Mjane wa Augustino Mrema ajumuishwa kwenye mirathi

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
Mahakama Kuu ya Tanzania, masjala ndogo ya Temeke jijini Dar es Salaam, imemaliza mvutano kuhusu nani wanastahili kunufaika na mali za aliyekuwa mwanasiasa mkongwe, Augustino Mrema aliyefariki Agosti 21 mwaka
jana.

Katika hukumu iliyotolewa jana na Jaji Augustine Rwizile, amewataja wanufaika hao kuwa ni pamoja na Doris Mkandala, maarufu kama Doreen Kimbi, aliyefunga ndoa na Mrema Machi 24, 2022 na Mrema akafariki siku 150 baada ya ndoa. Doris Mkandala, maarufu kama Doreen Kimbi, aliyefunga ndoa na Mrema Machi 24, 2022 na Mrema akafariki siku 150 baada ya ndoa.

Ndoa hiyo ilifungwa katika Parokia ya Uwomboni, Jimbo Katoliki la Moshi, wakati huo Mrema akiwa na umri wa miaka 77 na Doreen akiwa na umri wa miaka 38, ndoa ambayo ilipata umaarufu mkubwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii.

Hadi umauti unamkuta, Mrema alikuwa Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Labour Party (TLP) na alishawahi kushika wadhifa wa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani na pia Waziri wa Kazi na Ajira na Mbunge wa Vunjo.

Jaji Rwizile katika hukumu yake hiyo, amewajumuisha pia watoto watatu wa Mrema waliozaliwa nje ya ndoa kama wanufaika wa mali za mwanasiasa huyo sambamba na watoto wa marehemu ambao walizaliwa ndani ya ndoa.

Watoto hao wa nje ya ndoa ni Elizabeth Mrema (52), Elizabeth Mrema (43) na Goodlove Mrema (18), wakiungana na watoto wengine wa Mrema, Mary Mrema (48), Cresensia Mrema (45), Michael Mrema (40) na Edward Mrema (38).

Katika orodha hiyo ya watoto wanufaika wa mali za marehemu yumo Peter Mrema (37), ambaye ameteuliwa kuwa msimamizi wa mirathi, huku mahakama ikilikataa pingamizi lake la kutaka ajumuishwe kuwa msimamizi mwenza.

Alitaka hivyo akijenga hoja kuwa Peter Mrema ambaye aliteuliwa na kikao cha familia kuwa msimamizi, alimbagua kuhusu mali za marehemu na kumwacha katika orodha ya wanufaika na kuwaacha watoto wanne waliozaliwa nje ya ndoa.

Kwa mujibu wa Jaji, mvutano ulikuwa baina ya makundi mawili, kundi moja likiwa ni na mke wa marehemu na watoto waliozaliwa nje ya ndoa na Peter Mrema aliyeungana na watoto wengine wa marehemu Mrema.

Akipinga Doreen kuwa msimamizi mwenza, mtoto huyo wa marehemu (Peter) alidai Doreen sio mtu wa kumwamini na aliolewa na baba yao wakati ndoa yake (Doreen) ya awali haijavunjwa na amekuwa akibadili majina yake mara kwa mara.

Doreen alipinga madai hayo akisema walishaachana kwa talaka na mume wake wa kwanza na hivyo ndoa kati yake na Mrema ilikuwa ni halali, hoja ambayo pia ilikubaliwa na Jaji kwamba kulikuwa hakuna uthibitisho ana ndoa nyingine.

Kuhusu Doreen kuwa msimamizi Kuhusu ombi la Doreen kama anastahili kuwa msimamizi mwenza na Peter wa mirathi ya mumewe, Jaji alisema mtu yeyote anaweza kuteuliwa kuwa msimamizi hata kama sio mwanafamilia au mnufaika ilimradi tu asimamie mali vizuri.

"Hakuna ubishi kuwa muombaji(Peter) ana umri wa miaka 37 na hakuna ubishi ni mtoto wa marehemu na ndio maana alipendekezwa ili asimame kama msimamizi na ameiambia mahakama atatenda haki katika usimamizi huo" alisema Jaji.

Kwa upande mwingine, Jaji alisema Doreen ni mjane wa marehemu na kulingana na ushahidi, hayuko katika uhusiano mzuri na muombaji Peter Mrema. Kulingana na ushahidi wake, walifunga ndoa Machi 24, 2022 na mumewe alifariki Agosti 21, 2022 na muda mwingi mumewe alikuwa mgonjwa na ndio maana waliondoka Moshi na kwenda Hospitali ya Taifa Muhimnbili (MNH) kwa matibabu.

