The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

Vyama vingine vitakufa natural death na ndio utakuwa ukombozi wa Tanzania na ndio sisi kama Watanzania tutajua mkweli ni yupi na mlaghai wa kisiasa ni yupi
 
Vyama vingine vitakufa natural death na ndio utakuwa ukombozi wa Tanzania na ndio sisi kama Watanzania tutajua mkweli ni yupi na mlaghai wa kisiasa ni yupi

Well said ni muda tu ndio uliobaki lakini dalili zote zinaonyesha hata Baba wa Taifa aliwahi kusema haya
 
Vyama vingine vitakufa natural death na ndio utakuwa ukombozi wa Tanzania na ndio sisi kama Watanzania tutajua mkweli ni yupi na mlaghai wa kisiasa ni yupi

Tielopii iko njia moja kuelekea makaburini, labda utokee muujiza wa mji wa Naimi.
 
Yametimia sasa..

Mbona yalishatimia zamani tu. Tatizo linalowasumbua wengi ni ugonjwa wa mremamania - watamfuata popote pale. Walikuwa naye CCM, wakahama naye NCCR, wakahama naye TLP na bila shaka watarudi naye CCM. Uzuri ni kuwa sasa upinzani unaweza kupumua, mkereketwa na kachero nambari wani karudi kundini.
 
Toa maoni yako mkuu, siyo wote akina Yahaya humu, wewe unasemaje leo kuhusu Mrema, yaani hakuna ushindani humu.
Majibu yako wazi, Mrema alileta chachu katika upinzani lakini akiweka malengo yake binafsi mbele. Na kwavile watu walikuwa wamechoka na mfumo uliokuwepo jazba yao haikuona mapungufu aliyonayo upande wa pili wa Lyatonga na kumuona ndio mwokozi wao.
Baada ya watu kumshtukia, sasa amerudi kwenye rangi yake ya asili. KWA SASA HANA FAIDA YEYOTE KATIKA UPINZANI ZAIDI YA HASARA.
 
MWENYEKITI wa TLP, Augustine Mrema amemtaka Rais Jakaya Kikwete kuwafukuza mawaziri wawili ambao walitoa kauli zinazoonyesha kupingana na muswada wa sheria mpya ya madini wakati wa mkutano wa wadau juzi, akisema wamekiuka utaratibu wa uwajibikaji wa pamoja.

Mrema, ambaye alikumbana na hali kama hiyo mwaka 1995 wakati alipotofautiana hadharani na uamuzi wa Baraza la Mwaziri kuhusu mashamba ya mkonge, sasa anataka Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wassira na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige wawajibishwe kwa kutofautiana na mapendekezo ya serikali ya sheria mpya bya madini.

Mawaziri hao wawili jana walikaririwa na vyombo vya habari wakidai kuwa muswada wa madini umejaa kasoro na umelenga kuwanufaisha wachimbaji wakubwa na kuwabana wachimbaji wadogo.

Mrema, ambaye katika siku za karibuni amekuwa miongoni mwa watu wanaomuunga mkono Rais Kikwete, alisema kitendo cha mawaziri hao kujitokeza hadharani na kupinga muswada huo ni ukiukwaji wa sheria ya uwajibikaji wa pamoja na uasi kwa serikali yao ambayo wao wamepewa dhamana ya kuiongoza.

“Huu ni uasi, kimsingi maoni yao hutakiwa kutolewa kwenye kikoa cha Baraza la Mawaziri ambacho hufanyika kabla ya muswada huo kufikishwa bungeni. Kitendo cha mawaziri kuja kupinga mswada huo nje ya vikao vya baraza ni cha uhaini na adhabu yao ni kufukuzwa,” alisema Mrema ambaye alipoteza uwaziri kwa kosa hilo.

Mrema alifafanua kuwa muswada unapopelekwa bungeni unakuwa si mali ya waziri mwenye dhamana na wizara husika, bali ni mali ya serikali, hivyo mawaziri hawaruhusiwi kuupinga.

“Huo si muswada wa (Waziri wa Nishati na Madini, William) Ngeleja bali ni mali ya serikali ya CCM na waziri yeyote hana ruhusu ya kuupinga. Anayeona hajaridhika na maamuzi, anatakiwa kujiuzuru kabla ya kuupinga hadharani,” alisema Mrema.

