The Radar Scandal: Investigation & Progress

The Radar Scandal: Investigation & Progress

Idara ya Usalama wa Taifa inanuka na inaoza. Inatoa harufu ya mbaya sana kama maji ya kunde zilizovunda. Mie nafikiri cha kufnya hapa ni kuandika barua maalumu kwenda kwa Waziri Mkuu Uingereza atusaidie kwa kutumia vyombo vyake vya uchunguzi ili watuangalizie account za mafisadi wengine maana Tanzania imeshindwa kufanya hii kazi. Kama Chenge alikula hizo sasa baba yao Mkapa alilamba ngapi? Na huyu mtumishi wa TANESCO ni nani????
 
Ninamfahamu Sophia Simba kwa karibu, maneno aliyoyasema kuhusu Chenge ingawa sio mengi ila ni mazito sana kutoka kwa waziri wa serikali ya muungwana, najua kuwa mwisho wa Chenge uko njiani na wala sio swala la mjadala tena,

lakini je Chenge, atarudisha pesa za wananchi?
 
analo huyo..na sasa limemshika pabaya..ila sitashangaa nikiona bado anaendelea kudunda serikalini
 
ooh...tanzania unajengwa na wenye moyo unaliwa na wenye meno....!
 
Tuhuma za Chenge katika Gazeti la Guardian hizi hapa

BAE corruption investigation switches to Tanzania·

Focus on £28m radar deal with East African state
SFO's new director due to take over this month
David Leigh and Rob Evans The Guardian,
Saturday April 12 2008
Article history
About this article Close
This article appeared in the Guardian on Saturday April 12 2008 on p8 of the UK news section.
It was last updated at 00:06 on April 12 2008.
Following the uproar over its halted Saudi investigation, the Serious Fraud Office is expected to decide whether to bring fresh corruption charges against arms manufacturer BAE within six weeks, over a second arms deal, this time with Tanzania.

A minister from the east African state has denied that more than $1m (£507,500) in his offshore accounts came from BAE.

Investigators involved in a three-year inquiry after the controversial deal to sell Tanzania a £28m radar system identified the money in Jersey accounts controlled by the poverty-striken country's infrastructure minister, Andrew Chenge.

Tanzania's anti-corruption bureau, which has been working with authorities in the UK, Switzerland and Jersey, wants to establish if the money is linked to multi-million pound secret commission payments made by BAE.

Chenge does not dispute the money in his Jersey accounts. But he told the Guardian: "The obvious inference [of the investigations] is that I have received for my benefit 'corrupt payments' from BAE. This is untrue."

He said he was only involved in minor aspects of the radar deal, which was promoted by other ministries and approved by the Tanzanian cabinet. His bank records, he said, would show investigators that "there is no connection to the BAE Tanzanian radar deal".

His US lawyer from Cleveland, Ohio, J Lewis Madorsky, added: "While the matters in question took place a number of years ago, we can state ... that any and all allegations of illegality, impropriety, misconduct and unethical behaviour made against our client are categorically and vigorously denied".

Investigators say Chenge could be a valuable witness. The target of their investigation is not him but BAE. The arms company made the commission payments to a local agent in Tanzania to promote the £28m radar sale, through an elaborate chain of offshore companies and a Swiss bank.

The agent has now left the country and is wanted by Interpol.

These developments come at a key moment in the BAE saga. A landmark high court ruling on Thursday said that the decision to drop the SFO's Saudi inquiry was wrong.

In a huge embarrassment for the British and Saudi governments, the court rejected the claims that the inquiry had to be closed down for reasons of national security and because lives would be at risk.

And it took the extraordinary step of naming Prince Bandar, the crown prince's son, as the man behind what it said could be characterised as an attempt to pervert the course of justice.

Former prime minister Tony Blair caused uproar by personally forcing a halt to investigations into the Saudi deal. The Guardian subsequently disclosed that £1bn had been paid into accounts controlled by Prince Bandar during the deal. Bandar says the payments were not improper.

Inspectors from the Organisation for Economic Co-operation and Development (OECD) grilled British officials in London last week about their failure to get results from any of their BAE investigations. Britain signed up to an international treaty to outlaw bribery, but there have never been any prosecutions.

The Tanzania deal, although smaller in cash terms than the Saudi deals, is equally controversial: Tanzania is one of the world's poorest countries, and the UK government is paying more than £100m this year to help the heavily-indebted country's budget.

It was Blair again who forced the radar deal through the British cabinet, despite protests from the then international development secretary, Clare Short. She said the sale, for which Tanzania had to borrow yet more from a commercial bank, was corrupt and "stank".

A lengthy SFO investigation in the UK subsequently discovered that 31% of the deal's contract price had been diverted via Switzerland.

BAE transferred the money to a subsidiary, Red Diamond Trading, registered anonymously in the British Virgin Islands.

Red Diamond then moved the cash to a Swiss account in the name of a Panama company, Envers Trading Corporation. This entity had two Panamanian nominee directors. But it was secretly controlled by a Tanzanian middleman, Shailesh Vithlani, according to Dar es Salaam court papers.

Investigators are now checking whether Vithlani arranged to pass any money in turn to Tanzanian politicians and officials.

Sources said the bank in Jersey had promptly frozen transactions and filed a suspicious activity report when the Tanzanian inquiries began.

Vithlani, who is of Indian extraction but holds a British passport, is listed as wanted by Interpol.

He has been charged by the Tanzanian anti-corruption bureau with lying to investigators, but has left the country. His whereabouts are unknown.

According to the charges, Vithlani falsely denied he was the owner of the Panama company, and falsely claimed he had only handled a separate commission of 1% on the deal.

The SFO's new director, Richard Alderman, former head of UK tax investigations, is due to take over this month. The SFO refused to comment yesterday.

BAE, which has previously denied wrongdoing, also declined to comment, or to explain its chain of offshore payments, other than to say "BAE Systems continues to fully co-operate with the SFO investigation".

The company has recently launched an extensive public relations campaign and last week unveiled a report commissioned from a commercial consultancy, Oxford Economics, which claimed BAE was of key value to the UK economy
 
Ninamfahamu Sophia Simba kwa karibu, maneno aliyoyasema kuhusu Chenge ingawa sio mengi ila ni mazito sana kutoka kwa waziri wa serikali ya muungwana, najua kuwa mwisho wa Chenge uko njiani na wala sio swala la mjadala tena,

lakini je Chenge, atarudisha pesa za wananchi?

Mkuu FM, please mark my words.......The way the wheel is rotating jamaa hahitaji KURUDISHA fedha zetu TUTAZICHUKUA!!!

Jamani hii clip ya kwenye Thisday leo hata kama inaweza onekana kama maneno matupu lakini nimepata moyo na nina imani sana sababu tayari kuna magazeti mengine yamehoji waheshimiwa kule Dom Town na inaonekana wamenuia na wapo willing (and are definatelly able) kuvalia njuga hii maneno!!!
 
Mzee Andrea ni vema akapisha tu kiuungwana na kuipa nafasi serikali na umma kujiridhisha na matokeo ya uchunguzi huu unaodaiwa kufanywa dhidi yake ingawaje sioni uwazi juu ya zoezi zima,JK anakuwa ktk kipindi kigumu sana kimaamuzi kwa hali hii hivyo ni vema mzee wetu Andrea akamsaidia aliyemteua kwa kukaa pembeni ili mambo yakae hadharani,kuna Mawaziri na Manaibu ambao aliwatema walikuwa smart ila wenye media hawakuwapenda na kuwafanyia kampeni mbaya hatimaye wameondoka sasa ni wakti wa mkuu kufanya uteuzi kwa utashi wake kama mwenye dhamana ya kuipeleka salama Tanzania ni si magazeti wala wapambe.
 
Aaaah..PCB si ni washkaji tu.
Chenge is very powerful,na ndio maana ali survive hata reshuffle.Haya yote yalikuwa yanajulikana kwa wenzake wote.However, pia naamini kabisa kuwa enzi za Mkapa sidhani kama angekubali Chenge achunguzwe.Sasa sijui nia ya JK ni nini,lakini ntamsifu kwa kuruhusu huyu bwana achunguzwe

Uchunguzi wa nini tena wakati ushaidi umepatikana?. Wananchi wanatka kuona vitendo vinachukuliwa kwa watu kama hawa na akina Mkapa alike.

Jakaya tulikupa dhamana ya kuongoza nchi yetu kwa misngi ya haki na sheria kwa faida ya nchi na wananchi wote. Mpaka sasa inaonekana dhamana hiyo imekushinda kwani watu wengi walio ndani ya serikali yako ndiyo wanaongoza kwa wizi, rushwa, ufisadi na mambo mengi machafu. Safisha serikali yako kwa kukamata mafisadi wote na kuwapeleka ukonga kama ulivyompeleka Nguza na mwanae kocha papii bila ya kufanya kesi.
 
East African Business Week (Kampala)
been "advised" to resign to pave way for the smooth investigations. "The minister is in President Kikwete's delegation to India, China and later to the UK, but he has been advised to resign when he returns home," a source said.
"Mwacheni mzee wa watu apumzike kwa amani", hizo Paund 5M zitamsaidia mapumzikoni!!!
 
A fourth senior minister (name withheld) in President Jakaya Kikwete's cabinet is expected to tender his resignation following allegations related to his involvement in the radar scandal, East African Business Week can reveal.

Sasa wandugu......nani atakayebaki kuongoza?.....Kanyaga Twende hiyo.....tunatega macho na masikio....
 
Wizara aliyopo hivi sasa inamfaa sana tu. Hiyo ndio miundombinu ya kibantu......
CCM Oyeeeee.....Oyee...Zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM.....Zidumu....
 
Mimi hata sielewi.

Uchunguzi.unachunguza nini wakati AMEKIRI NI ZAKE?

au MIMI NDIO SIELEWI?
 
The East African Business reported this

T
he source told this paper that investigators in the UK have established that the minister has stashed about 5 million pounds into one of his UK bank accounts. Some of the money had been transferred to the account of one of the senior officials working with the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco). It was yet to be established why some of the money was transferred to the official's account

Following the ongoing investigations, the minister has been "advised" to resign to pave way for the smooth investigations. "The minister is in President Kikwete's delegation to India, China and later to the UK, but he has been advised to resign when he returns home," a source said

My Take:
Hii ni nia yake ya kutaka kuresign ila anaweza kudelay so tuendelee kuweka pressure kabla ya Ijumaa awe amesha resign.

Je huyo mtu mwingine huko TANESCO ni Dr. IDRISA???????????
 
