The road towards 2010 Elections | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The road towards 2010 Elections

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Alfa na Omega, Jan 23, 2007.

?

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

Poll closed Jan 2, 2010.
  1. Edward Lowassa

    0 vote(s)
    0.0%
  2. Dr. Slaa

    7 vote(s)
    38.9%
  3. Prof. Lipumba

    0 vote(s)
    0.0%
  4. Mizengo Pinda

    5 vote(s)
    27.8%
  5. Samwel Sitta

    0 vote(s)
    0.0%
  6. Jakaya Kikwete

    2 vote(s)
    11.1%
  7. Mark Mwandosya

    2 vote(s)
    11.1%
  8. Harisson Mwakyembe

    2 vote(s)
    11.1%
  9. None of The above

    0 vote(s)
    0.0%
  1. A

    Alfa na Omega Member

    #1
    Jan 23, 2007
    Joined: Jan 23, 2007
    Messages: 8
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Baada ya CCM kushinda kwa kishindo uchaguzi wa 2005 sasa yaanikwa vikali kwa maovu ya mwaka mmjo tu wa kuwa madarakani, skendo zimekuwa nyingi wananchi wamefungua macho sikujua watanzania wana mwamko katika tekinolojia ya habari na mawasiliamo namna hii kusambaza habari na kusomwa na watu wengi kiasi hiki.

    Kweli viongozi kama wamefikia hapo basi hata mimi minaanza kuamini niliyoyasoma humu, yanatisha sijui kama hii forum wataiacha hai kwasababu inawaumbua wengi ombi langu serikali ijirekebishe na isifikirie kufunga huu mtandao ''FORUM'' wa JF kwa sisi wanyonge tulio nyumbani na mbali na nyumbani huu ndiyo mtandao unaotupa habari za kweli kwasababu anayeandika ni mtu au kikundi cha watu wenye dhamira za dhati kwa taifa lao.

    Sisi watanzania wasomi tuishio ndani na nje ya Tanzania tunatoa ushauri huu:

    Ukiona unaandikwa sana JF jibu hoja au weka timu yako hapa kujibu mashambulizi kama wengine wanavyofanya hatutasimama tunakwenda mbele kwa mbele na siyo kutishia, hili siyo Gazeti, Redio au TV ambayo tunalipia kodi eti utatufungia.

    Nimetoa majina machache ambayo ni pendekezo kama wanaoonekana wanaweza kupendekezwa kuwa miongoni mwa wanaoweza kugombea 2010, kama una pendekezo basi toa pendekezo na moderators wanaweza kuongeza kwenye list au kuondoa mmojawapo wa niliowapendekeza.

    AU KAMA KUNA MTU ANA WAZO JINGINE TAFADHALI TUCHANGIE
     
    Last edited by a moderator: Jun 27, 2008
  2. M

    Mama Lao JF-Expert Member

    #2
    Jan 23, 2007
    Joined: Jan 16, 2007
    Messages: 238
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    eeeh...practising for 2010...hakika nitagombea. HASWA!
     
  3. J

    Jafar JF-Expert Member

    #3
    Jan 23, 2007
    Joined: Nov 3, 2006
    Messages: 1,138
    Likes Received: 12
    Trophy Points: 0
    Ninaunga mkono hoja.
     
  4. Lunyungu

    Lunyungu JF-Expert Member

    #4
    Jan 23, 2007
    Joined: Aug 7, 2006
    Messages: 8,836
    Likes Received: 75
    Trophy Points: 145
    Mimi nakubali kwa nguvu zangu zote .Lakini issue isiwe ni CCM pekee hata upinzani na madhambi mengine . Kwa sasa CCM ndiyo kichwa kila kukicha kuwa wameshika Serikali lakini Jambo iwe huru isije ikawa ina upande mmoja . Natua wengine tua vyama hapa lakini yote tunaweka kapuni Tanzania kwanza na mengine baadaye . Siamini katika Chama mimi naamini katika Tanzania .So huo ni ujumbe wangu na nasema naunga hoja .
     
  5. Mzee Mwanakijiji

    Mzee Mwanakijiji Platinum Member

    #5
    Jan 24, 2007
    Joined: Mar 10, 2006
    Messages: 31,362
    Likes Received: 6,393
    Trophy Points: 280
    Lunyungu, ile makala ya "Kuanguka kwa CCM" Imechapishwa kwenye Tanzania Daima leo... !!
     
  6. Field Marshall ES

    Field Marshall ES JF-Expert Member

    #6
    Jan 24, 2007
    Joined: Apr 27, 2006
    Messages: 12,659
    Likes Received: 69
    Trophy Points: 0
    Eeh bwana Mzee, hiyo makala iko all over bongo sio hilo tu, kuna mtu ameamua kuisambaza kila kona, mtandao wote wanayo hiyo makala, na ipo kila ofisi ya juu huku toka jana!

    Ndio maana ni muhimu tukawa na alternative maaana majibu lazima yanakuja!
     
  7. Wacha

    Wacha JF-Expert Member

    #7
    Jan 24, 2007
    Joined: Nov 23, 2006
    Messages: 856
    Likes Received: 18
    Trophy Points: 35
    Richmonduli ni mbwa mwitu ambaye amejitajirisha kwa kipindi kifupi na anaendelea kuuma. Mba mwitu ukiacha mfupa hula mpaka kuumaliza hivyo ndivyo nchi inavyokwenda hivi sasa hamna cha salie mtume. Record ya huyu jamaa tangu 1995 ilikuwa ndio hivyo tena unafikiri ataacha, sasa hivi kutokana na uozo na uvundo wa JK hatuwezi kufika hata hiyo 2010 ambayo watu wanaiota. Baada ya maonyo ya mwalimu ameamua kufanya kafara.

    Maziri mkuu asiye na mbele wala nyuma ni mbwa mwitu ambaye ni lazima ashitakiwe kwa kudharau bunge na kulifanya halina maana, anawajua wabunge wamehongwa alafu anakaa kimya? What a joke? Huyu ndiye mhujumu uchumi wa kweli namba moja sio wale wanaoiba kuku ambao hupigwa hadi kufa. Huyu ndiye anatakiwa kujibu maswali ya umeme, huyu anatakiwa kujibu maswali ya mbuga za wanyama kuuzwa kwa wageni ambao wamefungua majeshi yao kuwabughuzi wananchi, huyu ndiye anatakiwa kujibu shutuma za watanzania kupoteza maisha yao mikononi mwa wageni, huyu ndiye anatakiwa kujibu maswali mengi kuliko mtu yeyote katika kipindi cha mwaka mmoja.
     
  8. Mzee Mwanakijiji

    Mzee Mwanakijiji Platinum Member

    #8
    Jan 24, 2007
    Joined: Mar 10, 2006
    Messages: 31,362
    Likes Received: 6,393
    Trophy Points: 280
    Brutus, niliuliza kwa sababu walishatumia ile makala ya Mazingaombwe. rafiki yangu usiwe na haraka. Kwa sasa tunajenga hoja tu na kutengenisha hoja na mtu anayetoa hoja. Ni kwa sababu hiyo nimetoa ruhusa kwa makala zangu za kisiasa kuandikwa na mtu yeyote na kutumiwa na mtu yeyote yule. Vitu pekee ambavyo sijaruhusu kunakiliwa ni hadithi zangu, ushairi na kazi nyingine za sanaa. Tanzania Daima wamefanya vizuri kuandika "Mwandishi Maalum" na mimi sina tatizo nalo na lisikuumize kichwa ndugu yangu. Siku nitakapotoka hadharani na kusema mimi ndiye "Mwanakijiji" hawataamini which is good for me kwani kwangu hoja nataka zisimame zenyewe!!

    Mzee ES, na wale watakaojibu hawatahangaika kuuliza mwandishi huyo ni nani na jibu watakalopewa ni mtu mmoja "Mzee Mwanakijiji" au mtu mwingine yoyote! Hivyo badala ya kujaribu kutafuta kumharibia sifa mwandishi (wanaweza kutafuta kunivua uraia kwa sababu baba yangu alizaliwa upande wa pili wa Mto Songwe kabla haujahama na kuwa sehemu ya Malawi!) na Mama yangu alizaliwa siku Idi Amini alipochukua kipande cha Kagera na kufanya iwe Uganda! na mimi mwenyewe nilizaliwa kwenye ndege ya Uingereza ikiwa imeondoka tu Uwanja wa Ndege wa Dallas kuelekea Mexico! LOL So, I can't help but talk about Tanzania!!!!
     
  9. P

    Phillemon Mikael JF Gold Member

    #9
    Jan 25, 2007
    Joined: Nov 5, 2006
    Messages: 8,856
    Likes Received: 2,432
    Trophy Points: 280
    hawa wanamtandao taratibu wanaanza kuonyesha rangi zao,na ukizingatia membe [presidential hopeful] kapata uwaziri wa likizo pale foregn na muungwana EL Yupo magogoni ,kazi imeanza...sidhani hata huyu EL kama atafikia rekodi ya ziro ya vipindi viwili uwaziri mkuu,tayari anaandaliwa jungu achonganishwe na muungwana...ccm kweli haitafika 2010...
     
  10. Lunyungu

    Lunyungu JF-Expert Member

    #10
    Jan 25, 2007
    Joined: Aug 7, 2006
    Messages: 8,836
    Likes Received: 75
    Trophy Points: 145
    Napenda kusema kwamba Makala yako Mzee wa Kijijini baada ya kuona idhini yako niliipenyeza mimi Tanzania daima . Nilisha sema hii ni vita na tutapigana . Niliamua haya mawazo yako yasomwe nyumbani kusaidia kuwaamsha walio lala . Wewe ukiwa nazo nipe mimi nitafanya kaiz hiyo . Ni vyema kusema ili kuondoa kupoteza muda .Kama alisha sema itumiwe basi tumeitumia.
     
  11. Mzee Mwanakijiji

    Mzee Mwanakijiji Platinum Member

    #11
    Jan 25, 2007
    Joined: Mar 10, 2006
    Messages: 31,362
    Likes Received: 6,393
    Trophy Points: 280
    MSB, hamna maneno kabisa!
     
  12. M

    Mwanagenzi JF-Expert Member

    #12
    Jan 25, 2007
    Joined: Sep 11, 2006
    Messages: 690
    Likes Received: 137
    Trophy Points: 160
    Siyo anaandaliwa jungu, huenda baraza lote likavunjwa wakati wa kikao cha bunge cha Jan-Februari au Aprili na yeye kutupwa nje!
     
  13. M

    Mr. Clean Senior Member

    #13
    Jan 25, 2007
    Joined: Aug 7, 2006
    Messages: 195
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 35

    KULA TANO mgumu, btw tusubiri hayo masaa bado 12hrs........!


    ______________________
    "U Can't Change The Nature"
     
  14. Lunyungu

    Lunyungu JF-Expert Member

    #14
    Feb 5, 2007
    Joined: Aug 7, 2006
    Messages: 8,836
    Likes Received: 75
    Trophy Points: 145
    Wana JF
    Najua mko watu wa vyama tofauti hapa. Wako CCM, mko Chadema , Mkanda CUF na wengine UDP nk . Tumeandika sana na kunyoosha vidole . Tanzania ni yetu sote . Sasa baada ya kusoma mawazo yenu kwa muda nimeamka kuja na rai hapa. Ninaomba sasa kwa kuwa sote tuna imani kwa vyama vyetu , na kwa nia si Vyama ni Utanzania , basi ni wakati wa sisis kuamua kurudi na kuanza kujiandaa kugombea nafasi za uongozi na hasa wa Kisiasa na kuingia Bungeni kuliokoa Taifa . Tanzania sasa unaweza kugombea bila kupitia Chama cha siasa kwa maana ya kuwa na Mgombea binafsi. Tunataka kuona wagombea binafsi kwenye uchaguzi modogo wa Jimbo la Akukweti (RIP). Tuache maneno mengi hapa sasa tafakarinni wapi uanzie na uingie ndani kabisa uiokoe Tanzania yetu . Ukipenda Chama sawa na ukipenda kuwa Mgombea binafsi sawa .

    Naomba kutoa hoja .
     
  15. John Mnyika

    John Mnyika Verified User

    #15
    Feb 5, 2007
    Joined: Jun 16, 2006
    Messages: 715
    Likes Received: 21
    Trophy Points: 0
    Lunyungu,

    Wazo zuri ndugu yangu. Watanzania hususani vijana(viongozi wa kizazi kipya) jiandaani kugombea katika uchaguzi mkuu 2010. Ama walau kuwaunga mkono wagombea tunaoona wanafaa.

    Mabadiliko yanatokea pale baadhi ya wananchi makini wanapoamka nakuwa wakala wa mabadiliko wanayotaka kuyaona. Hawa ndio watakaowaongoza wengine kuelekea Tanzania tunayoitaka.

    Kuhusu Tunduru, umegusia kitu kimoja nyeti sana. "Mgombea Binafsi", ajitokeze mtu aonyeshe mfano. Mahakama imetoa haki na kuitaka serikali kuwasilisha bungeni mazingira ya haki hiyo kupatikana. Serikali mpaka sasa badala ya kuandaa sheria ya kuweka mazingira ambayo mahakama imeyapendekeza inahangaika kuandaa mazingira ya kukata rufaa.

