@
mgen
Mwana wa Mungu
Ushahidi mwingine uliotumiwa kwa ajili ya uungu wa Yesu ni kule kutumiwa sifa ya “Mwana wa Mungu” kwa Yesu.
Hata hivyo, kuna sehemu nyingi katika Agano la Kale ilipotumiwa sifa hiyo kwa watu wengine.
Mungu alimwita Israeli (Nabii Yakubu) “Mwanawe” pale alipomuelekeza Mtume Musa aende kwa Firauni katika Kutoka 4:22-23,
“Nawe umwambie Farao, BWANA asema hivi, Israeli ni mwanangu mimi, mzaliwa wa kwanza wangu; nami nimekuambia, Mpe mwanangu ruhusa aende, ili apate kunitumikia...”
Katika 2 Samweli 7:13-14, Mungu anamwita Nabii Suleimani Mwanawe, "Yeye ndiye atakayejenga nyumba kwa jina langu, nacho kiti cha enzi cha ufalme wake nitakifanya imara milele. Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu..."
Mungu alimuahidi Nabii Daudi kumfanya mwanawe katika Zaburi 89:26-27: “Yeye ataniita, Wewe baba yangu, Mungu wangu na mwamba wa wokovu wangu. Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza, Kuwa juu sana kuliko wafalme wa dunia.”
Malaika wanachukuliwa kuwa ni “wana wa Mungu” katika kitabu cha Ayubu 1:6, “Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za BWANA, Shetani naye akaenda kati yao”.
Katika Agano Jipya, kuna marejeo mengi ya “mwana wa Mungu” ya watu wengine wasio Yesu. Kwa mfano, pale mtunzi wa Injili kwa mujibu wa Luka amewaorodhesha wahenga wake hadi kwa Adamu, ameandika: Luka 3:38 “Wa Enoshi, wa Sethi, wa Adamu, wa Mungu”.
Baadhi ya watu wanadai kuwa kile cha kipekee kilichopo kwa Yesu ni kuwa yeye ndiye mwana wa pekee wa kuzaliwa
Mwana wa Mungu, huku hao wengine ni “wana wa Mungu tu.”
Hata hivyo, Mungu ananukuliwa akimwambia Mtume Daudi, katika Zaburi 2:7, “Nitaihubiri amri, BWANA aliniambia, Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.”
Pia inapaswa ijulikane kuwa hakuna hata sehemu moja katika Injili ambapo Yesu alijiita yeye mwenyewe kuwa yeye hasa ndiye “mwana wa Mungu”.
Badala yake, amenukuliwa kuwa amekariri kujiita “Mwana wa Adamu” (mfano Luka 9:22) kwa mara zisizohesabika.
Na katika Luka 4:41, kwa hakika amekataa kuitwa “Mwana wa Mungu”: “Pepo nao waliwatoka watu wengi, wakipiga kelele na kusema, Wewe u Mwana wa Mungu. Akawakemea, asiwaache kunena, kwa sababu walimjua kuwa ndiye Kristo.”
Kwa kuwa Wayahudi wanaamini kuwa Mungu ni Mmoja, na hana mke wala mtoto kwa maana halisi yoyote ile, ni wazi kuwa ibara “mwana wa Mungu” kwa Wayahudi ina maana ya “Mtumishi wa Mungu tu” yaani mtu aliye karibu na Mungu, kwa sababu ya huduma yake ya kiimani, akiwa kama mtoto kwa baba yake.
Wakristo waliokuja kutoka katika historia za kuwa walikuwa ni Wagiriki au Warumi, baadaye waliitumia vibaya istilahi hiyo.
Kwani katika urithi wao, “mwana wa Mungu” inamaanisha mungu ana mwili au mtu aliyezaliwa kwa muungano wa
kimwili kati ya mungu mwanamume na mwanamke.
Wakati Kanisa lilipoacha msingi wa Kiyahudi, lilitwaa dhana ya kipagani ya “mwana wa Mungu”, ambayo kwa ukamilifu, ilikuwa ni tofauti na matumizi ya Kiyahudi.
Kwa hiyo, matumizi ya istilahi “mwana wa Mungu” inafaaifahamike kuwa ni alama ya ufahamu ya kisemintiki yenye maana “mtumishi wa Mungu”, na sio katika ufahamu wa kipagani wa uhalisi wa kuwa kinda la Mungu. Katika Injili nne,
Yesu anarekodiwa akisema: “Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.” Mathayo 5:9.
Vivo hivyo, matumizi ya Yesu ya istilahi abba, “baba mpendwa” lazima ifahamike hivyo hivyo. Kuna ubishani miongoni mwa wasomi wa Agano Jipya juu ya nini maana ya abba kwa uhakika kabisa katika zama za Yesu na Wayahudi wa makundi mengine wa muongo huo huo walilitumia kwa upana gani.
Hivi karibuni kwa ukali kabisa, James Barr amedai kuwa hilo halikuonyesha wazi wazi ufahamu wa kuwa hilo lilikuwa linamuhusu yeye ila hilo kiwepesi kabisa linaashiria “baba” tu.
Ili kufikiria kuwa Mungu ni “Baba yetu wa mbinguni” haina maana mpya, kwa kuwa katika sala ya bwana amenukuliwa kuwa amewafundisha wanafunzi wake kumtambulisha Mungu katika njia hii hii
Tazama Matendo14:11-13. Katika mji wa Lystra (Uturuki), Paulo na Barnabas walihubiri, na wapagani walidai kuwa Paulo na Barnaba walikuwa ni miungu wenye miili. Walimwita Barnaba mungu wa Kirumi Zeus, na Paulo mungu wa Kirumi Hermes.