Tunapaswa kujiuliza ni kwanini JK ameamua kusfiri na huyu jamaa, what is it that prompted him to travel around with him at this particular moment. Kwa wenye kujiuliza na wanaweza kupata majibu hapo. JK anajua involvement ya Chenge kwenye deals za ufisadi kuliko mimi na wewe tunavyojua, lakini swali linakuja ni kwanini baada ya reshuffle alimrudisha tena? Tukiwa na jibu la hili swali, tunaweza kufahamu ni karata gani JK anataka kucheza, huenda tunakaribia kufungwa goli la kisigino, au kutakuwa na own goal. Huenda Balali ni Chenge, na balali mwenyewe tunayefikiri ana siri kubwa ya ufisadi ni nothing.
Kingine ni kuwa mwenyewe Chenge amesema hizo dola zaidi ya milioni moja alizonazo hazitokani na Radar, lakini mpato yake yanajulikana wazi, na kama sio Radar basi anaweza kutusaidia kutuambia alifanya biashara gani hadi kupata hela zote hizo, inawezekana anasema kweli siyo za Radar, ni za EPA!
 
PCCB tails Chenge

-Minister also confirmed as subject of impromptu twin raids of office and residence by radar deal investigators

THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

THE government's anti-corruption watchdog is now in the process of investigating the source of the over $1m (approx. 1.2bn/-) discovered in offshore bank accounts controlled by the Minister for Infrastructure Development, Andrew Chenge.

According to well-placed sources, the Prevention and Combating of Corruption Bureau (PCCB) will amongst other things seek to establish from Chenge himself how precisely he was able to amass such a huge fortune in his foreign bank accounts.

Although the PCCB Director General Edward Hoseah was yesterday not immediately available for comment, insiders have told THISDAY of the bureau's plans to request a 'written explanation' from the minister on the source of the money found not only to be in his possession, but in offshore bank accounts to boot.

The PCCB's move on Chenge is expected to be made once he returns home from an official trip as part of President Kikwete's delegation, now in Beijing for talks on strengthening bilateral ties and other matters with Chinese President Hu Jintao and his government.

The president and his delegation are scheduled to be back home by Saturday this week.

At the same time, government sources have also confirmed that Chenge was recently the subject of impromptu searches of his office and residence in Dar es Salaam, conducted by British and local investigators.

''Investigators from Britain's Serious Fraud Office (SFO) arrived in the country late last month (March) to help organize the twin raids on Chenge's office and home,'' a senior government official told THISDAY.

''The raids were aimed at looking for and securing documents which could link him (Chenge) directly to the radar issue,'' the official added.

It is understood that the SFO is working on clues that may prove that the million-dollar fortune found in Chenge's offshore bank accounts in Jersey originated from the UK arms manufacturer firm BAE Systems, which supplied the controversial 28 million pounds sterling (approx. 70bn/-) military radar system to the Tanzanian government in 2002.

At the time the highly-dubious deal was negotiated and concluded, Chenge was serving as attorney general and therefore chief legal advisor to the third phase government of ex-president Benjamin Mkapa.

Sources say the PCCB has been working closely with the British investigators, who have already released key information on Chenge's offshore bank accounts.

Hoseah himself is reported to have, at an international prosecutors' meeting in Amsterdam last month, agreed to cooperate further with the SFO in its probe against Chenge and any other Tanzanians suspected to have received hefty but illegal kickbacks in the radar deal.

Reports from Dodoma say the Prime Minister, Mizengo Pinda, is in line to face tough questions on Chenge's fate from members of parliament on Thursday this week, during the Prime Minister's Question Time session in the ongoing National Assembly sitting.

Opposition leaders both within and outside parliament have already begun calling for Chenge's resignation, urging the government to thoroughly investigate the corruption allegations now brought directly against the minister.

After the UK Guardian newspaper broke the news over the weekend, the key question now dominating the public domain is how he was able to stash away more than $1m (over 1.2bn/-) in offshore bank accounts, given past and present government salary rates.

Chenge himself has not disputed the money in his Jersey bank accounts, but he has denied suggestions that it came from corrupt payments from BAE Systems in favour of the dubious radar deal.
 
Chenge ashangaza

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

KUGUNDULIKA kwa akaunti ya mabilioni ya fedha inayohusishwa na Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, kumezidi kufichua masuala mbalimbali.

Katika hatua moja, taarifa kutoka serikalini zinaonyesha kuwa mamlaka kuu za dola ndizo zilizotoa kibali cha kuanza kwa uchunguzi dhidi ya waziri huyo, unaofanywa na Taasisi ya Kuchunguza Makosa Makubwa ya Jinai ya Uingereza (SFO), kwa kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU).

Ofisa mmoja wa juu serikalini aliyezungumza na Tanzania Daima kwa sharti la kutotajwa jina lake gazetini alisema kibali hicho ambacho hakina shaka kilitolewa kwa baraka za mamlaka hiyo kuu ya dola na hususan Ikulu, ndicho kilichowezesha kuingia nchini kwa maofisa hao wa SFO miezi kadhaa iliyopita.

"Unajua kwa mujibu wa sheria za nchi, uamuzi wa kumchunguza mtu mwenye wadhifa wa uwaziri hauwezi ukafanywa pasipo kwanza kibali chake au baraka kutoka katika mamkala za juu za dola," alisema ofisa huyo aliyezungumza na Tanzania Daima.

Wakati ofisa huyo wa juu serikalini akitoa habari hizo, Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amemtaka Rais Jakaya Kikwete, kumfuta kazi mara moja Chenge kutokana na kuhusishwa na tuhuma hizo nzito za ufisadi.

Lipumba alitoa wito huo jana alipozungumzia taarifa za waziri huyo kukutwa na zaidi ya sh bilioni moja katika akaunti yake, katika benki moja katika visiwa vya Jersey, Uingereza.

Mwenyekiti huyo wa CUF aliwaambia waandishi wa habari kwenye makao makuu ya chama hicho, Dar es Salaam jana kuwa, utajiri huo wa Chenge kwa namna yoyote ile ni wa kutilia shaka.

Aidha, Mwenyekiti huyo wa CUF alisema uamuzi huo wa Kikwete utaiwezesha TAKUKURU kuanza kumchunguza waziri huyo kabla ya kufikia hatua ya kumfungulia mashitaka.

"Iwapo Rais Kikwete anayo nia thabiti ya kupambana na rushwa nchini afanye haraka kumwondoa Chenge katika safu ya mawaziri wake. Haiingii akilini mtumishi wa serikali kumiliki zaidi ya sh bilioni moja. Tunaujua mshahara wa watumishi wa serikali, haiwezekani kuwa na kiwango hicho.

"Lazima TAKUKURU ifanye kazi yake ipasavyo na Chenge awekwe chini ya ulinzi, pasi zake za kusafiria zikamatwe," alisema Lipumba ambaye kitaaluma ni mchumi.

Alisema uchunguzi uliofanywa na SFO, umeshuku kwamba Shailesh Vithlani, mfanyabiashara anayehusishwa na ununuzi wa rada hiyo, alitoa fedha za rushwa kwa baadhi ya maofisa na wanasiasa wa Tanzania ili kufanikisha azima ya kuwezesha kununuliwa kwa rada ya kijeshi mwaka 2002.

Lipumba alisema haja ya kumchunguza Chenge, inatiwa chachu pia na kuwa kwake na uwezo wa kumuajiri wakili wa kujitegemea kutoka nchini Marekani, aliyetajwa kwa jina la J Lewis Madorsky, katika gazeti la The Guardian la nchini Uingereza la Jumamosi iliyopita.

"Hii ni rushwa dhahiri ndugu zangu. Wakili anayemtetea Chenge anaitwa J. Lewis Madorsky, anaishi Cleveland, Ohio, nchini Marekani. Gharama za chini kabisa za kuwa na wakili kwa nchi kama hiyo ni dola 200 kwa saa.

"Wakili huyo akiandika barua ya kumtetea mteja wake anaweza kusema ametumia saa nne kufanya kazi hiyo, hivyo malipo yake yanaweza kuwa dola 800 mpaka 1000… Chenge anapata wapi jeuri hiyo wakati nchi yetu ni maskini wa kutupwa?" alihoji Lipumba.

Aidha, alisema uamuzi wa Kikwete kumfukuza Chenge utainusuru Tanzania katika jicho la nchi wahisani na marafiki wa maendeleo ambao wanaweza kukata misaada yao kwenye bajeti ijayo, iwapo hatua hiyo haitachukuliwa.

Alisema hilo linatokana na ukweli kwamba, kitendo cha waziri kukutwa na kiasi kikubwa cha fedha katika akaunti yake ya nje ni doa na kinaweza kuwashtua wachangiaji wa bajeti kutoka nje.

Iwapo itabainika kuwa fedha hizo zimetokana na rushwa, kuna hatari hata ule mpango wa MCC uliosainiwa na Rais George Bush wa Marekani na Rais Kikwete jijini Dar es Salaam hivi karibuni, ukawa mashakani.

Kupitia mpango huo, Marekani imeipatia Tanzania msaada wa zaidi ya dola za Marekani milioni 750, kusaidia miradi kadhaa ya maendeleo katika sekta za miundombinu, maji na afya.

Wasi wasi kuhusu mpango huo unatokana na kauli ya Rais Bush kuwa serikali yake haipo tayari kuzipatia fedha nchi ambazo viongozi wake wanaiba fedha za umma.

Kabla ya kuibuka kwa taarifa hizo mwishoni mwa wiki iliyopita, Waziri huyo wa Miundombinu alishawahi kutajwa katika orodha ya watumishi 11 wa serikali, waliodaiwa kuwa ni mafisadi, iliyotolewa na wapinzani.

Viongozi hao walitajwa na Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, katika mkutano wa hadhara uliofanyika Dar es Salaam mwezi Septemba.

Aidha, Chenge aliwahi kukaririwa na vyombo vya habari akikiri kuwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Tangold, inayomilikiwa na serikali, kabla ya kuwataka wenye ushahidi juu ya tuhuma zake wamfikishe kwenye vyombo vya sheria.

Licha ya tuhuma hizo zote, Februari 12 mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alimteua kwa mara nyingine kuwa Waziri wa Miundombinu katika Serikali ya awamu ya nne, alipolazimika kuteua upya Baraza la Mawaziri, baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa.

Uteuzi huo ulizua malalamiko kutoka kwa wanasiasa wa upinzani na baadhi ya wananchi, walioeleza kushangazwa kwao na hatua hiyo ya Rais Kikwete, huku Chenge mwenyewe akisema kuwa mtu yeyote mwenye malalamiko dhidi ya uteuzi wake, aende akamuulize rais ambaye ndiye aliyefanya uteuzi huo.

