The road towards 2010 Elections

The road towards 2010 Elections

Kati ya hawa nani atafaa kutuongoza 2010-2015?

  • Edward Lowassa

    Votes: 0 0.0%
  • Dr. Slaa

    Votes: 7 38.9%
  • Prof. Lipumba

    Votes: 0 0.0%
  • Mizengo Pinda

    Votes: 5 27.8%
  • Samwel Sitta

    Votes: 0 0.0%
  • Jakaya Kikwete

    Votes: 2 11.1%
  • Mark Mwandosya

    Votes: 2 11.1%
  • Harisson Mwakyembe

    Votes: 2 11.1%
  • None of The above

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    18
  • Poll closed .
But i also mentioned Dk Slaa!

Dr. Slaa ingawa hana uzoefu mkubwa wa mambo ya kiserikali, lakini anafaa ila kwa point za mbali kidogo ukimlinganisha na SAS.

Kama upinzani wangetaka kusimamisha mgombea mmoja, hata mimi ningefurahia wakimpa Dr. Slaa, ingawa itakuwa ni sacrifice kwa kiti chake cha ubunge. Hilo litakuwa pigo kwa upinzani lakini as a unified candidate, it is a worth sacrifice to take.

____________________
 
1
. Naelewa kuwa una mapenzi makubwa na hao wakuu walioko hapo NYC, akina Dr. Migiro, Balozi Dr. ............, n.k. Maana nakumbuka uliwahi pia kumpendekeza balozi kuwa awe PM.

Mkuu KJ,

1. kwanza ninaomba ujifunze kuheshimu sheria za JF, wewe ni mtumzima sasa mambo ya ku-speculate location au ID ya member mwingine ni kinyume na sheria za JF, I have nothing to do na "wakuu walioko hapo NYC" unless kama wewe uko huko, au?

2. Sijawahi kupendekeza Dr. Mahiga kuwa PM, that is pure nonesense kama una ushahidi wa hayo maneno yangu naomba uyaweke hapa, na kama huna uombe radhi kwa wananchi hapa kwa kuandika uongo!

Never before nimewahi kupendekeza that kind of nonesense idea, tukiwa BCS, nilisema Lowassa ndiye mwenye nafasi 95% ya kuwa PM na akawa, nikasema Luhanjo atakuwa katibu ofisi ya rais akawa, nikasema Mama Migiro atakuwa waziri foreign akawa, nikasema Muungwana anatoa hela za kampeni Iran gazeti la African Cinfidential likathibitisha habari zangu, lakini za kuepednekeza Mahiga kuwa PM, naomba uzitoe hapa wazi watu wazione, ili nikupigie magoti mkuu na niiombe JF nzima msamaha kwa kukusingizia uongo!
 
1.
Ukweli ni kuwa hao wote wanafaa sana, kwani wana elimu na wameonyesha kuwa wana uwezo wa kukabiliana na makubwa yanayoikabili nchi na jumuiya za kimataifa. Pia wamepata upeo wa mwelekeo wa dunia na wapi TZ inatakiwa kwenda ili nayo isonge mbele.

Ahsante kwa kukubali hili, lakini sijasema kuwa Mahiga, anafaa kuwa rais, nimesema ninaelekea ku-conclude on Mama Migiro kufaa.

2.
Kosa lao ni kuwa wote wako karibu sana na Kikwete na kwahiyo hawawezi kujitosa kupambana naye, wanachoweza kufanya tu ni kumrithi. Urithi huu pia unaweza usiwe mzuri sana kwani wanaweza wakashindwa kukemea aliyofanya JK. This is not the case kwa SAS.

Mkuu tizama maneno yako mwenyewe yanavyojichanganya, unasema kosa lao, hawana kosa hawa na si kweli kuwa wote wako karibu na muungwana, na hata wakiwa ni hoja finyu sana kulaumu ukaribu wa wanasiasa, kwa sababu political skills za kiongozi haziwezi kujali ukaribu, Mwanawasa alikuwa karibu na Chiluba, so was muungwana na Mkapa, wewe unafikiri hizi habari za ufisadi wa Mkapa, sasa hivi zinatoka wapi kama sio kwenye "file" la mtandao? Hii ya ukaribu ni nothing!

Salim hawezi kuwa karibu na muungwana kwa sababu hajawahi kuwepo nchini kwa muda mrefu sana, na inaweza kuwa ni hoja pia ya kuwa out of touch na wananchi pamoja na taifa kwa ujumla!
 
1.

