Mkuu Rev. Kishoka,swali lako ni gumu lakini ni muhimu mno.Kwa Mtazamo wangu katika Orodha ya wana-ccm bado Salim Ahmed Salim ndiye mtu pekee anayefaa kuwa Kiongozi wa Nchi kwa sasa.Tatizo kubwa ninaloliona kwa Ndugu huyu ni Umri,kwani sasa hivi amekwishakuwa mtu mzima mid 60's.
Salim ni Muadilifu hana Makuu na si Fisadi.Kiongozi huyu ni mzoefu karibu kwenye nyadhifa zote za juu serikalini,kwenye kumbukumbu inaonyesha kuwa ameanza kuitumikia serikali toka akiwa mdogo wa umri wa miaka ya 20.Salim ni Miongoni mwa viongozi waanzilishi kwenye Chama cha Mapinduzi,kwa maana hiyo anajua vyema Muundo na madhumuni ya Chama cha Mapinduzi ambayo nia yake ya dhati ilikuwa ni kumkomboa Mkulima na Mfanyakazi,na sio kujali Wafanyabiashara na Wajasirimali kama ilivyo sasa.
Ndugu Rev Kishoka,Ni imani yangu kuwa kuna Viongozi wazuri katika Kambi ya Upinzani,Lakini bado Upinzani haujajiimarisha vyema vijijini ambako ndio kuna Wapiga kura wengi.Vyama vingi vya Upinzani vina nguvu kubwa Mijini ambako ndio kuna wasomi,wanaoangalia mambo kwa kina,lakini nguvu ya vyama hivi bado sio kubwa Vijijini.Inabidi vyama hivyo vitafute mbinu ya kujitawanya Vijijini,labda kwa kuanzisha Matangazo ya Redio ambayo yataeleza mipango yake ya maendeleo na kueleza Ufisadi na Ahadi za uongo za CCM.Kutawanya vipeperushi vinavyoonyesha mabaya ya CCM na kutoa njia mbadala, na mambo haya yafanywe labda kila baada ya miezi miwili/mitatu na sio kungoja wakati wa Uchaguzi.Suala hili linataka funds,na vyama vingi vya upinzania havina miradi mikubwa,vinaendeshwa kwa pesa ndogo ya Ruzuku.
Haitokuwa Rahisi kwa kiongozi yeyote Tanzania kuonekana Mzuri ikiwa tu atatoka CCM,kwani system nzima imeharibika...Ili kiongozi aonekane mzuri inabidi system yote ipanguliwe.Kwa mtazamo wa mtu mmoja mmoja Salim ndio pekee katika CCM anayeweza ku-deliver.Kuna Viongozi wengi Vijana ndani ya CCM ambao watakuja kuwa wazuri,ikiwa tu watazingatia miiko ya kazi zao,na kuwa hapo kwa lengo la kuwatumikia watanzania na sio kujilimbikizia mali.
Rais wetu wa sasa, Mh Mrisho Jakaya Kikwete,ameshindwa kabisa kazi!,Toka aingie madarakani amekuwa mtu wa kutoa ahadi zisizotekelezeka,na sasa serikali yake imeandamwa na kashfa ambazo hatujapata kuziona toka tupate Uhuru (1961).Muungwana huyu ataomba mwenyewe kutoendelea na Term yake ya pili,kwani humo ndani ya CCM kuna upinzani mkubwa dhidi yake,baada ya kugeukana na waliomuweka yeye kwenye Madaraka..