Wakati huo huo, Salehe Mohamed anaripoti kutoka Dodoma kuwa sakata hilo limeendelea kuwa gumzo kwa baadhi ya wabunge huku Mbunge wa Maswa, John Shibuda (CCM), kumtaka waziri huyo kujitokeza kujibu tuhuma zinazomkabili.

Shibuda alisema ili Watanzania wawe na imani na Chenge, na wasitumie hisia zao kumhukumu kwa kutumia rasilimali za nchi kwa masilahi binafsi, ni vema waziri huyo akaweka bayana vyanzo vya mapato vilivyomfanya awe na fedha nyingi kiasi hicho.

Aidha, Shibuda alionya tabia ya baadhi ya Watanzania wachache kujipatia utajiri na kutumia aina ya kisasa ya ukoloni kuendelea kuwanyonya Watanzania wenzao ambao kila kukicha umaskini unazidi kushika kasi.

Alisema Watanzania walishawaondoa wakoloni hapa nchini, lakini kuna baadhi ya watu wamerejesha ukoloni huo kwa kuwatumikisha Watanzania pamoja na kutumia rasilimali zao kwa masilahi yao.

Alisema utajiri wa viongozi si hoja, bali hoja ni kwa namna gani wamepata utajiri huo ambao unawatia shaka watu wengi na kuhisi kuwa wametumia madaraka yao kuupata kwa kuhujumu rasilimali za nchi.

Alisema nafasi alizowahi kushika Chenge ni nyeti na ni rahisi kuzitumia rasilimali za nchi kwa masilahi binafsi, hasa kuwekeza kwenye miradi ambayo anaona inaweza kuwa na faida nono na yenye kumrudishia fedha kwa haraka, hivyo kuwa na akaunti yenye fedha nyingi.

"Chenge anapaswa kujibu maswali yetu kuhusu utajiri wake, la sivyo tutaendelea na hukumu za hisia zetu hasa kwa kuchukua mali za nchi, jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo ya nchi," alisema Shibuda.

Naye Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibrod Slaa, alisema hilo si jambo geni kwao kwani walishamtaja Chenge kama mmoja kati ya mafisadi 11 ambao wamekula mali za nchi, lakini serikali na wananchi waliyafumbia macho madai hayo.

Alisema kitendo cha Uingereza kuanza kuchunguza akaunti ya Chenge na jinsi alivyozipata fedha hizo, ni dalili ya kuelekea kuumbuka kwa kiongozi huyo ambaye aliwahi kushika cheo cha uanasheria mkuu wa Serikali.

Alisema tabia ya Watanzania kutowaamini wenzao wanaposema jambo, ndiyo iliyoifikisha nchi hapa ilipo, kwani kama Watanzania wangesikiliza maoni waliyoyatoa wapinzani, Chenge asingeweza kuchaguliwa katika nafasi hiyo.

"Sasa gazeti la Uingereza na taasisi ya nchi hiyo ndivyo vinafanya uchunguzi kuhusu kashfa ya Chenge na hapa ndipo Watanzania tunaamini kuwa kuna ufisadi. Hii ni aibu," alisema Dk. Slaa.

Naye Naibu Spika wa Bunge, Anne Makinda, alisema taarifa hizo za Chenge amezipata kupitia kwenye vyombo vya habari na hazijafikishwa katika Ofisi ya Bunge, hivyo hawezi kuzizungumzia hadi zitakapowasilishwa mezani kwake.

"Mimi kama Watanzania wengine nazisoma taarifa za Chenge kwenye vyombo vya habari, zikifika ofisini kwangu nitakuwa katika nafasi nzuri ya kuzizungumzia rasmi," alisema Makinda.

Taarifa ya gazeti la The Guardian la Jumamosi iliyopita, ilieleza kuhusu kugundulika kwa zaidi ya dola milioni moja katika akaunti moja iliyoko katika Kisiwa cha Jersey, ambayo ni ya Waziri Chenge.



Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 61 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Hivi jamani, kama kweli mtu ana mapenzi na nchi yake, kwa nini ai-invest hizo billioni Tanzania angalao zikasaidia kuinua maisha ya walalahoi? Kuziweka nje ya nchi, kunaleta walakini fulani na nia ya sisi kuhoji kama kweli fedha hizi zimepatikana kihalali. Hivi ni viongozi wangapi wana fedha lukuki nje ya nchi?, na kama vyombo vya nje kama SFO hawatuambii hili, ni nani kesho atatueleza kuwa kiongozi wetu mwingine ana dollar billioni mbili uswis au uarabuni? watanzania kaeni mkao wa kula!! mkiambiwa hamuoni mpaka taarifa zitoke nje!! wnyw chama mpoooo???,hili hamtalikwepa hata kama mtajishaua kuwa ni suala binafsi, kwani hamjui chama kushika hatamu?? mmeumbuka!CCM mmeumbuka, mtake msitake, doa la mtu wenu linazidi kukiporomosha chama, na endeleeni tuu na utetezi wenu, lakini za ***** ni arobaini, ya Zimbabwe yanawangoja!!!!!!!!!!!!!!

na Joshua Jona jonathan, Dar es salaam, Tanzania., - 15.04.08 @ 10:54 | #6514

Leo nakuwa tofauti,nasema Chenge naye aachwe kama wengine,naye ana damu ya mtu,hana damu ya kunguni.Hizo fedha ni akiba yake kama wengine.Je,aliyenunua mgodi wa taifa wa mawe ya mkaa huko Kiwira Mbeya amefanyda nini? Je,waziri Mramba aliyeshupalia kununuliwa rada hiyo yenye utata akaunti yake imeonwa ina sh. ngapi? Je,huyo mhindi aloleta hiyo rada si yupo duniani,hayupo mbinguni,je,amefanywa nini? Je,huyo Balali si amefichwa huko ughaibuni,amefanywa nini? Chenge naye aachwe ili 'ngoma' iwe droo,tusitake wahalifu wengine watanue huku washukiwa tu wasumbuliwe.Kama wanavyoachwa wengine,Chenge naye aachwe huru!

na Matiku, Dsm,Tz, - 15.04.08 @ 10:56 | #6516

JAMANI MPO WAPI WACHANGIAJI AU MNALIA KAMA MIMI?

Haya kazi kwenu watanzania muamue cha kumfanya Chenge. mkuu wa nyumba ndio hivyo kaamua kumbeba hata kama ana miiba.

miaka 2 to 2010 si mingi watanzania tubadilike kabisa. SURA KAMILI YA NAMBARI WANI NDIO HII.

SINA YA KUSEMA HATA NIKISEMA HAMTASIKILIZA BADO MTAICHAGUA CCM TU. BUT FOR MI NEVER.

MUNGU WABARIKI WAVUJA JASHO WA TANGANYIKA OR sorry TANZANIA.

na emmanuel, Sweden, - 15.04.08 @ 10:58 | #6518

The list goes on and on.
Mramba
Masha
Lowassa
Mkapa
Mgonja
Balali
Rostam
Yona....
Mabilioni yenu mmewekeza Tz au huko Cayman isles kama Chenge? Marmo juzi alisema hukuna kiongozi aliyewahi kufanya udanganyifu wa mali zake tangu kuanzishwa kwa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma. Hii Sheria kweli inafanya kazi??? au ni danganya toto kutupumbaza kwamba wote ni safi.

na chombeza, bongo, - 15.04.08 @ 08:11 | #6522

Inasikitisha kuona watanzania tunaendelea kuwa na viongozi wanakumbatia MAFISADI,lakini tumefika hapa kwa kuwa MAFISADI hwa ushindi wa Kishindo! Namshauri Rais afanye KAZI YAKE si kuendekeza uswahiba na umtandao ! mi nafika mahali simtofautishi rais na ufisadi , mfano chenge yuko na rais ziarani ni aibu gani anabeba Rais!?KWA UBABAISHAJI HUU , TUTAMKUMBUKA NYERERE DAIMA!

na MA GG, Tanzania, - 15.04.08 @ 08:13 | #6524

Jamani CCM tunawachagua wenyewe baada ya kupewa fulana na kofia za kijani. Nao wakiingia madarakani wanatafuta jinsi ya kurudisha gharama zao za uchaguzi.

Chenge alikuwa hatakiwi Bariadi lakini aligawa takrima mpaka akashinda sasa anarudisha gharama zake za uchaguzi! Tuache kulalama.

na Kamoga, Mwanza, - 15.04.08 @ 08:14 | #6526


Emmanuel

afadhali hata kama tunguekuwa na uwezo wa kulia angalau tungepunguza majonzi na uchungu. yaani wengine machozi hayatoki lakini mioyo yetu inaripuka kwa uchungu.


watanzania tuamkeni jamani, hivi kweli mwaka 2010 tutakubali kuwaachia hawa MAFISADI waibe kura zetu na warudi tena IKULU.....???

saa nyengine najiuliza ni nini sisi watanzania tumemkosea mungu? kwanini hatupati viongozi waadilifu ??

na Mnyonge - 15.04.08 @ 08:16 | #6527

Matiku umesema sawa,lakini mawazo yako ni ya mtu aliyeishiwa na aliyekata tamaa,kwa hiyo kila mtanzania aibe nchi itajengwaje.

Ni akili gani hata kama unaiba kwenda kupeleka pesa nje ya nchi?? unawanufaisha wazungu huku watanzania wenzako wanakufa? wazungu wanazifanyia biashara hela hizo na zinazalisha matiku wewe!!
angeweka crdb, nbc n.k watanzania wangapi wangefaidi indirectly?

pia matiku ni kutokujua kwako na kwa rafiki yako Chenge viongozi wengi wa kiafrika wanaoweka pesa nje wengi huwa wanatapeliwa, maana mabenki yanajua pesa hizo ni za wizi! na wakimrusha hana pa kukimbilia wengi wanakufa kwa presha,imetokea kwa wengi matiku ndugu yangu .

Mjinga yeyote, mbinafsi yeyote atafanya kama alivyofanya chenge, huyo mkapa afadhali basi-- maana wananyakyusa wanapata ajira! kwa kusema hivi sitetei ufisadi wa mkapa.

Matiku mke wako akizini na wewe kwa hasira utazini nje ya ndoa, mtu akiua na aipokamatwa basi na mwingine aue kwa sababu yule wa kwanza hajakamatwa??

