Wewe hamna kitu.
Unataka msikitini watamke jina la Yesu...!
Au Korani iandike jina la Yesu..!
We unafikiri hayo Majini yenye Korani yao yatahimili vipi hapo ?
Kiarabu Yesu anaitwa Yasuan.
Majini yaliwatia changa la macho.
Nao wakaingia kingi.
Issa maana yake ni uzeruzeru yaani albinizim.
Fanya jaribio hili, ingia msikitini halafu tamka jina LA Yesu Kristo wa Nazareti halafu uone kasheshe lake, na unaweza ukauawa.
Nenda msikiti mwingine tamka Issa bin Mariam, utapewa na Zawadi.
Je Yesu wa Wakristo Ndiye Yule Isa wa Waislam?
NI upotofu wa dhahiri kudai kuwa Nabii Issa au Yesu hawahusiani, kwa kupachika shuhuda zisizohusiana na mada husika. Na baya zaidi ni kule kutumia hoja dhaifu na za uzushi kama alivyofanya wakristo wengi.
Wakristo walijaribu kutoa sababu sita, ikiwemo jina, ukoo, kuumbwa, kuzaliwa, Utume na matendo ya Nabii Issa au Yesu (a.s) kama hoja za kutofautisha majina hayo.
Kwanza ningependa ieleweke kwamba hakuna tofauti kati ya Yesu na Issa kama wanavyotaka kupotosha. Ila ninachoweza kukiri hapa ni kwamba "Yesu mfufuka" anayehubiriwa na Bwana Paulo huyo ni tofauti kabisa na Nabii Issa bin Mariamu. Na kwa mtu asiyeelewa vema maandiko kwa hali yoyote ile ndiye anayeweza kuchanganyikiwa juu ya "Yesu sahihi" ambaye ndiye Nabii Issa bin Mariam (a.s.). Na dawa yake ni kukubali kuelimishwa na si kujifanya kujua, matokeo yake ukapotosha ukweli. Hii ni hatari sana! Sasa hebu tuone upotofu wa sababu hizo wanazozitaja za kutofautisha "Yesu na Issa".
JINA
Wakristo wanasema kimatamshi jina "Yesu" kwa Kiarabu ni "Yasu". Hivyo ndivyo aitwavyo na Waarabu Wakristo tangu zama za kabla ya Muhammad na ndivyo aitwavyo ndani ya Injili ya Kiarabu iliyotafsiriwa na
Waraqa bin Naufal bin Asad kabla ya Utume wa Muhammad (Sahihi Muslim 1, Hadithi 301).
Jina Issa linatokana na jina Ayas lenye maana ya "
Wekundu uliozidiana na weupe" (Baidawi, Vol 1 Uk. 160) mwisho wa kukunuu.
Jibu ni kwamba siyo kweli jina "
Yesu" kwa Kiarabu ni "
Yasu" kama anavyodai wakristo. Ukweli ni kwamba Waarabu Wakristo jina "
Yasu" ndilo jina walilolipokea kutoka kwa wale waliowapelekea ukristo ulianzishwa nje ya Uarabuni miaka mitatu baada ya Yesu au Nabii Issa (a.s) kuondoka.
Na ndilo jina waliloliingiza ndani ya Injili ya Kiarabu.
Na hii inafanana na jinsi baadhi hata ya Watanzania walivyopokea jina la yule Nabii Mbatizaji kwa matamshi tofauti.
Baadhi yao walipokea kwa tamshi la "Yohana" (Kiyunani), wengine "John" (Kiingereza) na wengine "Yahya" (Kiarabu).
Ataonekana wa ajabu atakayedai leo kwamba tamshi mojawapo katika jina hilo hapo juu kwamba ni la Kitanzania (Kiswahili) eti kwa vile wanaolitumia jina hilo ni Watanzania na limeandikwa ndani ya Injili ya Kiswahili!
Pia Yesu kuitwa "mwokozi" hiyo siyo maana ya jina lake. Lakini "uwokozi" ni jina la kazi yake aliyopewa kuifanya (
Mathayo 18:11).
Hivyo, majina ya Yesu na Issa hayana maana yoyote zaidi ya kubaki kuwa ni majina tu. Na siyo lazima jina liwe na maana. Ila neno lenye maana ya "Wekundu uliozidiana na weupe" kwa Kiarabu (Baidawi Vol 1 Uk. 160) na siyo neno Issa.
(
Matthew 18:11 does not appear in several current Bibles such as the New International Version, the New Century Version, the Contemporary English Version, Revised Standard Version and the New Living Translation... and is not found in the most reliable Greek manuscripts, such as the Siniatic and Vatican...)
Kwa mantiki hiyo, sababu hiyo (ya jina) bado haijamtofautisha Yesu na Issa. Lakini kama ilivyo kwa Yohana, Yahya au John, basi Issa na Yesu ni yule yule mmoja aliyezaliwa na Bikira Mariam (Qur’an 3:45 na Luka 1:26-31).
Isitoshe, Qur’an Tukufu ilipoeleza kwamba Nabii Issa siyo Mungu (5:72), hakusulubiwa (4:157-158), na ametumwa kwa wana wa Israeli peke yao (3:49),
Waarabu waliokuwa Wakristo hapo kabla walimfahamu kwamba huyo ndiye "Yesu sahihi" aliyekana "Uungu" katika Biblia pia (Marko 12:29-34) na ndiye aliyenusuriwa kuuawa kama ilivyoelezwa na Qur’an Tukufu na Biblia pia (Waebrania 5:7) na kweli katumwa kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli peke yao (Mathayo 2:6 na 15:24).
Kilichofuatia baada ya kuelewa hivyo walisilimu na kumfuata Mtume Muhammad (s.a.w) ambaye ndiye Mtume pekee aliyetumwa ulimwengu mzima (Qur’an 21:107 na Yohana 16:7-14).
Pamoja na Waarabu hao, alisilimu pia aliyekuwa mfalme wa Ethiopia ya sasa (zamani Uhabeshi) Bw. Najash (Rejea historia ya maisha ya Nabii Muhammad (s.a.w.)