The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

The Rise and Fall of Augustine Lyatonga Mrema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KadaMpinzani, Aug 27, 2007.

 1. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  2007-08-27
  Na Simon Mhina

  Mwenyekiti wa TLP, Bw. Augustine Mrema, amesema wapinzani wameunda vikosi viwili, cha anga na nchi kavu kwa ajili ya kuishambulia CCM.

  Aidha, amesema ili kutekeleza azma hiyo, wameshakamilisha mipango ya kupata helikopta zingine nne.


  Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, mwanasiasa huyo alisema mipango ya wapinzani kuzunguka nchi nzima na kuwaeleza wananchi juu ya kilichomsibu Mbunge Zitto Kabwe, imepangwa na viongozi wote.


  Alisema maneno aliyonukuliwa akiyasema Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia yametungwa na CCM.


  "Mimi CCM naijua sana, wameshajua wamejifunga wenyewe na sisi tunataka tuongezee bao lingine! Wameunda vitengo vingi vya propaganda, kikiwemo kile cha kwenye vyombo vya habari," alisema.


  Hata hivyo, Bw. Mrema alisisitiza kuwa mbinu hizo chafu haziwezi kuwavunja nguvu kwa vile sio mpya, na kwamba CCM walizitumia dhidi yake na upinzani kwa miaka mingi.


  "Propaganda ya kwanza ilikuwa kwamba Mrema ni CCM, ya pili wakasema Mrema ni mbinafsi, sasa wameona tumeungana, wanaanzisha fitina, lakini wamekwama," alisema.


  Alisisitiza kuwa mwaka 2010, wataweka mgombe mmoja wa urais na mbunge mmoja wa upinzani kila jimbo.


  Bw. Mrema alisema wapinzani wamegundua kila walikopita kwamba wananchi wamefurahishwa na muungano wao.


  Alisema itakuwa ni kituko cha mwaka kwa viongozi wa upinzani kuvunja umoja huo.


  Hata hivyo, alisema hakuna uwezekano wa umoja huo kuvurugika kwa sababu hakuna mkakati wanaopanga, bila kushirikishana wote.


  Kuhusu 'brigedi' za mashambulizi, Bw. Mrema alisema wameamua kuunda kikosi cha anga na kile cha ardhini.


  Akifafanua, alisema kama ilivyo katika vita ya kawaida, mashambulizi ya anga yanarahisisha, lakini hayawezi kuleta ushindi, bila kushuka chini.

  Alisema kikosi cha anga ambacho kitatumia helkopta hizo, kitaongozwa na Mwenyekiti wa CHADEMA Bw. Freeman Mbowe.


  Alisema kikosi hicho, kitakachowajumuisha makomandoo kadhaa kama Zitto Kabwe, kitakuwa na lengo la kufanya mashambulizi ya nguvu katika vijiji na miji, ambayo ni ngome ya CCM, tena kwa haraka na kwa muda mfupi.


  Alisema kikosi cha ardhini, ambacho ndicho chenye jukumu kubwa, kitakuwa na viongozi watatu, Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), James Mbatia (NCCR) na yeye mwenyewe
  .

  Alisema viongozi hao watakuwa na jukumu la kupita kwa miguu sehemu ambazo zilifikiwa na helkopta, kwa ajili ya kuzisafisha na kuziteka.

  Alisema safari hizo zimeshaanza na CCM wameshagundua mkakati huo na kuona hatari inayowakabili, na ndio maana wameanza propaganda kupitia vyombo vya habari.


  SOURCE: Nipashe
   
 2. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2007
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  sasa mbatia , kasema nini?, ambacho kazuliwa na ccm kada mpinzani?
   
 3. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Aug 27, 2007
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  You dont reveal your tactics and ammunitions to your enemy. CCM wangeshtukizwa na vitu kama hivi ingewachanganya sana. unless mrema ni danganya toto tu na anatoa taarifa kwa ccm...
   