Matiku nategemea watanzania wengi wakisoma comment yako hutashinda kwa RAHA NAFSI YAKO ITAKUSUTA HAPO ULIPO HATA KAMA JINA HILI NI LA UONGO.

NA INAWEZEKANA KABISA WEWE NI CHENGE!!!!!

na Imani, USA, - 15.04.08 @ 08:17 | #6528

Li-nchi lina utajiri wa raslimali zote huku watu wake ni masikini wa kutupwa,vyakula bei juu,petroli bei juu,nk,kumbe viomgozi ndo waporaji wakubwa.Endeleeni kuimba amani,amani huku mnaporwa na wajanja,si muwaondolee mbali?

na Johnson, Dar es salaam., - 15.04.08 @ 08:20 | #6529

Matiku atakuwa alizaliwa chooni, au mimba ya mama yake alibakwa na wanaume wanne ka hiyo hamjui baba yake, au inawezekana matiku ni uzao wa nyumba ndogo maana huwa wana akili kama hizo , au inawezekana kabisa na ninahisia kuwa huyu Matiku atakuwa aliumwa kifaduro utotoni na mtindio wa ubongo kwa hiyo bado hajakaa sawa.

na Hussein, AR, - 15.04.08 @ 08:21 | #6570

bwana matiku hiyo ni kweli tupu, kama wameshindwa kutaja hata majina ya makampuniyaliyorejesha fedha za EPA kuna haja ghani ya kuendelea kuumiza kichwa na huku ukijua hamna hatua yoyote itachukuliwa dhidi yao, wale wa RICHMOND wamefanywa nini?!!!!!!!!! jamani kilio chetu ni kama cha samaki machozi huishia majini usijue hata kama samaki kalia, wacha waendelee kutunyonya sisi wanyonge, hasa wezi wa kuku ndo wamejaa keko na Ruanda. ukisema kiwira wanakuambia apumzike, hata huyu naye mwacheni apumuzike.
Rais alimjua fika huyu mtu, mkiwa mnamsema chenge mtakuwa mnamwonea.hata yeye alisema mwulize aliyemteua.

na yohana, mbeya, - 15.04.08 @ 08:21 | #6572

Kile chama kinachojiita ni nambari WANI, kumbe ni nambari katika RUSHWA, UFISADI na kumaliza nchi. Kwa staili hii hatutafika hata siku moja. Nilikuwa na matumaini sana na Serikali ya awamu ya nne,sasa yamekwisha kabisa. CCM ni aibu tupu. Serikali ina udhaifu sana sana.


na Philip Kimicho, Moshi, - 15.04.08 @ 08:23 | #6573

Imani matiku yuko sahihi na wewe pi huko sahihi, ila kwa kifupi nyote mmezungumzia kuwa nchi yetu imeoza na hatuna wa kuongoza ni kama mmesema hatuna Rais vile.

na msuluhishi, china, - 15.04.08 @ 08:23 | #6574

inuma sana. lakini mimi nawalaumu wananchi kwa kutoa kura za kishindo sasa ndio matiokeo yake hayo wamebweteka

na jk, dom, - 15.04.08 @ 08:30 | #6575

Hakuna kiongozi msafi nchii, wanaposema uchumi unakuwa kwa kasi maana yake ni kwamaba wakubwa hao wamefanikiwa kuingiza Mabilioni ya kamisheni kwenye account zao. Ndiyo maana Mkapa alikuwa akilipiga kelele uchumi unakuwa kwa kasi, lakini hakuna mtu wa kawaida anayeona mabadiliko katika maisha, bali ni wakubwa hao kukwapua pesa za wananchi, kupitia mikataba feki. Ipo siku tutawachoma moto.

na Mzalendo, DSM Bongoland, - 15.04.08 @ 08:35 | #6576

Bw mkubwa Hussein hapo juu umepoka,mimi Matiku akili yangu ni timamu kuliko yako,si mtoto haramu udhaniavyo bro,nashukuru ulivyonikashifu,ila tu mimi nawe acha tusubiri tuone mafisadi watafanywa nini? Haitoshi kumsakama Chenge peke yake,tiba ni kmshinikiza Mh Kikwete awaathibu mafisadi na warudishe fedha za umma walizopora.

na Matiku, Dar,Tz, - 15.04.08 @ 08:42 | #6578

NI UKWELI USIOPINGIKA KUWA SERIKALI YA KIKWETE IMEOZA. NI KITU GANI KILICHOMSUKUMA KIKWETE KUMTEUA TENA CHENGE HICHO NI KITENDAWILI LAKINI WASWAHILI HUSEMA KUWA ,WASWAHILI HUJUANA KWA KILEMBA HIVYO BASI KILEMBA =CHA KIKWETE NA CHA CHENGE VINAFANANA LA SIVYO ANGESIKIA KILIO CHA UMMA KWANI KILIO CHA UMMA NI KILIO CHA MUNGU ,NA KAMA HUSIKII KILIO CHA UMMA BASI WEWE NIMMOJA WA HAO MAFISADI.
HIVI HUYO MRAMBA NANI ASIYEJUA KUWA YEYE NI FISADI CHA MUHIMU WATU HAO WATENGWE NA JAMII NA UCHUNGUZI DHIDI YAO UANZE MARA MOJA ,MFANO MRAMBA ANAHOTELI YA KITALII ARUSHA LAKINI ANAMTUMIA MFANYBIASHARA LASWAI WA MOSHI ILI AONEKANE KUWA NDIYE ANAYEMILIKI HIYO HOTELI.
HIYO HAITOSHI MAGOROFA YALIYOJENGWA KARIAKOO NA VIJANA WA ROMBO HIZO ZOTE NI FEDHA ZETU AMBAZO MRAMBA AMEWAPA ILI WAFANYE BIASHARA PAMOJA NA ZOTE NI ZA WATANZANIA ,
CHA MUHIMU NI KUUNDWA TUME YA KUCHUNGUZA OROZA YA HAO MAFISADI.
KINYUME CHA HAYO KIKWETE NAYE NI MOJA YA HAO MAFISADI


na masudi ally, j,burg.sa, - 15.04.08 @ 08:46 | #6579

Ikiwa kweli Chenge ana fedha kiasi hicho jele mabosi wake wa zamani watakua na kiasi gani?
Kama Kikwete hajui kwa nini Tanzania inaendelea kua masikini, basi jibu amelipata.

na Rashid, Tanzania, - 15.04.08 @ 08:54 | #6582

MATIKU TUKO PAMOJA. TATIZO WATU HAWAELEWI NI NINI UNACHOSEMA. WATU TUMETOFAUTIANA UELEWA. WENGINE AKILI NA UELEWA WAO NI KAMA WA HUSSEIN.

NI NANI ATAJISHITAKI NA KUJIFUNGA MWENYEWE? (FOOD FOR THOUGHT)

na kukuz , singapore, - 15.04.08 @ 08:54 | #6583

Iko kazi,kila kukicha mafisadi yanaongezeka kutoka chama tawala. Wananchi tunahaha, mambo magumu kila kitu haikiwezeknai pesa haizpatikani kumbe zote zimefichwa / kuliwa na wakubwa ambao wantuongza nchini,aibu kwa serikali wananchi hatuna tena imani na uongzi wote watanzania pamoja na chama ambacho tulikiamini. Inaelekea uongozi wote wako hivyo hivyo ndio maana wanalindana. Tumechoshwa na mafisaidi sijuwi kilio chetu tupeleke kwa nani. Ewe Mwnyezi Mungu tusaidie

na Mtunga, Tanzania, - 15.04.08 @ 08:56 | #6584

Tanzania haina Rais kuna alama tu iliyochorwa labda hadi 2010 kama waTz wataamua kuchagua rais. Wanajuana wote ndo maana kiburi cha kutosha wanacho! Lowasa yupo katulia anakula kiulaini kwa vile anajua mambo ya JK yote na hii ni ethnic network yao inayokula nchi vizazi na vizazi hadi tutakapoamka toka usingizini!

na Kisia, , Igunga/ Tanzania, - 15.04.08 @ 09:01 | #6586

watanzania mapambano ya kudai haki ni kazi ngumu na inahitaji watu wenye ujasiri mkubwa na si kukata tamma, mimi na ni ya naamni kazi hii bado ni changa ni ya kudumu, na tusikate tamaa. hoja siyo chenge ni mfumo na inabidi mfumo ndio ouangaliwe upya na tuone njia bora za haraka na za uhakika kwenye kulishughulikia hili. kwani kwa maoni yangu bado chenge ni mtu mdogo sana na yeye ni sehemu tu washiriki wenye kufanya haya. tuanze kujifunga mikanda na tuelewe ni kazi ngumu na isiyo na mwisho maana washiriki ni miongoni mwetu maana hata kama sio ccm hata angekuwa kiongozi gani bado sheria zillizopo zinatoa mwanya wa kufanya haya. inawezekana chenge amefanya kazi ya halali na hasa kwa kuzingatia nae ni mwanasheria na angeweza kama wengine kujipatia pato hilo kwani yeye na mkono ni sawa tu maana nani asiyejua kwamba chenge anaweza kuwa mtumishi wa mkono, jee nani anajua mkono ana miliki nini na yeye pia ni kiongozi, au nani anajua kikwete mwenyewe ana miliki nini au lowasa na rostam wanamiiliki\nini. hivi tujiulize makamba anamilki nini na wengine wote, sasa hapa kosa sio wao bali ni mfumo ndio unaoruhusu wafanye wanayoyafanya, tujitahidi tutengeneze mfumo na tuusimamie ili\kila anaetaka kufanya kazi humo utaratibu uwe unajieleza na ndipo tufanye kazi ya kuangalia nani ni muaminifu na nani ni muhalifu, maana tukianza kuangalia acount za chenge basi tuangalie acount za wote kuanzia kikwete mwenyewe lakini hata wale waliotangulia maana nao wanamiliki utajiri mkubwa na hakuna mwenye kuweza kueleza alipataje.
tuwe wakweli tu, tusimuonee chenge kwa mazingira lakini tufanye iwe kwa wote hadi mkapa na jk wote tujue wao wana miliki nini pamoja na familia zao na marafiki za o maana kwa sasa hata rafiki anaweza kutumika kuhifadhi utajiri usio na maelezo.