Umri haujawahi kuwa important ishu kwenye uchaguzi wa rais wetu kwa hii mkuu ni none ishu au skill, na sio muhimu sana kama sio kabisaa.

2.

Unajua kurudia rudia neno moja bila ushahidi ni kupoteza muda wa wasomaji, CCM haiwezi kumuogopa mgombea urais anayeomba kugombea kupitia chama chake, kama sifa tunazozitaka sasa hivi ni kiongozi anayeweza kusimamia ufisadi na Salim hana record yoyote ya hata kukemea ufisadi, sasa huo u-serious wake uko wapi hasa?

Halafu hii habari kuwa Salim hapendi majungu, inatokea wapi? Ni lini Salim aliwahi kukemea majungu, au upendeleo ndani ya taifa letu?

3.

Unajua imefika wakati mkuu ukubali tu kuwa unampenda sana huyu jamaa, lakini huna hoja zaidi za kumtetea, kwa sababu hii sina hata sababu ya kuijibu!

4.

Salim aligombea urais, na wagombea wengine, ili ashinde ilibidi awashinde wagombea wengine, lakini akashindwa na kulia sana na kuapa kuwa hatarudia tena siasa za bongo, sasa hapa anyewaogopa wenziwe ni nani hasa? Siasa ni siasa ni mchezo mchafu na unachezwa na watu wachafu wachache, kwa bahati mbaya huwa Tanzania hatutoi urais tu bure bure,

amegombea ameshindwa urais, amekubali yaishe sasa mmetokea mnaojua better kuliko anavyojijua mwenyewe, kwa sababu kwangu mimi ni kwamba Salim amejiangalia vizuri na kukubali kuwa hana uwezo wa kushinda urais wa Tanzania, sasa sielewi hizi filimbi ni za nini hasa!

Mkuu FMES, Sio siri tena kuwa JK alishinda kwa kutumia rushwa, vitimbwi vya wanamtandao, na comment za wazi mwenyekiti wa CCM wakati huo kuwataka wajumbe wa mkutano mkuu wamchague JK. Hii ina maana kuwa, kama isingekuwa hizo undemocratic campaigns, SAS ambaye alishika nafasi ya pili labda ndie angekuwa mgombea wa CCM. Kama alivyoinyoosha AU, labda na nchi ingekuwa pasafi leo hii.

Kwa hiyo mimi napinga kabisa kampeni zozote zile zilizo na nia ya kumchafua mtu ambaye ameitumikia nchi kwa unyenyekevu na bila ya ubadhilifu. Kilichomfanya aseme hatashiriki kwenye siasa za uraisi za CCM ni kutokana na uzushi mwingi aliofanyiwa wakati wa uteuzi mwaka 2005. Lakini kama wananchi wakimlilia sio ajabu akakubali kujitosa 2010 ili kuiokoa nchi.

____________________________
 
Hivi kweli hizi tuhuma inawezekana ni za kweli?
Maana naona kuna wanachadema wengi tu humu ambao hata hawakujihangaisha kutaja jina lake!

Mimi binafsi i've met Mbowe na tumeshakuwa na brief conversation!
Lakini toka nikiwa na umri mdogo tu nilishawahi kuhudhuria mkutano wake!
Tena by that time watu ni wachache sana!

Na nilikuwa nikijiuliza maswali...Jamaa alikuwa na data kusema kweli!

Sijawahi kuwa karibu naye ama kufanya naye kazi so siwezi kusema a lot!
Isipokuwa hapo kwenye elimu nakupa changamoto!

1)CV yake iwekwe hapa!
2)CV ya Al haji Ali Hassan Mwinyi nayo imwagwe hapa!
Mushi samahani mjomba mbona sikuelewi, yaani unataka kuturudisha tena tulikotoka kwa Mzee Ruksa? Enzi yake ilipita, tuliyopata kwake tumejifunza, tunapaswa kusonga mbele. Kama hatukulielewa somo lile na tunataka kulirudia basi ni bora akarudi Mzee Ruksa mwenyewe, bado ana nguvu!
 
1

Mkuu KJ,

1. kwanza ninaomba ujifunze kuheshimu sheria za JF, wewe ni mtumzima sasa mambo ya ku-speculate location au ID ya member mwingine ni kinyume na sheria za JF, I have nothing to do na "wakuu walioko hapo NYC" unless kama wewe uko huko, au?

2. Sijawahi kupendekeza Dr. Mahiga kuwa PM, that is pure nonesense kama una ushahidi wa hayo maneno yangu naomba uyaweke hapa, na kama huna uombe radhi kwa wananchi hapa kwa kuandika uongo!

