Mkasa wa timu ya taifa ya Denmark na bahati ya mtende katika michuano ya Euro 1992

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Jan 1, 2017
20,716
45,121
Ulishawahi kusikia bahati ya mtende au ngekewa? Au mtu baada ya kuharibu anapewa second chance! Ndio kilichowakuta Denmark mwaka 1992 katika michuano ya Mataifa ya Ulaya.

Michuano ya Uefa Euro mwaka 1992 ilipangwa kufanyika katika majira ya joto huko nchini Sweden. Ilikuwa ni michuano ambayo inahusisha team 8 katika makundi mawili tu.

Kila kundi likiwa na timu 4 tu ambapo ukishika nafasi mbili tu za juu tayari una tiketi ya kwenda nusu fainali.

Timu zilizofuzu zilikuwa kama ifuatavyo; Kundi A kulikuwa na mwenyeji Sweden, Ufaransa, Endland na Yugoslavia.

Kundi B likiwa na Uholanzi, Ujerumani, Scotland na Urusi.

Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya mashindano kuanza, Yugoslavia kukaanza machafuko hali iliyopelekea kutengwa na jamii ya kimataifa na baadae kuvunjika kwa nchi. Hali hiyo ikapelekea kuondolewa kwa Yugoslavia katika michuano hiyo ya timu za taifa. Nafasi akapewa Denmark siku 10 kabla ya michuano kuanza.

Denmark kiasili hakufuzu, alishika nafasi ya pili kwenye kundi lake wakati wa kufuzu, hivyo kuchaguliwa kwao kukawa ni kama mtu aliyepewa second chance mara baadabya kuharibu. Ni sawa na mwanachuo anayeenda kusapua.

Wachezaji wa Denmark wakaulizwa mko tayari kwenda kupambana kama watapewq nafasi ya kushiriki Euro 1992 wakajibu ndio, ikumbukwe hapo msimu ulishaisha wachezaji walikuwa wanajiandaa kwenda likizo na familia zao. Hivyo wachezaji wa Denmark wakatoka huko likizo na kuelekea Sweden kupambana.

Mechi ya kwanza Denmark wanatoa droo na England. Mechi ya pili Denmark akapigwa na mwenyeji Sweden. Watu wakaanza kusema Denmark ni kama walienda kutalii katika michuano hiyo.

Mechi ya tatu, Denmark uso kwa macho na France. Denmark anashinda 2-1 na kuelekea zake Nusu Fainali. Watu wakawa kimya.

Nusu Fainali wakakutana na bingwa mtetezi Uholanzi ya akina Rijkaard, Bergkamp, Marco Van Basten, straika bora kabisa wa miaka ya mwisho mwa 1980 na mwanzoni mwa miaka 1990. Mechi inapigwa inaenda mpaka extra time 2-2.
Kwenye mikwaju ya penati golikipa Peter Schmeichel anapangua penati ya Van Basten na kuwapeleka Denmark Fainal. Watu hawakuamini. Dunia ikapigwa na mshangao!!

Denmark ikaingia Fainal na Ujerumani iliyokuwa bingwa wa dunia. Kama kawaida, Denmark wakaendelea kuwa underdog.

Fainali ikapigwa, Denmark akicheza muda mwingi kwa kujihami na kwa tahadhari kubwa, anampiga Ujerumani bao 2-0 na kutwaa ubingwa kinyume na matarajio ya wengi.

Straika wao Henrik Larsen akawa ni mfungaji bora wa mashindano akiwa na magoli matatu akifungana na wachezaji wengine wawili.

Ukawa ndio ubingwa wa kwanza na wa pekee kwa Denmark mpaka sasa.

Kitendo cha Denmark kutwaa ubingwa huo ikachukuliwa ni mojanya matukio ya kushangaza kuwahi kutokea katika mchezo wa soka!!

Adios Amigo
5E016724-34FA-42C1-B65C-D6625164EA32.jpeg
D0B598DE-AF52-4A5A-8479-9B4801003350.jpeg
 
Hii inataka kufanana na hii ya wa Morocco ingawa wao walifuzu ec kihalali.

Yugoslavia ilkua ikikiwasha sana enzi hizo ila tu alkua na roho ya kuchukiwa na wenzake kama ilivo Urusi.
 
View attachment 2479700View attachment 2479702
Ngekewa kama hii ilitokea kwa Tukuyu Stars kama kumbukumbu zangu ziko vizuri.
Mwaka waliopanda daraja kuna timu zilipanga matokea zikatolea wakaingizwa wao looser.

Kupanda daraja na ubingwa mwaka huo huo.
 
Back
Top Bottom