na ikram, tz, - 15.04.08 @ 09:02 | #6587

kauza ng'ombe au............. si angejenga hata hotel jimboni kwake. haoni wabunge wa kaskazini wanavyofanya mambo. wameiba wakajenga kwao na wananchi wanapata ajira. tuchunguze labda ana uraia wa huko

na john, zimbabwe, - 15.04.08 @ 09:03 | #6588

Viongozi wa Tanzania hawana nia ya kweli ya kuwatumikia wananchi, watanzania tuamke tutafute njia ya kuwaondoa viongozi kama chenge, kumtegemea rais awaondoe itachukua muda kupata rais mwenye uwezo huo. rais anwekwa madarakani kwa kura za wananchi lakini badala ya kuwasikiliza anawqaogopa baadhi ya marafiki zake aliowachagua mwenyewe, huu ni usaliti kwa wananchi.watanzania wanasaidiwa na mungu tu na si viongozi wao na ndiyo maana mijambazi kama chenge inaumbuliwa na watu wa nje. mtakumbuka chenge alijitahidi sana kuzuia ripoti ya richmond isisomwe bungeni ili isije ikafungua njia ya kuumbuka kwa mtandao wa mafisadi.
Tanzania inashangaza na kuhuzunisha, tunaona fahari kuitwa maskini wakati wanaotufanya tuwe masikini tunawajua. Tunakuwaje na waziri mkuu mishen town kama Lowasa! na baadhi ya waandishi wa habari nao kwa kuendekeza njaa zao wanaendelea kumtetea , wanini watu kama hao wasisusiwe kama walivyomfanyia yule zezeta mapuri na ikasaidia kumtupa nje ya ulingo wa siasa za bongo?
Mafisadi na wote wanaowashabikia Mungu atawapa kipigo mmoja mmoja, subirini.

na chedi, tz, - 15.04.08 @ 09:07 | #6590



Ni aibu kwa watanzania mbele ya mataifa mengine juu ya umasikini wakati rasilimali zinafujwa na hakuna wa kuchukua hatua.tumechoka na ubabaishaji mbeleni kitaeleweka.

na MLYAFIMEMILE, Tanzania, - 15.04.08 @ 09:10 | #6591

Watanzania hatuna haja ya kusikitika, uwezo wa kufanya mabadiliko tulikuwa nao, nia tulikuwa nayo na sabababu pia.
Tatizo ni hizo tshirt na khanga na mifuko ya chumvi.
Wahenga walisema"Majuto mjukuu"; kama hiyo haitoshi, Yesu aliwaambia wale wanawake waliokuwa wakimlilia, wasimlilie Yeye bali wajililie wao na watoto wao.
Serikali hii iliyopo madarakani ni ya kishikaji, imejaa wasanii watupu. Mtu kama Mginja na Mramba bado wanatamba kwa jema lipi walilolitenda?
Kikwete hana ubavu wa kumkamata mtu, kwani mafisadi hao hao ndo wamemuweka madarakani.
Lililobaki ni kwa watanzania wote kutubu na kumlilia Mungu, kwa kumsingizia kuwa Kiongozi aliyeko madarakani ni chaguo lake.

na Man, Dar, - 15.04.08 @ 09:12 | #6592

Sasa tumekwisha,nyakati za kufa kwa Tanzania kumekaribia ni kusambaratika kwa hali ya juu.Mwanasheria Mkuu na Waziri wu Miundombinu aliyeaminika na serikali yenye watu makini wa usalama wa Taifa.Wanafika mahali kila moja anajibu kama mtoto wa chekechea eti hayo ni mambo binafsi.Tumekwisha...Kila moja sasa anashika lake.Nchi kama Tanzania, hali mbaya sana watanzania wanakufa kwa magonjwa yanayotibika,wanashida kubwa ya miundombinu, elimu shida kubwa watoto wa TZ wanasoma wakikaa ardhini,hospitalini hakuna dawa, lakini raisi anambeba ***** muuaji huyo na kumpatia nafasi ya wizi zaidi.Tumekwisha, lakini mkono wa Mungu mliuchokoza Butiama utawaandama moja baada ya mwingine. Lakini pia Kikwete aseme ana chuki gani binafsi na Magufuli, Kiasi cha kusambaratisha wizara hiyo?Sadaka ya tofauti zenu ni mauti kwa Watanzania, uwe wazi na mkweli.Au ndiyo tabia ya serikali ya TZ, ya kuwa hata kama ulikuwa serikalini muda wote unapokuwa Raisi unaanza kudai kuwa hujui ya awamu iliyopita, nayo haiingii masikioni mwa watu wazima.Haya sasa Kikwete tuambie mahusiano yako binafsi na Chenge, tutarudia tena niambie rafiki yako nami nitakuambia wewe ni mtu wa namna gani.Tusichague wapambe binafsi katika ofisi za nchi.Haya kazi kwako Kikwete kunyoa au kusuka.

na Ngadaya, Rome-Italy, - 15.04.08 @ 09:14 | #6594

Sasa umefika wakati wa kudai katiba mpya kwa nguvu zote ili kusiwepo na utata wa kuwakamata akina Mkapa na wengine wote wanaofilisi nchi yetu kwa udhaifu wa katiba iliyopo.Katiba iliyopo inamlinda mkapa asikamatwe na kufikishwa mbele ya sheria.Watanzania tuamke TUONDOKANE na mafisadi kwa njia ya kura ifikapo 2010.

na RUME, DSM, - 15.04.08 @ 09:15 | #6595

Ehe sheria ya mswahili mpaka isukumwe na mkoloni wake? Ssa inamaana mwingereza anauchungu kuliko bwanamkubwa aliemwachia nchi? Tusubiri akina nanihi nao Chenga ndo mlango wa mafisadi wengine kufichuliwa peupe. Swala ni staili ya kufichuka zaidi. Mengine yatakapoibuka toka ughaibuni na wafadhili watakapogoma ndipo kitaeleweka kitu. Ninyi wanasheria mtajua lukuki wazalendo kwani mnasubiri nini kuwashtaki mafisadi? Mlisomeshwa kwa ajili ya Taifa, sasa nanyi mnanyamaza ili mzipate za mafisadi? Hii ni miaka ya kuaibishwa, hela za ufisadi zinarudi kwa wenyewe sasa.

na ngwanabhugali, USA, - 15.04.08 @ 09:16 | #6597

MIMI NATOFAUTIANA NANYI WOTE.TUSHIKE PANGA NA BUNDUKI TUWANG'OE.KWA KURA HAWATOKI MAPINDUZI TU NDO NJIA.NI RAHISI SANA.HOJA ZIMETOLEWA HAWATAKI KUSIKILIZA.....KILICHOBAKI NI KUMWAMBIA GEN.MSUGURI ATUSAIDIE TUWANG'OE KWA NGUVU.

na mwanamapinduzi, buturi trm, - 15.04.08 @ 09:24 | #6600

Daa kweli watanzania watazamiwa!!! yaani kwanini mna zungukazunguka simseme tu kwamba Rais JK anawe tu na kukaa pembeni labda hali ya hewa inaweza kutulia.

Mpaka hivi sasa sijui ni kwanini Mkuu wa Kaya anashindwa kutuonyesha watazamiwa kwamba hatukukosea kumpa KAYA.

Cheki na hizi kadhaa utajua nachomaanisha
1. WALARUSHWA NAWAFAHAMU NAWAPA MUDA WA KUJIREKEBISHA

2. List ya WAUZA MADAWA YA KULEVYA TUKAMPA (MTUHUMIWA MMOJA KAPEWA UBUNGE SIJUI KONTENA ZAKE ZILIISHIA WAPI)

3.HATUTASAINI MKATABA MWINGINE MPAKA HII ILIYOPO TUIPITIE "DEC 2005".

4.TUTAUSHUHULIKIA MPASUKO WA KISIASA ZANZIBAR MWAKA WA PILI SASA NI MADUDU TU.

5.BALALI KAIBA YUKO NJE YA NCHI, WAMAREKANI KUPITIA BALOZI WAO "MKIMUHITAJI TUTAMRUDISHA", MPAKA SASA GIIIIIII!!!!!

6.MIONGONI MWA WATUHUMIWA WA RIPORT YA KAMPUNI YA UFUZI WA UMEME Richmond Tanzania Limited LLC, NDIO WAJUMBE KWENYE KAMATI TEULE YA RAIS KUCHUNGUZA MAFISADI WA EPA,

7. CHENGE ANARUDISHWA KWENYE BARAZA LA MAWAZIRI WAKATI ANATUHUMA KIBAO ZA MIKATABA.

rubishiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii


Kuna mtu mmoja ambaye akiondoka wote hawa wataondoka

na Thengondo, Tanzania, - 15.04.08 @ 09:28 | #6601

mambo ya kutukanana ktk mtandao hayatakiwi kama uanataka kumtukana mtu mtukane kwa hoja na yeye atajua kuwa katukana. Baadhi ya watu hawajamjua Matiku kaeleza nini na kwa upeo wao mdogo wakaanza kutukana.Matiku naye kakeleka sana na huenda kakata tamaa hasa hasa akiangalia kila siku kuna mabomu makubwa na mbaya zaidi yale yaliyopita hayajapewa utatuzi, swala la Richmond,Hosea,EPA,Mkapa,Sumaye,kigoda,mramba,balaa
mke wa Mkiapa na hata Kikwete mwenyewe.Kwa hiyo tuache kabisa kutoa ****** hapa.

na jandu, msumbiji, - 15.04.08 @ 09:45 | #6604


JAMANI MADHAMBI HAYA YATATENDEKA MPAKA LINI?????????

KWA NINI WATU HAWANA HURUMA????

MBONA MNAJIPENDA HIVYO?????

KULE AMANA WAKINA MAMA WANALALA MZUNGU WA 4, WAKATI KUNA WATU WAMEHIFADHI MABILIO NJE YA NCHI.

HII NI LAANA JAMANI...

NASEMA ACHENIIIIIIIIIIII

OTHERWISE MTAPUKUTIKA KAMA SENENE

EE MUNGU UTUSAMEHE NA KUTUREHEMU


na mhubiri, tz, - 15.04.08 @ 09:57 | #6607

HAWA MAFISADI, WAJUE MOJA
NI KWAMBA KILIO HIKI CHA WATANZANIA HAKITAWAACHA.

SIKU MOJA MUNGU ATASIKIA TU KAMA ILIVYOKUWA KWA WAISRAELI KULE MISRI.
ALIPOSIKIA ALIMTUMA MUSA KUWA TOA KWA FARAO WAENDE KUMTUMIKIA KTK NCHI YA AHADI. IKO SIKU NA SISI WATANZANIA MUNGU ATATUCHAGULIA MUSA KATIKATI YETU ILI ATUONDOLEE UFISADI HUU.