Never before nimewahi kupendekeza that kind of nonesense idea, tukiwa BCS, nilisema Lowassa ndiye mwenye nafasi 95% ya kuwa PM na akawa, nikasema Luhanjo atakuwa katibu ofisi ya rais akawa, nikasema Mama Migiro atakuwa waziri foreign akawa, nikasema Muungwana anatoa hela za kampeni Iran gazeti la African Cinfidentila likathibitisha habari zangu, lakini za kuepednekeza Mahiga kuwa PM, naomba uzitoe hapa wazi watu wazione, ili nikupigie magoti mkuu na niiombe JF nzima msamaha kwa kukusingizia uongo!

Mkuu heshma mbele.
Kwa utabiri/maoni yako nani raisi 2011?
 
Mushi samahani mjomba mbona sikuelewi, yaani unataka kuturudisha tena tulikotoka kwa Mzee Ruksa? Enzi yake ilipita, tuliyopata kwake tumejifunza, tunapaswa kusonga mbele. Kama hatukulielewa somo lile na tunataka kulirudia basi ni bora akarudi Mzee Ruksa mwenyewe, bado ana nguvu!

Mi nakwambia Mwalimu angekuwa hai halafu aseme Freeman for president watu wasinge uliza haya mambo wanayodai ya cv na ndio maana nika mention mzee wa rhuksa Al haji Ali Hassan Mwinyi!
 
1.
Salim ni msomi wa madarasa na vitendo tusimpakazie kwa vile alisoma akiwa ofisini. Ameweza kuitumia elimu yake kisomi katika kiwango cha juu kabisa na akiwa na umri mchanga sana. Hii ni kuonyesha kuwa hakupewa vyeti. Zaidi ya hayo, vyeti vya kupewa havitoki Columbia University, hiki ni kati ya vyuo bora duniani na SAS akitokea 3rd world, hawezi kuwa na jina la kumfanya apewe degree. Kitengo chake cha international affairs hapo Columbia Unv., ni kati ya vilivyo bora zaidi duniani. Baadhi ya Alumni wanaojivunia ni pamoja na Madeline Albright.

There you go, na kukwepa ukweli wa uwezo mdogo wa elimu ya Salim, the man amekwenda ubalozini akiwa na umri wa miaka 22, amekwenda akiwa hana shule ya kutosha, hana degree kabisa! Amesoma akiwa ubalozini, sasa nimekuuliza je Mweneyekiti wa Chadema anegepewa the same chance angeshindwa kusoma akiwa ubalozini?

Derek Jeter pamoja na Robert De-Niro, ni majuzi tu wamepewa degree na hiyo shule, je ina maana ni wasomi sana hao? Mama Mongella aliombwa kuwa Mwalimu pale je ina maana ni msomi sana kutoka 3rd World? Mkuu Salim alisoma Cuba sio Columbia, huko alipewa tu akiwa ubalozini, ukitafuta CV ya mtoto wake wa kiume ambaye ni mwanasheria, then utakuta kuwa huyo ni msomi wa kweli, lakini sio Salim, huwezi kumhesabu au kumuweka kwenye kundi la wasomi kama kina Mwandosya na Mwakyembe!

2.
Binafsi yangu, siko tayari kuongozwa na raisi aliyeishia form six katika karne hii ya 21, ingawa nafikiri Mbowe ana some other certificates. Mbowe ameishia hapo baada ya kusoma kwenye the best schools primary na secondary. Hii ni dalili ya upungufu fulani ambao hata pesa haikuweza kuuondoa. Hizi degree za kutafuta wakati tunataka uongozi, hazitufai maana shule sio darasa tu, ni pamoja na kupata muda wa kutosha kutumia ulivyosomeshwa katika ulimwengu halisi. Kwa hiyo kama Freeman akimaliza shule kesho, anahitaji afanyie kazi aliyofundishwa kwa angalau miaka 10 hivi ili tumtambue kuwa aliyaelewa aliyofundishwa. Tuko karne ya 21, ni muhimu tukaheshimu nguvu ya elimu. Hii haina maana ya PhDs, bali angalau a good first degree ni mwanzo mzuri wa kupima uwezo wa mtu.

Mwenyekiti wa sasa wa Chadema, amesoma mpaka From Six ya zamani ambayo ni tofauti na ya sasa, akaingia kwenye biashara akiwa na umri sawa na wa Salim alipokuwa akienda ubalozini, lakini mind you kuwa Salim hakufika hiyo Form Six,

Halafu tizama unavyojichanganya, unasema hutaki degree za kutafuta ukubwani, lakini degree za Salim alizozitafuta akiwa kazini ubalozini kwako ni sawa! Unasema ni wa-Tanzania wote walioishia Form Six, wanaamiliki Billicanas popote walipo bongo?

