Pacome Aitwa timu ya Taifa ya Ivory Cost kwa Mara ya Pili

Smart codetz

Senior Member
Jan 25, 2023
180
703
20240319_122408.jpg

Kiungo wa Klabu ya Yanga Sc Pacome ZouZou ameongezwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Ivory Coast kuchukua nafasi ya Ibrahim Sangare, anayeitumikia Klabu ya Nottingham Forest ya Uingereza baada ya mchezaji huyo kupata majeraha siku chache kabla ya kuripoti kambini.

Taarifa iliyotolewa na shirikisho la soka nchini Ivory Coast imeonyesha kuwa mastaa watatu walioitwa awali wametemwa kutokana na majeraha yanayowakabili ambapo Séko Fofana, Ibrahim Sangaré na Evan Ndicka wote wameachwa kutokana na kuwa na majeraha huku nafasi zao zikizibwa na Kader Keita,Pacome Zouzoua na Emmanuel Agbadou.

“Shirikisho la Soka la Ivory Coast linafahamisha waandishi wa habari na umma kwamba wachezaji, Séko Fofana, Ibrahim Sangaré na Evan Ndicka, walioitwa na Kocha Emerse Faé, kwa mechi mbili za kirafiki, Ivory Coast-Benin mnamo Machi 23, 2024 huko Amiens (Ufaransa) na Ivory Coast -Uruguay mnamo Machi 26, 2024 huko Lens (Ufaransa), hawatapatikani kwa sababu za matibabu ya majeraham hivyo kwa madhumuni haya, Séko Fofana (Al-Ettifaq FC) mwenye maumivu amebadilishwa na Kader Keita (CFR Cluj, Romania) na Ibrahim Sangaré, ambaye alijisikia vibaya baada ya mechi na klabu yake ya Nottingham Forest, nafasi yake inachukuliwa na Zouzoua Pacôme (Young Africans SC, Tanzania).” Ilisomeka Taarifa hiyo iliyotolew Shirikisho la soka nchini Ivory Coast.

Pia taarifa hiyo iliendelea kuwa “Emmanuel Agbadou (Reims, Ufaransa) aliitwa kuchukua nafasi ya Evan Ndicka ambaye pia alijisikia vibaya mazoezini”.

Pacome amekua na wakati mzuri tangu ajiunge na Yanga sc akitokea Asec Mimosa ya nchini kwa Ivory Coast ambapo mpaka sasa amefunga jumla ya mabao saba katika ligi kuu nchini huku akiisaidia klabu yake ya Yanga sc kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Afrika.

Sports Leo
 
Hizi ni habari njema kwa Mamelodi Sundowns, maana yenyewe imewazuia nyota wake watatu Ronwen Williams, Themba Zwane na Teboho Mokoena kujiunga na timu ya taifa ya Bafana Bafana
 
Pacome anaenda kupambana na Darwin Nunez wa Uruguay !
Hakika ni Mchezaji wa daraja la juu .
 
Kuna watu wameumbuliwa wakitaka kuwahadaa Mamelodi. Angekuwa aliumia kweli mnadhani hii safari angekwenda?
Akili za wapi hizi? Kuna madaktari kutoka Ivory coast wamekuja kuthibitisha kama aliumia au lah? Kiufupi ni Yanga na Pacome wenyewe ndio wameridhia aende timu ya taifa. Kama wangeamua kutotaka Pacome aende basi wangetoa taarifa kwa shirikisho la soka Ivory coast kuwa Pacome ni majeruhi ili tu kuwazubaisha Mamelod na hakuna mtu yeyote kutoka Ivory coast angepanda ndege ili kuja kumpima afya Pacome. Tumia akili kufikiria sio kujiandikiaga tu
 
Record zinaongea
 

Attachments

  • 5142992C-C045-44FC-A747-8581D15485D2.jpeg
    5142992C-C045-44FC-A747-8581D15485D2.jpeg
    1.2 MB · Views: 3
Wa Ivory Coast kuwa na vipaji sishangai labda huyo Pacome angekua anatokea Malawi kule juu watu wamecheza mpira kwa viwango vya juu mno wacha waendelee kula matunda yao ya kujua Mpira sisi tuendelee kula hela za Fine za Wachezaji wenye imani za kishirikina..
 
Back
Top Bottom