The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

Mrema bado ana ile kasumba ya udikteta aliyokuwa nayo wakati akiwa waziri wa Mambo ya Ndani ya kuwapa watu siku saba bila kuangalia sheria inasemaje mtu akipingana naye kwake ni mtovu wa nidhamu, kuna wakati alilazimisha watu wapande miti mbele ya maduka yao bila kuangalia hali halisi wala kutumia busara, wahindi wengi Dar pale mtaa wa uhuru na samora ilibidi wabomoe velanda zao za sementi hadi kwenye lami barabarani ili wapande miti, ni mambo haya haya ya kiimla aliyoyapeleka NCCR hadi TLP sasa anataka sumu hiyo isambae hadi serikalini.
 
Ngurudoto,
Mkono ni mbunge tu. Wassira ni waziri katika serikali. Kwa hiyo ni haki ya kumuuliza maswali yanayohusiana na maamuzi ya serikali hata kama Buhemba na Nyamongo hayamo kwenye eneo lake la uwakilishi.
 
This is the Wassira I used to know

Jasusi

Serikali yaparaganyika

lC.gif
Mwandishi Wetu​
Aprili 21, 2010
rC.jpg
bul2.gif
Mawaziri, watendaji kila mtu na njia yake
bul2.gif
Dk. Slaa asema ni dalili za mwanzo za ufalme uliogawanyika
IKIWA katika maandalizi ya kuomba kura kurejea tena madarakani, Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, haiko pamoja, ushahidi wa hili ukiwa matukio kadhaa likiwamo la karibuni zaidi la mawaziri kupingana waziwazi nje katika suala lililopitishwa ndani ya Baraza la Mawaziri, Raia Mwema limebaini.
Wiki iliyopita Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira akichangia katika muswada wa Sheria ya Madini wa mwaka 2010 aliupinga muswada huo akisema kwamba haukuwa na maslahi kwa umma wa Watanzania.
Wasira alifanya hivyo mbele ya Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, na mbele ya wabunge wengine na wadau mbalimbali wa madini nchini katika mkutano wa wadau hao wa madini uliokuwa umeitishwa kuudurusu muswada kabla ya kuuwasilishwa bungeni. Miswaada huwasilishwa bungeni baada ya Baraza la Mawaziri kuiridhia.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu, Philip Marmo, ameiambia Raia Mwema kuwa muswada huo wa Sheria ya Madini wa mwaka 2010, ulijadiliwa kwa kina kwenye Baraza la Mawaziri.
Lakini katika maoni yake nje ya Baraza la Mawaziri, Wasira ambaye ni Mbunge wa Bunda, Mara alihoji: "Nchi inapata nini na wananchi watapata nini?" na baada ya kuhoji alishauri kuwa lazima muswada wa sheria hiyo kwa makusudi ulenge kusaidia wachimbaji wadogo ambao ndio msingi mkubwa wa maendeleo ya sekta ya madini.
Waziri huyo ambaye alisema wazi kuwa alikuwa akizungumza kama mdau wa madini akiwa hana elimu ya sheria, alisema suala la madini ni suala nyeti nchini na kwa hali yoyote sheria inayotarajiwa kutoa mwongozo wa madini, lazima ijibu hoja muhimu za manufaa kwa Taifa na wananchi.
"Haya mapendekezo yanatofautiana hata na Sera ya Taifa ya Madini," alisema Wasira huku akifungua ukurasa wa 16 wa kitabu cha sera hiyo cha Septemba 2009, kilichotiwa saini na Waziri Ngeleja na kusoma sehemu iliyoandikwa Policy Statement.