Mimi ninaheshimu sana kazi ya Mwenyekiti wa sasa wa Chadema, kwa sababu kisiasa kama sio kazi zake nzito huko Chadema, tusingekuwa na hizi siasa tulizonazo kwenye taifa letu sasa hivi, wasomi kina Lipumba wameshindwa kabisa kusimama kidete against CCM, sasa kwa sababu hajawahi kutokea mwingine wa calliber yake, ni lazima kumpa heshima yake, ningeeelewa kuwa humtaki kwa sababu za policies zake au siasa zake, lakini eti elimu na the rest ni hoja finyu sana, the matter of fact ni none-ishu!
 
1.
La uongozi na ukabila chamani tumeshaliongelea sana. Kama yeye akiwa mwenyekiti ameweza kuruhusu wabunge 5 kati ya 6 kutokea mkoani kwake bila kuliona kuwa lina ualakini, then hafai kabisa kukamata nchi. Hili pia ni swali kwa viongozi wengine wa CHADEMA hasa wale waliopo humu mtandaoni watueleze msimamo wao kuhusiana na hili jambo. Zitto, Mnyika na wengine tutashukuru kama mtatujibu kwa nini mmelikalia hili kimya?

Binafsi siamini kuwa this is case, kwa sababu Mwalimu kuwa na wasadizi kina Butiku, Apiyo, Musuguri haikuwa na maana kuwa alikuwa mkabila, hiii ishu imesemwa sana hapa JF kabla hujaja na hili jina, na limetolewa majibu sana na viongozi wa Chadema hapa JF, mimi nilishalifuta kuwa it is a none ishu, lakini unaweza kulikumbatia as an-ishu,

Kwangu the man ambaye ameweza kuki-promote Chadema, mpaka kufikia level iliyopo sasa, ninaaamini kuwa ana-deserve a fair considerations kama wananchi wengine wote, mimi ninaaamini kuwa mwananchi yoyote ambaye ni raia wa Tanzania, anaweza kugombea urais, kufaaa ni another ishu ambayo inahitaji kuwa carefully debated kulingana na matatizo ya taifa, sasa hivi tatizo letu as a nation ni ufisadi, sio elimu wala uchumi, kwa sababu uchumi wetu hata ukiwa mzuri, unaharibiwa na viongozi mafisadi kwa hiyo anayefaa ni yule anayeweza kupambana na ufisadi, sasa Salim ataliweza hilo?

2.
Kwa hiyo, ukikata ukatavyo, SAS kwa mawazo yangu ana nafasi kubwa ya kumuondoa JK in 2010 kuliko wengi tulionao, tatizo ni kwa yeye tu kukubali kuuchukua huu mzigo mkubwa.[/

Ukitaka utakavyo, hizi ni lgha za kwenye vilabu vya pombe za kienyeji, zisiletwe huku JF, Salim amegombea na Kikwete akashindwa mpaka kuapa kuacha siasa za bongo, tena Kikwete amemshinda akiwa sio rais, sasa unasema Salim atamshinda Kikwete akiwa rais? Kuukubali kuuchukua mzigo atakaopewa na nani?
 
1.

Ahsante kwa kukubali hili, lakini sijasema kuwa Mahiga, anafaa kuwa rais, nimesema ninaelekea ku-conclude on Mama Migiro kufaa.

2.

Mkuu tizama maneno yako mwenyewe yanavyojichanganya, unasema kosa lao, hawana kosa hawa na si kweli kuwa wote wako karibu na muungwana, na hata wakiwa ni hoja finyu sana kulaumu ukaribu wa wanasiasa, kwa sababu political skills za kiongozi haziwezi kujali ukaribu, Mwanawasa alikuwa karibu na Chiluba, so was muungwana na Mkapa, wewe unafikiri hizi habari za ufisadi wa Mkapa, sasa hivi zinatoka wapi kama sio kwenye "file" la mtandao? Hii ya ukaribu ni nothing!

Salim hawezi kuwa karibu na muungwana kwa sababu hajawahi kuwepo nchini kwa muda mrefu sana, na inaweza kuwa ni hoja pia ya kuwa out of touch na wananchi pamoja na taifa kwa ujumla!

