Lekanjobe Kubinika
JF-Expert Member
- Dec 6, 2006
- 3,019
- 580
OK. Lakini tusisahau kwamba hakuna mtu mbaya asiyekuwa na uzuri, and the converse is also true.
Si ni mrema aliyelifanya jiji la DSM lipambwe na vivuli vya miti tunavyoviona sasa? Vipi veranda za wahindi jijini ambazo zilijaa tope na wahindi wakalazimishwa na mrema kujengea concrete pavements? Mmesahau majumba yaliyokuwa yanaonekana kama magofu mijini kwa kupauka lakini amri ya siku saba ya mrema ikayageuza peponi kwa usafi baada ya kukarabatiwa na kupakwa rangi? Ni nani aliyeanzisha police posts kila mtaa kama sio mrema akiwa mambo ya ndani? Au tusemeje sijui, makonda kuvaa sare sio mrema aliyeanzisha kwa zilezile amri za siku saba? Wanawake kufunguka akili kwamba wawapeleke waume zao vituo vya polisi kama wanadundwa sio mrema ambaye alikuwa kipenzi cha wanawake isipokuwa mkewe tu?
Nakumbuka wakati fulani madaktari wa Muhimbili waliandamana kwenda ikulu kupitia wizara ya mambo ya ndani, mapolisi wakataka kuwapiga mabomu ya machozi na kuwazuia, lakini mrema aliwauliza kama waandamanaji hao wameshika silaha yoyote au wanafanya fujo, akaambiwa wanatembea tu na hawafanyi fujo yoyote ila kuyabana magari yanayopita. Mrema akawaambia mapolisi wawaache madaktari waeleze hisia zao kwa amani wasibughudhiwe, akaonekana dirishani kwake akiyafuatilia maandamano hayo yakipita pale kwake, tena baadaye alikwenda mwenyewe tena kwa mguu ikulu kuhakikisha anachoambiwa na wasaidizi wake ni sahihi. Nilishangaa maafisa wa polisi wakiwapanga na kuwaongoza waandamanaji sehemu ya kukaa kwenye lango la kuingilia kwa waziri mkuu na kuwaruhusu viongozi wa waandamanaji kuingia ndani wengine wakilindwa pale langoni kwa amani, raha mustarehe. Pamoja na maneno ya kiuchokozi waandamanaji wengine waliyokuwa wanamrushia afisa wa polisi, yeye aliziba masikio kwa pamba akitazama tu ingawa angeweza kufanya kitu mbaya kama angetaka. Hiyo yote ilikuwa ni amri ya mrema ambaye alimonitor yeye mwenyewe binafsi na tena alichanganyika nao na kuchat au kuwapungia mkono. Je, kuna waziri gani kabla na baada ya mrema kaonyesha ushirikiano huo? Tena wakati ule bosi wake Rais alikuwa Zimbabwe kikazi, ambapo maandamano hayo mapolisi wangegeuza tafsiri kuwa ni uhaini ili wajihalalishie vipigo.
Acha bwana, kweli mrema ana hasi nyingi sana, lakini historia itamkumbuka katika chanya nyingi sana, baadhi yake hizo hapo juu. Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Watanzania wa leo ni waelewa sana sio kama enzi zile. Humdanganyi mtu isipokuwa kama mtu huyo naye anatafuta kukudanganya, kazi ikawa kutafuta nani mdanganyaji zaidi. Nani kakwambia kuna mwanasiasa anayeheshimu haki 100% Ukitaka kuwa mwanasiasa mwenye mafanikio makubwa ni lazima uwe msanii uliyebobea. Jibu unaloliita ni sahihi kwa leo sio jibu sahihi la jana na hatujui kesho itakuwaje.
Ndiyo maana naichukia siasa upeo. Sina hakika kama hata huko akhera mwanasiasa anayo nafasi kama inatokea akiwa ndani ya uanasiasa, ni kama na ilivyo vigumu kwa matajiri kuingia mbinguni au tuseme ngamia kupita tundu la sindano. Ni sawa na makaburi meupe kwa kupakwa chokaa nje lakini ndani kumejaa mifupa. I hate politics! Lazima uwe mbinafsi kwa sababu vinginevyo siasa sio mahali pako. Unapotoa khanga unategemea kukubaliwa na hao unaowapatia khanga. Huo uchungu wanaodai wanao kwa wanachi na maumivu yao sio kweli, wanao uchungu na matumbo yao. Kwani uchungu huo una tija kwa kupewa nafasi ya uongozi wa siasa tu, mbona hawafanyi lolote msipowachagua?
A good politician - relatively though - ni yule anayejitoa kufanya kazi bega kwa bega na wananchi katika jitihada ya kuikwamua jamii kuondokana na matatizo yanayowakabili, pasipo kujiwekea matumaini ya kulipwa fadhila kwa kupewa returns za kuchaguliwa tena na kujitafutia sifa kwa kutumia migongo ya wasio na hatia. Nene mvifile hilo.