TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Mlikuja vizuri ila mahali mkaharibu kisa mnataka mapato sawa na mitandao mingine
Mi nilitafakari sana nikaishia kuwaza kuwa wameuza mechi technically ili kampuni binafsi wafanye biashara pia.

Baada ya maafisa wa umma kuanza kutumia TTCL nilijua Tpesa nayo itabamba. Nilivyoangalia tariff zao, nikajisemea kimoyomoyo kuwa hawa wachezaji wamebet timu mwenyeji apoteze!
 
Hiv zipogo simu za mezani ambazo zinatumia laini ya kawaida na kutumia cellular network? Yaani simu iwe ya mezani lakini inatumia cellular network, zipo?

Lengo: iwe tu inakaa nyumbani fixed kwaajili ya kupokea calls na isichukuliwe na madogo wakasepa nayo mitaani.
 
Ndugu mteja,

Una tatizo lolote unapotumia mtandao wetu? Una ushauri wowote ili tuiboreshe huduma yetu?

Tafadhali itumie mada (thread) hii ili tukusaidie kwa urahisi.

Unapokuwa na tatizo, ili tukusaidie kirahisi zingatia haya:

- Ni tatizo gani? (T-PESA, SMS, Calls, Internet, usajili, kukatika kwa mawasiliano n.k)

- Maeneo gani? (Tukifahamu maana ulipo, inakuwa rahisi kukuelekeza wapi uende ili upate msaada toka kwa wakala wetu aliye karibu nawe)

- Tatizo limeanza lini na limejirudia au kuendelea kuwa kero kwako kwa muda gani?

- Kama ni ushauri, zingatia ya juu lakini tutafurahi tukijua kwanini unapendekeza unachopendekeza.

- Kama ni pongezi, zingatia ya juu na tungependa pia upendekeze lipi tufanye kuzidi kuiboresha huduma kwako.


Zifuatazo ni ofisi zetu za huduma kwa wateja ndani ya jiji la Dar es Salaam.


1. POSTA
Mtaa wa Samora, jengo la Extelecom ghorofa la Chini.


2. KARIAKOO
Mtaa wa Makamba/Msimbazi, jengo la Akamba Bus Service.

3. UPANGA
Mtaa wa Magole/Maliki, karibu na Diamond Jubilee.


4. MAGOMENI
Mtaa wa Minaki/Fundiki, karibu na Manispaa ya Kinondoni.


5. KIJITONYAMA
Kijitonyama Sayansi, barabara ya Ali Hassan Mwinyi/ Rose Garden.


6. OYSTERBAY
Barabara ya Haile Selassie.


7. UBUNGO
Jengo la Ubungo Plaza/ Ghorofa la chini.


8. MBEZI BEACH
Mbezi Makonde/ Jengo la Shamo Tower.


9. TABATA
Tabata Bima, barabara ya Segerea karibu na kanisa la Romani Katoliki.


10. CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.
Jirani na tawi la benki ya NBC, jirani na kilipo kituo cha polisi cha UDSM.


11. BARABARA YA PUGU
Barabara ya Mwalimu Nyerere, karibu na Sigara.


12. WAGENI
Uwanja wa ndege.


13. PUGU
Jengo la Quality Centre, ghorofa la chini.


14. KISUTU
Mtaa wa Mchafukoge/Libya jengo la Haad Plaza.


15. TEGETA SHOP
Jengo la Kibo Complex, ghorofa la chini.


16. MWANANYAMALA SHOP
Mwananyamala A, barabara ya Mwinjuma yalipo makutano ya Mwananyamala A.


17. KURASINI
Kurasini Exchange Area, jirani na Chuo cha Diplomasia.


Wasiliana nasi:
022 210 0100
0738 151 511
www.ttcl.co.tz


#RudiNyumbaniKumenoga
View attachment 1529645


Karibu.

Rudi Nyumbani Kumenoga

Nikihitaji fiber Kwa matumizi ya nyumbani gharama za mwezi zikoje? Mna unlimited package?
 
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 09-02-2021 saa 10:30 jioni

145232747_10159352404517884_1629290877579951300_o.jpg
145232747_10159352404517884_1629290877579951300_o.jpg
 
Back
Top Bottom