FMES, Naiona passion yako ya kumsupport mama Migiro. Lakini ukweli ni kuwa, tusimzulie majungu SAS kwa vile tu kuna wengine tunaowapendelea. Kwa kusema kuwa SAS yuko out of touch ni kichekesho maana SAS amekaa na kuingoza nchi kwa kipindi almost sawa na kile alichokaa nje.

Hii inampa upeo wa kipekee kuona tofauti zinazotakiwa kufanyika TZ na sio kama JK ambaye haelewi nini kifanyike zaidi ya kuwa omba omba.

Kama kukaa kwake nje ni kikwazo, inakwaje Mama Migiro ambaye hivi sasa yuko nje awe bora kuliko SAS ambaye tokea amalize AU 2001, amekuwa nyumbani TZ?

Ni vema kama kuna kigezo cha kumfanya SAS asifae, tukakionyesha na kukijadili lakini hivi vya uzushi, ni vema kuachana navyo ili tumpate mtu atakayetufaa mwaka 2010.
 
Ushauri wangu wa bure kwa Dk Slaa huu hapa...

Atafute Coalition ya nguvu kutoka vyama vyote vya upinzani pamoja na wana CCM wazito wenye kukerwa na ufisadi! Hata ikiwezekana makamu wake atoke CCM!

Pili natoa changamoto tuweke majina ya wana CCM ambao wameonyesha wazi kukerwa na ufisadi na kuukemea wazi mithili ya wakina Slaa! Baadhi ni hawa..

1)Judge Joseph Sinde Warioba aliyeweka wazi anataka kuona mafisadi wakikamatwa na kufunguliwa mashtaka mara moja!

2)Alhaji Mwinyi anaweza kuendorse! Yeye aliwaonya wenzake kuwa dunia ya sasa ni tofauti hivyo ufisadi haufai tena! Awekwe kwenye coalition!

3)Butiku ana ushawishi awekwe kwenye coalition na ipewe jina kabisa la Utaifa!

4)Aloyce Kimaro.

Kama kuna wengine naomba tuwaweke hapa na tuendelee kujadili.
 
FMES,
Naiona passion yako ya kumsupport mama Migiro. Lakini ukweli ni kuwa, tusimzulie majungu SAS kwa vile tu kuna wengine tunaowapendelea. Kwa kusema kuwa SAS yuko out of touch ni kichekesho maana SAS amekaa na kuingoza nchi kwa kipindi almost sawa na kile alichokaa nje. Hii inampa upeo wa kipekee kuona tofauti zinazotakiwa kufanyika TZ na sio kama JK ambaye haelewi nini kifanyike zaidi ya kuwa omba omba. Kama kukaa kwake nje ni kikwazo, inakwaje Mama Migiro ambaye hivi sasa yuko nje awe bora kuliko SAS ambaye tokea amalize AU 2001, amekuwa nyumbani TZ?

Ni vema kama kuna kigezo cha kumfanya SAS asifae, tukakionyesha na kukijadili lakini hivi vya uzushi, ni vema kuachana navyo ili tumpate mtu atakayetufaa mwaka 2010.

___________________

Bado nasikilizia maoni zaidi kuhusu Salim Ila mwanzoni nilipendekeza Slaa and Salim kwasababu Salim ana ushawishi pia kwa wana CCM na pia inapokuja kwa Zanzibar, ila bado hajaweza kukemea ufisadi hadharani hivyo bado nina mashaka hapo!
 
1.
Sio siri tena kuwa JK alishinda kwa kutumia rushwa, vitimbwi vya wanamtandao, na comment za wazi mwenyekiti wa CCM wakati huo kuwataka wajumbe wa mkutano mkuu wamchague JK. Hii ina maana kuwa, kama isingekuwa hizo undemocratic campaigns, SAS ambaye alishika nafasi ya pili labda ndie angekuwa mgombea wa CCM. Kama alivyoinyoosha AU, labda na nchi ingekuwa pasafi leo hii.

Hivi Salim wakati anaamua kugombea urais ni nani aliyemwambia kuwa kampeni zitakuwa safi? Hivi hizo kampeni za kina Jaluo na Clintons ni safi sana? Hivi unajua Tanzania tungekuwa Democratic toka mwanzo, basi Salim asingeeenda nje ubalozini akiwa hana elimu? Rushwa hata Salim aliitumia lakini hakuwa na hela za kutosha, halafu ni AU ipi aliyoinyooosha unless kama ziko mbili, kwa sababu Darfour si walianza Salim akiwa AU au alilimaliza hilo tatizo? Mauaji ya Rwanda Salim hakuwa AU?

