Nilileta andiko la sahih bhukhari mbusu jiwe mwenzako akasema kitabu Cha sahih bhukhari ni uongo mtupu ,
Ndio maana sikuwekei andiko mpaka ukiri kukiamini kwanza , ili nikiliweka usiniletee bla bla
Mpaka govi la ukafiri liganduke ..
Kifo Cha Yesu
Kuhusiana na suala la kifo cha Yesu msalabani - ingawa ni wazi kwamba Yesu, kama alivyokuwa kwa mitume wengine kabla yake, walipatwa na masaibu makubwa kwa sababu ya kujaribu kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa watu ambao hawakuonyesha nia na ari ya kuupokea.
Na alikuwa anajua vizuri kwamba hili lingemtokea, hata hivyo hakufikia kiwango cha kuuliwa na hususan kuuliwa kulikopangwa na Mungu - kama alivyodai Paulo baadaye, yaani kuuliwa ili kumwokoa mwanadamu kutoka kwenye minyororo ya dhambi.
Katika Bustani ya Gethsemane, Yesu aliomba kwa unyenyekevu na shauku kwa Mwenyezi Mungu kuwa "kikombe kinipite" (Mathayo 26:39), ambapo kikombe hiki kinamaanisha kukamatwa na kufa kwake.
Hivi kweli tunaamini kwamba mja mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu anaweza kuomba rehema akanyimwa?
Wazo zima la kuteswa na kufa kwa Yesu msalabani ili awe kafara ya dhambi za wanadamu halikubaliani na hoja za kiakili na mantiki linapohusishwa na Mwenyezi Mungu ambaye ni muadilifu.
Je, inawezekana kwa Mwenyezi Mungu ambaye ni mwadilifu kwa kiwango cha juu kabisa akakataa kumsamehe Adam - na kizazi chake baada yake kwa ajili ya dhambi lake tu (Adam) - mpaka Yesu afe?
Je, inawezekana kwa Mwenyezi Mungu ambaye ni muadilifu amlazimishe mmoja wa waja wake akataka na kuruhusu kudhalilishwa na kuuwawa kwa mmoja wa mitume wake aliyekuwa mnyenyekevu na mtii sana kwake?
Je, inawezekana kwa Mwenyezi Mungu ambaye ni muadilifu amlazimishe mmoja wa waja wake afe kwa ajili ya dhambi za watu wengine?
Katika Uislam, hatudhani kuwa hili linawezekana.
Tukiliangalia hili kutokana na mtazamo wa upendo wa Mwenyezi Mungu, hoja zile zile zinajitokeza kuhusiana na uadilifu wa Mwenyezi Mungu:
Je, Mungu mwenye upendo mkubwa kwa waja wake angewaadhibu wanaadam wote bila kuja Yesu?
Je, Mwenyezi Mungu mwenye upendo mkubwa kwa waja wake angehitaji kuwa ni lazima mmoja wa waja wake wema na waaminifu (Yesu) adhalilishwe na kuuawa ili awasamehe wanadamu madhambi yao?
Yeyote na kila mtu anaweza kushangaa na kujiuliza hii ni
Aina gani ya upendo wa Mungu unaoweza kudai kiasi cha gharama kikubwa kiasi hicho na cha kutisha namna hii.
Uislam unashikilia kwa nguvu msimamo kwamba kila mtu anawajibika kwa vitendo vyake: kila mtu ataadhibiwa kwa maovu yake.
Hai-ingii akilini kwamba Mwenyezi Mungu ambaye ni muadilifu anaweza kumuadhibu mtu kwa dhambi alizofanya mtu mwingine.
"Kila nafsi italipwa kutokana na matendo yake na nafsi haitaulizwa juu ya matendo ya nafsi nyingine". (Qur'an 6:164)
Hakuna mtu anayeweza au atakaye adhibiwa kwa dhambi za mtu mwingine.
Mwenyezi Mungu anatuambia kwamba kila mmoja wetu atalipwa au kuadhibiwa kutokana na aliyoyafanya yeye mwenyewe katika maisha yake.
"Na Mwenyezi Mungu hamtwishi yeyote mzigo mkubwa kuliko ule anaoweza kuubeba.
Kila jema nafsi inalolifanya ni kwa faida yake, kila uovu inaoufanya ni kwa hasara yake." (Qur'an 2:286)