Hata hivyo, Mrema naye aliungana na kundi linaoukosoa muswaada huo ambalo linataka ufanyiwe marekebisho ili ukidhi maslahi ya Watanzania walio masikini.

Alisema madini yaliyopo ni mali ya Watanzania na yanasitahili kutumika kwa ajili ya kuinua uchumi wa taifa.

Alisema sheria yoyote inayotungwa kuhusu madini inapaswa kuzingatia maslahi ya Watanzania ambao wengi wao ni walala hoi.

Wakati Mrema akitoa mapendekezo hayo, katibu mkuu wa NCCR-Mageuzi Samuel Ruhuza alisifu uamuzi wa mawaziri hao kutofautiana na baraza lao akidai huo ni ujasiri mkubwa waliouonyesha mbele ya jamii.

Alisema kitendo hicho kimeonyesha wazi kuwa ndani ya Baraza la Mawaziri kuna matatizo yaliyosababaisha wajumbe kutofautiana.

“Ingawa kimsingi viongozi hao wanatakiwa kujuzuru nafasi zao, wameonyesha ujasili mkubwa... hiyo inaonyesha kuwa ndani ya Baraza la Mawaziri kuna matatizo yaliyofanya mswada huo upite bila ya maafikiano,” alisema Ruhuza.

“Labda kwa kuwa Wasira aliwahi kuwa upinzani, lakini kitendo hicho kinaonyesha ndani ya Baraza la Mawaziri kuna matatizo makubwa kwa kuwa muswada hujadiliwa huko kabla ya kufika bungeni,” alisema.

Aliwataka wabunge wote kushikamana kupinga sheria zote zisizo na manufaa kwa wananchi.

Alisema kitendo cha kupeleka miswada ya dharura bungeni, kinapaswa kuangaliwa upya kwa kuwa kufanya hivyo kutaweza kuliingiza taifa kwenye migogoro


Chanzo: Mwananchi
http://www.mwananchi.co.tz/habari/4-habari-za-kitaifa/792-mrema-atamka-jk-awatimue-wassira-maige
 
Mrema anawazimu yeye kazoea yes yes tu..Mi nampongeza sana Wasira kwa kupinga wazi wazi muswad huu.this is the kind of a minister we real want.Sio kila hoja ikiwasilishwa na Waziri mwenzako basi unaunga mkono huo ni ujinga..Mrema naye atulie kashachoka kisiasa apumzike kwa amani alee wajukuu zake kama alivyosema mwenzake Keenja.
 
Mrema kaishiwa. Waziri, kama mbunge, anayo haki ya kuuliza maswali na siyo tu kuwa mtu wa "yes sir." Kwa Wassira inaeleweka mwaka huu wa uchaguzi hali ni ngumu kule Bunda. Mgodi wa Buhemba dhahabu imeisha bila wakazi wa kule kufaidika chochote, na hayo ndiyo maswali tunayomsubiri kumwuliza wakati wa kampeni.

Kwa hivi naona ameanza kujihami, ingawa mi nafikiri it is too late. Kuna sokomoko bado linafurukuta Nyamongo, na ingawa hili si eneo lake lakini tunaweza kumwuliza kama jirani mwakilishi serikali imechukua hatua gani. Kama Mrema anataka kuomba kazi kutoka kwa serikali ya Kikwete aseme tu siyo kujifanya lap dog wa CCM.
 
Ukisoma gazeti unaweza kufikiri ni issue, ila hizo hoja zilikuwa katika semina ya wabunge, na Wasira ni mbunge wa Bunda..Jasusi atamuuliza Wasira habari za Buhemba na Nyamongo wakati wa Kampeni ya Mkono Musoma Vijijini (ilipo Buhemba) na Nyamongo jimbo la Tarime?? It doesnt make any sense habari za majimbo mengine kama Bunda vile hakuna matatizo yao wenyewe Bunda....basi lisiishe jirani wa Mkoa, hata Buzwagi napo sio mbali na Mara au Longido, Arusha nae aulizwa Mb jirani...hakuna ukomo kwa hilo.