2.
Kwa hiyo mimi napinga kabisa kampeni zozote zile zilizo na nia ya kumchafua mtu ambaye ameitumikia nchi kwa unyenyekevu na bila ya ubadhilifu. Kilichomfanya aseme hatashiriki kwenye siasa za uraisi za CCM ni kutokana na uzushi mwingi aliofanyiwa wakati wa uteuzi mwaka 2005. Lakini kama wananchi wakimlilia sio ajabu akakubali kujitosa 2010 ili kuiokoa nchi.

Kama huwezi kampeni chafu ina maana huwezi kuwa rais, Dr. Slaa aliposema wazi majina ya mafisadi kuna baadhi ya Viongozi wa CCM waliojaribu kumjibu kwa maneno mengi ya kashfa na uongo, hivi umeona wakifanikiwa kumtisha au kuharibu jina la Slaaa? Hakuna mwananchi wa Tanzania atakayemlilia Salim, kiongozi wasiyemjua na ambaye hana record za kuliongoza taifa letu, huyo agombee huko UN wanakmjua sana, hapa bongo haitakuja kutokea, haiwezekani mtu mmoja tu Salim apewe nafasi zote hizo, za kupelekwa nje akiwa hana elimu, na umri mdogo, kupewa pewa tu, mpaka hata alipojaribu mwenyewe bado hawezi no hatuhitaji viongozi magoi goi wa kulia machozi wakishindwa uchaguzi, kama Salim angekuwa kama mnavyosema basi angejitoa kwenye uchaguzi kabla haujaisha na kusema wazi kuwa hawezi kushirikia siasa za kampeni chafu, lakini ameshiriki mpaka mwisho ndio baadaye eti sizitaki mbichi hizi!
 
1.

Hivi Salim wakati anaamua kugombea urais ni nani aliyemwambia kuwa kampeni zitakuwa safi? Hivi hizo kampeni za kina Jaluo na Clintons ni safi sana? Hivi unajua Tanzania tungekuwa Democratic toka mwanzo, basi Salim asingeeenda nje ubalozini akiwa hana elimu? Rushwa hata Salim aliitumia lakini hakuwa na hela za kutosha, halafu ni AU ipi aliyoinyooosha unless kama ziko mbili, kwa sababu Darfour si walianza Salim akiwa AU au alilimaliza hilo tatizo? Mauaji ya Rwanda Salim hakuwa AU?

2.

Kama huwezi kampeni chafu ina maana huwezi kuwa rais, Dr. Slaa aliposema wazi majina ya mafisadi kuna baadhi ya Viongozi wa CCM waliojaribu kumjibu kwa maneno mengi ya kashfa na uongo, hivi umeona wakifanikiwa kumtisha au kuharibu jina la Slaaa? Hakuna mwananchi wa Tanzania atakayemlilia Salim, kiongozi wasiyemjua na ambaye hana record za kuliongoza taifa letu, huyo agombee huko UN wanakmjua sana, hapa bongo haitakuja kutokea, haiwezekani mtu mmoja tu Salim apewe nafasi zote hizo, za kupelekwa nje akiwa hana elimu, na umri mdogo, kupewa pewa tu, mpaka hata alipojaribu mwenyewe bado hawezi no hatuhitaji viongozi magoi goi wa kulia machozi wakishindwa uchaguzi, kama Salim angekuwa kama mnavyosema basi angejitoa kwenye uchaguzi kabla haujaisha na kusema wazi kuwa hawezi kushirikia siasa za kampeni chafu, lakini ameshiriki mpaka mwisho ndio baadaye eti sizitaki mbichi hizi!

Sasa mbona husemi una muendorse nani na kwanini?
 
1.
Naiona passion yako ya kumsupport mama Migiro. Lakini ukweli ni kuwa, tusimzulie majungu SAS kwa vile tu kuna wengine tunaowapendelea. Kwa kusema kuwa SAS yuko out of touch ni kichekesho maana SAS amekaa na kuingoza nchi kwa kipindi almost sawa na kile alichokaa nje. Hii inampa upeo wa kipekee kuona tofauti zinazotakiwa kufanyika TZ na sio kama JK ambaye haelewi nini kifanyike zaidi ya kuwa omba omba. Kama kukaa kwake nje ni kikwazo, inakwaje Mama Migiro ambaye hivi sasa yuko nje awe bora kuliko SAS ambaye tokea amalize AU 2001, amekuwa nyumbani TZ?