"Katika kuamua hili, nashawishika kusema kwa kuwa Doreen hana uhusiano mzuri na Peter, sio sahihi kumteua kuwa msimamizi mwenza kwa kuwa wawili hawatakubaliana katika masuala muhimu," alisema Jaji Rwizile.

Nani wanastahili kuwa wanufaika?

Jaji alisema kuhusu nani wana uhalali wa kisheria wa kuwa wanufaika, alisema mali hizo zinapaswa kuganywa kwa mke na watoto wa marehemu kama sheria inavyoelekeza pale mtu anapokufa bila kuacha wosia.

"Ni ushahidi wa muombaji (Peter) kuwa watoto wanaotajwa kwenye pingamizi lililowasilishwa na mjane sio watoto wa marehemu hivyo wasiwemo kwenye orodha ya wanufaika na ushahidi wake uliungwa mkono na dada yake," alisema.

Kulingana na Jaji, muombaji huyo ambaye ni mtoto wa marehemu alisema wakati wa uhai wake, baba yake hakuwahi kuwatambulisha kwenye familia yao na wala hajawahi kutamka au kuthibitisha kuwa hao ni watoto wake pia.

Hata hivyo, watoto hao, Goodlove Mrema, Elizabeth Mrema na Elizabeth Mrema Junior walitoa ushahidi kuwa wao ni watoto halali wa Mrema na katika kuthibitisha hilo waliwasilisha vyeti vya kuzaliwa, Jaji alisema ushahidi pekee uliopo ni vyeti vya kuzaliwa ambavyo watoto hao waliviwasilisha kortini na havijawahi kuthibitishwa kuwa ni feki au vilipatikana isivyo halali na vilipokelewa mahakamani kama vielelezo bila pingamizi lolote.

Kwa mujibu wa Jaji, sheria iko wazi kuwa jina la mzazi linaloingizwa kwenye rejista ya msajili na kutunzwa inatosha kabisa kuthibitisha kuhusu nani ni mzazi halali wa mtoto.

"Kwa hiyo nasema Godlove, Elizabeth Senior na Elizabeth Junior nao ni watoto wa marehemu na waorodheshwe katika orodha ya vilivyopokelewa kama ushahidi.
 
Kimsingi hakustahili kupata mgao wa mali kwani hizo mali alizikuta na hakushiriki kuzipata wakati mume wake anazipata yeye hakuwa mke wa mrema. Ila tafsiri ya mahakama imeamua apate. Kama kupata angepata sehemu ndogo sana kutokana na muda mfupi alioishi kwenye ndoa hiyo. Kwa wanandugu inauma sana mtu kupewa urithi wa mali wakati amedumu muda mfupi na hakuna mali iliyopatikana akiwa kwenye ndoa hiyo
 
sasa hapo, mgao unafanyika kwa kutumia sheria ipi? sheria ya kiserikali? au ya kimila? kama ni ya kiserikali jambo ambalo naona ndio linadondokea kwa mrema, mgao wa mjane huwa upi na wa watoto huwa upi na msimamo wa watoto wa kambo huwa upi (kwa hao walioleta vyeti kuthibitisha kwamba ni watoto wa mrema)?
 
Mambo ya urithi wakati mwingine yana ugumu, lakini mtu anatakiwa kuwa na msimamo ni mfumo gani wa urithi ufanyike baada ya kifo chake. mfano aeleze wazi kwamba Sharia (Kiislam) ifuatwe, au Kimila au Sheria ya nchi au kufuata usia atakaouandika. Watu wengi hawaweki wazi kwa kuogopa mfarakano wengine wanahisi kama hawatakufa au uchuro.
 
hata kwenye usia atakaoandika, unasemaje ikitokea muislam akaandika kwenye wasia mgao unaopingana na sharia ya kiislam, kwa kigezo kwamba takwa la muusia ndio la kuheshimiwa katika wosia?mfano amegawa mgao sawa kwa watoto halali na watoto wa kambo, au amegawa nusu kwa mke n.k
 
Ndoa yenyewe haikutengeneza hata mtoto mmoja useme huo urithi atarithi mtoto wa marehemu. Huyo mama angepata sehemu ndogo sana kutokana na muda aliodumu kwenye ndoa hiyo na mali zilizopatikana wakiwa pamoja. Hii mbaya sana, yaani mtu anaolewa anakuta mwanaume ana mali, muda mfupi mwanaume anafariki, sasa huyo mwanamke anastahili nini kupata mirathi wakati hizo mali alizikuta? Hapo ni kurudi kwao tu akaendelee na maisha yake na asitake urithi aone aibu na awe muungwana.
 
huyo amewachezea tu wachaga, ingekuwa sumbawanga wala asingesubutu hata kusogea kwenye mirathi.
 
Back
Top Bottom