The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

 • Edward Lowassa

  Votes: 0 0.0%
 • Dr. Slaa

  Votes: 7 38.9%
 • Prof. Lipumba

  Votes: 0 0.0%
 • Mizengo Pinda

  Votes: 5 27.8%
 • Samwel Sitta

  Votes: 0 0.0%
 • Jakaya Kikwete

  Votes: 2 11.1%
 • Mark Mwandosya

  Votes: 2 11.1%
 • Harisson Mwakyembe

  Votes: 2 11.1%
 • None of The above

  Votes: 0 0.0%

 • Total voters
  18
 • Poll closed .

Elisante Yona

Senior Member
Oct 6, 2009
130
195
Ndugu Kwanza napenda kuwapongeza JF kwa kuwa hewani tena Mungu Abariki Kazi yenu,

Kwa hili la kuelekea uchaguzi wa 2010 shughuli ni ngumu kwa chama tawala kwa sababu hawaja timiza ahadi zao hasa ile ya kuleta maisha bora kwa kila Mtanzania,pili suala ajira ambalo Mheshimiwa aliahadi kwamba atawapatia vijana Ajira hakuna kitu,

Kwa maoni yangu ninawaomba Watanzania wenzangu tumpigie kura mtu ambaye ukimwangalia utasema anaweza kututoa hatua moja kwenda nyingine

Hawa jamaa hasa wabunge wamepoteza muda mwingi kujadili ufisadi na Richmond na kusahau kuwa wananchi kwenye majimbo yao wana matatizo kwa mfano Barabara ni mbovu vijiji,Hakuna maji safi na salama,Hospitali ndio dawa hakuna wagonjwa wanalala wanne kwenye kitanda kimoja,lakini mbunge anatembelea Prado ya milioni 70 hadi 80

Wananchi tuwe makini na tusidanganyike na virushwa vyao vya soda,wali,kuku,na bia na kuuza haki yetu kwa miaka mitano

Ni hayo tu.

Elisante Yona,

Mimi ni member wa siku nyingi,I have status

Thank you and God bless JF
 

Baija Bolobi

JF-Expert Member
Feb 25, 2009
1,094
2,000
Hii Poll ifunguliwe tena maana inafaa kuwaonyesha watanzania walio wengi. Mimi nampa Dr. Slaa hata kama mmeifunga mapema.
 

kimanga

Member
Mar 3, 2010
21
20
Hello,

Katika uchaguzi wa mwaka huu, mimi naona Dr. Slaa anafaa sana hii inatokana na uchungu alionao kwa taifa masikini la Watanzania.
 

Fatma

Member
Jul 25, 2009
16
0
Dr. Slaa is the best choice for 2010 president - he is serious, hataki upuuzi na uchungu wa nchi na watu wake. Bravo Dr. Slaa
 

Augustine Moshi

JF-Expert Member
Apr 22, 2006
2,545
2,000
One thing is certain: the plight of our people will not change, and will in fact get worse, if we vote JK and hic cronies back into power. Change for the better is possible, but it requires voting CCM out first.

Tumekuwa kichekesho. Naona hata ndugu zetu wa SA wamependekeza mipango ifanyike ili watalii wa kipindi cha World Cup ambao watapenda kwenda Serengeti wapelekwe sehemu ya Kenya iliyo karibu na Tanzania. Baada ya kukagua Tanzania, wameona hapakaliki

Tumekuwa nchi ambayo wagonjwa wanalala hata watatu kwenye kitanda kimoja, watoto wanasomea chini, hakuna umeme, hakuna maji na hakuna barabara. It will only get worse if we return JK and his cronies back to Ikulu.

Inabidi kuwe na mabadiliko.

 

Mdau

JF-Expert Member
Mar 29, 2008
1,790
1,500
mambo mazuri!!!
sasa mie nilisoma kwenye gazeti fulani, kuwa kuna viongozi wa upinzani ambao wamependekeza vyama viungane na kusimamisha mghombea mmoja ili wasirejee makosa walioyafanya Uchaguzi uliopita, hili waungwana mnalisemaje?
Jee kusimamisha wagombea wengi hatuhisi kuwa tunaweza kuifanya CCM kushinda kirahisi kwa kutumia ghilba na kuwagawa wapinzani.
nnaomba kuwakilisha

Hivi iliishia wapi hii?
 

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
2,000
Kichwamaji,

I do not underestimate Wapinzani, however they are underestimating CCM and Wananchi.