YATOSHA KUTESWA NA WACHACHE JAMANI.

na mhubiri, tz, - 15.04.08 @ 10:04 | #6608

Chenge umetuacha wanachama wa CCM uchi wa mnyama mbele ya umma wa watanzania

na R.Makangala, Masaki, DSM, - 15.04.08 @ 10:09 | #6610

Nimeishiwa maneno ya kusema,Tanzania inahitaji mabadiliko makubwa ya kisiasa kama tusipofanya mabadiliko ya dhati mwaka 2010 tusije kumlaumu mtu kwasababu kila mara tunakosea kuchagua sasa tumeona wenyewe.Chenge kahusika kuandaa mikataba yote mibovu(madini,ununuzi wa ndege ya rais na nk)nchi inaangamia yeye anajineemesha pamoja na familia yake.Nakumbuka majibu yake ya jeuri wakati bunge lilipofanya makosa makubwa ya kumsimamisha mhe Zito kuhudhuria vikao vya bunge mwaka jana.Mhe Matiku nakuomba sana ujaribu kuleta mchango wa maana na sio wa kukatisha tamaa na wachangiaji wengine tuepuke kutumia lugha za kashfa tunapotofautiana na mawazo na wengine.
Mungu ibariki Tanzania

na JIMMY V GERALD, ARUSHA,TANZANIA, - 15.04.08 @ 10:11 | #6612

Leo naanza kwa kupiga mayowe kwamba WATANZANIA MAFISADI MMETUCHOSHA!! Kha!? Tafuteni nchi yenu mkajisikie au Serikali iwatengee kisiwa chenu mkayafanye hayo mabaya huko nasi walala hoi tujisikie kwa upande wetu. EEH, ni nchi gani hapa duniani kila kukicha mafisadi huongezeka? Hii inaonyesha udhaifu mkubwa katika utawala. OLE WENU MAFISADI IPO SIKU NITAKAA PALE ALIPO JK. Itakuwa ni suka, amri moja tu kwamba kwa kila mtumishi mwenye biashara awapishe wengine na account yenye zaidi ya shs 1,000,000= mwenye nayo afilisiwe mali zake zote.

na RichmondEPA, Tanzaniabara, - 15.04.08 @ 10:15 | #6613

Ndugu zangu watanzania sote haya mambo yanatuuma ,ila naomba tunapojadiliana hapa tujenge utamaduni wa kuvumiliana kimawazo,si vizuri kutoleana maneno kama haayo ya ndugu yangu Hussein,haifai hata kidogo si utamaduni wetu watanzania binafsi yangu Bwana Matiku nimemuelewa alikuwa na maana gani kutokana na hoja yake hapo juu,alichosisitiza kuwa MAFISADIwako wengi na kuna listi ndefu tu ya MAFISADI sasa kama kweli serikali inania ya kuwatia ADABU mafisadi hao waanze na wale wa nyuma halafu wafute watu kama akina CHENGE,kama hawataki kuanza na wale wengine basi na CHENGE nae aachwe,nafikiri kwa ufahamu wangu hicho ndicho alichokuwa anakisema KAKA MATIKU haopo juu,alichokuwa anataka kusema kumsakama CHENGE peke yake ni kumuonea hawa wengine vipi??kuina MH MKAPA (HUYU FISADI NAMBA MOJA)KUNA BASILI MRAMBA,ROSTAM AZIZ(MUIRANI ***** MKUBWA HUYU) DANIEL YONA,KARAMAGI,LOWASA,BALALI (MPAKA SASA SERIKALI HAIJUI YUKO HOSPITAL GANI MAREKANI "HUSSEIN UNASIKIA SERIKALI YAKO HIYO)orodha ni ndefu sanaaaa sasa hussein naamini wewe ni muugwana kwa kutumia hapahapa muombe radhi mtanzania mwenzio Bwana Matiku
nini mimi mdau mwana wa matonya
UK

na mwana wa matonya, leeds uk , - 15.04.08 @ 10:19 | #6616

Jamani mbona simsikii Kikwete akisema kasi mya, Ari mpya na nguvu mpya? au ameshindwa? du Rais hatuna. masikini Tanzania, Mungu tuokoe. Kikwete uko wapi? au nawewe sawa na Mkapa? ****!

na Mr. Clean, Dar, - 15.04.08 @ 10:24 | #6618

Hivi JK unadhani unapompa uwaziri mwenye fedha zote hizo pamoja na tuhuma anaweza kweli kuwatumikia wananci na kufanya kazi kwa bidii na juhudi zote kuletea nchi maendeleo? Itakuwa bora uamue kumtema kusafisha serikali yako, au kubaki naye na serikali yako yote iwe imepakwa matope mbele ya umma wa watanzania na jumuia za kimataifa

na J.J., Oysterbay, DSM, - 15.04.08 @ 10:27 | #6621

Kama walivyo sema wachangiaji wengine sioni kigezo cha kumhusisha raisi kumtaka amwajibishe Chenge! Wasio mwelewa Matiku ni kwamba,tumeona jinsi CCM na uongozi wake unavyo tetea kwa nguvu zote ufisadi na uhuni wote! Wapo viongozi wa juu kama Mkapa na JK walio kosa uadilifu wao binafsi watawezaje kuchukua hatua kwa walio chini yao? Nikiini macho namwambia hata Lipumba kumtaka kiongozi wa mafisadi kama JK achukue hatua kwa walio chini yake ni kujidanganya na kupoteza malengo! Hapa nasema,we need a mass rebelion against this corrupt goverment and its system! Haiti wamefanya nini? Watz tuache unafiki na woga tutoke nje na tueleze hisia zetu na nguvu ya uma itajibu! Aluta kontinua!

na Mtz pure, Hillbrow. Joberg. RSA, - 15.04.08 @ 10:28 | #6622

Mimi naamini kuwa bepari Chenge ametumwa na shetani ili kuendelea kuwakandamiza Watanzania ili wazidi kuwa masikini.Na sio yeye pekee,wapo wengi ambao wanafahamika na wananchi.Kuwa tajiri si dhambi,lakini kwa mfanyakazi wa serikali inatia shaka.Inasikitisha kuona hata baada ya uhuru,kumuondoa bwanyenye wa kikoloni tukadhani kuwa tunaingia kwenye neema,kumbe unfortunately waafrika wenzetu wanatufanyia mambo yaleyale,tena wengine zaidi.Huyu jamaa ameamua kwenda kuficha fedha huko Jersey kisiwani,but kwa msaada wa Mwenyezi Mungu tumefunuliwa.Naamini kuwa wengi watafuata,tutawajua.Amina

Angekuwa Nyerere angefukuza hawa watu haraka,lakini huyu bwana mkubwa wa sasa...Nina wasiwasi.Kwa sababu tatizo ni kama alivyosema Mwalimu,inategemea umeingiaje Ikulu...

na David, Dar, - 15.04.08 @ 10:29 | #6623

Inakuwa vigumu sana kuamini kuwa kila kitu kitaendelea kubakia kama kilivyo. WaTz tumekuwa wepesi wa kupelekwa na upepo. Tumekuwa waoga sana wa kuthubutu. Hali hii inatisha, nadhani ni wakati wa kuangalia mfumo wa utawala ndani ya nchi yetu, la sivyo kama alivyosema MATIKU, sio chenge TU wa kusakamwa!!!. Ni aibu isiyo na kifani waTz wanavyopanga foleni kwa mataifa yaliyoendelea kuomba kuchangiwa kwa budget yao, wakati watu wawili walioliibia taifa wana uwezo wa unaotosha kufidia mapungufu ya budget. NADHANI NI CHINI YA 30% YA MAPATO YA NCHI YANATUMIKA KWA SHUGHULI ZILIZOKUSUDIWA.
NINI KIFANYIKE WAKATI WATANZANIA WALIOWENGI WAMEPUMBAZWA AU KUHONGWA KWA
GHARAMA NDOGO SIYOTIMIA sh 2000. CHAGUZI ZIKIFANYIKA MAWAKALA WANAUZA KURA! VIONGOZI WA UPINZANI WALIOCHAGULIWA NA WANANCHI WANANUNULIWA. WANANCHI WAKIELIMISHWA KUHUSU UBADHIRIFU UNAOFANYWA NA CCM WANAISHIA KUSEMA HATA NYIE MNGEFANYA HIVYO HIVYO.
USALAMA WA TAIFA NI USALAMA WA CCM.

NADHANI KUNA HAJA YA KUTOSHA YA KUANGALI MFUMO MZIMA NA KATIBA YA NCHI.

WABUNGE WENGI WANASHINDWA KUHOJI SERIKALI KWA KUWA KESHO HAWATAPITISHWA NA CHAMA CHAO, hivyo ni kusimamia uozo tu!

MAWAZIRI WANATOKANA NA WABUNGE HIVYO BUNGE NALO LINAKUWA SEHEMU YA SERIKALI, sasa unategemea nini?

NADHANI KATIBA IBADILISHWE NA MAWAZIRI WOTE WASIWE WABUNGE, ili ukigombea ubunge ujue daima uwazairi hupati na hakuna kujipendekeza ukitegemea utatupiwa mfupa. Hili lingefanyika tungekuwa na mawaziri na wabunge wawajibikaji zaidi.

Nihitimishe kwa kusema, tisikate tamaa ila tujue kuwa mambo mabaya yapo mengi, nafikiri tunayoyafahamu ni chini ya 5% ya uozo na uharamia uliofanyiwa watanzania.

Kama tunataka mabadiliko, daima ni wajibu wetu waTz popote pale tulipo duniani. Hakuna kaburu wala mzungu atakaye tujengea nchi, na daima viongozi katika mfumo mbovu watabaki kuneemesha matumbo yao na familia zao.

TUSIKUBALI PROPAGANDA ZA SERIKALI KUMBUKA NI JUZI TU WAZIRI MARMO ALIWAMBIA WATANZANIA KUWA HAKUNA KUONGOZI ALIYEWAHI KUDANGANYA JUU YA UTAJIRI WAKE, NADHANI PIA CHENGE ATAKUWA ALILIELEZA HILI. JE, TUNA UWEZA NA NAFASIFI YA KUHOJI??????.

na Paul, DK, - 15.04.08 @ 10:31 | #6624

Ni yale yale ya watanzania kushituka wanaposikia habara kama hizi na kusahau baada ya mda kesho yake na kuendelea kulalamika kuwa maisha ni magumu sana, uwezo wa kubadili mwelekeo wa taifa hili uko kwa watanzania wenyewe na si kwa nchi wahisani wala Bush.

