The Radar Scandal: Investigation & Progress

Huyu jamaa si ndiye aliyepata kura nyingi sana za NEC? ama walikuwa wanachangua kulingana na kiwango cha ufisadi?

Nakumbuka wimbo wa miaka ileeeeeeeeeee Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo woteee sasa hawa wezi sijui wanaimba nini...
 
Kwani hujui kuwa usalama ua taifa hawafanyikazi ya taifa ila wanafanya kazi ya kulinda maslahi ya mafisadi, kwanza tunahitaji maelezo yao ya kuhusika na kuchukua hela EPA

Ila kwa kweli jamani mimi tangu nizaliwe sijui hawa watu wanaoitwa usalama wa taifa wanafanya nini.. Labda sifahamu vuzuri mambo ya serekali ila kwa kweli kwa mtazamo wangu ni mzigo tuu kwa serekali kwani watu hawa wanakula na kulala bure.. wanaweza kuchukuwa hela mahali popote bila kuulizwa na wizara husika.. wana magari ya kifahari kuliko serekali ya UK, Mhh hawa watu bwana.. Mimi siwachukii ila nachukia unafiki wao.. wanaangalia usalama wa nani wakati nchi inakwisha???? Wafanye kazi basi ili tuweze kuona matumizi yetu wanayotumia ni sawa? I am tied of this people called Usalama wa Taifa....

Ina maana kuwa hawafahamu kuwa Chenge ni Fisadi? kwa nini walikubali arudishwe kwenye baraza lililopita?Au naye ni usalama wa taifa? kwani nilikuwa naongea na baadhi ya watu mahali uatasikia karibu kila mkuu wa mkoa ni usalama wa taifa.. kwa hiyo siwezi kushtuka kusikia kuwa naye ni usalama wa taifa ndio maana wanamuogopa
 
Mimi ninachokiona nyie watu wangu mnajikanyaga saana mara ashitakiwe ccm mara chenge kimsingi bila ya kuleta uhuni anayetakiwa kushitakiwa ni yule ambaye aliyetenda kosa na si vinginevyo haiwezekani hata kidogo mtoto amekosa ashitakiwe baba
 
Jiulizeni ni kwa nini hakuna hata moja aliyeshitakiwa kutokana na UFISADI unaoendelea Bongo? Walisema ati timu ya taifa ilikuwa ni kichwa cha mwendawazimu, WTZ waliyakubali maneno hayo hadi pale alipokuja kunguru wa kuruka ruka kwa jina Max, Je ni nani hasa kichwa cha mwendawazimu?

Richimonduli ndio imetoka hiyo, EPA na mabillioni yaliyopotea BOT just tinking... ... ... hata walioua nao kama DITO bado wanapeta........
 
Swala siyo kuchaguliowa kwa kura nyigi unjua wakati unafanyika uchaguzi haya yoote tulikuwa bado hatujayajua hata hivyo mara nyingine hata mwanao anaweza akawa fisadi usijue itakuwa kiongozi wako na kama unavyojuas tanzania ni kubwa saana
 

Kikwete anaweka historia yake mwenyewe mkuu! Hii inatisha!
 
Tatizo letu ni kuwa kila mmoja wetu anaweza kujiita usalama wa taifa na hakuna wa kuverify kama ni kweli au la...mfumo wa hofu tuliojijengea dhidi ya taasisi hiyo ndo unaifanya ifanye inavofanya....na sijui ni nani huwa anawachunguza pia na wao (cheks and balances) au ndo kama hivo wajifanyia wanavofanya bila kuulizwa? CAG anaangalia mahesabu yao?
 

This is a very interesting subject..najua CIA, FBI, Scotland yard..wote activities zao end of the day wanareport somewer...usalama wetu no one really knws...they work for the interests of CCM not Tanzanians..coz usalama hawajawahi kusema maovu yoyote ya CCM..Lakini upinzani wakiplan campaign tuu..watajaa humo utafikiri kuna mtu anataka kupindua nchi...they really need to re-evaluate their position with the interests of the tanzanian people in mind...
 