Mfano, wakati listi ya mafisadi ilipotoka, jambo la Kwanza Serikali na CCM walilifanya ni kujiuliza, je jambo hili lafungika na laweza kufika mahakamani? Jibu likawa hapana (do not ask for my source on this!), next CCM wakaanza technical mashambulizi na kuzima moto baada ya Mafisadi watajwa kudai watakwenda mahakamani (Mgonja, Ruta, Karamagi). Ukiangalia majibu ya Mkono, yalikuwa tofauti sana na alitumia technicalities and absence of subsance materials kuhusiana na tuhuma hizo.

Kilichotokea ni kuwa ile "Sensetion" ya orodha na mikutano ya hadhara ikatapakaa, lakini hakuna lililofuata.

Sisi Watanzania, tumeanza kukosoana ni nani ana haki kukemea ufisadi, huku mafisadi wakipeta na mkuu wao akitangaza rasmi ana imani na serikali yake.

Suala la BOT lina pembe tatu. EPA, Majengo na pesa za Meremeta, Tangold, Deep Green and Mwananchi. Kama kawaida, politicians wa Upinzani wakakimbilia majukwaa wakiwa na facts nusu nusu zisizo na misuli, CAG na Meghji wakasema tunafanya uchunguzi wa BOT, kila mtu akakaa kimya kusubiri ripoti binafsi ya CAG ambayo haiwi a Public thing mpaka Meghji na Kikwete waipitie.

Ripoti ya EY kwa CAG kuhusu BOT ni kuhusiana na EPA pekee na si zile pembe mbili zilizobakia. Sasa kama Uinzani ulikuwa na nondo za kutosha na kutaka kufanya hili ni jambo la Taifa, wangekuwa wajanja kumwaga habari hizi kama Udako na ushahidi wote, waache CCM wakihangaika kutafuta mchawi (kama ile barua ya Jitu Patel), halafu Upinzani ukawasilisha hoja Bungeni kuchunguza hayo mambo matatu ya BOT!

Ninachojaribu kufanya ni kusaidia Upinzani kutumuia nguvu zake katika Bunge kushikisha adabu CCM na mafisadi na si kuuza magazeti halafu 2010 unasikia Chadema ina viti 6, CUF 20 (vyote vya Pemba), TLP, UDP na NCCR wana viti 2 kila mmoja jumla ya viti 32 katika Bunge la viti 250!

Kesi za Mtikila za Wagombea huru na hata hii ya sasa ya Kadhi, Serikali na CCM wanaziogopa. Infact alishinda kesi ya Wagombea Huru, Tume ya Uchaguzi ikakiuka uamuzi wa Mahakama (Uchaguzi Tunduru) na hakuna hata mmoja kwenye Upinzani ameshinikiza suala la Ugombea Huru kufuatilia tamko la Mahakama (ingawa bado si Sheria, lakini tamko la mahakama halifutiki)!

There are better ways to play the game, so if some of us see a better way to win why not share? We are not looking for methods on how Opposition gather the facts, but it is how to use those facts effectivelly to your advantage!

I wonder if I was right on he money!
 

Omutwale

JF-Expert Member
Feb 4, 2008
1,431
2,000
Mjomba Eeeh!
Ulipoanguka Jangwani walisema ni uchovu wa kampeni mfululizo bila mapumziko. Hatukuhoji sana
Sasa tumesikia tena na huko Magogoni unaanguka anguka hovyo. Eti unashindwa masharti ya mwezi mchanga! Toba
Si siku zote mwasema; utamaduni wetu vijiti kupokezana?! Sasa vp wewe wang'an'gania?
Kuachia kiti kitamu si upumbavu; Afya ni bora kuliko cheo, waache nao wachukue tu......!
Natania tu Mjomba; Nikipata nauli nitakuletea wapiga dua.


Duh! Kumbe Tulikwishasema hii kitu siku nyingi eehhh!
Ni muhimu kukumbuka kuwa hii ilikuwa sredi kamili na kichwa cha habari "Mjomba Eeeh! Pumzika tu 2010"
Ukifuatilia michang iliyotililika kwenye hii sredi, ukaunganisha na Cheche ya Wiki hii na kisha ukarejea ripoti ya Dr. Mfisi usipopata picha ya Uchaguzi baada ya Uchaguzi na kabla ya Uchaguzi basi hujaelewa kitu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom