The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Nafikiri umefika wakati wa watanzania kuchagua mtu bila kuongelea chama, maana hivi vyama baadae wanabanwa wanashindwa kuwatetea wananchi kwa kulinda masirahi ya vyama vyao, tuongelee zaidi mtu badala ya vyama, kama inawezekana kuundwa coalition hata kwa kushirikiana na watu waliotoka CCM na vyama vya upinzani na kutafuta mtu ambaye anajali zaidi masirahi ya watanzania.
 
Dr Slaa hongera sana kwa kushinda kesi yako, natumai sasa utaweka nguvu zako na utatathmini kwa umakini maombi yetu ili uwe mgombea wa Urais mwaka 2010. Wengi tuna imani nawe kwenye mapambano dhidi ya Ufisadi, kuondoa umasikini nchini, kuinua uchumi wa nchi, kuboresha huduma za afya na miondombinu, kuleta uwazi kwenye masuala ya haki na kisheria nchini.

CCM haifai tena kuiongoza Tanzania, CCM ni kama mgonjwa wa Kifua Kikuu cha Ufisadi kwani hata wale waliokuwa waadilifu na wakaamua kujiunga na CCM, huishia kuambukizwa na kugeuzwa MAFISADI. Ndani ya CCM kumebakia waadilifu na wazalendo wachache sana ambao hawawezi kuleta mabadiliko yeyote, Ni wewe Dr Slaa ambaye una uwezo wa kuongoza vuguvugu la mabadiliko.

Dr. Slaa for President 2010 (Usalama wa Taifa la Viongozi Mafisadi na Polisi Tanzania msije kusema hii nayo ni Uhaini Nyambaaaf)
 
ni sawa kabisa mtu akaandaliwa wakati bado tunapambana na mfumo mbaya, mjue kuwa slaa ameonyesha ukomavu wa hali ya juu, kama siyo yeye hawa wanaoitwa mafisadi leo wangekuwa wanatanua tu. ni vema tukaunda kitu kama taasisi ya slaa ime kama taa, wengi watafuata na najua hata hapa jf kuna wengi tuu. tukitekeleza hili mafisadi watashtuka, mnakumbuka a story of the bull in the market?

ni hivi, dume la ngombe lilivamia sokoni, kila mchuuzi alikuwa amepanga bidhaa zake tena yaonekana ni vikombe na vyungu vya udongo, hivyo kila mchuuzi alipoliona dume lile likiruka bila mwelekeo akaaknza kulitimua lielekee upande mwingine bidhaa zake zisalimike, muda si mrefu na bila mipangilio kila mmoja akilifukuza likaanza kuvunja hapa na pale fujp tupu.

hivyo mafisadi nao wako hivyo moja likiguswa linajitetea kumbe katika utetezi huo linamtaja na mwenzake.
 
Nafikiri kuna kazi kubwa ya kufanya Tanzania na nikiangalia naona kama Slaa sasa amepata nguvu za kutosha kuendeleza mapambano baada ya kuvuka kisiki kilichokuwa kimewekwa. Bao ni lazima. Sasa ni Moto tuuuuu.
 
Dr. Slaa for President!
Jamani mwee, kinaendela nini hapa mbona wengine tupo kizani?
Ama Chadema wanataka kufanya Uchaguzi ujao ndani ya chama kama wanavyofanya Marekani..
 
Ni vigumu sana kuwashinda hawa Mafisadi kwa sasa katika post ya Upresident, ukizingatia watatumia pesa za BOT kuwadanganya watanzania, na ikibidi za kina Chenge na lowassa.

Ninachoweza kushauri ni kuwa pale ambapo wapinzani wanaweza kufika inabidi wafanye nchini juu kuwaelimisha wananchi wa maeneo hayo na kushinda ubunge, hii itasaidia sana ukikuta sehemu nyingi zina upinzani, itawasaidia pia wao kuweza kupata nguvu pia za kuweza kucompete zaidi next time

Hili swala la kuwaelimisha wananchi ndio Jaji Warioba analipinga inabidi wananchi ndio wawaelimishe viongozi na sio viongozi wawape somo wananchi. Kila kitu lazima kianzie kwa wananachi sio kianzie kwa viongozi kishuke chini.

Kwa kweli nimepevuka sana baada ya kusoma habari hii ya huyu Mzee Warioba hata amesababisha nianze kuamini kuwa itabidi mkombozi mwingine atoke mwitongo kwa Julius Nyerere ndio maana labda hawa watu mungu anawapa maono namna hii hata kuweza kusema wakiwa ndani ya CCM,ni wangapi wameweza kusema kiasi na huku wakiwa bado CCM kama sio huyu na yule mwingine Butiku?

Unabii wa mwalimu utatimia siku moja ya kuwa "Upinzani wa kweli utatoka ndani yao wenyewe,CCM"
 
Dr. Slaa for President!
Jamani mwee, kinaendela nini hapa mbona wengine tupo kizani?
Ama Chadema wanataka kufanya Uchaguzi ujao ndani ya chama kama wanavyofanya Marekani..

HAPANA MSHIKAJI ANAKUBALIKA NA JAMII KULIKO MAELEZA HAYA NINAYOKUPA BELIEVE ME OR NOT.
 
Tuongeze number ya MP, pale bungeni ili tuwe na mshiko wa hoja zetu, habari urais itakuja tu baadaye, wabunge pinzani pale bungeni ni wachache ingekuwa vyema tukaelekeza nguvu yetu kuwapata wabunge wengi ili tuwe na say
 
Tuongeze number ya MP, pale bungeni ili tuwe na mshiko wa hoja zetu, habari urais itakuja tu baadaye, wabunge pinzani pale bungeni ni wachache ingekuwa vyema tukaelekeza nguvu yetu kuwapata wabunge wengi ili tuwe na say
Hao wenzako ndio kina nani hapa JF?
 
IsayaMwita,
Nafahamu vizuri kuwa Dr.Slaa anakubalika sana lakini je, hili sio swala la chama chenyewe?... Je, wenzetu mnazo fununu kuwa Chadema watafanya mchujano wa wazi kati ya kina Freeman, Zitto na Dr. Slaa na wengine Kitaifa?..maanake kumfagilia Dr. Slaa peke yake hakutoshi ndani ya kijiwe hiki kama anavyojaribu kugfanya Geeque ndiko kunanipa hoja unless kuna maelezo zaidi ambayo sikuyasoma.

Again sometime kisiasa mtu anayetisha sana hasa ktk maswala ya ufisadi huwa hapendwi sana kwa sababu wananchi huogopa sheria kali hasa pale ilipokosekana..

Dr. Slaa binafsi nampenda kama kiongozi atakayeweza kusimamia maswala fulani specific akiwa kama Waziri mkuu, Mwanasheria mkuu ama nafasi ambayo anaweza kutumia nguvu zake direct kwa wahusika badala ya kutafuta mtazamo wa wananchi ambao mtu kama yeye watamwita MNOKO.
Kiongozi wa nchi na hasa rais anatakiwa mtu mwenye mvuto, anayeweza kujenga hoja na Muungwana kwa lugha ya Kitanganyika

Sidhani kama Dr. Slaa anaweza pita chaguzi nzito za mikoani kwa sababu nyingi na za kipuuzi lakini zinaweza ku cost chama kizima uchaguzi mkuu... ANAOGOPWA!
 
IsayaMwita,
Nafahamu vizuri kuwa Dr.Slaa anakubalika sana lakini je, hili sio swala la chama chenyewe?... Je, wenzetu mnazo fununu kuwa Chadema watafanya mchujano wa wazi kati ya kina Freeman, Zitto na Dr. Slaa na wengine Kitaifa?..maanake kumfagilia Dr. Slaa peke yake hakutoshi ndani ya kijiwe hiki kama anavyojaribu kugfanya Geeque ndiko kunanipa hoja unless kuna maelezo zaidi ambayo sikuyasoma.
Again sometime kisiasa mtu anayetisha sana hasa ktk maswala ya ufisadi huwa hapendwi sana kwa sababu wananchi huogopa sheria kali hasa pale ilipokosekana..
Dr. Slaa binafsi nampenda kama kiongozi atakayeweza kusimamia maswala fulani specific akiwa kama Waziri mkuu, Mwanasheria mkuu ama nafasi ambayo anaweza kutumia nguvu zake direct kwa wahusika badala ya kutafuta mtazamo wa wananchi ambao mtu kama yeye watamwita MNOKO.
Kiongozi wa nchi na hasa rais anatakiwa mtu mwenye mvuto, anayeweza kujenga hoja na Muungwana kwa lugha ya Kitanganyika...Sidhani kama Dr. Slaa anaweza pita chaguzi nzito za mikoani kwa sababu nyingi na za kipuuzi lakini zinaweza ku cost chama kizima uchaguzi mkuu... ANAOGOPWA!

kwa mujibu wa ushirikiano uliopo kati ya chadema,cuf,nccr na tlp, 2010 wanasimamisha mgombea mmoja, labda tujaribu kuona vyama vingine vinamtazamaje
 
Waridi,
kwa mujibu wa ushirikiano uliopo kati ya chadema,cuf,nccr na tlp, 2010 wanasimamisha mgombea mmoja, labda tujaribu kuona vyama vingine vinamtazamaje
Nilipitwa na hili... Duh this is very very Good news kabisa.. sasa nimewapata wakubwa na nakubaliana na hoja nzima ya Dr. Slaa..lakini ktk tungule langu la Kikerewe naogopa sana ujinga wa Mdanganyika!..
 
Waridi,

Nilipitwa na hili... Duh this is very very Good news kabisa.. sasa nimewapata wakubwa na nakubaliana na hoja nzima ya Dr. Slaa..lakini ktk tungule langu la Kikerewe naogopa sana ujinga wa Mdanganyika!..
Wakuu... Naomba hizi hoja mbili (Kuhusu Mengi na Dr. Slaa kufaa kuwa Pres candidates) nizifunge kwa muda kwakuwa kuna hoja kubwa inakuja na ambayo nadhani itaweza kubadili sura kabisa ya mijadala hii. Naomba msiendelee kujadili hizi hoja mbili kwa sasa hadi mwishoni au hata kabla ya Ijumaa wiki hii wahusika watakapotoa kauli zao ambazo ndizo zitakuwa guidelines za mijadala hii. Natumaini mjadala unaokuja (wiki hii) utaibua maswali mengi na kupanua mijadala hii.

Shukrani,

Invisible
 
Wajipanga kwa urais

Mwandishi Wetu Mei 21, 2008

Slaa, Hamad kusimama upinzani


Zitto kuwaunga mkono


Masha, Membe watajwa CCM

MIAKA miwili tu kabla ya Rais Jakaya Kikwete kumaliza kipindi chake cha kwanza mwaka 2010 na huku serikali yake ikiandamwa na kashfa za ufisadi, wanasiasa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na wale wa upinzani wanajipanga kwa nia ya kujiandaa kushika nafasi hiyo, Raia Mwema imefahamishwa.

Habari zinaeleza kwamba kwa sasa baadhi ya wana CCM wanajenga msingi wa kuwawezesha kumrithi Rais Kikwete katika uchaguzi mkuu ujao lakini wakishindwa, angalau basi kwa uchaguzi mwingine wa 2015; huku wapinzani wao wakipania kuchukua madaraka mwaka 2010, wakitumia kuyumba kwa nchi katika sehemu kubwa ya awamu ya kwanza ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne.

Kwa mujibu wa habari hizo, tayari mazungumzo na mikakati imekuwa ikifanyika katika maeneo mbalimbali nchini kwa nia ya kuangalia wanasiasa wanaoweza kushika nafasi ya urais, lakini pia kuwazuia wale ambao wanahofiwa kuweza kuharibu mikakati hiyo.

Wanasiasa kadhaa wakubwa nchini wa sasa, wastaafu na hata wale walioguswa na kashfa, wamekuwa wakitajwa moja kwa moja kujihusisha katika mikakati hiyo ama kwa kupima upepo kama wanaweza kujitokeza wao au kwa kuandaa watu wanaowaunga mkono.

Kwa upande wa upinzani, wanasiasa wapya kabisa wanatajwa kuweza kuibuka na kwa kupishwa na wanasiasa waliogombea katika Uchaguzi Mkuu uliopita, ikiwa ni mkakati unaoelezwa kujaribu kuwavuta wapiga kura wengi.

Imeelezwa kwamba waliogombea katika chaguzi za nyuma ikiwa ni pamoja na ule wa mwaka 2005, kupitia vyama vya upinzani, wanaweza kuwaunga mkono wagombea watakaouzika katika uchaguzi wa mwaka 2010.

Wanaopewa nafasi kubwa zaidi ya kuweza kusimamishwa kwa nafasi ya urais kwa upande wa upinzani ni pamoja na Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa na Kiongozi wa Upinzani ndani ya Bunge, Hamad Rashid Mohamed, ambao wanaelezwa kuweza kukubaliana mmoja akawa Mgombea Mwenza.

Wanasiasa hao wa upinzani wanaelezwa kusukumwa zaidi na wabunge wenzao pamoja na watu wa kawaida wanaofuatilia mwenendo wa kisiasa nchini hasa kutokana na mchango wao ndani ya Bunge ambalo limebadili hali ya kisiasa nchini kwa kurudisha mwamko wa wabunge na wananchi.