    Akitokea Mtikila mmoja, akataka kugombea Tunduru nahisi atanyimwa fomu, akinyimwa ama kuwekewa pingamizi, naye akienda mahakamani kuweka pingamizi naamini Tunduru hapatakuwa na Mbunge mapema kama inavyotarajiwa.

    Ajitokeze mtu basi!!!!!!!!!

    JJ
     
  16. Mzee Mwanakijiji

    Mzee Mwanakijiji Platinum Member

    #16
    Feb 5, 2007
    Joined: Mar 10, 2006
    Messages: 31,362
    Likes Received: 6,393
    Trophy Points: 280
    inabidi nianze kufungasha...!!
     
  17. Lunyungu

    Lunyungu JF-Expert Member

    #17
    Feb 5, 2007
    Joined: Aug 7, 2006
    Messages: 8,836
    Likes Received: 75
    Trophy Points: 145
    Tunduru ndiyo hapo inapotakiwa Watanzania waanze kuchukua haki zao . Amri imesha tolewa mahakamani na kama CCM wana hangaika na rufaa sawa . It is about time Mgombea binafasi kusimama maana sheria na Katiba inampa haki . Wanasheria tuelezeni ile ruling ilikuwa na maana gani . Mgombea hawezi kuwapo hadi Bunge lipitishe sheria ? If no why waiting ? Mnawalea CCM wamelewa madaraka , wanaleta ushabiki na kuanza kutugawa .

    Tuache kuandika pekee , tufanye na vitendo. Nenda hata CCM hatuna maneno we will support you kama una mawazo ambayo tuna yasoma hapa toka kwako juu ya haki za msingi na CCM kuacha uharamia kwa jina la kuungwa mkono na wengi .

    CCM wajiulize why Dar wamejitokeza watu wachache sana ? Je JK kaamini kwamba kweli alipata 80%

    Issue ni vijana kuingia sasa kwenye mapambano . Nendeni hata CCM japouwa najua vijana hamna nafasi kama si mwana mtandao ama mtoto wa fulani na bado vijana ni Taifa la kesho kwao .

    Tuache maneno mengi
    Let's get into actuon and the time is right and is now . Anza kwenda jimboni kwako . Fungua darasa kuanzia leo slowly ujumbe utafika na tuweze kuokoa Tanzania .
     
  18. M

    Mgumu Senior Member

    #18
    Feb 5, 2007
    Joined: Nov 3, 2006
    Messages: 112
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 0
    Mzee MKJJ usifungashe ndugu yangu, kwani nafasi ni chache sana, bila kusahau siasa zetu fitna mbele.

    Watakao penda kugombea ruksa ila wengi tunatakiwa tuwe nje ya system, kuwapa pressure watawala mambo yatakuwa poa.

    Hebu angalia watawala wanavyochanganyikiwa jinsi tunavyowala nyama, hata vijiweni mtaani wanapata hizi habari, japo watoa habari hawasemi moja kwa moja wanazipata jamboforum ' a pressure group' watawala inabidi wachague kujirekebisha au kwenda na maji.

    Mimi nitagombea tu, kama itapitishwa sheria ya kufuta marupupu yanayopufusha wabunge
     
  19. Mtu wa Pwani

    Mtu wa Pwani JF-Expert Member

    #19
    Feb 5, 2007
    Joined: Dec 26, 2006
    Messages: 4,095
    Likes Received: 27
    Trophy Points: 135
    mambo mazuri!!!
    sasa mie nilisoma kwenye gazeti fulani, kuwa kuna viongozi wa upinzani ambao wamependekeza vyama viungane na kusimamisha mghombea mmoja ili wasirejee makosa walioyafanya Uchaguzi uliopita, hili waungwana mnalisemaje?
    Jee kusimamisha wagombea wengi hatuhisi kuwa tunaweza kuifanya CCM kushinda kirahisi kwa kutumia ghilba na kuwagawa wapinzani.
    nnaomba kuwakilisha
     
  20. Kichuguu

    Kichuguu Platinum Member

    #20
    Feb 5, 2007
    Joined: Oct 11, 2006
    Messages: 7,203
    Likes Received: 867
    Trophy Points: 280
    Kutakuwa na Takrima?
     
Loading...