Katika sehemu hiyo, kipengele cha ii cha kitabu hicho ambacho gazeti hili limefanikiwa kupata nakala yake inasema: "Serikali itachukua hatua za lazima kuwawezesha Watanzania kushiriki katika uwekezaji wa kati na mkubwa wa uchimbaji madini (The Government will take necessary measures to enable Tanzanians to participate in medium and large scale mining.)"
"Je, haiwezekani kuwawezesha watu masikini, wawekezaji wa ndani?" alihoji Wasira akitoa mfano wa Sweden ambayo uchumi wake unategemea madini kutokana na kuwezesha wachimbaji wadogo wazawa.
Waziri Wasira alisema wazi kuwa sheria lazima ijibu hoja za sera, na Ilani ya Uchaguzi ya CCM ambavyo vinataka wachimbaji wadogo kuendelezwa na kuwa msingi wa uchumi mambo ambayo katika muswada huo hayakujionyesha.
Lakini wakati Wasira akisema hayo hasa Muswada huo wa madini kushindwa kujibu Sera ya Taifa ya Madini, Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka, naye anabaini kuwa muswada huo umekwenda kinyume cha Sera ya Taifa ya Madini na hasa katika kipengele cha kutaka migodi ya madini ya vito kuendeshwa na wazawa kwa asilimia isiyopungua 50.
"Sera inataka Watanzania waweze kuendesha migodi ya vito kwa asilimia isiyopungua 50 lakini sheria inataka miaka 25 kwa migodi mikubwa. Hii si sahihi na ni kinyume cha sera," alisema Sendeka ambaye anatoka katika jimbo lenye mgodi wa madini pekee duniani wa Tanzanite, ulioko mkoani Manyara.
Ukurasa wa 18, sehemu 5.7 kitabu hicho cha muswada inazungumzia maendeleo ya madini ya vito, ambako msingi mkuu wa sehemu hiyo unatajwa kuwa ni kuwawezesha Watanzania kushiriki katika uchimbaji wa madini ya vito. Katika sehemu ya policy statement kuhusu sehemu hiyo kipengele cha ii kinasema; "Serikali itahakikisha uchimbaji mkubwa wa madini ya vito unakuwa mikononi mwa Watanzania kwa asilimia isiyopungua 50."
Kwa maoni yake, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbroad Slaa hali hii ya Waziri Ngeleja kuwasilisha muswada wenye vipengele vinavyopingana na sera aliyotoa takriban miezi minane tu, bila watendaji wa wizara hiyo kubaini kasoro hiyo na kisha Baraza la Mawaziri kujadili muswada huo bila kubaini kasoro na hatimaye Waziri Wasira kukosoa, ikizingatiwa kuwa ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri, ni dalili za ufalme uliogawanyika.
"Hii inathibitisha kuwa masuala mengi (yakiwamo ya sera) yanabaki kuwa ya kisiasa zaidi kuliko utekelezaji unaozingatia maslahi ya nchi. Kwanza , wadau wamezungumza na imebainika kuwa hawajapata muda wa kutosha kujadili muswada huu, ambao maswali ni mengi zaidi kwa kuwa umeletwa kwa hati ya dharura, upitishwe bungeni kumbe unapingana hata na sera waliyotunga wenyewe," alisema Dk. Slaa katika mahojiano na Raia Mwema.
