Timu ya Taifa ya Romania ilienda World Cup ya mwaka 1998 pale Ufaransa wakiwa wamepaka Bleach karibia wachezaji wote

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,722
45,128
Nimeona wananchi kesho wana mechi ya ligi ya mabingwa afrika, ni mechi muhimu sana kiasi wakaamua kuipa jina “Pacome Day” huku wakinogesha na style ya nywele ya mchezaji wao Pacome.

Style hiyo kutumiwa na wachezaji wengi wa timu sio ngeni katika shughuli za michezo hasa kabumbu.

Mwaka 1998 wakati wa michuano ya kombe la dunia la FIFA pale katika ardhi ya Wafaransa, timu ya taifa ya Romania ilienda kushiriki kwa namna yake.

Asilimia 99 ya wachezaji walipaka “bleach” na kuwa kivutio miongoni mwa watazamaji waliojitokeza kutazama michuano hiyo inayotajwa ndio bora kuwahi kutokea.

Vyombo vya habari vilikuwa vinavutiwa zaidi na mechi kikosi cha Romania kwani waliweza kupata picha mbalimbali kwajili ya media zao.

Bahati mbaya Romania alitolewa Round ya 16 bora dhidi ya moja ya timu bora za wakati ule Croatia ya akina Davor Suker na Zvonomir Boban.

Haya wananchi ni zamu yenu kupaka “bleach” kikosi kizima nasubiria kumuona mwanangu Zawadi Mauya.
IMG_0001.jpeg
IMG_0002.jpeg
 
Nimeona wananchi kesho wana mechi ya ligi ya mabingwa afrika, ni mechi muhimu sana kiasi wakaamua kuipa jina “Pacome Day” huku wakinogesha na style ya nywele ya mchezaji wao Pacome.

Style hiyo kutumiwa na wachezaji wengi wa timu sio ngeni katika shughuli za michezo hasa kabumbu.

Mwaka 1998 wakati wa michuano ya kombe la dunia la FIFA pale katika ardhi ya Wafaransa, timu ya taifa ya Romania ilienda kushiriki kwa namna yake.

Asilimia 99 ya wachezaji walipaka “bleach” na kuwa kivutio miongoni mwa watazamaji waliojitokeza kutazama michuano hiyo inayotajwa ndio bora kuwahi kutokea.

Vyombo vya habari vilikuwa vinavutiwa zaidi na mechi kikosi cha Romania kwani waliweza kupata picha mbalimbali kwajili ya media zao.

Bahati mbaya Romania alitolewa Round ya 16 bora dhidi ya moja ya timu bora za wakati ule Croatia ya akina Davor Suker na Zvonomir Boban.

Haya wananchi ni zamu yenu kupaka “bleach” kikosi kizima nasubiria kumuona mwanangu Zawadi Mauya.View attachment 2913020View attachment 2913021
Utopolo wanasema walimuiga Pacome
 
Back
Top Bottom