1
. Hizi ndio siasa anazozikataa Obama.
Obama has nopthing to do na siasa za urais wa bongo, na besides hata yeye huko naye anachafua wenziwe kwa mfano aliposmea kuwa "Bearings" za Makeni zinaanza kuharibika, na jana Liberman amesema amezi-check zinaonekana hazina kasoro, kwa hiyo mkuu siasa chafu hata huko majuu zipo sio bongo tu!
2.
Kwa wewe kusema kuwa Migiro ni zaidi ya SAS, sio tu kuwa ni kichekesho, bali inaonyesha tunapokuwa na upendeleo huwa na dira zetu hupotea.
Mama Migiro, hakusoma akiwa mtu mzima yaani balozi, mama Migiro ana historia pale Mlimani, wewe you know better on this sasa nashangaa hata kujaribu ku-argue ont this elimu ya Mama Migiro haiwezi kulinganishwa na ya Salim ya utu uzima bro tena akiwa ofisini, watu vichwa husoma kuaniza wakiwa watoto, sio watu wazima tena ofisini, ndio maana yangu hiyo mkuu!
3.
Migiro hakustahili hata hiyo nafasi maana hakuwahi hata kuwa diplomat let alone kufahamu shughuli za UN. Ndio maana hata waandishi wa habari walimshikia bango sana katibu mkuu wa UN na mama migiro kuwa kwa nini alipewa hiyo nafasi. Yeye ni mwanasheria aliyefaulu vizuri sana lakini hajashika madaraka yeyote zaidi ya ya le ya UDSM, Wizara ya Akina Mama na Watoto na muda kiduchu MOFA.
Mama Migiro, sasa hivi ni naibu katibu wa UN, Salim hajawahi kushika hiyo nafasi, that is what counts usije ukachekesha mbele ya watu walioenda shule, kinachojali ni nani amewahi kushika madaraka makubwa zaidi ya dunia kati yao, halafu unaonekana eti unayajua sana mambo ya ndani ya UN huku ukiwa bongo, Duh hiyo kali sana!
3.
Ukilinganisha na SAS ambaye sio tu kuwa amesomea mambo ya diplomasia, pia amekuwa ubalozini tokea akiwa na miaka 21 (CUBA). Aliendelea kuwa balozi Egypty, India, China, UN n.k., na wakati huo huo aliteuliwa kwenye jumuiya kibao za kimataifa, zote hizi akiwa na umri chini ya miaka 40.
Salim alipelekwa ubalozini akiwa na miaka 22 na hana elimu kabisaa hata ya Form Six, lakini Mama Migiro ameenda huko huko akiwa Doctor tayari, hiyo ni maoja ya tofauti zao!
4.
Salim pia alifanikiwa kuwa mwafrika wa kwanza kugombea ukatibu mkuu wa UN 1981 na kufanikiwa kupata kiasi cha kura kinachohitajika dhidi ya katibu mkuu wa wakati ule Kurt Walheim, lakini veto tu ya wamarekani ndio iliyomkosesha. Mama Migiro hakugomebea nafasi yake, alipewa hiyo nafasi tu kama shukrani na Korea kwa TZ, ambao pia wakati huo huo walituhonga pesa za kujenga daraja Kigoma, ili tu tuwapigie kampeni Africa, maana sisi tulikuwa tunaongoza UN Security Council. Hivi sasa inasemekana mama Migiro anapata upinzani mkubwa kutoka kwa watumishi wengine wa UN ambao wanaona kuwa hakustahili kupewa hicho kiti.
Alimshinda kura huyo M-Austria baada ya kugundulika kuwa ni former NAZI, lakini Salim hakushinda ukatibu, Ghali wa Egypt ndiye Muafrika wa kwanza kushinda ukatibu wa UN, sio Salim, Korea kwa nini ilishindwa kumpa nafasi Salim, lakini ikampa Mama Migiro? Hayo yako ni maneno ya kawaida bongo hasa kwa wapenzi wa Yanga na Simba, kuwa isingekluwa kipa wao tungewafunga wale as if kazi ya kipa ni kulala golini!
5.
Kwa hiyo usimpake SAS matope, tunachotakiwa tumuombee mama Migiro naye afanikiwe. Kama una sababu za kiukweli na ni vema kuziweka wazi tuzijadili lakini uchochezi na uzushi hautakusaidia wala wasomaji wengine maana mambo mengi ya hawa wakuu yanajulikana.
Sina sababu ya kumpaka Salim, aliyelia machozi ndani na mkewe wiki nzima baada ya kupigwa kipigo kwenye ule uchaguzi wa rais Dodoma, na kuamua kuacha kabisa siasa, na ninaheshimu uamuzi wake kuwa hawezi siasa za bongo, sasa abaki tu huko nje maana siasa za bongo ni kwa wanaume wa shoka mkuu!
6.
Kikwete aligombea uraisi mara mbili, SAS amegombea uraisi hadi hivi sasa mara moja tu. Kwa hiyo hata kwa mizengwe hiyo unayotaka kumuwekea, bado ana-qualify. Salim ndie mtu pekee Kikwete anayemuogopa katika kinyang'anyiro cha uraisi, ulizia utaambiwa.
Eti did I get it right? Umesema kuwa Kikwete anamuogopa Salim? You must be kidding me bro! Salim hakatazwi kugombea tena aje tu kama anataka, ila one thing ni hawezi kupewa urais bure kama ule ubalozi, kama Kikwete anamuogopa aje basi mkuu kugombea urais next time, hiyo ni haki yake hakatazwi!
Anyways, ninaona niishie hapa mkuu, maana naona una mpango wa kujaza hii forum na none hojas, naona nikutakie ugombeaji mwema na upigaji debe pia wa Salim, great debate, ingawa bado umeshindwa kusema ukweli kuhusu kumpendekeza Mahiga kuwa PM, na nashangaa umelkikwepa kabisa hilo, next time hakikisha unaandika ukweli mkuu, wengine huwa hatupendi hadithi na huwa tuna kumbu kumbu ya kila tunachoandika hapa,
Tukutane tena mkuu next topic!