Wasira Bunda anapendwa sana na watu, Ukwasi wa Miradi ya Maji aliyoleta Bunda pale akiwa Waziri wa Maji miezi kumi tu...Hakuna wauza kobe na wauza Nyoka watakaomuweza pale Bunda 2010, liandike hilo sisi tunaojua Buhemba iko kwa Mh. Mkono na sio Bunda kwa Mhe.Waziri Wasira(MB)...Kwa Mkoa wa Mara nadhani ndiye atakayepita bila kupingwa kama 2005 sababu ya performance yake Jimboni na ukaribu na watu wake..respect!
 
"Huo si muswada wa (Waziri wa Nishati na Madini, William) Ngeleja bali ni mali ya serikali ya CCM na waziri yeyote hana ruhusu ya kuupinga. Anayeona hajaridhika na maamuzi, anatakiwa kujiuzuru kabla ya kuupinga hadharani," alisema Mrema.

This guy is a Muppet.....muswada ni mali ya CCM? sasa si upitishwe na NEC basi? yeye alifukuzwa kwa kutoa siri za baraza lka mawaziri sasa huu muswada ni siri gani?
 
Nimesikia na Peter Kisumo a.k.a "Mwanasiasa anayeheshimika" naye akisema Wasira na Maige wajiuzuru. Hapo ndipo unapoona nchi hii imeshauzwa. Hivi mtu kama Peter Kisumo ukijiuliza huu Uenyekiti wa Bodi ya Vodacom ameupataje jibu utalipata vipi ? Si kwa kupigia debe mambo kama haya ? Stupid, Alafu mtu huyu ndo unaweza kumweka kundi moja na watu kama EDWARD MORINGE SOKOINE (RIP) ? Huyu hana tofati na Kingunge Ngombale Mwiru
 
Nimesikia na Peter Kisumo a.k.a "Mwanasiasa anayeheshimika" naye akisema Wasira na Maige wajiuzuru. Hapo ndipo unapoona nchi hii imeshauzwa. Hivi mtu kama Peter Kisumo ukijiuliza huu Uenyekiti wa Bodi ya Vodacom ameupataje jibu utalipata vipi ? Si kwa kupigia debe mambo kama haya ? Stupid, Alafu mtu huyu ndo unaweza kumweka kundi moja na watu kama EDWARD MORINGE SOKOINE (RIP) ? Huyu hana tofati na Kingunge Ngombale Mwiru

Huyu ni machinery ya EL na RA na ndio alimnadi JK pale kibaha alipotangaza kugombea....migononi mwa RA na EL.....inabidi pia ujue wamiliki wa VODACOM...ALPHATEL.....
 
Nimesikia na Peter Kisumo a.k.a "Mwanasiasa anayeheshimika" naye akisema Wasira na Maige wajiuzuru. Hapo ndipo unapoona nchi hii imeshauzwa. Hivi mtu kama Peter Kisumo ukijiuliza huu Uenyekiti wa Bodi ya Vodacom ameupataje jibu utalipata vipi ? Si kwa kupigia debe mambo kama haya ? Stupid, Alafu mtu huyu ndo unaweza kumweka kundi moja na watu kama EDWARD MORINGE SOKOINE (RIP) ? Huyu hana tofati na Kingunge Ngombale Mwiru

Ndio maana kapiga kelele nyingi juu ya muswada wa kupeleka makampuni ya simu DSE ili Watanzania wayamiliki...sadly na rais kakataa ku-assent hiyo bill....kenya wameipeleka safaricom NSE siku nyingi
 
Ni ukweli usiopingika kuwa Mrema kachoka kisiasa inabidi sasa aache mambo ya Siasa mvuto wake ulishaisha zamani
 
Wasira na Maige Mashujaa ktk hili...Muswada wa Madini unachomolewa hautojadiliwa until futher notice...Heshima ya Mzee Peter Kisumo cku hz sawa na bure tu...
 
Mzee Safari

Asante kwa hilo, Mimi ndo maana nimeishajichokea na nchi hii, Yaani kila mtu sasa hivi ni mwizi tu sijui tunawarisisha ni watoto wetu ? Tazama sasa hawa vijana walioko serekalini kama Masha na mwenzie Ngereja tulitegemea labda wangelikuja na mawazo mpya lakini kumbe ni yale yale tu. Sadly, Wapiga kura wengi Tz ni bendera yafata upepo. Hakuna changes zozote zile zitakuja Octoba kwa kifupi tumeliwa.
 
Back
Top Bottom