Dk. Slaa aliunganisha tukio hilo la mawaziri kupishana na mmoja wao kuwasilisha muswada unaotofautiana na sera, na tukio la hivi karibuni la Rais Jakaya Kikwete, ambaye ni Mwenyekiti wa CCM, kumteua Husna Mwilima aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa CCM aliyefukuzwa kwa hoja kuwa ni mtendaji asiye na uwezo kikazi, hoja iliyoshangiliwa na Mwenyekiti wa Umoja huo, Sofia Simba, ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utawala Bora ni mkanganyiko mwingine na dalili ya ufalme uliogawanyika.
Raia Mwema ilizungumza na Waziri Marmo katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kuhusu masuala mawili ya msingi. Kwanza ni kutaka kujua kama muswada huo ulijadiliwa kwenye Baraza la Mawaziri, lakini pili azungumzie mkanganyiko huo kwa kuhusisha umakini wa Baraza hilo la Mawaziri katika kuchambua masuala ya nchi. Mazungumzo hayo yalikuwa hivi:
Raia Mwema: Waziri huu Muswada wa Sheria ya Madini wa mwaka 2010, pamoja na ule wa Sheria ya Mifugo wa Waziri Dk. John Magufuli ambao ulikataliwa bungeni, yote ilipitia mchakato wa kujadiliwa katika Baraza la Mawaziri?
Waziri Marmo: Ooh! hiyo sawa, yote ilijadiliwa kwa kina katika Baraza la Mawaziri.
Raia Mwema: Kuna mambo mawili yamejitokeza. Kwanza, muswada umebeba vipengele tofauti na matakwa ya sera ya madini, pili, mawaziri licha ya kuwa na fursa ya kujadili, wametofautiana hadharani mbele ya wadau na kwa kawaida, kikao cha Baraza la Mawaziri kinaongozwa na Rais au Makamu kama Rais hayupo, au hata Waziri Mkuu kama wote wawili hawapo. Unazungumziaji umakini wenu na mgongano wa mawaziri?
Waziri Marmo: Mhh! Hiyo hapana bwana, siwezi kuzungumzia…achana na mambo hayo.
Mbali na Wasira, muswada huo pia ulipingwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige ambaye hata hivyo haingii kwenye Baraza la Mawaziri. Wanaoingia kwenye vikao vya baraza hilo ni mawaziri pekee.
Pamoja na viongozi hao, wadau wengine pia walipinga muswada huo, wengi wakitaka kutoundwa kwa chombo cha ushauri wa masuala ya madini kama inavyopendekezwa na muswada huo na badala yake, iundwe mamlaka ya madini, itakayokuwa na jukumu la kusimamia sekta yote ya madini huku ikiwa huru nje ya minyororo ya Serikali.
Katika mkutano huu wa Bunge, Waziri mwingine aliyeonja ‘kibano' kutokana na kutojiandaa kwa kuzingatia matakwa ya wadau ni Magufuli ambaye alilazimika ‘kuchomoa' muswada wake bungeni baada ya wabunge kuujadili kwa hoja kali, zenye tafsiri kuwa muswada huo utakwenda kinyume cha maslahi ya wafugaji na Taifa kwa ujumla.
Baada ya kuchomoa muswada huo, Magufuli alilazimika kufanya semina kwa kuwashirikisha wadau ili kuwasilikiza upya na kuingiza mapendekezo yao . Semina hiyo ilifanyika siku moja na ile ya Nishati ya Madini kuzungumzia muswada wake wa sheria ya madini wa mwaka 2010.
Lakini hali kama hiyo pia iliwahi kumpata Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utawala Bora, Sofia Simba, ambaye katika mkutano wa uliopita wa Bunge, mkutano wa 18, aliwasilisha Muswada wa Sheria ya Usalama wa Taifa, ambao ulipingwa na wabunge wengi, wakiwamo wabunge waandamizi wa CCM kama John Malecela. Simba alichomoa muswada wake na kwenda kujiandaa upya.
hs3.gif
 
