TRA unahimiza matumizi ya EFD halafu mnawazimia wafanyabiashara kuzitumia kwa Ujumbe 'Device Blocked by TRA'

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,227
5,950
Wako wafanyabiashara kadhaa EFD zao zimezimwa na TRA na zinaonyesha ujumbe mzuri kabisa DEVICE BLOCKED BY TRA bila kusema sababu.

Hii inawezekanaje wakati ambao TRA inahamasisha toa risiti dai risiti?!
 
TRA hii ya kidata imekua ya hovyo sana. Kama Karikaoo wamefunga mashine nyingi sana afu wanapita kutoa offence.
 
Zima afu washa hiyo machine,then tupe picha ya karatasi ndogo itayotoka hapo ili tuamini unachosema au ni wew tu matumizi yako mabovu au z report hujatuma na zimeshafika nne...weka picha
Wewe acha nadharia sisi tuko field tunakupa hali halisi
 
Binafs halijanikuta,
Ila kama Ni kweli Basi wanakosea

Kama Kuna Changamoto namba za mfanyabiashara wanazo, muite myaongee

Kufungia mashine Ni kimtafutia kosa kusud la kutotoa risiti ili mumpige faini
 
Wako wafanyabiashara kadhaa EFD zao zimezimwa na TRA na zinaonyesha ujumbe mzuri kabisa DEVICE BLOCKED BY TRA bila kusema sababu. Hii inawezekanaje wakati ambao TRA inahamasisha toa risiti dai risiti?!

Wafanyakazi watakuja na kudai rushwa. Huu ni uhuju uchumi
 
Wako wafanyabiashara kadhaa EFD zao zimezimwa na TRA na zinaonyesha ujumbe mzuri kabisa DEVICE BLOCKED BY TRA bila kusema sababu. Hii inawezekanaje wakati ambao TRA inahamasisha toa risiti dai risiti?!
Ukiona mpaka EFD mashine imekuwa blocked, ujue hao wafanyabiashara ni defaulters linking!. Siku hizi kukiwa na issues zozote, kwanza unatumiwa SMS, kisha unapigiwa simu ufike TRA, ukikaidi ndipo sasa EFD machine inakuwa blocked na ujumbe ufike TRA.
P
 
Utaratibu ni lazima useme sababu ya kublock na jina la Afisa uliyeblock.
 
Ukiona mpaka EFD mashine imekuwa blocked, ujue hao wafanyabiashara ni defaulters linking!. Siku hizi kukiwa na issues zozote, kwanza unatumiwa SMS, kisha unapigiwa simu ufike TRA, ukikaidi ndipo sasa EFD machine inakuwa blocked na ujumbe ufike TRA.
P
Na waTz tulivyo jeuri anasubiri mpaka ifungwe ndo aende uskute hapo alishapigiwa simu sana aende na kuleta dharau anasubiri aseme anaonewa.
 
Wako wafanyabiashara kadhaa EFD zao zimezimwa na TRA na zinaonyesha ujumbe mzuri kabisa DEVICE BLOCKED BY TRA bila kusema sababu. Hii inawezekanaje wakati ambao TRA inahamasisha toa risiti dai risiti?!

Imejaa memory hadi ukalipie tena waifungue
 
Machine haipaswi kuwa blocked by any means.Machine haipaswi kuwa nyenzo ya kufanya biashara au kukusanya Kodi bali inapaswa kuwa mkataba wa mnunuzi na muuzaji.Changamoto ni kuwa serikali imegeuza machine kama Lungu la kukusanyia Kodi na Maafisa wajanja wajanja wametumia machine for plundering and primitive personal wealth accumulation.
 
Mtandao wa TRA upo chini sana muda mwingine unaacha kulipa kodi kisa mtandao hii mambo ipo Tanzania tuu na tushazoea..
 
Zima afu washa hiyo machine,then tupe picha ya karatasi ndogo itayotoka hapo ili tuamini unachosema au ni wew tu matumizi yako mabovu au z report hujatuma na zimeshafika nne...weka picha
Sizani kama Z report zikifika nne bila kutuma inakuwa hivyo, kwa maana Mimi binafsi kipindi cha sikukuu nafunga biashara Tar 23 December na kuja kufungua ni tar 3January na mashine naifungia humo humo na nikirudi inafanya kazi kama kawaida na Hata nikienda kukadiriwa hawaulizi kwanini siku zote hizo hujatuma z report kwa maana wanajua ni msimu wa sikukuu lazma bishara nyingi watu wako likizo......

Na hata kama ni katikati ya mwaka siku za kazi wakiniuliza kwanini sijatuma Z report wiki nzima natoa maelezo tu kwamba nilikuwa msibani au nilisafiri mbali na eneo la biashara na wanaelewa....

Kama ingekuwa hivyo unavyosema Watu wengi sana wangepata shida...

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom