The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
Lowassa kasafishwa na NEC,lengo lao na Lowassa inaweza ikawa mapema zaidi ya hapo,ila what i know ni kwamba Dk. Hussein Mwinyi is Going to take Over then after Muungwana.
 
CCM ninayoifahamu kidogo haina "mpango" wa KUMWONDOA Kikwete hiyo 2010 labda kwa mapenzi ya Mungu. Na ninavyowafahamu WaTz na CCM yao mmh!
 
Lowassa kasafishwa na NEC,lengo lao na Lowassa inaweza ikawa mapema zaidi ya hapo,ila what i know ni kwamba Dk. Hussein Mwinyi is Going to take Over then after Muungwana.

Lowassa anajipanga kurithi shoga yake ndiyo maana wanamsafisha. Hiyo ndoto yake ya kuwa Rais namsifu kweli
 
Lowassa anajipanga kurithi shoga yake ndiyo maana wanamsafisha. Hiyo ndoto yake ya kuwa Rais namsifu kweli

Lowassa hafai kuwa RAis wa Nchi hata siku moja,wewe unajiuzuru kwa kosa ambalo unasema hulijui,atatuingiza matatani..

ni mmoja wa watu ambo mie niliwadharao sana,angejitetee Bungeni na siyo kujieleza pembeni,ni tabia za ajabu na kuishiwa sera.
 
zanzibar atachukua hussein mwinyi, na bara atakaa kikwete.
zanzibar upinzani atasimama sharif, na bara watasimama msururu mzima.

watakaoshika nyadhifa sio watakaokuwa wanapendwa na watu, lakini ccm ina nguvu kiasi cha kuwa bado haiwezi kupokonywa urais.
 
Naomba kutoa changamoto kwa wote wana CCM na wale ambao si Wana CCM.

Je ni nani mawazoni mwenu mnafikiri atafaa kuwa mgombea wa Urais wa Muungano kwa upande unaoutaka? Naomba ukitoa jina utoe na sababu pamoja na wasifu wa kutosha kutokana na mgombea huyu unayemdhania.

Ni nani watafaa kugombea Urais Zanzibar? same rule apply, name, reason and work history.

Natanguliza shukrani.

Mimi bado napendekeza kile nilichopendekeza mwanzoni.

2010 - Kikwete ataendelea
2015 - Dr Hussein Mwinyi
2025 - Ridhiwani Kikwete
2035 - Binti wa Karume atakuwa raisi wa kwanza Tanzania Mwanamke.
 
Rev Kishoka,

Mada uliyo ianzisha ni nzuri na ni muhimu sana katika kujadili mustakbali wa nchi yetu.

Wengi wa wachangiaji wamemzungumzia Dr Salim kuwa angefaa kuwa Rais wetu lakini yaliyotokeakwa sasa ni history. Hata hivyo mimi nasema Dr Salim bado ana nafasi la kulitumikia taifa letu katika nafasi ya juu na ningependelea awe Rais ( Mgombea wa Urais ) kwa upande wa Zanzibar comes 2010.

Sifa na vigezo vya chaguo langu hili ni nyingi na ni obvious, lakini kwa kujazia tu pamoja na udhoefu mkubwa katika medani za kimataifa na kitaifa, Dr Salim atasaidia kuondoa/kupunguza kile kinachoitwa mpasuko ndani ya Zanzibar.

Kuna hii notion (sijui imetoka wapi) kuwa Mpemba hawezi kuwa Rais Zanzibar hata kama ana uwezo kiasi gani, Salim atasaidia sana kupunguza munkari wa wa wapemba wa kuona wanabaguliwa.

Tatizo kubwa litakuwa wahafidhina wa Unguja ( Commando, Dr Bilali, Shamhuna, Nahodha, Seif Khatib et al ) watamkataa ( kama walivyo mkataa kabla ) Bado naamini rungu la NEC - Taifa lilotumika kumuingiza Karume 2000 ( japo NEC_ Zanzibar walimkataa) inabidi litumike tena mara kumuingiza Salim

Rais wa Muungano

2010 haina ubishi ni JK tena atleast kwa "utaratibu" wa Ki- CCM. Na 2015 naamini Benard Membe could make good presidency kwa vigezo vya elimu, exposure na udhoefu. Kwenye mtiririko huo kuna akina Mwandosya, Asha-Rose Migiro, na wale vijana wanaojiita Victoria Club ( Ngereja, Masha, Maige ) could do better given a chance
 
Mimi bado napendekeza kile nilichopendekeza mwanzoni.

2010 - Kikwete ataendelea
2015 - Dr Hussein Mwinyi
2025 - Ridhiwani Kikwete
2035 - Binti wa Karume atakuwa raisi wa kwanza Tanzania Mwanamke.

Mimi nadhani itakuwa hivi:

Zanzibar - 2010 Dr Hussein Mwinyi
Tanzania - 2010 Kikwete ataendelea

Zanzibar - 2015 Balozi Ali Karume
Tanzania - 2015 Dr Hussein Mwinyi
 
Kwa upande wa CCM kigezo muhimu ni lazima uwe huna uwezo (competence), uwe na uwezo wa ujanjaujanja, uswahili, kampeni za chinichini, n.k. Kwa sifa hizi Salim, Warioba weka pembeni. Ingiza Membe, Masha, Nchimbi, Chiligati, Makala, etc.
 
Kwa upande wa CCM kigezo muhimu ni lazima uwe huna uwezo (competence), uwe na uwezo wa ujanjaujanja, uswahili, kampeni za chinichini, n.k. Kwa sifa hizi Salim, Warioba weka pembeni. Ingiza Membe, Masha, Nchimbi, Chiligati, Makala, etc.

Mkuu umemsahau waziri wako wa fedha........ ustaadhi enhee! Mkulo
 
Kwa upande wa CCM kigezo muhimu ni lazima uwe huna uwezo (competence), uwe na uwezo wa ujanjaujanja, uswahili, kampeni za chinichini, n.k. Kwa sifa hizi Salim, Warioba weka pembeni. Ingiza Membe, Masha, Nchimbi, Chiligati, Makala, etc.

Swali la Rev ni nani tunayemuona anafaa kuwa Rais 2010, hivyo ni lazima awe na uwezo kutokana na tunavyomuona sisi na siyo vice versa.
 
Binafsi napendekeza wafuatao:

1. Dr.Wilbroad Slaa

Ni mzoefu, shujaa na mtu mwenye uthubutu. Ni mzalendo na hatetereki kwenye maamuzi yake. Ameweza kusimama na kujenga hoja mbalimbali kwa manufaa ya wananchi walio wengi.

2. Dr.Mohamed Shein

Ni mzoefu na hana makundi. Hana papara. Hana ubinafsi. Hachezi siasa za majitaka. Atakuwa kiongozi mzuri kama urais wake usipokuwa na ubia na mtu.

Nyongeza:

1. Mhe. Rais J.M.Kikwete. Huyu ameshindwa kurejesha matumaini ya Watanzania. Alionekana mzoefu na aliyejiandaa kuongoza nchi ili isonge mbele. Ukweli umejidhihirisha kwamba hakuwa mtu wa hivyo. Ameshindwa kuwawajibisha viongozi wabovu na kukemea uovu.Ameshindwa kuendeleza uchumi, na kuboresha huduma za jamii. Napendekeza asirudie kugombea 2010.
 
CCM ninayoifahamu kidogo haina "mpango" wa KUMWONDOA Kikwete hiyo 2010 labda kwa mapenzi ya Mungu. Na ninavyowafahamu WaTz na CCM yao mmh!

Kimsingi wewe ndio umedhihirisha kwamba umekomaa kisiasa.Maana mtu aliyekomaa kisiasa anatakuja na maoni yenye kuelezea ukweli wa mambo kama ulivosema wewe.Itakuwa ni kupoteza muda hapa kuanza kufikiria suala la mgombea wa CCM mwaka 2010. Ni wazi kwamba mgombea wa CCM mwaka 2010 nafasi ya urais wa muungano ni Mh.

Rais Jakaya Kikwete. Hilo wala halina ubishi. Labda kwa wale wenye hulka ya kuweka ligi isiyokuwa na maana ndio wanaweza kupingana na ukweli huo. Hata wanaCCM makini wanaoota ndoto za urais hawaoti ndoto za urais kwa 2010, bali wamejielekeza mwaka 2015 pindi kipindi chake kitakapokuwa kimeisha.