Mrema kaishiwa. Waziri, kama mbunge, anayo haki ya kuuliza maswali na siyo tu kuwa mtu wa "yes sir." Kwa Wassira inaeleweka mwaka huu wa uchaguzi hali ni ngumu kule Bunda. Mgodi wa Buhemba dhahabu imeisha bila wakazi wa kule kufaidika chochote, na hayo ndiyo maswali tunayomsubiri kumwuliza wakati wa kampeni.

Kwa hivi naona ameanza kujihami, ingawa mi nafikiri it is too late. Kuna sokomoko bado linafurukuta Nyamongo, na ingawa hili si eneo lake lakini tunaweza kumwuliza kama jirani mwakilishi serikali imechukua hatua gani. Kama Mrema anataka kuomba kazi kutoka kwa serikali ya Kikwete aseme tu siyo kujifanya lap dog wa CCM.

Jasusi, ndio Wasira ni kiongozi wa Serikali (Waziri) na Mkono ni Mbunge....Ktk maelezo unafikiri licha ya kiherehere cha kuchambua Muswada wa Madini, unafikir ni kujihami and its too late kiuchaguzi..Sasa, kama hali ya Waziri wa Kilimo na Chakula (dhamana yake ya 1-kwa-1) kisiasa ni mbaya sababu ya Buhemba na Nyamongo ambapo ni jirani kwa sababu ya mustakabli wa Madini, je hali ya Waziri wa Nshati na Madini mwenyewe hali yake kisiasa si itakuwa haielezeki basi sasa?

Jasusi, umetuchanganyia mambo pamoja na maeneo ya majimbo Nyamongo, Buhemba na Bunda..
 
Ngurudoto,
Mkono ni mbunge tu. Wassira ni waziri katika serikali. Kwa hiyo ni haki ya kumuuliza maswali yanayohusiana na maamuzi ya serikali hata kama Buhemba na Nyamongo hayamo kwenye eneo lake la uwakilishi.

Jasusi, ndio Wasira ni kiongozi wa Serikali (Waziri) na Mkono ni Mbunge....Ktk maelezo unafikiri licha ya kiherehere cha kuchambua Muswada wa Madini, unafikir ni kujihami and its too late kiuchaguzi..Sasa, kama hali ya Waziri wa Kilimo na Chakula (dhamana yake ya 1-kwa-1) kisiasa ni mbaya sababu ya Buhemba na Nyamongo ambapo ni jirani kwa sababu ya mustakabli wa Madini, je hali ya Waziri wa Nshati na Madini mwenyewe hali yake kisiasa si itakuwa haielezeki basi sasa?

Jasusi, umetuchanganyia mambo pamoja na maeneo ya majimbo Nyamongo, Buhemba na Bunda..
 
Malaria sugu inaelekea unatumia muda wako mwingi kwenye vijiwe vya kahawa ambako kunakuwa na story za kipumbavu kila mara.Kila wakati unapenda kuleta story zenye mwelekeo wa kidini dini sijui inakusaidia nini ?.Jaribu kuleta mada za kusaidia jamii si kila mtu anapenda kusoma habari za ohoo mara nani alizuia ujenzi wa chuo kikuu cha waislamu hatujapumzika ohoo waislamu wananyimwa elimu ukikaa kidogo ohoo waislamu walipigania uhuru wa Tanganyika lakini wakawekwa pembeni sijui kesho utakuja na story gani !!!!!!!!!!!!.
 
"...mtu aliyefilisika kisiasa, kijamii au kitamaduni atatafuta uhalalali ndani ya jamii kwa kupitia aidha DINI, UKABILA, RANGI na vitu vya namna hii!....NYERERE"
 
Zinguo na itikaf nini? Je, ni mambo ya mashetani? Yawezekana Mrema amekwisha kisiasa sio kwa sababu ya waislamu, ni kwa sababu hana jipya! Haya ni mambo ya Shekh Yahya!!
 
Ni wazi mrema alivuma kwa kasi ya ajabu. historia alioweka kuwa mgombea urais upinzani kuchukua 33% haijavunjwa na haitegemei kuvunjwa hivi karibuni.
lkn kiongozi huyu tayari aliwahi kukosana na waislam na hadi kufikia kukaliwa "ITIKAF" ya kumfanya aanguke kisiasa na kutokuwa na nguvu.
miaka sas tangu itikafu hiyo ikaliwe na tayari Mrema sasa amefilisika kisias. hana mvuto. jee mrema anahitaji kuomba radhi na kupata "zinguo" ili arudi ktk kisiasa?