Sijasema ninampa Mama Migiro, full support lakini ninasema kuwa ninaelekea huko, angekuwa hayuko out of touch basi asingelia kuhusu kampeni chafu za kugombea urais, na pia asingewachukua Warioba na Butiku kuwa wapiga debe wake hizo zote ni dalili za kuwa out of touch na bongo na wananchi wake, kama ni kuomba omba Salim, ndiye aliyekuwa akitumwa na Mwalimu kila wakati kuomba omba nje kwa hiyo kuomba omba haikuanza leo mkuu, Mama Migiro alikuwa waziri wa nje akaitwa UN kuwa Mwafrika wa kwanza Mwanamke kushika nafasi hiyo nzito sana ya dunia, ambayo Salim na CV yake hakuweza kupata, kama ni usomi sidhani kama unaweza kuwalinganisha Salim na Mama Migiro not even close yaaani ni mbali sana, Salim hayuko nyumbani alirudi tu kuvizia urais, alipokosa tu akakimbia yuko Abuja mkuu hayuko nyumbani, lakini najua kuwa atasubiri tena uchaguzi wa rais na kurudi tena avizie!

2.
Ni vema kama kuna kigezo cha kumfanya SAS asifae, tukakionyesha na kukijadili lakini hivi vya uzushi, ni vema kuachana navyo ili tumpate mtu atakayetufaa mwaka 2010.

Mkuu siasa nyingi za dunia zinasema kuwa ukishagombea urais mara tatu ukashindwa, ni vyema kuacha tu ili wengine nao wajaribu, Salim has his time, sasa ni wakati wa wengine, na wapo wengi sana mkuuu!
 
1.

Sijasema ninampa Mama Migiro, full support lakini ninasema kuwa ninaelekea huko, angekuwa hayuko out of touch basi asingelia kuhusu kampeni chafu za kugombea urais, na pia asingewachukua Warioba na Butiku kuwa wapiga debe wake hizo zote ni dalili za kuwa out of touch na bongo na wananchi wake, kama ni kuomba omba Salim, ndiye aliyekuwa akitumwa na Mwalimu kila wakati kuomba omba nje kwa hiyo kuomba omba haikuanza leo mkuu, Mama Migiro alikuwa waziri wa nje akaitwa UN kuwa Mwafrika wa kwanza Mwanamke kushika nafasi hiyo nzito sana ya dunia, ambayo Salim na CV yake hakuweza kupata, kama ni usomi sidhani kama unaweza kuwalinganisha Salim na Mama Migiro not even close yaaani ni mbali sana, Salim hayuko nyumbani alirudi tu kuvizia urais, alipokosa tu akakimbia yuko Abuja mkuu hayuko nyumbani, lakini najua kuwa atasubiri tena uchaguzi wa rais na kurudi tena avizie!

2.

Mkuu siasa nyingi za dunia zinasema kuwa ukishagombea urais mara tatu ukashindwa, ni vyema kuacha tu ili wengine nao wajaribu, Salim has his time, sasa ni wakati wa wengine, na wapo wengi sana mkuuu!

Kubwa Jinga unakubaliana na haya?
 
Sasa mbona husemi una muendorse nani na kwanini?

Hapana sina haraka sana, kwa sababu this is a very serious ishu mkuu ndio maana ninachukua my time lakini very soon nitasema tu!
 
Hapana sina haraka sana, kwa sababu this is a very serious ishu mkuu ndio maana ninachukua my time lakini very soon nitasema tu!

Nakubaliana na wewe base on this assumption:
Kwamba ifikapo mwaka 2010 issue inaweza isiwe ufisadi no more!

Unajua wenzetu wanapopiga kura wanakwenda kwa issues na mara nyingine single issue ie costly war, poor economy, jobs etc

Sisi the main issue tunayoiface taifa letu at this time and moment ni UFISADI!

Hivyo basi hilo kuwa issue nzito na possibly single to decide the nomination!

Again ni less than two years now kuelekea uchaguzi mkuu na hakuna dalili za ufisadi kushughulikiwa kwa style wananchi wanayoitaka!

So mimi nime weigh in na nina muendorse Slaa ila aje na convincing coalition na ndio maana nikasema tutaje baadhi ya wazalendo bila kujali vyama ili tupime possibilty ya coalition!
 
1.
There you go, na kukwepa ukweli wa uwezo mdogo wa elimu ya Salim, the man amekwenda ubalozini akiwa na umri wa miaka 22, amekwenda akiwa hana shule ya kutosha, hana degree kabisa! Amesoma akiwa ubalozini, sasa nimekuuliza je Mweneyekiti wa Chadema anegepewa the same chance angeshindwa kusoma akiwa ubalozini?

SAS kwa wakati ule na kwa akili yake ya kupindukia ndio vilivyompeleka India. Walikuwapo vijana wengi lakini hawakuweza kufanya aliyoweza kuyafanya SAS.

Kwa Mbowe kama ingekuwa ni 1964, elimu yake ingekuwa sawa, lakini yeye alienda shule miaka ya 80s. Mbowe alikuwa na nafasi nzuri kuliko waTZ wengi kwenda mbali kishule kwani wazazi wake walikuwa na uwezo, lakini hakuweza kusonga mbele. Hivi sasa, 2008, tunategemea viongozi wetu, hasa walio vijana, kuwa na elimu ya kutosha. Nafasi za kusoma hivi sasa zipo sio kama ilivyokuwa 60s.

Derek Jeter pamoja na Robert De-Niro, ni majuzi tu wamepewa degree na hiyo shule, je ina maana ni wasomi sana hao? Mama Mongella aliombwa kuwa Mwalimu pale je ina maana ni msomi sana kutoka 3rd World? Mkuu Salim alisoma Cuba sio Columbia, huko alipewa tu akiwa ubalozini, ukitafuta CV ya mtoto wake wa kiume ambaye ni mwanasheria, then utakuta kuwa huyo ni msomi wa kweli, lakini sio Salim, huwezi kumhesabu au kumuweka kwenye kundi la wasomi kama kina Mwandosya na Mwakyembe!

SAS amesomea Columbia University, an Ivy League University. Ina rank 1-5 kwenye vyuo siku zote US. Hiyo ya Cuba ni news kwangu. Ya Mongela na akina DeNiro hayaondoi ukali wa shule ya SAS. Wengine waliosomea Columbia ni kijana Barack Obama.

2.
Mwenyekiti wa sasa wa Chadema, amesoma mpaka From Six ya zamani ambayo ni tofauti na ya sasa, akaingia kwenye biashara akiwa na umri sawa na wa Salim alipokuwa akienda ubalozini, lakini mind you kuwa Salim hakufika hiyo Form Six,

Kiwango cha Mbowe cha elimu ni hatari kwa yeye kupewa nchi. Dr. Slaa, Zitto, Halima, Lucy wote wana shule zinazofaa zaidi ya Mbowe. Form Six yake sio ya zamani, ni ya miaka ya 80s, na hii excuse ina-apply tu kwa akina Mwinyi, Kawawa na wengine wa marika yao. Mbowe hakufanya jitihada kujiendeleza kielimu mpaka alipogombea uraisi licha ya kuwa na uwezo wa kifedha.

Halafu tizama unavyojichanganya, unasema hutaki degree za kutafuta ukubwani, lakini degree za Salim alizozitafuta akiwa kazini ubalozini kwako ni sawa! Unasema ni wa-Tanzania wote walioishia Form Six, wanaamiliki Billicanas popote walipo bongo?

Mimi ninaheshimu sana kazi ya Mwenyekiti wa sasa wa Chadema, kwa sababu kisiasa kama sio kazi zake nzito huko Chadema, tusingekuwa na hizi siasa tulizonazo kwenye taifa letu sasa hivi, wasomi kina Lipumba wameshindwa kabisa kusimama kidete against CCM, sasa kwa sababu hajawahi kutokea mwingine wa calliber yake, ni lazima kumpa heshima yake, ningeeelewa kuwa humtaki kwa sababu za policies zake au siasa zake, lakini eti elimu na the rest ni hoja finyu sana, the matter of fact ni none-ishu!

Hata na mimi pia naiheshimu kazi yake Mbowe hasa kwa mazingira ya kisiasa anayofanyia kazi. Lakini hii haimuepushi kuto kukosolewa.

____________________
 
Nakubaliana na wewe base on this assumption:
Kwamba ifikapo mwaka 2010 issue inaweza isiwe ufisadi no more!

Unajua wenzetu wanapopiga kura wanakwenda kwa issues na mara nyingine single issue ie costly war, poor economy, jobs etc

Sisi the main issue tunayoiface taifa letu at this time and moment ni UFISADI!

Hivyo basi hilo kuwa issue nzito na possibly single to decide the nomination!

Again ni less than two years now kuelekea uchaguzi mkuu na hakuna dalili za ufisadi kushughulikiwa kwa style wananchi wanayoitaka!

So mimi nime weigh in na nina muendorse Slaa ila aje na convincing coalition na ndio maana nikasema tutaje baadhi ya wazalendo bila kujali vyama ili tupime possibilty ya coalition!

Dr. Slaa anafaa, lakini ni kwa ticket ya chama/vyama vipi?
___
 
Back
Top Bottom