Sababu kubwa ni kwamba huo ndio utamaduni wa chama.Sasa kama kuna mtu anamkataa JK na CCM kwa ujumla kwa sababu zozote zile, basi hilo ni suala lake binafsi na ni haki yake kufanya hivyo.

Sasa kwa mtu yeyote asiyeridhika na uongozi wa JK/CCM njia pekee na inayoweza kutekelezeka ni kumkataa kwenye kura tu,sio hapa JF wala kwingineko.itakuwa ni kusumbua vichwa vya watu hapa kuanzisha mjadala ambao hauna tija na ni dhahiri kwamba uko kinyume na hali halisi ya mambo.

Kama tunazungumzia urais wa Tanzania visiwani,hilo sawa. Linajadilika kwa sababu Rais wa sasa Mh.Aman Karume, anazuiwa na katiba ya Zanzibar kuendelea na kipindi cha tatu cha utawala. Hivyo ni lazima CCM impitishe mwanachama mwingine kuwania nafasi hiyo.

Sasa, kwa upande wa Zanzibar mimi binafsi, kwa mtizamo wangu na kwa vigezo vyangu,namauona Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh.Dr.Mohamed Shein kama anafaa.Sababu ziko nyingi,lakini kwa kutaja baadhi tu:
1.Ni mzanzibar
2.Ana akili timamu
3.Ni msomi mzuri
4.Ni mtulivu
5.Ana uzoefu wa uongozi.Nina amini kwa kufikia ngazi ya umakamu wa Rais wa jamhuri ya muungano kumempa nafasi ya kupata uzoefu wa uongozi.

Lakini zaidi ni kwamba ofisi yake ya makamu wa rais wa muungano ndio kiungo cha Muungano wa bara na visiwani.

Kwa hiyo, kwa kuwepo kwake katika ofisi hiyo kumempa nafasi ya kuijua vema Tanzania bara na hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kuyashughulikia masuala ya muungano kwa umakini na ufanisi wa hali ya juu.
 
Rev. Kishoka,
Mkuu utanisamehe sana, najua umetaka majina lakini nitatoka nje na kabla ya yote ni lazima nikueleze azma yangu ktk swala hili.

Jina la mtu kutuongoza nalipinga sana kwa sababu hakuna mtu mmoja anayeweza kuongoza nchi..Hata ile yenye ubora ktk sekta zote!.. Tumewahi kuzungumza haya huko nyuma na kama leo tutaendelea kufikiria hivyo basi yaonyesha wazi kuwa sisi ni mfano bora wa viongozi hao hao.

Mkuu huyo mtu ataongoza kitu gani ikiwa nchi nzima ni corrupt!... ebu soma tena ile report ya EPA, mkuu inatisha jinsi viongozi wetu walivyojaa kiburi.
Haiwezekani kabisa wananchi wakamtazama mtu ama niseme nahodha wakati hawana chombo madhubuti cha kusafiria.

CCM ambayo ndio chombo imeingiwa na tobo kibao za kuingiza maji as a fact baadhi ya machine zake hazifanyi kazi.. kibaya zaidsi ni kwamba tunadanganywa kuwa hakuna tatizo!

Sasa kama tutasimama hapa na kusema nani anaweza kutuongoza ktk jahazi ambalo linaingiza maji sidhani kama ni akili hata kidogo...Labda tuulizane nani anaweza kuliziba jahazi hili ama tunahitaji chombo kipya kabla ya kumtafuta nahodha..

Sam,
Mkuu ni makosa makubwa sana kufikiria kwamba tatizo la Tanzania ni UCHUMI sio SIASA.

Kinachotakiwa haswa ni UCHUMI kutawala SIASA lakini Tanzania hadi leo hii SIASA ndizo zinatawala UCHUMI... hivyo ni muhimu kutazama siasa hizo kwanza.

Unachoshindwa kutazama hapa labda kutokana na unazi ama upendo wako ni kwamba UCHUMI wa nchi yoyote ile huongozwa na sera za chama!.. Zimbabwe leo ipo hatarini Kiuchumi ni kutokana na SIASA!..wao kama sisi, Kisha basi hata Marekani leo inashuka chini ni kutokana na SIASA ingwajewao siasa hizo hutazama malengo ya KIUCHUMI na hao Wachina watapanda juu ni kutokana na SIASA kutawala Uchumi!...kwa sababu ni SIASA ambayo inaunda policies zinazoiwezesha nchi kufanya biashara na kulinda maslahi ya nchi hiyo!..Kwa hiyo muhimu sana ufahamu chanzo cha kila kitu ktk mazingira yake.

Sasa basi usije rudisha SIASA kwa mtazamo wa zamani yaani siasa za magharibi na mashariki laaa! siku hizi ni SIASA zinazoambatana na UCHUMI zikiongozwa na mrengo...Tanzania hatuna kitu hicho...tunakwenda kufuata upepo!..that's where the problem starts!
UHUJUMU UCHUMI huu haukutokea kwa bahati mbaya hata kidogo!... Ni SIASA za AZIMIO la ZANZIBAR ndizo zilizoweka tobo kubwa.

Sasa nambie katika Azimio hilo la Zanzibar ni mtaalam gani wa Uchumi alihusishwa?..
Je, sio sisi tuliomlaumu mwalimu kwa Azimio la Arusha na kudai kwamba mwalimu hakuwasikia wataalam wa uchumi?... na kitu gani hasa kinachoplaumiwa leo kutokana na kushindwa kwetu kiuchumi kama sio siasa za mwalimu..

Mkuu hata mimi binafsi ambaye siku zote humtetea mwalimu najua fika kwamba matatizo yoite yaliyotukuta wakati wake yalisababishwa na SIASA..Iwe kupungua kwa mikopo, vita ya Uganda ama ukame wa chakula!...
Tanzania yenye maziwa makuu zaidi ya matano haiwezi kuwa ktk kundi moja na Ethiopia hata kidogo.

Siasa ndizo zinatunangusha na hao wote Mafisadi unaowazungumzia ndio Wanasiasa, Wabunge, Mawaziri na Wataalam wenye sauti ya wapi jahazi hili liende!..Ndio manahodha, mainjinia, navigator na kadhalika...hivyo hatuwezi kukuza uchumi ktk jahazi lenye kuingiza maji hata kama tutajitahidi kiasi gani..

Tuzibe tobo zilizopo kwanza na haiwezekani kuziba tobo hizi Kiuchumi ila kisiasa kwanza kwa sababu Katiba na sheria za nchi yoyote ile hupitishwa na wanasiasa sio wataalam -wanasheria.
Mwanasheria (hakimu) ataifanya kazi yake ikiwa mashtaka yatafunguliwa lakini kama hakuna kesi inayokwenda mahakamani mkuu sijui huyo hakimu utamweka wapi kuwa ndio muhimu!..
Siku zote mkuu kwanza tazama mzizi wa kitu kabla kuharukia matawi ya juu..Uchumi wa nchi hauendi hivyo!
 
Kimsingi wewe ndio umedhihirisha kwamba umekomaa kisiasa.Maana mtu aliyekomaa kisiasa anatakuja na maoni yenye kuelezea ukweli wa mambo kama ulivosema wewe.Itakuwa ni kupoteza muda hapa kuanza kufikiria suala la mgombea wa CCM mwaka 2010. Ni wazi kwamba mgombea wa CCM mwaka 2010 nafasi ya urais wa muungano ni Mh.Rais Jakaya Kikwete.Hilo wala halina ubishi.Labda kwa wale wenye hulka ya kuweka ligi isiyokuwa na maana ndio wanaweza kupingana na ukweli huo.Hata wanaCCM makini wanaoota ndoto za urais hawaoti ndoto za urais kwa 2010,bali wamejielekeza mwaka 2015 pindi kipindi chake kitakapokuwa kimeisha.Sababu kubwa ni kwamba huo ndio utamaduni wa chama.Sasa kama kuna mtu anamkataa JK na CCM kwa ujumla kwa sababu zozote zile, basi hilo ni suala lake binafsi na ni haki yake kufanya hivyo.Sasa kwa mtu yeyote asiyeridhika na uongozi wa JK/CCM njia pekee na inayoweza kutekelezeka ni kumkataa kwenye kura tu,sio hapa JF wala kwingineko.itakuwa ni kusumbua vichwa vya watu hapa kuanzisha mjadala ambao hauna tija na ni dhahiri kwamba uko kinyume na hali halisi ya mambo.
Kama tunazungumzia urais wa Tanzania visiwani,hilo sawa. Linajadilika kwa sababu Rais wa sasa Mh.Aman Karume,anazuiwa na katiba ya Zanzibar kuendelea na kipindi cha tatu cha utawala.Hivyo ni lazima CCM impitishe mwanachama mwingine kuwania nafasi hiyo.
Sasa, kwa upande wa Zanzibar mimi binafsi,kwa mtizamo wangu na kwa vigezo vyangu,namauona Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Mh.Dr.Mohamed Shein kama anafaa.Sababu ziko nyingi,lakini kwa kutaja baadhi tu:
1.Ni mzanzibar
2.Ana akili timamu
3.Ni msomi mzuri
4.Ni mtulivu
5.Ana uzoefu wa uongozi.Nina amini kwa kufikia ngazi ya umakamu wa Rais wa jamhuri ya muungano kumempa nafasi ya kupata uzoefu wa uongozi.Lakini zaidi ni kwamba ofisi yake ya makamu wa rais wa muungano ndio kiungo cha Muungano wa bara na visiwani.Kwa hiyo, kwa kuwepo kwake katika ofisi hiyo kumempa nafasi ya kuijua vema Tanzania bara na hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kuyashughulikia masuala ya muungano kwa umakini na ufanisi wa hali ya juu.

