The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Jamani, mimi hizi tuhuma za ufisadi wa watu zimeshanichosha! Hivi ni wapi duniani zaidi ya Afrika ambapo serikali inakuwa na mafisadi na maskendo kibao halafu hakuna hatua zozote za maana zinazochukuliwa dhidi ya watuhumiwa? Hii haingii akilini kabisa hata kwa mimi mwenye akili ya wastani.

Hivi ni wapi duniani penye demokrasia ya kweli ambapo watu watakichagua chama kilichopo madarakani kuendelea kutawala huku viongozi wa serikali yake wakiendelea kuiba (allegedly) na kuitafuna nchi huku wananchi wake wengi wakiishi maisha ya kifukara? Hivi ni watu gani duniani wanaoweza kuwachagua viongozi ambao ni mafisadi na wasiotetea maslahi yao?

Nina mengi ya kusema na nimechoka kusikia watu wakituhumiwa kwa ufisadi na nimechoka kuona watu wakiendelea kuwapigia makofi na vigelegele mafisadi ambao hata hawawajali.

Aaaagh...nimechoka hata kuandika...

Ngabu,

inasikitisha sana lakini taratibu watu wanapata elimu na wanajifunza cha kufanya. Cha muhimu hapa kwanza ni kuwachukia hawa watu.

Mimi sicheki na mafisadi, siongei nao nicely wakati najua kuwa ni mafisadi this much. Call me Makathi lakini ninachukia hawa mafisadi with a passion.

Magazeti muhimu na makini kama Thisday na mengine yatawafuata hadi mwisho. Magazeti ya kiswahilil kama raia mwema, mwanahalisi na Tanzania Daima yataandika habari zao. Wananchi wakijua kila kinachofanyika watafanya the right thing inshallah!
 
Mwanakijiji,

Fafanua maana nimetoka kapa hapo.

Naona Wazungu wamekosea, hizo milioni ni shilingi sio pounds au dola
kwi kwi kwi!!!!!

Si ajabu Chenge alikuwa analundika tu, alisahau ni dola na akadhani ni pesa za madafu.

Mtanzania you gat it! Ni pounds na sio madafu. Chenge ameonyesa kibri kwa muda mrefu sana. Kama unakumbuka matamshi yake baada Dr Slaa kutoa list ya mafisadi utajua ni mtu wa namna gani.

Taratibu tunamzunguka bila kujali pesa zake. We will make him run for his money. Atalipa wanasheria hadi akome. Huu ni mwanzo na mengine yatafanyika sirini.

Chenge ahesabu muda kama Lowasa ... tik tak tik tak tik tak ..
 
Kwasasa namsikia Bw. Chenge anahojiwa na BBC, anasema hawezi kusema chochote. Anasema ataweza kusema pale uchunguzi utakapomalizika na kujulikana kwamba si za rushwa. Na endapo zitaonekana kwamba ni za rushwa hata sema lolote kwani chanzo chake kitakuwa kinajulikana.

Bw. Chenge amesema hivyo ni vijisenti tu... inatisha.
 
Huuu....!!
Bila wahalifu police watakosa kazi!!...Bila kesi mahakimu Watakosa kazi...
Bila mafisadi!!!?............sijui

Nafikiri tuanze kutathimini haya mambo kwa logic!!Tusi jiachie sana!! kama kiongozi ana iba basi hata mimi mfuasi nitafanya hivyo!!

viongozi wangu!!
Im sorry
 
Umefika wakati wa kumwamsha JK maana naona amelala asije akasema waTZ hawakuniamsha, hii hatari 25B ziko CRDB halafu mnasema TZ masikini, hii nchi tajiri sana ila inaliwa na wachache.
 
🙄🙄🙄🙄🙄🙄😕😉😉😱😱🙄😱
 
Umefika wakati wa kumwamsha JK maana naona amelala asije akasema waTZ hawakuniamsha, hii hatari 25B ziko CRDB halafu mnasema TZ masikini, hii nchi tajiri sana ila inaliwa na wachache.

JK anajua kila kinachoendelea na kukaa kwake kimya kunazua maswali mengi sana!
 
Hivi amerudi au amerudisha na JK, kama alitakiwa kurudi US alikwenda kufanya nini, alikwenda huko kwa gharama za nani?
 
sielewi hata niseme nini, wakati watu wanakufa na njaa, wanakopwa mazao, watoto wanakaa chini, ndugu zetu wanakosa matibabu, wao wanatibiwa nje ya nchi. Watoto na jamaa zao wanasomea nje, wakirudi ndio waajiriwa wa serikali. Mwanangu (Wenetu) anakaa chini, mvua ikinyesha hasomi manake paa linavuja. Wanalipwa mishahara na marupurupu kibao bado WANATUIBIA. Ikija wakati wa kura HAWASHINDI, wanaiba KURA kupitia tume walizoziapisha kulinda yale wayatakayo.

Naanza kupoteza matumaini ya kuishi, kila siku BORA la JANA, yanaibuka mapya. Sijui......................
 
JK anajua kila kinachoendelea na kukaa kwake kimya kunazua maswali mengi sana!

Nafikiri JK akiacha kumwajibisha wananchi watajua cha kufanya maana sasa issue zote zipo wazi. JK nina wasiwasi na kipindi chake cha pili kama atakipata naona atandika hitoria kwa kuwa rahisi kwa miaka 5 tu.
 
Kwakweli Chenge anatisha, wakati anahojiwa na BBC leo amesema HIVYO VISENTI, mwandishi alipombana na kumuuliza hivi fedha zote hizo unasema ni viji sent? AMEJIBU KWAMBA INATEGEMEANA NA VIWANGO VYA MTU. Huyu ndiye Chenge, waziri katika Serikali yetu masikini.
 
Kwa vile anachunguzwa ingekuwa vizuri zaidi ajiuzulu ili apishe uchunguzi huru. Kwani kuna ulazima gani wa yeye kuendelea na uwaziri!!!??? mwambieni asing'ang'nie madaraka, watu hawamtaki na hawampendi. Nasikia eti kijiwe chake ni kwenye bar moja maarufu ndani ya Movenpick.

Kwa uswahili jeuri ya wanasiasa wetu hilo litakuwa gumu! Atang'ang'nia hapo hadi afie hapo. Hivi hawa jamaa magodoro yao yemetengenezwa kwa noti za TZ SHS??? Hawawaonei huruma watu wanaokufa kwa kwakukosa hata ASPRIN???
 
Kimefika kipindi ambacho Mungu ameanza kuitembelea Tanzania,
ambapo Mafisadi wote mtaanza kukanyagana wenyewe na wenyewe mtakimbia na kuacha wasafi waendelee.Mungu ibariki Tanzania Mungu ibariki Afrika.Chenge amua kujiuzulu 7bu hapo ulipo hauna pa kupumulia na umeaibisha mke wako na watoto wako na ukiona umepata shutuma za namna hiyo I think the best way uachie ngazi kwa 7bu Watanzania hawakupendi na hawakutaki na mimi pia kama Mzalendo nakutosa tuu.
Na nikifikiria vizuri hata Mungu mwenye enzi amekutosa mpaka urudi mbele zake kwa TOBA na kabla ya toba urudishe mali za WATANZANIA wengi walio masikini ndipo utasamehewa,failure to do so utakutana na Sir GOD.JF naifagilia sana.
 
Amesema nini?

Visenti? atutajie basi ana kiasi gani jumla na alizipataje.A million bucks mjinga anatutukana kuiita visenti.

Kasema kweli au mnampandishia disc tu?
 
Huyu raisi wetu ni mtu wa ajabu sana. Akiulizwa kwa nini tanzania ni maskini anajibu eti hata yeye haelewi ni kipi ambacho hatujafanya. Pamoja na uozo wote huu, Kikwete akirejea madarakani 2010, nitaamini ngozi nyeusi tumelaaniwa!!!
 
chenge anadharau sana shauri ya kiburi cha pesa za wizi, aliwahi kuulizwa kuhusu yeye kuwa kwenye list of shame akajibu kuwa hawezi kujibu utumbo!!!
 
huenda kuna uhusiano wa moja kwa moja na ushindi wake wa kishindo kwenye kuira za nec, that means walioko ccm hasa nec walishinda kwa kuhonga
 
yafaa tuombe balozi za ulaya zimpige chenge marufuku kuruka ulaya na marekani, viongozi wetu wanaogopa sana sanctions ya namna hii, wanajua wasipoenda ulaya haya mapesa hawana pa kutanulia, kwa kuwa hawa ni viburi watupu naona wazungu watusaidie kuwakomesha waanze na chenge
 
Nchi sasa inayumba

Mwandishi Wetu Aprili 16, 2008


Lowassa, Rostam, Chenge, Mkapa ‘moto’

Kikwete, CCM, Bunge watishwa

CHAMA cha Mapinduzi (CCM) na Serikali zake vinasukwasukwa kiasi kwamba kuna hofu kwamba kama hali haitabadilika nchi itafika pabaya, imeelezwa.

Watu mbalimbali waliozungumza na Raia Mwema wiki hii wanalitaja suala la kuzuiwa kwa Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz kujitetea kuwa dalili za mwisho za jinsi hali ilivyo mbaya ndani ya CCM, hali ambayo inaigusa pia Serikali.

Watu hao wanataja pia tukio la Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, ambaye ana fedha nyingi za kigeni nje ya nchi kuwa ufa mwingine ndani ya CCM na Serikali ambako Chenge anaheshimiwa sana.

Yanatajwa pia matukio kama ya wizi ndani ya Benki Kuu (BoT) kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), mikataba mibaya ya uchimbaji madini na kushindwa kwa Rais Jakaya Kikwete kuchukua hatua thabiti juu ya watuhumiwa, wengine watu wa karibu naye, kuwa ambayo yanatia doa katika mchakato wa nchi kujiletea maendeleo.

Ni mambo hayo, habari zinasema, ambayo yameibua mgawanyiko kwenye CCM na serikalini katika makundi ya wanasiasa wenye nguvu upande mmoja kiasi kwamba sasa mazungumzo ya wazi yameibua mjadala wa kuanza kutafuta mrithi wa Rais Kikwete, miaka miwili kabla ya kipindi chake cha kwanza kwisha.

Anasema mwanasiasa mmoja kuhusu mjadala huo: “ Katika mfumo wa vyama vingi tulioiga kwa wenzetu kama mnakuwa na kipindi mlichojiwekea basi mnamuacha huyo aliyepo amalize kipindi hicho. Lakini mkianza kumjadili hata kabla ya kipindi chake cha kwanza kwisha, hiyo ina maana kwamba kwenye chama chenu kuna matatizo makubwa.”

Lakini vyanzo mbalimbali vya habari vinasema sababu kubwa ya kukua kwa mtikisiko huo ni jinsi Kikwete “alivyoliachia gurudumu” la kile kinachoitwa mapambano dhidi ya ufisadi, huku likiwakumba watu waliokaribu naye na hata wasaidizi wake ndani na nje ya serikali.

Matuko ya hivi karibuni yakiwamo yale yaliyotokea bungeni mjini Dodoma na baadaye katika vikao vya CCM kijijini Butiama, yamechochea moto wa mtikisiko huo ndani ya CCM na serikali yake.



stori inaendelea
 
Back
Top Bottom