Hamad Rashid amelithibitishia Raia Mwema jana kwamba ameshauriwa kujiandaa kuwania urais mwaka 2015 lakini baadhi wametaka aanze mwaka 2010, akiwataja baadhi ya wabunge waliomshauri, wakiwamo hata wa Chama cha Mapinduzi (CCM).

“Ni kweli nina nia ya kuwania urais lakini si wa Zanzibar na kwamba nilijiandaa kwa mwaka 2015, lakini wabunge wenzangu baadhi kutoka CCM wamenishauri nianze kujitokeza mwaka 2010,” alisema Hamad, ambaye amewahi kuwa ndani ya Serikali ya Muungano katika wizara za Fedha na baadaye Mambo ya Ndani.

Akizungumzia suala hilo, Dk. Slaa alisema sasa ni mapema mno kuzungumzia mambo ya urais kutokana na nchi kuwa katika harakati za kupambana na ufisadi unaoihusisha hata Ikulu yenyewe.

Alisema Dk. Slaa: “Bado tuko mbali tukipambana na ufisadi. Nchi haitaki wanaokimbilia Ikulu. Inataka wenye ujasiri wa kusafisha Ikulu. Ukisema nawe unakimbilia Ikulu, unakuwa unataka ukafanye biashara au ukachote Ikulu. Wakati ukifika, hayo tutayajadili.”

Kwingineko kumekuwa na minong’ono kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Chacha Wangwe pia ana nia ya kugombea kwa tiketi ya chama. Nia ya kuwania urais ya viongozi hao wawili huenda ikawagombanisha na mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, aliyesimama mwaka 2005 na ambaye inaaminika angependa asimame tena mwaka 2010.

Alipoulizwa kuhusu habari hizo za yeye kutajwa kuwania urais, Chache Wangwe alisema, “Ni kweli, ikiwa chama changu kitanipendekeza, nitakua tayari kugombea.”

Mkanganyiko mwingine wa Chadema unaweza kutokana na habari kwamba Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, akizungumza na Watanzania walioko Houston, Marekani alikokuwa kwa ziara hivi karibuni, alisema atawaunga mkono Dk. Slaa na Hamad kama mazingira ya kisiasa yatawafikisha watu hao wawili katika kugombea mwaka 2010.

Siku za karibuni zimeshuhudia kutoaminiana miongoni mwa viongozi wa Chadema na hata kumhusisha Zitto na madai ya kuwa na urafiki wa karibu na Rais Kikwete, kiasi cha Kikwete kutaka kumteua kuwa waziri katika Serikali kabla ya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ya Februari mwaka huu.

Zitto ameiambia Raia Mwema wiki katika mahojiano kuwa wakati hapingi kuwa ana ukaribu wa kiasi fulani wa siku nyingi na Rais Kikwete, hakuna wakati alipotaka kuingia katika serikali yake.

“Sijawahi kuombwa na Rais Kikwete kuingia katika serikali. Msimamo wangu siku zote umekuwa ni kutumikia taifa bila kujali itikadi. Hata Rais anajua hili, kwamba siwezi kuhama chama au kwenda kinyume na maamuzi ya chama changu. Kwamba Rais Kikwete ni rafiki yangu, si kweli. Ninafahamiana naye kitambo. Ninajua ananiheshimu sana. Lakini hakuwa chaguo langu la urais wakati wa mchakato wa chama chao na hata katika uchaguzi mkuu,” alisema Zitto.

Lakini wafuatiliaji wa masuala ya kisiasa wanasema Zitto hajawahi kusikika akimshambulia Rais Kikwete katika hotuba zake na mara kadhaa amekuwa akimsifia katika maamuzi yake mbalimbali ambayo yamepingwa na wenzake. Hata kuingizwa kwake katika Kamati ya Madini ya Jaji Mark Bomani kulizua maswali mengi kutoka kwa wanasiasa wa CCM iliyombana alipoibua hoja ya mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, na wa Upinzani.

Wengi hawaamini maelezo ya Zitto kwani anaonekana ni mtu mwenye kujiandaa kutokana na kuwa kwake na mahusiano ya karibu sana na wastaafu kama Jaji Joseph Warioba na Dk. Salim Ahmed Salim, watu ambao wana ushawishi mkubwa katika jamii.

Alipoulizwa kuhusu hili Zitto alisema kuwa yeye anawaheshimu sana viongozi wastaafu na hupenda kujifunza kutoka kwao na mahusiano yake nao hayana maana ya kutafuta kuungwa mkono.