Walimsomea albadiri ili afe,hiyo itikaf ndo kitu gani,acha kuongopea eti waltaka aanguke kisiasa,ukweli ni walitaka afe,na tatizo lilikuwa issue ya mabucha ya nguruwe.
 
leteni mijadala yenye manufaa kwa jamii si ya udini maana haitujengi chochote zaidi inaeneza chuki zisizokuwa na maana:mmph:
 
Ni wazi mrema alivuma kwa kasi ya ajabu. historia alioweka kuwa mgombea urais upinzani kuchukua 33% haijavunjwa na haitegemei kuvunjwa hivi karibuni.
lkn kiongozi huyu tayari aliwahi kukosana na waislam na hadi kufikia kukaliwa "ITIKAF" ya kumfanya aanguke kisiasa na kutokuwa na nguvu.
miaka sas tangu itikafu hiyo ikaliwe na tayari Mrema sasa amefilisika kisias. hana mvuto. jee mrema anahitaji kuomba radhi na kupata "zinguo" ili arudi ktk kisiasa?

hapa ume-proove ukenge na uchawi wa allah na muhammad!!! need to say more?
 
hapa ume-proove ukenge na uchawi wa allah na muhammad!!! need to say more?

macho_mdiliko, please punguza jazba. With all due respect, maneno uliyotumia hapa si sawa! Huyu "Allah na Muhammad" kuna watu wana imani naye. Hili si ustaarabu na sidhani kama mmoja wa "Great Thinkers" unaweza tumia haya maneno.

Nashauri futa haya maneno yako, ili usimkwaze mtu aliye na imani na Allah na Muhammad.
 
Walimsomea albadiri ili afe,hiyo itikaf ndo kitu gani,acha kuongopea eti waltaka aanguke kisiasa,ukweli ni walitaka afe,na tatizo lilikuwa issue ya mabucha ya nguruwe.

kweli bwana walimsomea jamaa ati afe! Jamaa hadi leo na kesho anakula dona kama kawaida.
 
mbona waislam haohao hawajamwombea lipumba anayetoka kwenye chama cha kiislamu cha cuf...........................????????????????
kwani wote wanaoshindwa urais ni kwa sababu ya waislamu ??kama ndivyo basi ndugu zangu waislamu mnaimani mbovu sana ya kuombea mabaya watu kitu amabcho Mungu wa kweli wa wakristo hapendi???????????????????........
ndio maana sheikh yahaya kafanikiwa kwa kuwaroga watu wasimpinge jk japo walionesha uchu wa kweli nwa kumpinga na tena kwa point za msingi..........
Ni wazi mrema alivuma kwa kasi ya ajabu. historia alioweka kuwa mgombea urais upinzani kuchukua 33% haijavunjwa na haitegemei kuvunjwa hivi karibuni.
lkn kiongozi huyu tayari aliwahi kukosana na waislam na hadi kufikia kukaliwa "ITIKAF" ya kumfanya aanguke kisiasa na kutokuwa na nguvu.
miaka sas tangu itikafu hiyo ikaliwe na tayari Mrema sasa amefilisika kisias. hana mvuto. jee mrema anahitaji kuomba radhi na kupata "zinguo" ili arudi ktk kisiasa?
 
Hivi mrema anaposema kuwa biashara ya Uraisi hailipi na sasa ameamua kuingia jimboni anamaanisha kuwa yeye ni mfanya biashara ya Siasa?. Na je wanavunjo wapo tayari kuchagua mtu anaefanya biashara ya siasa badala ya mtu ambaye yupo kwa ajili ya kwenda kutetea maslahi yao bungeni?. Naomba maoni yenu wana JF
 
Ni mgonjwa yule tangu siku nyingi. Naona Albadiri ya Mwembechai na Mtoro zimefanya kazi kwa kweli. hata ongea yake ni kama mtoto, si yule niliyemjua wakati anatoa siku sabasaba wakati akiwa waziri mkuu msaidizi. Ajabu na kweli anajisifia ati wanasisiem walikuwa wanamshangilia na alipendeza pale jukwaani. UKISTAAJABU YA FIR-AUNI UTAYAONA YA IBILISI
 
Back
Top Bottom