 4. K

  Kasana JF-Expert Member

  #4
  Aug 27, 2007
  Joined: Apr 3, 2007
  Messages: 414
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  sisi tukaze buti tusonge mbele!
  katika msafara wa kenge na mamba wapo.....
   
 5. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #5
  Aug 27, 2007
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Alicho zuliwa Mbatia hiki hapa
  http://www.majira.co.tz/kurasa.php?soma=tanzania&habariNamba=3589

  kwamba
  Kauli hiyo ya Bw. Mrema inafuatia taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo habari hapo jana kuwa, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, Bw. James Mbatia na Chama cha Wananchi (CUF), vimeanza kutilia shaka ziara hiyo kwa maelezo kuwa, itainufaisha zaidi CHADEMA, kupitia umaarufu wa Bw. Kabwe.

  Bw. Mbatia alinukuliwa akisema, anatofautiana na hatua ya CHADEMA kuzunguka nchi nzima kuzungumzia suala la Bw. Kabwe, kwa sababu hawakushauriana kufanya hivyo katika makubaliano yao ya ushirikiano wa kisiasa.

  Aidha, ilidaiwa kuwa wanachama wa CUF hawaoni faida kwa chama chao kushiriki kwenye ziara hiyo, kwa madai itakijengea umaarufu zaidi CHADEMA. Hali hiyo imedaiwa ndiyo iliyosababisha baadhi ya viongozi wa chama hicho kutokuwemo kwenye msafara uliondoka juzi kwenda Kigoma.

  Mwenyekiti huyo wa TLP alisisitiza kuwa taarifa hizo zimetolewa na maadui wao kwa lengo la kuvuruga umoja wao katika kipindi hiki kabla ya kuanza kwa ziara yao ya kuzunguka nchi nzima kuishtaki Serikali kwa wananchi.
   
 6. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #6
  Aug 27, 2007
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Haya aliyonukuu Rwabugiri hapo juu yanaashiria kwamba wapinzani wanaweza kuupoteza mtaji aliowapatia Zitto. Na CCM watanyonga hapo hapo. Wanatakiwa kujipanga kisayansi hasa ili kuukwepa ujanja wa CCM maana huko kuna walobobea zaidi katika mchezo huo. Si vibaya wakiajiri mchezaji nyota kutoka timu pinzani (wajifunze kwa SIMBA na Athumani Iddi), waongezee na kocha mahiri ambaye watamsikiliza. Na mazoezi ya nguvu! ndiyo kazi iliyopo.
   
 7. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #7
  Aug 27, 2007
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,694
  Trophy Points: 280
  Kwa nini upinzani wasifanye counter throgh media kuhusu hayo madai ya mbatia?Inabidi sa hivi upinzani wafanye counter na kuigeuzia CCM kibao kwa wananchi hadi ionekane mbaya na haifai kuwaongoza yaani waone tu kila shida waliyo nayo ni kwa sababu ya
  chama kokoro walichochagua
   
 8. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #8
  Aug 27, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  hawa wapinzani badala ya kuongea mambo ya faragha wao wanatundika kwenye akadamnasi sasa sijui wanafikiria nini hawa watu !
   
 9. D

  DAR si LAMU JF-Expert Member

  #9
  Aug 27, 2007
  Joined: Mar 31, 2007
  Messages: 2,942
  Likes Received: 286
  Trophy Points: 180
  ..huyo ndo mrema,kama ulikuwa unamsikia!
   
 10. Ngurumo

  Ngurumo Verified User

  #10
  Aug 27, 2007
  Joined: May 26, 2007
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Unadhani hata Mrema asingesema CCM walikuwa hawajajua? Nao wana watu wao ndani ya opposition. Ni vigumu kwa upinzani kufanya mkakati kama huu usivuje, kwa sababu suala kama la kuleta helikopta lina taratibu na vibali vinavyopaswa kutolewa. Haiwezi kuwa siri sana, hasa kwa kuwa sasa hviv CCM wanahaha kuwapiku wapinzani.

  Hoja hapa ni kwamba katika hili la madini CCM hawajapata hoja ya kuwaeleza wananchi. Sasa hivi nao wamezamia katika kumchafua Zitto ili asiamainike kwa wananchi. Kazi ngumu.

  Nadhani upinzani unapaswa kuwa na siri zake, lakini si hizi hapa. Haya yote walishayajua. Wala sioni kama kazi hii inapswa kufanywa siri.

  Zaidi ya hayo, naonaa kama Mrema amefanya vema kuwaumbua CCM kwa kumlisha maneno Mbatia. Walifanyia kwenye vyombo vya habari, naye kawaumbua huko huko. Jamii itaamua nani anasema kweli.
   
 11. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #11
  Aug 27, 2007
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Ngurumo,

  Hata mimi nimeshangaa watu wanamlaumu Mrema kwa hili. Kiujumla Mrema ametoa jibu zuri sana hasa kupinga uvumi ambao ulikuwa unaanza kuenea kwamba wapinzani wameanza kutofautiana.
   
 12. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #12
  Aug 27, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  hivi ni kwa nini na nashindwa kupata jibu, yaani tz hamna watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiri kama akina einstein na kuwazidi akili ccm na kuitoa madarakani ? kwa kweli hili swali najiuliza kila siku na sipati jibu naomba mnisaidie.
   
 13. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #13
  Aug 29, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  HALAFU HAPO HAPO TENA..............


  Mgombea urais mwenza wa Mrema ajisalimisha CCM

  2007-08-28 17:53:56
  Na Haji Mbaruku, Jijini

  Aliyekuwa mgombea mwenza urais wa Bw.Augustine Mrema wa TLP katika uchaguzi wa mwaka 2005, Bi. Rukia Kiote ametangaza kurudi CCM na kumsihi Bw. Mrema asione soo lolote kurudi tena CCM.
  Bi.Rukia alitangaza kurudi tena CCM akiwa na watu wengine waliodai kuwa ni wanachama wa vyama vya TLP na CUF, mbele ya Rais Abeid Aman Karume wa Zanzibar.
  Bi. Rukia akadai kwenye mkutano huo wa hadhara kuwa ameamua kurudi CCM baada ya kugundua kuwa alikuwa amepotea.
  Amewataka wale wote wanaoendelea kung?ang?ania upinzani kurudi CCM kwa vile ndicho chama chenye demokrasia ya kweli.

  SOURCE: Alasiri
   
 14. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #14
  Aug 29, 2007
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Vikoso hivyo viundwe pia wawepo apiganaji wa kusimamia sera za vyama husika na sio kwenda kwenye majukwaa tuu .
   
 15. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #15
  Aug 30, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  hapo ndipo watakaposhindwa mzee.
   
 16. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #16
  Sep 1, 2007
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Wapo wote mwanza leo sasa muongo ni Mbatia ama gazeti la mtandao majira na mtanzania.
   
 17. k

  kichwamaji JF-Expert Member

  #17
  Sep 2, 2007
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 233
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ama kweli, Mrema ni mzee wa michapo. Ametuvunja mbavu katika mkutano wa hadhara Mwanza, kwamba Zitto ni mbwa wake. Eti yeye amechoka na kuzeeka, lakini walau anaweza kuwaamuru mbwa wake akina Zitto na Dk. Slaa, "kamata yule, kamata yule." Mbavu hatuna!
   
 18. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #18
  Sep 2, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  source ????
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Sep 2, 2007
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Kadampinzani,

  Ndugu yangu unauliza source ndio yale yaleeee...Alikuwepo ktk mkutano magazeti yenu hayaandiki ila habari za CCM sasa hiyo source itatoka wapi?.. Jamaa kaipata LIVE bado mna question source yake.. damn!
   
 20. KadaMpinzani

  KadaMpinzani JF-Expert Member

  #20
  Sep 2, 2007
  Joined: Jan 31, 2007
  Messages: 3,749
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 0
  hahaaaa, sikujua mzee kama alikuwepo kwenye huo mkutano wa hadhara ! teh teh eti magazeti yetu !! haya Mkuu Mkandara nimekupata
   
Loading...