Watanzania kumbukeni nchi yenu ya ahadi iliwapa Mungu ni Tanzania na hakuna Tanzania nyingine ila hii. Kwahiyo muache kuishi kama mnasubiri kwenda mahali pengine, vizazi vijavyo vitafukua makaburi yetu kuchunguza kama tulikuwa na akili au la kwa mabo tunayoyafanya.

Wapo watu wengi kama Chenge na mtaona mengi zaidi ya haya yanakuja, just stay tuned kama akina Fina Mango na Masudi wa Power Breakfast wanavyosemaga!

Mathias Paul Lyamunda
Compassion International Tanzania
Arusha.

na Mathias Lyamunda, Arusha, - 15.04.08 @ 10:33 | #6627

WATOA MAONI WENZANGU SIHALALISHI UFISADI LAKINI NINALOTAKA KUSEMA NI "UJINGA WA MAFISADI" WAKIFIKIRI NI WEREVU.
TANZANIA NA AFRIKA KWA UJUMLA KUNA UFISADI WA KIJINGA.
NAUITA UFISADI WA KIJINGA KWANI UNANUFAISHA NCHI ZA NJE KULIKO NDANI TANZANIA. HAO MAFISADI WOTE WALAU WANGELIANZISHA MAKAMPUNI MBALIMBALI MFANO. MABASI, KUJENGA NYUMBA BORA ZA KUUZIA WANANCHI, KUENEZA KILIMO CHA MATREKTA NCHINI N.K
MALI ZAO ZINGETAIFISHWA ZINGENUFAISHA TAIFA KWANI ZIKO NDANI YA NCHI.

na Msomi TzDaima - 15.04.08 @ 10:54 | #6631

Mambo ya ufisadi kweli sisi watanazania tumechoshwa nayo.Naomba wahusika wa ngazi za juu ambao wanajua maendeleo ya nchi haswa Raisi kikwete kusikiliza sauti za watu kwani kwani ndio sauti ya mungu .Hii itapelekea kuweka nchi kwenye hali ya amani na wepesi wa maendeleo.
Kama nchi ikikutwa na janga au balaa lolote huwa watu wanamkumbuka MUNGU basi Wtanzania na viongozi turudishe imani juu ya nchi yetu na watanzani kwa kutenda haki .Kama kiongozi mwenye mamlaka haya mambo si ya kukaa kimya ni kuyafanyi kazi ili kuponya roho za watanzania.
Twafahamu juhudi zako J.K hata katika jambo hili fanya kweli.
Sikiliza kilo cha walala hoi kwani machozi yao yataenda mbele za mungu na damu yao ikimwagika itadaiwa juu yako.
Pia kila kiongozi kwenye ngazi yeyote ile mwogope sana Mungu.
Zaidi ya yote namalizi kwa kusema lisemwalo lazima lifanyiwe kazi.
MUNGU IPONYE TANZANIA

na Nsanganiye, Kisarawe, - 15.04.08 @ 11:02 | #6635

Mambo ya ufisadi kweli sisi watanazania tumechoshwa nayo.Naomba wahusika wa ngazi za juu ambao wanajua maendeleo ya nchi haswa Raisi kikwete kusikiliza sauti za watu kwani kwani ndio sauti ya mungu .Hii itapelekea kuweka nchi kwenye hali ya amani na wepesi wa maendeleo.
Kama nchi ikikutwa na janga au balaa lolote huwa watu wanamkumbuka MUNGU basi Wtanzania na viongozi turudishe imani juu ya nchi yetu na watanzani kwa kutenda haki .Kama kiongozi mwenye mamlaka haya mambo si ya kukaa kimya ni kuyafanyi kazi ili kuponya roho za watanzania.
Twafahamu juhudi zako J.K hata katika jambo hili fanya kweli.
Sikiliza kilo cha walala hoi kwani machozi yao yataenda mbele za mungu na damu yao ikimwagika itadaiwa juu yako.
Pia kila kiongozi kwenye ngazi yeyote ile mwogope sana Mungu.
Zaidi ya yote namalizi kwa kusema lisemwalo lazima lifanyiwe kazi.
MUNGU IPONYE TANZANIA

na Nsanganiye, Kisarawe, Tz, - 15.04.08 @ 11:03 | #6636

Kila kukicha ufisadi na wahusika si wageni masikioni mwetu ni walewale.EPA,RADAR,MIKATABA MIBOVU YA MADINI,NDEGE MBOVU YA RAIS,RICHMOND na sasa GENERAL TYRE.Hivi tunakwenda wapi watanzania,mbona tumewakabidhi yetu nchi majambazi,hatuna njia mbadala ?.Tusimame imara tuseme wote kwa pamoja sasa inatosha mafisadi hawana nafasi ya kutuongoza tena.Mwaka 2010 uwe ni mwaka wa mabadiliko,tusikubali kudanganywa na kanga,kapelo,tshart na takrima kwaujumla wake.

RICHARD MONDULI

na G KABONDE, ARUSHA,TANZANIA, - 15.04.08 @ 11:05 | #6637

WAKATI DON CHENGE ANABEBA HIYO CASH MH FISADI ANAYEOGOPWA ALIKUWA WAZIRI WA MAMBO YA NJE,MINADHANI KIPINDI HICHO ALIKUWA LIKIZO BONGO HIVYO AKUJUA KILICHOTOKEA.DANADANA ZINAENDELEA KAMA KAWA.LIST OF SHAME SASA TUMEIDHINISHIWA NA HAO WAPINZANI WA UK,SLAA UNASHIRIKIANA NA SERIKALI YA UK NINI?

na kimune - 15.04.08 @ 11:05 | #6638

Jamani viongozi wetu tuhurumieni sisi masikini. Kumbe aliyekuwa anatujali ni "Nyerere" Tunaliwa jasho letu na hakuna wa kutuonea huruma. Ipo siku Mungu atatukumbuka. Ole wenu.

na Furaha Manyama, Musoma, TZ, - 15.04.08 @ 11:05 | #6639

Wandugu hebu tutafakari sehemu hii ya habari: "KIBALI HICHO AMBACHO HAKINA SHAKA KILITOLEWA KWA BARAKA ZA MAMLAKA HIYO KUU YA DOLA NA HUSUSAN IKULU, NDICHO KILICHOWEZESHA KUINGIA NCHINI KWA MAOFISA HAO WA SFO MIEZI KADHAA ILIYOPITA."

Inaonyesha wazi kwamba JK alikuwa na taarifa hii wakati akimchagua Chenge 12/02/2008 kwenye baraza jipya la mawaziri. Hapakuna mawili:
1. JK amemchagua tena Chenge ili aumbuke akiwa Waziri na kumuhaibisha mbele ya umma wa waTanzania

2. JK yuko kwenye nafasi ya kumtetea Chenge kuhusiana na mapesa hayo, aidha ni halali au wameshiriki pamoja

na John Shaaban, Murutunguru, UK, - 15.04.08 @ 11:06 | #6640

KUING'OA CCM SI SULUHISHO BALI WATANZANIA TUBADILIKE: UO'NGOFU UNAHITAJIKA:
Viongozi hawa wachukua mali ya serikali bila shaka wamelelewa hivyo kuanzia shule ya msingi.
-waliona kuiba daftari, vitabu, kalamu za shule sio wizi kwani hawajamwibia mtu binafsi.
kuhalalisha kuiibia, shule, benki, yaliyokuwa maduka ya ushirika, vyama vya ushirika lilikuwa ni jambo la kawaida katika jamii ya watanzania.
watu wengi wamekuwa wakitafuta nafasi kama hizi kufirisi maana hakuna mhusika mmoja mwenye uchungu. Kwa hiyo ni "dhambi ndogo" ya jamii ya watanzania. Mtu anapokuwa waziri bado ana mawazo hayo kwamba hajaiba kwani hakumwibia mtu mmoja.
Dini zetu kubwa za Kikristo na Kiislam hazijawahubiria kwa nguvu watanzania kuhusu dhambi ya namna hii kwamba ni sawa na uuaji!! Ndio maana baadhi ya nchi za Asia kama China viongozi mafisadi huwekwa kitanzi kwani wanajua uzito wa kuiibia taifa au serikali.
Labda wangeongoza hata CUF au CHADEMA wangeendeleza ufisadi huo kwani baadhi ya viongozi hao walifirisi mashirika ya umma, shule, kampuni n.k.
KWA HIYO TUNAPOMSIHI RAIS KUWAWAJIBISHA MAFISADI TUTILIE MAANANI KWAMBA LAZIMA WATANZANIA KUO'NGOKA NA HIVYO KUONA WIZI NI KUCHUKUA CHOCHOTE AMBACHO SIO HAKI YAKO, KUCHUKUA CHOCHOTE BILA BILA KUPEWA BILA YA KUTOA JASHO.

na Fredy K. - 15.04.08 @ 11:07 | #6641

Watanzania wote wezi,tunatofautiana staili ya kuiba tu.Hakuna aliye msafi na ndio maana tunabaki kubwabwaja hatuchukui hatua yeyote.Ni nani anayeishi kulingana na Kipato Chake halali hata huyo Kikwete Urais hakuupata Kihalali ndio maana aliwachafua wenzie na Hakuna anachokifanya masiha yemepanda na sisi tumekaa kulalamika tu.Mpaka lini?Let us cut their Head off if we mean Business.
Semzaba.

na Semzaba, tanzania, - 15.04.08 @ 11:21 | #6643

Hakuna haja ya kulalamika watanzania tunatakiwa kubadilika. Wakushikiwa bango ni Kikwete atwambie kama alikuwa hajui hili la Chenge na mengine mengi - Richmond, Kiwira Coal Mine, EPA

na Jerry M., Tanzania, - 15.04.08 @ 11:23 | #6644

CHAKUBANGA AMPIGA MKOLONI
Hii ni hadithi iliyovutia mno enzi hizo za shule ya msingi. Chakubanga alimtandika ngumi mkoloni mpaka koti likawa linapepea. Ni hadithi nzuri. Yu wapi CHAKUBANGA awatwishe ngumi WAKOLONI MAMBOLEO. Give me a gun I will Fix them

na TICO, Mwanza, - 15.04.08 @ 11:25 | #6645

Tatizo hili si la Chenge tu. nI TATIZO LA KIMAADILI. Asilimia kubwa ya Watanzania sasa hivi ni Mafisadi ni kwa vile tu hatupati nafasi ya kuwa sehemu za kufanyia ufisadi. Kila mahali sasa hivi kuna ufisadi kinachotofautisha ni kiwango tu cha ufisadi. Watumishi karibu wote ama wanafanya vitendo vya kifisadi ama wanatamani kutenda vitendo hivyo kwenye sehemu zao za kiutumishi. Angalia ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali, ni ULAJI TU KWA KWENDA MBELE. Kufanya kazi kwa uaminifu sasa hivi ni ujinga kwa mtazamo wa Watanzania. TUFANYE NINI?. UADILIFU UANZIE KWA RAIS MWENYEWE KISHA ATEUE WASADIDIZI WAKE AMBAO NI WAADILIFU. VIONGOZI WA JUU WAKIWA WAADILIFU WANANCHI NAO WATAWAIGA NAO WATAKUWA WAADILIFU. KWA SABABU KIONGOZI WA CHINI ANAWEZA KUWA MWAMINIFU LAKINI AKAPEWA MAAGIZO YA KIFISADI NA BOSI WAKE. HAYA YANAFANYIKA SANA NA TUNAYAONA.