Shein pamoja na yote hayo hafai. Huyu jamaa ni soft mno na kwenye politics za kibabe kama za Zanzibar watam bully sana. Tumuache hapoa alipo walau sasa anapumua kidog maana zama zile za Lowassa alikuwa anafunika kila kitu na kumuachia mzee kazi za kukagua bucha za nyama na mitaro tu
 
Mkandara,

Nimekupata na hapajaharibika neno!

Umeongea kwa ufasaha sana na hoja yangu kujtaka majina na wasifu ni kujua je ni nani kati yetu sisi Watanzania awe wa CCM au si wa CCM ambaye tunamuamini anaweza kutuongoza 2010? Kutuongoza huku si kwa mkao mmoja bali ni kwa jinsi ulivyonyumbulisha
 
Listi hii ilitolewa na INVISBLE..Nafikiri kuna majina ya kujadili humu..Hata hivyo bado sijataka kutoa full support kwa yoyote sasa hivi hadi pale tutakapoona kweli tunayempigia kura ni mzalendo.
  1. Dr. Wilbroad Slaa
  2. Dr. Husein Mwinyi
  3. Ndugu R. Mengi
  4. Zitto?
  5. Freeman?
  6. Mrema?
  7. Membe?
  8. Mwakyembe?
  9. Mwanakijiji? (Hahaha hapo najua nachokoza)
  10. Maalim Seif?
  11. Lipumba?
  12. Dr. Mvungi?
  13. Mbatia?
Nani hasa?
 
Rev. Kishoka,
Basi kama tunamtafuta mkombozi wetu nadiriki kusema kuna watu wawili tu wote toka Chadema Freeman Mbowe na Dr. Slaa...watu hawa hawaogopi na wakipata mwanya wamekwisha.

Na kama tutaangalia CCM basi namkubali Salim A salim kwa sababu ktk hali tuliyokuwa nayo sasa hivi anatakiwa MJAMAA peke yake... iwe turudi nyumba Mungu atatusaidia mbeleni..Salim pekee ndiye anaheshimika na jeshi letu na mweye msimamo usiopendwa na viongozi WOTE walioshika madaraka sasa hivi.

Ukombozi kwanza kutoka makucha ya Mafisadi... hapa nakubaliana sana na lugha ya Jmushi1...
Mrema kusema kweli simuamini sana kwa sababu kisha wahi kutugeuka zamani akawa fisadi kama hawa..Mrema ana nunulika kirahisi!
 
Mkandara

Huko alikopita SAS umewahi kufuatilia, achilia mbali alipokuwa UN. Wakati akiwa PM, AU n.k.

Hii thread nilikuwa naipiga chenga kumbe watu wanapiga kampeni hapa, haya ngoja tuone lakini mawazo yangu CCM kumeoza sana wasituambie ati wana wapiga kura wengi vijijini, mfumuko wa bei utawajanjarusha walioka vijijini na vile vile wengi wana ndugu mijini CCM wang'olewe tu hiyo ndio dawa ili wawe wapinzani. CCM wanachofahamu ni kuwapa wageni tax holiday etc.
 
Back
Top Bottom