MB ,
 
miundo mbinu yenu, Imekuwa ni kkwazo kwa watumiaji wa barabara

Eneo: Chuo cha Teku, Mbeya.

Hii ni jana, Ngazi iliwekwa kati kati ya barabara kushikilia cble

1612956589359.png





Hii ni leo, Magari makubwa yanapata changamoto


2.PNG


 
Nilinunua vocha za ttcl za tshs5000 ikiwa za 2000 zipo2 na tsh1000 ipo1,hii ya tsh 1000 ilikubali kuingia kama salio hizi zingine zimegoma,toka trh 2feb21 hadi sasa nishaongea na huduma kwa wateja zaidi ya mara nne jibu lao ni vocha zilikuwa hazijaidhinishwa kwa ajili ya matumizi.hivyo tatizo hilo wataripeleka sehemu husika baada ya saa24 zitakuwa tayari kwa matumizi,toka 2feb21 hadi leo hizo saa 24 bado?pia mtaingiza vp vocha sokoni kabla hazijawa verified?
 
Nilinunua vocha za ttcl za tshs5000 ikiwa za 2000 zipo2 na tsh1000 ipo1,hii ya tsh 1000 ilikubali kuingia kama salio hizi zingine zimegoma,toka trh 2feb21 hadi sasa nishaongea na huduma kwa wateja zaidi ya mara nne jibu lao ni vocha zilikuwa hazijaidhinishwa kwa ajili ya matumizi.hivyo tatizo hilo wataripeleka sehemu husika baada ya saa24 zitakuwa tayari kwa matumizi,toka 2feb21 hadi leo hizo saa 24 bado?pia mtaingiza vp vocha sokoni kabla hazijawa verified?
Nimeshangaa wanavyotoa huduma kwa wateja, wamekusubirisha muda mrefu hivyo what if ulikua una hiyo pesa tu na ndiyo umenunua vicha upige simu kuna dharura, mimi ndiyo maana ni lazima niwe na mbadala wa line, halotel wanajitahidi ila hawa wengine wanatoa huduma chini ya ubora sana
 
Nimeshangaa wanavyotoa huduma kwa wateja, wamekusubirisha muda mrefu hivyo what if ulikua una hiyo pesa tu na ndiyo umenunua vicha upige simu kuna dharura, mimi ndiyo maana ni lazima niwe na mbadala wa line, halotel wanajitahidi ila hawa wengine wanatoa huduma chini ya ubora sana
Mbaya zaidi hata waliopo hapa hawaleti mrejesho wowote akija kiongozi mwingine akabinafusisha utasikia wafanyakazi wanavyopiga kelele kama wana uchungu na nchi
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (T-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)

- Maeneo gani? (Tukifahamu maana ulipo, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate msaada toka kwa wakala wetu aliye karibu nawe)

- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?

- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza.

- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.


Zifuatazo ni ofisi zetu za huduma kwa wateja ndani ya jiji la Dar es Salaam.


1. POSTA
Mtaa wa Samora, jengo la Extelecom ghorofa la Chini.


2. KARIAKOO
Mtaa wa Makamba/Msimbazi, jengo la Akamba Bus Service.

3. UPANGA
Mtaa wa Magole/Maliki, karibu na Diamond Jubilee.


4. MAGOMENI
Mtaa wa Minaki/Fundiki, karibu na Manispaa ya Kinondoni.


5. KIJITONYAMA
Kijitonyama Sayansi, barabara ya Ali Hassan Mwinyi/ Rose Garden.


6. OYSTERBAY
Barabara ya Haile Selassie.


7. UBUNGO
Jengo la Ubungo Plaza/ Ghorofa la chini.


8. MBEZI BEACH
Mbezi Makonde/ Jengo la Shamo Tower.


9. TABATA
Tabata Bima, barabara ya Segerea karibu na kanisa la Romani Katoliki.


10. CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.
Jirani na tawi la benki ya NBC, jirani na kilipo kituo cha polisi cha UDSM.


11. BARABARA YA PUGU
Barabara ya Mwalimu Nyerere, karibu na Sigara.


12. WAGENI
Uwanja wa ndege.


13. PUGU
Jengo la Quality Centre, ghorofa la chini.


14. KISUTU
Mtaa wa Mchafukoge/Libya jengo la Haad Plaza.


15. TEGETA SHOP
Jengo la Kibo Complex, ghorofa la chini.


16. MWANANYAMALA SHOP
Mwananyamala A, barabara ya Mwinjuma yalipo makutano ya Mwananyamala A.


17. KURASINI
Kurasini Exchange Area, jirani na Chuo cha Diplomasia.


Wasiliana nasi:
022 210 0100
0738 151 511
www.ttcl.co.tz


#RudiNyumbaniKumenoga
View attachment 1529645


Karibu.

Rudi Nyumbani Kumenoga
Nyie ni wapumbavu wakubwa hivi customer care hamna watu tunapiga simu hazipokelewi maana yake nini halafu shirika likibinafusishwa mnapiga kelele au hamjui mnatumia kodi zetu
 
Back
Top Bottom