na Mwangodo G.J.M, Iringa, - 15.04.08 @ 11:29 | #6646

Tubadili jina la nchi tuitwe Bongoland (ufisadi)kwasababu tumeshindwa kuwag'oa mafisadi tunawakumbatia.Uchaguzi wa ubunge jimbo la kiteto unadhiirisha kuwa watanzania sio watu makini kipindi hicho kashfa za richmond,epa,zilikuwa zimepamba moto lakini wapiga kura kiteto wakashindwa kukiadabisha chama cha mafisadi(ccm)

na Halfan M, Sanawari,Tz, - 15.04.08 @ 11:29 | #6647

Nimefurahishwa sanaa na maoni ya wasomaji katika safu hii. Ombo langu ni kutaka uitafutie nafasi katika gazeti lako ili watu wengi zaidi waweze kusoma maoni hayo, Kwani wengi hawana uwezo wa kuifikia mitandao. ikiwezekana anzisha hata kijarida cha maoni pale panapokuwepo na mjadala mzito wenye maslahi kwa taifa.

na Masao D. F, Mpwapwa/ Tanzania, - 15.04.08 @ 11:33 | #6649

ni mshangao tu! mungu ni mkubwa na bado

na bahati nassoro, dar es salaam/tanzania, - 15.04.08 @ 11:36 | #6650

Wananchi wajifunze kwamba hakuna kitu kinachotoka bure kwa maana hiyo wananchi wanapopewa na kofia za yeboyebo na fulana za shuka ya hospitali wakati wa upasuaji haya ndio malipo yake, watu mnadanganyika na vitu vya siku mbili huku mnafidia kwa kukosa vitanda hospitalini,shule, zahanati hebu watanzania tuhamkeni kwa maana watu hawafai wako kwa matubo yao na familia zao lakini siku itafika tu watu tutakapoanza kutembea barabarani na kuwatoa maofisini kwao kama serikali inashindwa kuwatoa kwa taratibu siku hiyo watu hawatajali kama kuna virungu au risasi kwa maana watu wameshachoka MAFISADI WAKUBWA ******.

na Jesse, Tanzania, - 15.04.08 @ 11:37 | #6651



KWA KWELI CCM NI NAMBARI ONE KWA KUFUGA WEZI!
HUYU NI MMOJA TU ILA KUNA WENGINE WENGI BADO WAMEJIFICHA.KWA HALI HI SIRUDI TENA TANZANIA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

CCM INAZIDI KUPOTEZA UAMINIFU KWA WATANZANIA.VIONGOZI WA NCHI HII MTAENDELEA MPAKA LINI KUMNYANYASA MLIPA KODI?HII INASIKITISHA SANA.

KIONGOZI ALIYEKUWA NA HURUMA NA WALIPA KODI KATIKA NCHI HII NI MWL.NYERERE PEKE YAKE LAKINI KILA ALIYEKUJA BAADA YA HAPO ANA UCHU WA KUJILIMBIKIZIA YEYE NA JAMAA ZAKE WALIOMZUNGUKA.
UKIMYA WA WATANZANIA USIWAFANYE MKAWAONA KUWA NI MAMBUMBUMBU KWANI SIKU WATAKAYOAMUA KUSEMA SASA INATOSHA NCHI HAITAKALIKA HIYO!
NINAWASIKITIKIA WATOTO WA WAKULIMA WA TANZANIA KWANI WANAISHI MAISHA YA KUBAHATISHA WAKATI VIONGOZI WAO WAMEJAZA PESA KWENYE AKAUNTI ZILIZOPO KWENYE BENKI ZA NCHI ZA WATU.NA VIONGOZI HAO HAWAISHI KUWAHUBIRIA WAKULIMA KUWA KILIMO NDIYO UTI WA MGONGO NA MAENDELEO YATAPATIKANA KWA KILIMO,JE,HII NI KWELI?HUU SASA NI WAKATI WA KUAMKA JAMANI.HATUTAKI VIONGOZI WA KUJAZA MATUMBO YAO,TUNATAKA VIONGOZI WA KUBORESHA HALI ZA WATU WA CHINI ILI NAO WAISHI KWENYE NYUMBA NZURI,WAWE NA UHAKIKA WA MATIBABU NA ELIMU BORA ILI WATU HAWA WAJE WAIJENGE TANZANIA KWA MOYO.

UCHAGUZI WA MWAKA 2010 ASIYE NA MWANA AELEKE JIWE.SIJUI CCM MTAWAAMBIA NINI WATANZANIA AMBACHO WATAWAELEWA."YOU CAN FOOL SOME PEOPLE SOMETIMES BUT YOU CAN NOT FOOL ALL THE PEOPLE AT A TIME".
KAZI KWENU !!!!!!!!

na Betty Brown, Copenhagen,Denmark, - 15.04.08 @ 11:44 | #6652
 
Tunapaswa kujiuliza ni kwanini JK ameamua kusfiri na huyu jamaa, what is it that prompted him to travel around with him at this particular moment. Kwa wenye kujiuliza na wanaweza kupata majibu hapo. JK anajua involvement ya Chenge kwenye deals za ufisadi kuliko mimi na wewe tunavyojua, lakini swali linakuja ni kwanini baada ya reshuffle alimrudisha tena? Tukiwa na jibu la hili swali, tunaweza kufahamu ni karata gani JK anataka kucheza, huenda tunakaribia kufungwa goli la kisigino, au kutakuwa na own goal. Huenda Balali ni Chenge, na balali mwenyewe tunayefikiri ana siri kubwa ya ufisadi ni nothing.
Kingine ni kuwa mwenyewe Chenge amesema hizo dola zaidi ya milioni moja alizonazo hazitokani na Radar, lakini mpato yake yanajulikana wazi, na kama sio Radar basi anaweza kutusaidia kutuambia alifanya biashara gani hadi kupata hela zote hizo, inawezekana anasema kweli siyo za Radar, ni za EPA!
pia hii toka Mtanzania Daima
...KIBALI HICHO AMBACHO HAKINA SHAKA KILITOLEWA KWA BARAKA ZA MAMLAKA HIYO KUU YA DOLA NA HUSUSAN IKULU, NDICHO KILICHOWEZESHA KUINGIA NCHINI KWA MAOFISA HAO WA SFO MIEZI KADHAA ILIYOPITA.
Mkuu Bongolander niko na wewe. Hapa ni wazi kwamba JK alikuwa na taarifa hii wakati akimchagua Chenge 12/02/2008 kwenye baraza jipya la mawaziri. Kuna mawili:

1. JK amemchagua tena Chenge ili aumbuke akiwa Waziri, kumuhaibisha mbele ya umma wa waTanzania (tht's own goal mkuu) pasi na kuonekana kuwa firm-on-issues kama alivyofanya kwa balali (replace l with z)

2. JK yuko kwenye nafasi ya kumtetea Chenge kuhusiana na mapesa hayo, kuwa aidha ni halali (maana wameshiriki pamoja au amemuahidi share, kutimiza misemo ya "wajinga ndio waliwao" na/au "watasema sama" kama asemavyo mzee wa UWAZI NA UKWELI...)
 
Wizara aliyopo hivi sasa inamfaa sana tu. Hiyo ndio miundombinu ya kibantu......
CCM Oyeeeee.....Oyee...Zidumu fikra za mwenyekiti wa CCM.....Zidumu....

Mwazange,

Umekula nini leo,Kwa hili Fikra za Mwenyekiti haziwezi kudumu kwa wezi,Kmati kuu inakaa mwezi ujao na mie nakuapia Maumuzi yale ya Butiama ndiyo yatakapotoka.

Hoja ya kuwang'oa mafisadi ndani ya Chama italewa na hakika Chengi ndio Mwisho wake,Asipotoka basi Kwenye Bunge lijalo utawasilishwa ushahidi wa kumng'oa kama ilivyokuwa kwa EL..na kamati ianweza kuundwa kama spika akitaka Natural Justice.ila watu wameshaapa kumuumbua Chenge,kuanzia ofisi aliyokuwapo mpaka hapa alipo.
 
pia hii toka Mtanzania Daima

Mkuu Bongolander niko na wewe. Hapa ni wazi kwamba JK alikuwa na taarifa hii wakati akimchagua Chenge 12/02/2008 kwenye baraza jipya la mawaziri. Kuna mawili:

1. JK amemchagua tena Chenge ili aumbuke akiwa Waziri, kumuhaibisha mbele ya umma wa waTanzania (tht's own goal mkuu) pasi na kuonekana kuwa firm-on-issues kama alivyofanya kwa balali (replace l with z)

2. JK yuko kwenye nafasi ya kumtetea Chenge kuhusiana na mapesa hayo, kuwa aidha ni halali (maana wameshiriki pamoja au amemuahidi share, kutimiza misemo ya "wajinga ndio waliwao" na/au "watasema sama" kama asemavyo mzee wa UWAZI NA UKWELI...)

Unayosema ni jambo linalowezekana.

Lakini tusisahau dhana moja ambapo kiongozi ni kioo cha jamii husika, na kabla hujamteua kiongozi lazima ufanye uchunguzi wa kina kuhusu uwezo wake wa kuifanya kazi unayotaka aifanye. Tabia yake ya ndani na nje ikiwa ni pamoja (ubadhirifu, ufuska, ulevi,kutunza siri n.k). Hili limekuwa ni failure kwa muungwana

Kama kila kiongozi unayemteua anakuwa na matatizo then kwa nini tusiseme na yeye ni mmojwapo lakini anajifanya hafanani nao???
Maana kuna msemo usemao "KAA NAO, KULA NAO LAKINI USIFANANE NAO"
 
Back
Top Bottom