Gavana
JF-Expert Member
- Jul 19, 2008
- 33,635
- 8,957
Isa ni mjumbe tu wa Allah na hawezi kutamka maneno kama haya.
Mathayo 28:18
Yesu akaja kwao, akasema nao, akawaambia,
[emoji117]Nimepewa mamlaka yote mbinguni na duniani.
{Isa hana mamlaka Mbinguni na Duniani}
19 Basi, enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;
{Isa hajui kabisa maana ya Baba, Maana na Roho Mtakatifu. Neno [emoji117]Mwana, analifananisha na neno [emoji117]Mtoto, kumbe sio}
20 na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dahari.
{ Isa hayupo na sisi sasa na wala hajulikani alipo hadi hivi sasa}
Yohana 14:2
Nyumbani mwa Baba yangu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia; maana naenda kuwaandalia mahali.
{Isa hana Baba}
Yohana 14:3
Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo.
{Isa ni kama Muhamadi hawajui watakavyoganywa wao wala wafuasi wao}
Yohana 14:4 Nami niendako mwaijua njia.
{Isa haijui njia ya Mbinguni kama Muhammadi}
Yohana 14:5 Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia?
{ Isa hajawahi kuwa na Wanafunzi 12 aliowateua wafuatane naye kama akina Yohana wa Yesu}
Yohana 14:6 Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
{ isa ni kama Muhamadi anayesema
" Surah Al-Ah-qaaf: Ayah 9.
قُلۡ مَا كُنتُ بِدۡعٗا مِّنَ ٱلرُّسُلِ وَمَآ أَدۡرِي مَا يُفۡعَلُ بِي وَلَا بِكُمۡۖ إِنۡ أَتَّبِعُ إِلَّا مَا يُوحَىٰٓ إِلَيَّ وَمَآ أَنَا۠ إِلَّا نَذِيرٞ مُّبِينٞ
Sema: Mimi si kiroja miongoni mwa Mitume. Wala sijui nitakavyo fanywa wala nyinyi. Mimi nafuata niliyo funuliwa tu kwa Wahyi, wala mimi si chochote ila ni mwonyaji mwenye kudhihirisha wazi"
Hivi mtu anayeongea maneno kama a hapo juu anaaminikanaje kuwa ni Mtume....![emoji848] ndio Bosi wa Isa huyo.
Yesu ana sifa za Kimungu zaidi ya Zilioni ukimlinganisha na Isa Bin Marriam aliyezaliwa na kuzikwa Madina.
Yesu hakuwa Mungu wala mwana wa Mungu bali alikuwa Mtume wa Mungu tu.
Yeye hakupewa ujumbe wa utume kwa ajili ya watu wote wa kabila zote. Bali yeye alikuwa Mtume kwa ajili ya wana wa Israeli tu.
Mwenyewe alijua mipaka ya utume wake. Kwahiyo alisema:
1. Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. (Mathayo 15:24).
2. Wakati mwanamke mmoja asiyekuwa mwana wa Israeli alipokuja kwa Yesu Kristo kuomba baraka zake, Yesu akakataa na zaidi ya kukataa aliwatusi wasiokuwa Waisraeli. “Akasema si vyema kukitwaa chakula cha watoto na kuwatupia m’mbwa.” (Mathayo 15:26, Marko 7:27).
3. Hao thenashara (kumi na mbili) Yesu aliwatuma, akawaagiza, akisema, katika njia ya mataifa msiende, wala katika mji wowote wa Wasamaria msiingie. Afadhali shikeni njia kuwaendea kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli. (Mathayo 10:5-6).
4. Baadhi ya Wakristo wanadhani kwamba wakati Waisraeli wote wamefikishiwa ujumbe, kisha makabila mengine pia yahubiriwe. Lakini dhana hii si sahihi bali ni kinyume cha mafundisho ya Bwana Yesu. Yeye amesema kwamba: “Lakini watakapo wafukuza katika mji huu, kimbilieni mwingine; kwa maana ni kweli nawambia, hamtaimaliza miji ya Israeli hata ajapo mwana wa Adamu. (Mathayo 10:23).
5. Bwana Petro mwanafunzi wa Yesu Kristo aliwahubiri wasiokuwa Waisraeli. Wanafunzi wengine, baada ya kupata habari hii walimpinga Bwana Petro kwa kosa lake. Biblia inasema kwamba: “Basi mitume na ndugu waliokuwako katika Uyahudi wakapata habari ya kwamba watu wa mataifa nao wamelipokea neno la Mungu. Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemu, wale walio wa tohara wakashindana naye, wakisema, uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao. “ (Matendo 11:1-3).
6. Aya za Biblia zifuatazo zinaeleza kwamba Bwana Yesu alikuwa mfalme na mtawala wa Mayahudi. (Mathayo 2:6, 27:29, 27:42, Yohana 1:49.
7. Bwana Paulo ambaye ni mpinzani na mhalifu (anti Christ) wa Bwana Yesu, baada ya kuchukia alianza mahubiri nje ya Wasiraeli. Biblia inasema kwamba: “Hata Sila na Timotheo walipoteremka kutoka Makedonia, Paulo akasongwa sana na bila neno, aliwashuhudia Wayahudi ya kwamba Yesu ni Kristo walipopingana naye na kumtukana Mungu,
akakung'uta mavazi yake, akawaambia, damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu, mimi ni safi; tangu sasa ninakwenda kwa watu wa mataifa. (Matendo 18:5-6).