The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

Aisee huyu mzee hana watoto humu wamshauri aache hizi mambo za siasa biashara
 
SIONI TOFAUTI YA MREMA NA MKULU.........they are all walking ghosts!
 
Hivi mrema anaposema kuwa biashara ya Uraisi hailipi na sasa ameamua kuingia jimboni anamaanisha kuwa yeye ni mfanya biashara ya Siasa?. Na je wanavunjo wapo tayari kuchagua mtu anaefanya biashara ya siasa badala ya mtu ambaye yupo kwa ajili ya kwenda kutetea maslahi yao bungeni?. Naomba maoni yenu wana JF


Mi simlaumu mrema yule MZee anamatatizo ya akili... ikiwa ni moja ya magonjwa kibao ya uzeeni... mi ningeshauri wakamuweke sylum.... hadi siku atakapowavulia nguo hadharani ndio watajua kuwa anaumwa... ingekuwa ulaya wangeshamuweka sylum siku nyingi
 
Mrema ametumwa na inafahamika anaharibu siasa ya nchi hii
 
Anayo haki kubadili strategy aonavyo inafaa.Alianza na biashara ya Jumla ( Urais), ameona hailipi , kahamia biashara ya rejareja.... its fair.
 
Uzuri wa nji hii wajinga hawaishi ,yaani unaweza ukafanya lolote na ukapata wafuasi.....huyu jama amedata kabisa..ila kuna wajinga wanamsikiliza.... ..eti kamsifia JK kuwa ndiye anafaa kuwa rais at the same time wanamsimamisha mgombea wa urais toka TLP..kwa nini wasitumie hiyo nguvu na hela katika chaguzi za Ubunge ,Udiwani nk??All in all ametumwa kuvuruga mipangilio ya siasa za upinzani ....stay tuned!
 
Anayo haki kubadili strategy aonavyo inafaa.Alianza na biashara ya Jumla ( Urais), ameona hailipi , kahamia biashara ya rejareja.... its fair.


lakini sasa mbona kama aliomba fadhila/huruma ya CCM 'wamwachie' kule vunjo..ina maana kwa hali ya kawaida hata ubunge hauwezi.....in fact hata udiwani inaweza kuwa issue....
 
Anamsifu JK kwa upande mmoja anamwekea mpinzani kwenye kinyang'anyiro cha Urais. Mrema 1995 sio huyu!
 
mzee kwishne huyu,lakini sitashangaa akishinda huko Vunjo.
 
Mwenyekiti wa TLP, Augustino Mrema, amesema kama wapinzani watakuwa hawaungi mkono mafanikio ya Rais Jakaya Kikwete na kumsakama yeye kwa kumuunga mkono, atajiondoa upinzani kwa sababu hataki upinzani wa kinafiki na wenye majungu.

“Kila ninapokuwa nikimsifia Rais wangu Kikwete wapinzani wananisema na watu wengine kwamba mimi ni kada wa CCM (Chama cha Mapinduzi) ninayetaka kusambaratisha chama changu. Sasa ninasema hivi, kama mtakuwa mnaendelea kunisema na hamtaunga mkono yale yanayofanywa na Rais, nitajiondoa upinzani.

Upinzani ni nini bwana! Mtu anapofanya jambo zuri ni lazima umpongeze. Rais Kikwete amefanya mambo mazuri sana katika nchi hii. Tumpongeze na huo ndio upinzani wa kweli na siyo ule wa kukanusha kila jema linalofanywa,” amesema

Amesema CCM ni watu wazuri na walimwalika Dodoma katika mkutano wao na wamemchangia zaidi ya sh. milioni mbili ambazo atakwenda kuchukulia fomu katika jimbo la Vunjo na kudai kuwa atakayethubutu kugombea jimbo hilo nyasi zitakauka kwani mwaka huu hana mchezo.
 
NO hajawahi; maan mentally yuko CCM; physicall upinzani; naona hata physical anataka kuirudisha sasa
 
Mrema hajawahi na walahafikirii kuwa kwenye upinzani anafanya kazi aliyotumwa kudhoofisha upinzani. Ndo kazi yake huyo!
 
tatizo tanzania ni nchi ya wajinga, lazima mjinga awaongoze, nyinyi huku ni kelele tuuuuuuuu, do something for a change........
 
anaonyesha sura yake kamili, tatizo lake ni 'u-opportunist'
 
Kwa kauli yake aliyowahi kutoa wakati akiwa waziri wa mambo ya ndani kuwa mtu yoyote atakaye toka ccm kwenda upinzani ni mwenda wazimu, basi yeye ni mwenda wazimu tu bado kuvua nguo na kula majalalani.
 
Back
Top Bottom