Changamoto zinazowakabili wafanyabiashara Tanzania

AbaMukulu

JF-Expert Member
Jan 1, 2018
2,048
3,568
Nimeona wito wa Waziri wa Fedha kwa wafanyabiashara kwamba tuwasilishe changamoto zetu ambazo zinatukabili. Waziri Mpango ameahidi kufanyiwa kazi kwa changamoto hizo. Baada ya hapo nikaonelea kuanzisha uzi hapa JF ili yapatikane mawazo mengi zaidi na pia watu wajadili kwa uhuru zaidi kuhusu changamoto hizo. Natumai wahusika Wizara ya Fedha na Mipango watauona na kuyafanyia kazi yaliyomo humu.

Moja kwa moja niende kwenye changamoto ambazo nimekumbana nazo katika biashara kama mfanyabiashara wa kati.

1. Gharama kubwa za kununua na kutengeneza EFD machine
Machine ya EFD inauzwa kuanzia 580,000/= na kuendelea. Gharama hizi ni kubwa sana kwa mfanyabiashara. Pia gharama za kutengeneza machine hizi kubwa sana. Printer hutengenezwa kwa sh 150,000/= (na maranyingi sana ndio uharibika. Machine yangu nimetengeneza mara 2), kutengeneza motherbody ni sh 100,000/=

2. Mfumo wa ukadiriaji kodi na uwazi wa data za mlipakodi
Nimekutana na changamoto ya kukadiriwa kodi kubwa na hili limetokana na mkadiriaji wa tra kusema serikali inatumia mfumo wa kuongeza kiwango cha kodi kila baada ya miaka 3. Suala hili haliakisi ufanyaji wa biashara kwani baada ya miaka hiyo mitatu bado biashara inaweza kuwa na mzunguko ule ule au mmiliki akaamua kupunguza mtaji kwenye aina hiyo ya biashara. Haya ukiwaambia wakadiriaji wa kodi hawakuelewi kabisa.

TRA pia inahitajika itengeneze mfumo ili walipa kodi waweze kuona kabisa madeni yao wanayodaiwa kwenye system ya TRA tofauti na sasa hivi ambapo inabidi uende kwenye ofisi yao na kuuliza unadaiwa kiasi gani. Account hiyo iwe inaonyesha historia ya malipo ya mlipakodi na madeni kama yapo. Kuna cases za wafanyabiashara kuambiwa hawana malimbikizo ya madeni halafu mwisho wa siku TRA hao hao wanakuibukia na kukuambia una malimbikizo ya nyuma. Na hili limefanyika kwangu mimi wakati nilishapewa kabisa tax clearence certificate.

3. Mazingira na sera mbaya za biashara
Sera ya kuwaruhusu machinga/wafanyabiashara wadogo kufanya biashara eneo lolote wanalotaka sio sera rafiki kwenye biashara.

Mfanyabiashara wa kati ambae yuko kwenye frem anabeba gharama mbali mbali kama vile kodi ya mapato, kodi ya pango, leseni ya biashara, cheti cha zimamoto, mishahara ya wafanyakazi. Kumbuka hizi gharama anazilipa kutoka sehemu ya faida yake. Kwa hiyo mfanyabiashara huyu akiweka faida ya 1000 kwa kila item anayouza inamlipa mambo yote hayo.

Ukirudi kwa machinga yeye kwa sababu hana gharama hizo hapo juu kwenye uendeshaji wake wa biashara huenda hata akaweka faida ya 500 kwenye kila item atakayouza. Na hayo wanafanya huku wakiwa wamepanga aina za bidhaa ambazo zinafanana tunazouza watu wenye frem. Na sheria imemruhusu kabisa apange mbele ya duka langu. Kwa mtazamo wa kiushindani hili halipo sawa kabisa.

Kuwepo kwa machinga kila sehemu kumeleta matokeo yafuatayo

A. Ukwepaji wa kodi.

Wafanyabiashara wa kati wameacha frem na kuwa na vijana machinga ambao ndio wanauza bidhaa zao. Na hili limewezekana sababu hakuna utaratibu imara wa kufuatilia kama machinga hawavuki mapato ya 4M kwa mwaka. Ukweli huu uko wazi machinga wanavuka mapato ya 4M kwa mwaka.

Kwa mfano machinga ambaye atafanya kazi kwa siku 308 (toa Jumapili 52 za mapumziko) inabidi asivuke kiwango cha 13 000/siku ili awe hajavuka mapato ya 4M/mwaka. Ukiangalia kuna machinga anauza item ambayo inathamani zaidi ya hiyo na yuko sehem yenye mzunguko wa biashara. Kwa maana hiyo anavuka kiwango cha 4M.