Last time I checked Usalama wa taifa wanareport kwa Rais...so baada ya hapo ni juu ya rais na baraza la mawaziri kufuata au kutokufuata mapendekezo/ushauri wao. Swali (ma)rais wetu wanafuata mapendekezo na ushauri wa Usalama wa Taifa au wanayatupa kapuni?

Kuhusu hao Alphabet Boys kama unajua Executive Order 12333 utajua wanareport kwa nani.
 
kwa mara ya mwisho tuliambiwa yuko safarini na Muheshimiwa Raisi nchini India, China na America. Sasa hatuna uhakika yuko wapi baada ya msanga huu kufumuka.
 

Ni wazo zuri sana hili. Lakini nilikuwa naomba kutoa ushauri ili kufanikisha zoezi hili vyema. Kwanini tusifungue mashitaka juu ya mafisadi yote kwa pamoja badala ya kumpeleka Chenge pekee yake mahakamani?. Hapa nina maana Mkapa, Yona, Mkono, Chenge, Mgonja, Mramba, Karamagi, Msabaha, Lowasa, Rostam Azizi, Mzindakaya na wengine wengi.
Kumpeleka Chenge pekee mahakamani ni sawa na kupunguza matawi machache sana katika mti lakini mzizi mkuu wa ufisadi bado utakuwa palepale.
Katika Tanzania Ufisadi wa kutisha umeanza katika awamu ya tatu enzi ya mlafi mkapa, hivyo ingekuwa ni vyema na busara kumkamata Mkapa, kumnyang'anya kila kitu then tuwakamate mafisadi wengine wote na adhabu yao iwe ni kifo kama wafanyavyo China. Tukinyonga hawa mafisadi itakuwa ni fundisho kwa viongozi wengine wajao, lakini tukiwa kila siku ni maneno na kuunda tume basi ufisadi hautakwisha katika Tanzania.
 
Hii regime ya Mr. Kikwete is by far the most INCOMPETENT administration ever. Haijawahi kutokea. Kwa serikali ya kawaida ile scandal moja ya Radar tu ilikuwa inatosha kuleta mapinduzi (kusafisha) ya nguvu ndani ya serikali. Lakini tunaendelea kuona series ya ubadhirifu na scandals one after the other. Iko wapi ile motto yako ya "Ari mpya nguvu mpya", ziko wapi zile ahadi "tam tam" za kuinua maisha ya watanzania? Kutokana na mambo yaliyojiri siku za karibuni kama vile kutoweka na kutotafutwa kwa governor wa zamani wa BOT, kudanganywa kwamba mamilioni ya EPA yameanza kurudishwa bila kutajwa majina ya wahusika, Richmond gate, na ma uvundo mengine kama hili la A. Chenge nimeamua ku conclude kuwa serikali ya Mh. Kikwete inakumbatia mafisadi kwa kila njia. Na ninafikiri sitakuwa na makosa nikisema kuwa sina imani na raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 


The UK is looking after UK...na sisi tujiangalie wenyewe. Angalia jinsi hawa wanavyoungana kulinda huu uchafu wa BAE, yote hii ni kwa sababu nchi yao itaaibika.
 
Akitokea China na India baada ya bosi wake na Membe kuelekea U.S
 
Mwanakijiji,
Motion ya kumng;oa chenge ilishapoangwa siku nyingi ila walikuwa wansubiri ushahidi wa kutosha,madokezo yalishapatikana na kazi imebakia kuwaeleza umma wa watanzania tu kabla unge halijamuangamiza.

suala linalonipa taabu ni kwamba,Je CCM wako tayari kumung'oa Chenge?na Cehenge atakubali kung'oka kama Lowassa bila kuharibu chochote kuhsu wakubwa??
ni moja ya maswali magumu sana kwa sasa ambayo majibu yake inabidi yapatikane mapema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…