“Nimekuwa na mahusiano na wazee hawa kama viongozi. Sio hawa tu. Ninazungumza na mzee Kaduma (Ibrahim), mzee Butiku (Joseph), mzee Kimiti (Paul) na mzee Jackson Makweta. Pia ninazungumza sana na Spika Samuel Sitta. Huwezi kusema hawa wote wananiandaa mimi kuwa Rais. Huo ni woga tu wa watu. Ni hulka yangu kuheshimu wakubwa na kujifunza ndiyo maana ukinikuta na Hamad Rashid hutaona mahusiano ya kiubunge. Utaona mahusiano ya mwalimu na mwanafunzi,” anasema Zitto ambaye mwaka jana gazeti moja la kila wiki lilimshutumu kwa kujipendekeza kwa viongozi wakubwa.

Kwa upande wa CCM, habari zinaeleza kwamba tayari makundi yameanza kujipanga kwa uchaguzi mkuu wa Rais mwaka 2010 na wa 2015 kama Rais Jakaya Kikwete atafanikiwa kushinda patashika ya mwaka 2010 na kuendelea muhula wa pili ambao ni wa mwisho kwa mujibu wa katiba.

Makundi hayo yanajipanga mapema na kwa kuanzia imeelezwa kwamba wanasiasa na wafanyabiashara wanajiandaa kuweza kupata wajumbe wa kutosha katika Mkutano Mkuu wakati wa uchaguzi, wajumbe ambao ndio watakuwa waamuzi wakubwa wa mgombea kutoka chama hicho.

Licha ya kwamba kuna fununu za wagombea wengine kujitokeza kushindana na Rais Kikwete katika kinyanganyiro cha ndani ya CCM mwaka 2010, inaonekana uwezekano wa ushindi ni mdogo kutokana na utamaduni wa CCM kuendeleza muhula wa pili wa Rais aliyeko madarakani utaendelea. Hata hivyo, hali inaweza kubadilika kama Kikwete atakumbwa na dhoruba yoyote kubwa ya kisiasa kabla au kuelekea 2010.

Magazeti kadhaa, hivi karibuni, yalimtaja Profesa Mark Mwandosya kama mgombea anayetajwa kuweza kumkabili Rais Kikwete ikifika mwaka 2010. Mwandosya alikuwamo katika hatua za mwisho za mbio za urais mwaka 2005.

Wengine wanaotajwa kwa sasa kwa upande wa CCM kujiandaa ama kuandaliwa kumrithi Kikwete, iwe 2010 au 2015, ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani Lawrance Masha na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

Kumekuwapo pia na mijadala ya Watanzania, na hasa walioko nje, inayotaka Dk. Salim agombee ama kupitia CCM au kupitia muungano wa vyama vya upinzani. Yeye na Profesa Mwandosya walishindwa na Kikwete 2005, wote wakiwa wamefikia hatua ya mwisho kabisa.
 
kikwete anaweza kuwa forced kutumia brutality na corruption kuliko ya 2005 ili ku cling to power.

One thing is certain, kama ataondoka ni kwa kutaka yeye mwenyewe lakini hakuna kitakachomzuia kuiba kura na pesa ili kurudi Ikulu mpaka 2015.

Hatuna utamaduni wa a one term president.
 
Wajipanga kwa urais

Mwandishi Wetu Mei 21, 2008

........
Kumekuwapo pia na mijadala ya Watanzania, na hasa walioko nje, inayotaka Dk. Salim agombee ama kupitia CCM au kupitia muungano wa vyama vya upinzani. Yeye na Profesa Mwandosya walishindwa na Kikwete 2005, wote wakiwa wamefikia hatua ya mwisho kabisa.
Natumai hapa inazungumzwa JF
 
Kwa hiyo Hamad Rashid mwaka 2010 siyo kwamba anataka kugombea kwa lengo la kushinda bali anataka "kuanza kujitokeza"!
 
Mi nakwambia tuna kazi, unafikiri kazi ndogo?

Na huyu ni one of the brightest bulbs of the lot, amewahi kufanya kazi ya Uwaziri and all na sasa ni kiongozi wa upinzani bungeni lakini kupanga maneno tu kazi.

Halafu hapo hapo anadaiwa kuwa katika joint ticket na Slaa, huku Slaa anabonda kuzungumzia Ikulu mapema (rightfully I believe) huku mgombea mwenza wake kashaanza kujiweka sawa na kuongea.

And this disease called Chacha Wangwe has the audacity to entertain thinking it has a snowball's chance in hell of becoming president.

If Chacha Wangwe will become president then I will be the British Monarch.
 
Back
Top Bottom