B. Afya za walaji zipo hatarini. Ni rahisi sana kuuza bidhaa zilizoisha muda wake kupitia machinga. Hakuna mamlaka yoyote ya kumlinda mtumiaji inayopita kukagua ubora au mwisho wa muda wa matumizi wa bidhaa kama vile vipodozi, dawa za meno ambazo zinauzwa. Na pia hawatoi risiti kwa hiyo ni vigumu mtumiaji kulalamika kwenye mamlaka husuka bila kuwa na kielelezo cha risiti.

C.Kupungua kwa vipato kwa ambao wana fremu. Baada ya machinga kuruhusiwa kufanya biashara sehemu yoyote basi wameachana na fremu kabisa na kwenda kupanga vitu barabarani. Hali hiyo imepelekea kushuka kwa kipato cha wenye nyumba na pia kudumuza ukuaji wa sekta ya nyumba na ujenzi mpya.

D. Uharibifu wa mazingira na miundombinu. Katika maeneo yote ambayo machinga wapo basi utakuta wamejenga vibanda juu ya mitaro ya kupitishia maji ya mvua. Hali hii inasababisha kulemewa kwa miataro hii wakati wa mvua. Hali hii nimeiona Mbagala Zakheem na Buguruni.

Pili katika hawa wajasiriamali wadogo kuna wapishi wa samaki, kuku na nyama ambao humwaga mafuta yaliyotumika muda mrefu kwenye maeneo hayo pembezoni mwa barabara.

4. Urasimu wa kuhuisha leseni ya biashara

Kila mwaka mfanyabishara analazimika kuacha biashara yake na kwenda kujaza taarifa za kuhuisha leseni wakati hakuna taarifa yoyote ya mfanyabiashara iliyobadilika. Pawepo na mfumo wa kielektroniki ambao unatuwezesha wafanyabiashara kuhuisha leseni zetu za biashara bila usumbufu wa kupoteza muda mwingi kufuatilia kwenye majengo ya halmashauri. Mfumo huo uwe unatunza taarifa zetu na kuepusha kujaza jaza fom kila mwaka.

Karibuni muongeze changamoto nyingine wanajamvi.
 
Changamoto kubwa kwa sasa inayokabili sector ya biashara ni KUSHUKA KWA PURCHASING POWER ya wateja.
Kwa maana hiyo serikali iongeze expenditure ili purchasing power ipande.
Changamoto itabaki kwa sekta binafsi.
Sekta binafsi imedorora na miongoni mwa sababu zake ni serikali kurudisha tenda nyingi zifanywe na mashirika/wakala wa serikali. Mfano TBA anapewa tenda nyingi sana za ujenzi.
 
Imani yangu kubwa ni kuwa, siku hii nchi wakiamua kukusanya kodi kwa tekinolojia, watashangaa namna nchi itakavyokuwa inakusanya kodi kubwa sana sana.
 
Tatizo wafanyakazi wengi wa tra hawajawahi hata kumiliki genge la kuuza embe,wao wanajua kutukamua tu.

katika vitu vinanikera sana mimi ni mda wa kulipa mapato au leseni,unawapelekea pesa lakini wao hawakujali ndio kwanza watakuzarau na kukukalisha ofisini kwao siku nzima.wakati mda huo uliopoteza ulitakiwa uwe dukani unafanya biashara.

Maafisa biashara wengi hawana msaada kwa wafanya biashara wanaacha kuwa ofisini kutoa leseni kwa kasi ya hali ya juu wao wanajali posho za vikao tu.
 
Mimi upande wa makodi tu naona makadirio yanakuwa makubwa mno kiasi kwamba unaweza kuta mwisho wa mwaka hela zote umepeleka tra na kwenye chumba.
Upande wa leseni nakuunga mkono. Ilitakiwa tuweze ku update mtandaoni tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani mfanyabiashara wanakuona kama takataka tu.
Tatizo wafanyakazi wengi wa tra hawajawahi hata kumiliki genge la kuuza embe,wao wanajua kutukamua tu.

katika vitu vinanikera sana mimi ni mda wa kulipa mapato au leseni,unawapelekea pesa lakini wao hawakujali ndio kwanza watakuzarau na kukukalisha ofisini kwao siku nzima.wakati mda huo uliopoteza ulitakiwa uwe dukani unafanya biashara.

Maafisa biashara wengi hawana msaada kwa wafanya biashara wanaacha kuwa ofisini kutoa leseni kwa kasi ya hali ya juu wao wanajali posho za vikao tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom