Naomba kuwauliza ndugu zangu, kulikuwa na idea ya kumwandikia barua Fisadi Andy au Jak kuhusiana na hatua tunayotaka huyu fisadi achukue au achukuliwe, kulikuwa na hitimisho la ile suggestion?
Sijui hitimisho lilikuwaje lakini nafikiri JK haitaji kundikiwa barua kwa kuwa nina uhakika anaingia Boardin hapa na kuona maoni ya watu, unajua watu hawawezi kukulupuka na kuanza kumsema mtu furani bila kuwa na tetesindo maana waswahili wakasema "Kila lisemwalo lipo kama halipo basi laja" hatutaki tukimshauri akulupuke no he should take his time to investigate lakini la chenge lilikuwa wazi sana, kila mtu alikuwa analiona kama linavyooneka la Mkapa
Uchunguzi wa nini tena wakati ushaidi umepatikana?. Wananchi wanatka kuona vitendo vinachukuliwa kwa watu kama hawa na akina Mkapa alike
CHENGE MJUMBE WA KAMATI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI NA MJUMBE WA KAMATI YA MAADILI YA CCM. Kamati ya Maadili ndiyo iliyopitisha waraka uliowasilishwa katika NEC ya Butiama iliyopaswa kujadili UFISADI wa EPA na Richmond????? Sasa ndio huyooooooooo!!!! Ataendelea katika kamati ya Maadili na Usalama ya CCM?
Waheshimiwa wana JF ni wakati muafaka sasa kwa watanzania kubadilika na kutumia taaluma zetu kutokomeza ufisadi huu.
Napenda kupata ushauli wa kisheria kutoka kwa wanasheria wetu, je hapa Chenge hana kesi ya kujibu? na kama ipo ni utalatibu upi utumike kumfikisha mahakamani hata kama ataendelea na wadhifa wake wa uwaziri? Kama mwananchi wa kawaida ninayo haki ya kumfunguria mashita kwa kuhujum uchumi wa nchi?
Naombeni mawazo yetu ili niweze kushugurikia huyu fisadi mkubwa.